Tundu Lissu: Mpambanaji aliyeuanza uanaharakati utotoni

Angalia tbc kuna viroja bi.kiroboto amechakachua kura za maamuzi sasa wanaitxa majina juu ya marekebisho ya vifungu kwenye mswada wa sheria maadili ya mahakama

Spika bi Kiroboto umempatia kweli. Hili jina linamfaa sana!
 
Tundu Lissu unanipa raha, taifa linahitaji watu wanaoona mbali kama wewe. Dumisha mapambano dhidi ya mfumo dume wa chama tawala.
 
So, you wanted him to pretend, not to be himself, as is the case with CCM politics, so as to be appreciated by Werema and other like-minded CCM species? Ooh, by the way, there is nothing really surprising about your argument-the CCM status quo has never been impressed by intellectual prowess, which is why they can send to an important gathering such an intellectually empty representative as...

But be reminded and warned that these are times of sincerity and straightforwardness-faking and artificiality can no longer be tolerated and honoured in this country. We have just seen this in the prematurely concluded pubic hearing about the new constitution. With the exception of CCM stalwarts, people of this country will no longer bear with business as usual politicians. Insincere and fake politicians will be named, shamed and shunned. If there is one enemy that is surely and quickly killing CCM, of course to the pleasure and delight of the country, is insincerity, artificiality and faking.

Thanks;
I was just reading this thread as a guest and you pull me to sign In.To you Ruta! We do not have time left for Blah Blah,its time for immediate words and action in order to safe our Country.
 
Tundu Lissu, we acha tu

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 16th April 2011 @ 14:30 Imesomwa na watu: 488; Jumla ya maoni: 0

BUNGE la Tanzania leo limelazimika kupiga kura kuamua kukubali au kukataa mapendekezo ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ya kuwaondoa wakuu wa mikoa na wilaya katika kamati za maadili za mahakama.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliamuru ipigwe kura ya kumuuliza Mbunge mmoja mmoja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kumuomba hivyo kwa kuwa idadi ya sauti za wabunge waliokuwa wamesema ndiyo au siyo wakati wa kura ya jumla zilikuwa zimekaribiana.

Wabunge walipiga kura za ndiyo au hapana wakati Bunge lilipokaa kama kamati mjini Dodoma kupitia vifungu vya muswada wa sheria ya uendeshaji wa Mahakama wa mwaka 2011 uliowasilishwa jana bungeni.

Kabla ya wabunge kupiga kura za sauti kwa ujumla na Mbunge mmoja mmoja kusema ndiyo kama anakubali mapendekeo ya Lissu au hapana kama hayakubali, kulikuwa na mvutano kati ya Mbunge huyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.

Mvutano huo ulitokana na mapendekezo ya Lissu ya kubadili vifungu kadhaa kwenye muswada huo ili sheria inayotungwa iwe na manufaa, Kombani na Werema waliyakataa na kusema kuwa Mbunge huyo alikuwa anapotosha.

Kwa nyakati tofauti, mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, Mbunge wa Viti Maalum, Stella Manyanya, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi walisimama kupinga mapendekezo ya Lissu.

Manyanya alisema bungeni kuwa, Lissu alikuwa anaingiza masuala ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) bungeni, na kwamba, Mbunge huyo alikuwa anapoteza muda.

Lissu alimjibu kwa kusema, Manyanya alikuwa hajui anachokisema, na kwamba anamsamehe. Lissu alihoji mantiki ya Werema kusema kuwa huu si muda mwafaka wa kuyakubali mapendekezo ya Mbunge huyo na akasema "Ni upi muda huo kama si huu".

"Tunataka kukeep politicians at bay, mahakama zifanye kazi kwa uhuru" amesema Lissu na akawaeleza wabunge kuwa wanapopiga kuwa watambue kuwa wanapiga kwa ajili ya Watanzania na si Chadema.

Kwa mujibu wa Lissu, amependekeza Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya wasiwe wajumbe kwenye kamati za maadili ya mahakama kwa kuwa viongozi hao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwamba wakijumuishwa huko watazivuruga kamati hizo kwa kupeleka itikadi za chama chao.

Lissu amewaambia wabunge kuwa , mamlaka ya kudhibiti nidhamu isiende nje ya utumishi wa Mahakama.

Mnadhimu huyo wa kambi ya Upinzani Bungeni amesema, masuala ya kimaadili ya mahakama yashughulikiwe kwa taratibu za kimahakama na kwamba, heshima ya mahakama ilindwe kwa kuwazuia wanasiasa kufanya kazi za taaluma ya fani hiyo kwa kuwa hawayafahamu na hayawahusu.

"Hawa watawala, makada wa CCM wasiingie katika kamati za maadili za mahakama" amesema Mbunge huyo na akadai kuwa viongozi hao wakiingia kwenye kamati hizo wataingiza mambo ya siasa kwenye masuala ya taaluma.

Wakati wabunge wanaanza kupiga kura kwa kuitwa jina mmoja mmoja, hakukuwa na utulivu bungeni hasa wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipoulizwa kwamba anakubali au kukataa mapendekezo hayo.

Pinda alisema ndiyo, Zitto akasimama kumpongeza, Makinda akasema hakusikia Waziri Mkuu alisema nini, akaulizwa tena, Waziri Mkuu akarudia kusema ndiyo, akaulizwa tena, akasema ' nimesema ndiyo'. Hakukuwa na utulivu bungeni, Makinda akawakemea wabunge kwa kusema "acheni mambo yasiyofaa…kelele zisizo na sababu zikome".

Zitto amempongeza Pinda kwa kuunga mkoon pendekezo la Lissu hasa ikizingatiwa kuwa Pinda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM.

Lissu aliwaeleza wabunge kuwa wajali maslahi ya Watanzania, kwa kwa hawatungi sheria kwa ajili yake. "Msiniangalie mimi, wafikirieni Watanzania" amesema Mbunge huyo na akasema, inawezekana anawaudhi sana baadhi ya wabunge lakini sheria inawahusu Watanzania si yeye.

Spika amesema, Bunge lina wabunge 350, wabunge 128 hawakuwepo wakati wa kupiga kura, wabunge 69 walikubali pendekezo la Lissu, 152 walilikataa.

Wakati wabunge wakiwa katika hatua za mwisho za kupitia vifungu, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alipinga mapendekezo ya kuweka kiwango katika kila bajeti kwa ajili ya mfuko wa mahakama ili uwahudumie majaji na mahakimu kwa kuwa wanadhalilika.

Mbunge huyo alipendekeza kuwa bajeti ya mahakama izingatie mahitaji ya mahakama, wabunge wengi wamepiga kura kukataa pendekezo hilo.

Sitta amesema, yeye ni mwanasheria mzoefu, pendekezo la Lissu linapinga ibara ya 99 ya Katiba ya Tanzania, Mbunge huyo akasema, anamheshimu sana Waziri huyo lakini amekosea, na akasema wabunge wapige kura ili ifahamike ni akina nani wanatetea mahakama.

Lukuvi amesema, pendekezo ya Lissu ni sahihi lakini fedha kwa ajili ya mahakama zitatengwa kulingana na uwezo wa nchi kwa kuwa hata Wizara na Bunge hawapati fedha kwa mujibu wa mahitaji yao.

Makinda amempongeza Lissu kwa kazi kubwa aliyoifanya na akasema alichokifanya Mbunge huyo ndiyo kazi yake.

Jumla Maoni (0)
Tuma Maoni yako Jina la Kwanza:
Jina la mwisho: Baruapepe: Barua Pepe imekosewa. Maoni yako: Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
 
PHP:
"Tunataka kukeep politicians at bay, mahakama zifanye kazi kwa  uhuru"  amesema Lissu na akawaeleza wabunge kuwa wanapopiga kuwa watambue  kuwa  wanapiga kwa ajili ya Watanzania na si Chadema. 

Kwa mujibu wa Lissu, amependekeza Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya  wasiwe  wajumbe kwenye kamati za maadili ya mahakama kwa kuwa viongozi  hao ni  makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwamba wakijumuishwa huko   watazivuruga kamati hizo kwa kupeleka itikadi za chama chao.

Hizi hoja zina mashiko sana ila basi tu CCM wao ni "DR. NO"........................................hawataki mabadiliko lakini wangelipenda waendelee kututawala............how absurd......................
 
Angalia tbc kuna viroja bi.kiroboto amechakachua kura za maamuzi sasa wanaitxa majina juu ya marekebisho ya vifungu kwenye mswada wa sheria maadili ya mahakama

ha haaaa haaaaaaaa haaaaaaa ... yaani umeigharamia starehe ya weekend yangu yooote ... huyu ni nani ..... s'''''pika au naibu
 
inakera imeonyesha jinsi gani wabunge wanateteya masilai ya chama furani na siwatanzania kupigakura wananza kuitana mubungehakuwepo hajuwi kilichojadiliwa anasema ndiyo

Hiyo isikuumize kichwa, muhimu ni wapinzani kuibua hoja na watawala (wabunge wa ccm) kuikataa halafu wananchi kuamua.. usifikiri wananchi hawafuatilii ila wao ccm kwa ujinga wao wanafikiri wananchi hawafuatilii ndio maana kila kitu kiletwacho na wapinzani wanakikataa kumbe nikwa maslahi ya taifa letu na sio chama.
 
tundu lisu ni mashine.ccm wameweka siasa mbele.naamini kwd mjadala wa leo hakuna mwanasheria au mwanamahakama ataipenda ccm!
 
Kamati ya Bunge iliyokaa kupisha Muswada tajwa hapo juu inapendekeza Mkuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya kuwa wenyeviti wa kamati za nidhamu za Mahakama katika ngazi ya mkoa na Wilaya!

Mhe. Lissu alijenga hoja kupinga wanasiasa kuwa ndio kamati za nidhamu za mahakama kwakuwa kunaweza kuingilia uhuru wa mahakama. CCM hawaoni hilo wanapinga kwa kuzomea, yaani wabunge walitumia fedha za Umma kwa kutetea maslahi ya Umma walikuwa Zitto na Lissu peke yako wakiungwa mkono na wabunge wa CDM na baadhi ya wabunge wa CUF.

CCM bado hawa jajua ubovu wao, hawa jui nini kina waumiza hawajui kansa inayowala mpaka leo, Eti wamejiandaa na kuvua gamba, .

CCM wanatetea sheria za kibepari, Watanzania wanawaona, CCM imedhiirisha uwezo wake na CCM inajitafutia chuki yenyewe, mchawi wa CCM ni uwezo CCM na utashi wao katika kutetea Watanzani, sasa CCM wanataka kuifanya Mahakama sehemu ya Jumuiya za Chama! CCM wameisahau Jembe na Nyundo; Kwa mtindo huo Mtaendelea kuchukiwa na kila Mtanzania na mtategemea kura za wizi tu! Waziri Mkuu alikuwa anamuunga mkono Lissu lakini Makinda anamlazimisha akatae.

Mwana-sheria Mkuu anatia aibu, Wereme amenifanya nihoji alikuwa vipi Jaji kama huo ndio uwezo wake!

Mtu yeyote aliyeona hicho kipindi amejua faida za kuongeza wabunge wa Upinzani CCM, wameonyesha hasara ya kuendelea kuwa na wabunge wengi wa CCM.
 
Makada wa chama kuwa wenyeviti wa kamati za nidhamu mahakamani? Duh, Mungu saidia. Ila nafikiri mambo mengi wanafanya kwa ku-beep tu. na baadae yatakuwa "mawazo yao binafsi" Tusubiri jaji mkuu nae atoe mapendekezo yake kwa hilo!!
 
Kamati ya Bunge iliyokaa kupisha Muswada tajwa hapo juu inapendekeza Mkuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya kuwa wenyeviti wa kamati za nidhamu za Mahakama katika ngazi ya mkoa na Wilaya!

Mhe. Lissu alijenga hoja kupinga wanasiasa kuwa ndio kamati za nidhamu za mahakama kwakuwa kunaweza kuingilia uhuru wa mahakama. CCM hawaoni hilo wanapinga kwa kuzomea, yaani wabunge walitumia fedha za Umma kwa kutetea maslahi ya Umma walikuwa Zitto na Lissu peke yako wakiungwa mkono na wabunge wa CDM na baadhi ya wabunge wa CUF.

CCM bado hawa jajua ubovu wao, hawa jui nini kina waumiza hawajui kansa inayowala mpaka leo, Eti wamejiandaa na kuvua gamba, .

CCM wanatetea sheria za kibepari, Watanzania wanawaona, CCM imedhiirisha uwezo wake na CCM inajitafutia chuki yenyewe, mchawi wa CCM ni uwezo CCM na utashi wao katika kutetea Watanzani, sasa CCM wanataka kuifanya Mahakama sehemu ya Jumuiya za Chama! CCM wameisahau Jembe na Nyundo; Kwa mtindo huo Mtaendelea kuchukiwa na kila Mtanzania na mtategemea kura za wizi tu! Waziri Mkuu alikuwa anamuunga mkono Lissu lakini Makinda anamlazimisha akatae.

Mwana-sheria Mkuu anatia aibu, Wereme amenifanya nihoji alikuwa vipi Jaji kama huo ndio uwezo wake!

Mtu yeyote aliyeona hicho kipindi amejua faida za kuongeza wabunge wa Upinzani CCM, wameonyesha hasara ya kuendelea kuwa na wabunge wengi wa CCM.

Huo ni ukweli na hakuna adui mkubwa wa ccm kuliko ccm yenyewe, acha waelekee kwenye anguko maana wamelitaka wenyewe..
 
hii inashangaza sana. uchungu ninaouona sasa imefikamahali wabunge hawaangalii hoja yenye maslahi kwa umma bali ushabiki tu wa chama. hawawezi kuunga hoja nzuri kwa kuwa tu imetolewa na mbunge wa upinzani. hakika tz tunaelekea kusiko sasa
 
Ccm mambumbu ni wengi na inawezekana hata sheria zenyewe hawazijui ndo maana wao kusema ndio ni rahisi sana kuliko kusema hapana mi naona kuna haja ya kuwapa darasa la sheria na umuhimu wake kwa jamii ya watz
 
Nadhani wabunge wanafanya makosa sana pale wanapofanya maamuzi kwa kuegemea zaidi ‘itikadi’ zao. Matokeo yake ni kuwa na sheria mbovu kama hii waliyopitasha jana. Naamini wengi wa waliokataa mapendekezo ya Mh. Lissu ni kwa sababu tu anatoka upinzani. Na inawezekana kabisa ‘chief-whip’ was CCM alishatoa maelekezo kuwa hoja za serikali (ya ccm) waziunge mkono na kama ni kusosoa basi wakosoe trivial things kama; comma, full-stop, etc kama ambavyo tumeona baadhi ya wenyeviti wa kamati za kudumu wamekuwa wanafanya.
Badala ya kuongelema mambo ya msingi e.g madhara ya kuwafanya wanasiasa wasimamie nidhani ya kiutendaji katika mahakama za mikoa na Wilaya Mwenyekiti wa kamati husika na sheria hii Mh Simbachawene (I believe) ameishia kukosoa vitu hivyo nilivyotaja hapo juu (comma, full stop na mambo kama hayo)!

Jana kwenye post yangu nyingine niliomba kama kuna mtu anaweza kutuwekea orodha ya wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Education credentials zao ili tuweze kuwaelewesha wabunge wetu ni blunder gani waliofanya leo Dodoma. Kama tujuavyo wengi wa Elimu ya wengi wa wakuu hawa wa Mikoa na Wilaya ni ya mashaka na hasa katika taaluma ya Sheria. Kwa mfano, haiingii akilini kwa standard 7 or even Form VI leaver ambaye hana uelewa wala uzoefu wa kutafsiri sheria (mahakama kazi yake kubwa ni kutafsiri sheria) achunguze watu wanao-pratice sheria? Wabunge wanaona shida gani au kuna hasara ipi kama Taifa kuwa na mfumo wa kusimamia utendaji na utoaji wa huduma za kimahakama ndani ya Taaluma na ethics za Taaluma yenyewe?
Tanganyika Law Society nao wanaweza kutusaidia hapa kwa kutumia experience yao watueleze nini madhara (na faida if any) ya watendaji wa kimahakama kusimimiwa na wanasiasa.
 
Mm nimesikitishwa sana na maamuz ya wabunge wa chama cha kifisadi inaonesha huyu mwanamke hawezi uspika na anafanana na mhusika ndani ya kitabu cha tamthilia 'Kivuli Kinaishi' Bi Kirembwe anayewalazimisha wananchi wake kusema nyeusi kuwa nyeupe.
Pia Giningi ndani ya tamthilia hii ndo ccm ;make mahakama zina matatizo ambayo kama hoja mbili za AG Lissu zingeingia ktk muswaada basi ufanis wa mahakama ungekuwa mkubwa.
Kwanza kuachana na wanasiasa ambao hawana ujuzi wa sheria kusimamia nidhamu ya mahakama.
Na pili kama hoja yake ile ingekubalika ya kuhakikisha mahakama inawekewa sheria ya kuwasaidia kupata fedha inayotosha na ktk muda muafaka ;lingeondoa rushwa inayoshamiri ktk mahakama zetu

Nataka niwambie W.Fedha mh Z.KABWE na AG T.LISSU kwamba "kivuli kinaishi"na tunawapenda mno wabunge wa CDM.
 
Sasa wale ni wabunge wanavurunda vile,je hizo kamati za maadili za wanasiasa zitakuwaje?
 
hii inashangaza sana. uchungu ninaouona sasa imefikamahali wabunge hawaangalii hoja yenye maslahi kwa umma bali ushabiki tu wa chama. hawawezi kuunga hoja nzuri kwa kuwa tu imetolewa na mbunge wa upinzani. hakika tz tunaelekea kusiko sasa

Kwa kweli ni aibu sana, CCM ina hadi Ma-Prof wakina Mghembe wamedhalilisha elimu zao katika hili maana nilitegemea wakati wa kupiga kura ningeona tofauti ya Propaganda na Proffesionalism! Nilidhani watu kama Sophia Simba, Diana Chilolo, Zungu, Maji Marefu na Azani etc ndio wange sema hapana siyo hadi Samweli Sitta; Lowasa, Magufuri na Mwakyembe (Nilikuwa na hamu sana kusikia wanasema nini hawa) hawakuwepo sijui wangesema lipi Lakini Waziri Mkuu peke yake alisema hapana tena mara mbili ingawa Spika alilazimisha kwa vurugu kuwa Waziri mkuu hakusema ndio akijifanya kuwa hasikii anachosema Waziri Mkuu. Kwa kweli Zitto alitumia akili nyingi sana kusema kuwa wapige kura kwa kuita majina imesaidia kujua akili za mbunge mmoja mmoja! Watanzani wanahitaji kuwaongeza wakina zitto na Lissu wengi Bungeni maana CCM haipo hata kidogo kwa maslahi ya watanzania

CCM hawajui kabisa dhana ya vyama vingi wao wana-dhani ni kupingana na CDM kwa kila jambo! hata kama hilo jambo lina maslahi ya kitaifa! Yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM (Mbunge wa Ismani nadhani) alionyesha kuunga mkono Lissu ila anazunguka aliogopa kusema moja kwa moja huku akitetemea Maana kilicho muogopesha ni Lissu kusema kuwa rekodi imewekwa ni nani wanatetea Mahakama! Jamaa aliogopa sana. CCM ni ajabu sana kwa kweli bado inaota ndoto za 1980 za Mgombewa wao kugombea na Giza!
 
Nadhani wabunge wanafanya makosa sana pale wanapofanya maamuzi kwa kuegemea zaidi ‘itikadi' zao. Matokeo yake ni kuwa na sheria mbovu kama hii waliyopitasha jana. Naamini wengi wa waliokataa mapendekezo ya Mh. Lissu ni kwa sababu tu anatoka upinzani. Na inawezekana kabisa ‘chief-whip' was CCM alishatoa maelekezo kuwa hoja za serikali (ya ccm) waziunge mkono na kama ni kusosoa basi wakosoe trivial things kama; comma, full-stop, etc kama ambavyo tumeona baadhi ya wenyeviti wa kamati za kudumu wamekuwa wanafanya.
Badala ya kuongelema mambo ya msingi e.g madhara ya kuwafanya wanasiasa wasimamie nidhani ya kiutendaji katika mahakama za mikoa na Wilaya Mwenyekiti wa kamati husika na sheria hii Mh Simbachawene (I believe) ameishia kukosoa vitu hivyo nilivyotaja hapo juu (comma, full stop na mambo kama hayo)!

Jana kwenye post yangu nyingine niliomba kama kuna mtu anaweza kutuwekea orodha ya wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Education credentials zao ili tuweze kuwaelewesha wabunge wetu ni blunder gani waliofanya leo Dodoma. Kama tujuavyo wengi wa Elimu ya wengi wa wakuu hawa wa Mikoa na Wilaya ni ya mashaka na hasa katika taaluma ya Sheria. Kwa mfano, haiingii akilini kwa standard 7 or even Form VI leaver ambaye hana uelewa wala uzoefu wa kutafsiri sheria (mahakama kazi yake kubwa ni kutafsiri sheria) achunguze watu wanao-pratice sheria? Wabunge wanaona shida gani au kuna hasara ipi kama Taifa kuwa na mfumo wa kusimamia utendaji na utoaji wa huduma za kimahakama ndani ya Taaluma na ethics za Taaluma yenyewe?
Tanganyika Law Society nao wanaweza kutusaidia hapa kwa kutumia experience yao watueleze nini madhara (na faida if any) ya watendaji wa kimahakama kusimimiwa na wanasiasa.

Hili unalosema ni la muhimu sana, Kama alivyowai kusema Jenerali Ulimwengu Wakuu wa Wilaya ni watu wanachaguliwa bila kujua hata vigezo gani vinatumika katika kipindi hiki cha Kikwete tumeona wakuu wa wilaya vichefuchefu hadi kutapika! Ulimwengu alisema Kuna Darsa la saba hadi PhD, General wa Jeshi hadi CPl wa Jeshi ni vyeo ambavyo kwangu mimi nadhaani vinge futwa kupunguza gharama zisizo za lazima.
 
Back
Top Bottom