Tundu Lissu: Mpambanaji aliyeuanza uanaharakati utotoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu: Mpambanaji aliyeuanza uanaharakati utotoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LENGEJU BOB, Nov 2, 2010.

 1. L

  LENGEJU BOB Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetafuta sana 'Title' inayofaa,yenye uzito unaomstahili Ndugu Tundu Lisu (hapendi kuitwa mheshimiwa).Ashukuriwe Mungu wa Majeshi kwa kupatia zawadi hii.

  Kinana amejipa moyo, kwamba pamoja na Tsunami ya mabadiliko ktk uchaguzi huu, bado CCM inaamini itabakiwa na asilimia zaidi 70 ya wabunge ktk Bunge lijalo.. Kitu ambacho Kinana amejisahaulisha ni kwamba, katika karne hii ya mabadiliko mkazo utawekwa zaidi kwenye Nguvu ya hoja na sio hoja ya wengi.

  Nina hakika kuna miswada ya serikali haitapita kama ilivyozoeleka si kwa kukukataliwa na wengi bali kwa watu wachache kujenga hoja zenye mashiko, zinazowakilisha fikra za WaTZ Milioni 40 na si matakwa ya 70% ya wabunge wa CCM... Mbunge mmoja wa aina ya Lisu tija yake mjengoni ni zaidi ya wabunge 100 wa 'Ndiyo mzee'....!

  SOMA zaidi kumjua (updated June 2011) kwa hisani ya Gazeti la Raia Mwema:

   
 2. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Karibu jamvini....
   
 3. J

  Jwagu Senior Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 19, 2007
  Messages: 156
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NAUNGANA SANA NA WEWE kwani bunge lijalo likiwa na Tundu, Mwanyika, Zito, mdee, Mbowe, Mremas, nguvu ya hoja ndio itakuwa Slaa ya wanyonge na watetewa
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kumbe hela zipo kila mwaka,wananchi wana lazimishwa kuchangia gharama za kuendesha shule,....mwishoni hela zinarudishwa hazina eti zimebaki,kweli?

  Msome Tundu Lissu

   
 5. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hiki kichwa bana.........I concur kabisa 100%
   
 6. Mzee Dogo

  Mzee Dogo JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Leo robo ya tatu ya mwaka wa serikali but baadhi ya halmashauri hazijapokea fedha za utekelezaji wa miradi na maandalizi kwa ajili ya bajeti ijayo tayari yameanza, je ni lini serikali itatoa fedha hizo kwa ajili ya miradi iliyoidhinishwa na bunge?
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Truly CCM is a party of heartless beasts that will never see any good for our country's development.
   
 8. K

  Kide Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  tunahitaji viongozi wa aina ya kina Lisu ili nchi iweze kusonga mbele...yaani bil 30 zinarudishwa wakati hapo kibaha bila 65elfu ya dawati dogo haanzi form 1 na kule kilwa ni 55elfu pia!ni nini hki hawa TAMISEMI wanatufanyia waTZ??
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nina hamu kweli na bunge lijalo aisee
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Serikali ya CCM ni wizi mtupu, hakuna kitu pale!!
  Jibu sahihi: Operation Ufisadi Toka ili Watanzania tuanze kupata tena maendeleo!!!!!
   
 11. M

  Msharika JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  bunge litakuwa vululu vululu. Speake ataweza tumia ubabe wake?
   
 12. H

  Hosida Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda sana Hiyo Hoja ya Lissu. Nawasihi wabunge wengine wamuunge mkono ili waiwajibishe serikali kwa niaba ya waliowatuma pale mjengoni.
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama habari hizi ni kweli basi hapo Serikali imechemsha maana dhiki iliyojaa huko vijijini ilikuwa haistahili kurejesha fedha hizo hazina. Kuna miradi mingi haijakamilishwa huko kwenye halmashauri na mashule mengi yanatia simanzi na watoto wanaendelea kukaa sakafuni.

  Hoja hii ya Lissu itawaamsha na kuelewa kwamba wanahitaji kuwa responsible kwa wananchi au angalau kuwaonea huruma kidogo. Cha ajabu hao wakuu wa halmashauri ndiyo wanaoongoza kwa kodi zisizo na kichwa wala miguuu wakati wamekalia mahela. Pathetic!
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Zinaliwa hizo.
   
 15. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Una maanisha makinda au mimi?
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Lissu, Mnyika wawasha moto


  na Joseph Senga

  WABUNGE wawili, Tundu Lissu wa Singida Mashariki na John Mnyika wa Ubungo, wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kwa nyakati tofauti walitoa matamko yanayoashiria kuibana zaidi serikali katika kikao kijacho cha Bunge kuhusu masuala mbalimbali yanayoligusa taifa hususan kwa kipindi hiki.

  Tundu Lissu akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Singida alitangaza azma ya kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge akiomba iundwe kamati maalumu ya Bunge kuchunguza matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

  Mbunge huyo alitangaza azma hiyo huku akifafanua sababu za chama chake kuwakataza wananchi wa Singida kutoa michango ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Akirejea takwimu za mahesabu ya Tamisemi, alisema kwa mwaka wa fedha 2008/2009 na 2009/2010 zaidi ya shilingi bilioni 30 zilizotengwa na Bunge kwa shughuli za maendeleo zilirudishwa hazina.

  "Tungependa kujua… nafikiri wananchi wa Tanzania wanapenda kujua hizi fedha zimerudi kweli hazina au zimetumika kwa mambo mengine tusiyoyajua.

  "…Na ni sababu gani zilizofanya zisitumike wakati Watanzania nchi nzima wanachangishwa fedha kwa nguvu bila kuwepo sheria, bila kuwepo utaratibu wowote unaotambuliwa na sheria za nchi hii ili kujenga na kuendesha mashule.

  "Hii ni moja ya sababu ya kupeleka hoja binafsi ya kutaka Bunge liichunguze hii ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili Bunge linalotoa fedha liridhike kwamba kweli hizi fedha hazijatumika kweli au zimetumika kwa mambo mengine," alisema.

  Kwa mujibu wa Lissu, hotuba ya Waziri Mkuu aliyoitoa katika kikao cha Bunge cha Juni mwaka wa fedha wa 2009/2010 serikali kupitia Bunge hilo ilitenga shilingi 2,151,000 za sekta ya elimu kwa ajili ya mkoa wa Singida.

  "Bunge limekuwa likitoa fedha kila mwaka kuendeshea shughuli hizi za elimu kwa mikoa yote ya Tanzania nzima, kwa halmashauri zote za wilaya. Na kikubwa ni kwamba Bunge limetenga fedha za kutosha, ni lazima tujue fedha hizi zinatumikaje na zile zinazorudi kwa nini zinarudi na zimefanya nini baada ya kurudi wakati wananchi wanaendelea kuchangishwa mashuleni kila siku?" alisema mbunge huyo kwa kujiamini zaidi.

  Lissu ambaye pia ni mkurugenzi wa sheria na mambo ya katiba wa CHADEMA alifafanua kuwa katika kiasi hicho cha fedha za elimu kwa mkoa wa Singida, hadi kufikia Machi mwaka jana ni sh 1,187,000 tu ndizo zilizokuwa zimetumika na kwamba sh 905,000,000 zilirudishwa hazina baada ya kukosa kazi ya kufanya.

  "Katika miaka miwili mkoa wa Singida umerudisha Hazina zaidi ya shilingi 1,350,000,000 zilizokuwa zimeletwa na hazina kwa ajili ya kugharamia elimu peke yake na haya ni mahesabu ya serikali, ni mahesabu ya Waziri Mkuu bungeni, sasa wananchi wanachangishwa kwa sababu gani? Alihoji mbunge huyo huku akionyesha kukerwa na hali hiyo ya ‘changiachangia'.

  "Kwa sababu hiyo tumesema na nimesema wananchi wangu hawatachangishwa, wananchi wangu hawatanyang'anywa tena mali zao, na pili hii habari itakwenda bungeni, hii hoja itakwenda bungeni …natazamia kwa hiyo kupeleka hoja binafsi bungeni ya kutaka iundwe kamati maalumu ya Bunge kuchunguza matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)," alisisitiza Lissu.

  Wakati Lissu akitoa tamko hilo, Mnyika kwa upande wake ameitaka serikali kuacha kuilipa fidia kampuni ya Dowans na badala yake ianze kulipa madeni ya ndani inayodaiwa na maelfu ya Watanzania walalahoi.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho tawi la Mburahati jijini Dar es Salaam jana wakati wa ziara yake ya kichama, alisema serikali inatakiwa kukumbuka na kuzingatia matatizo ya wananchi wake ambao wamekuwa wakidai haki zao kwa kipindi kirefu bila mafanikio.

  Akifafanua zaidi katika hoja hiyo, alieleza kwamba iwapo serikali kupitia shirika la umeme TANESCO inazo fedha nyingi kiasi cha shilingi bilioni 94 ambazo inataka kuilipa Dowans, ni vyema kwanza ikalipa madeni ya ndani yakiwemo ya DECI, wazee wastaafu waliokuwa Shirikisho la Afrika Mashariki na malimbikizo ya mishahara ya walimu na malipo ya mikopo ya wanafunzi.

  "Kama kweli serikali inazo fedha nyingi kiasi hicho (shilingi bilioni 94), ni vyema ianze kulipa madeni ya ndani kwanza, walipe deni la Deci, wazee wetu wastaafu wa lililokuwa Shirikisho la Afrika Mashariki, mikopo ya wanafunzi na mengineyo ambayo ni muhimu sana kuliko hilo la kuilipa kampuni hewa," aliongeza.

  Mbunge huyo ambaye baadaye alihutubia mikutano miwili ya hadhara, yenye lengo la kusalimiana na wananchi wa jimbo hilo, alisema serikali pia inatakiwa kuwataja Watanzania wanaohusika na kampuni ya Dowans kabla ya kulipa deni hilo ambalo alidai kuwa wote wanajulikana.

  Akifafanua zaidi mbunge huyo alisema mwananchi ndiye ambaye amekuwa akibeba mzigo wa kulipa madeni kama hayo likiwemo deni linaloihusisha kampuni ya kufua umeme ya IPTL; deni ambalo linasabisha kushindwa kwa mwananchi wa kawaida kuweka umeme ndani ya nyumba kutokana na mzigo huo.

  "Leo mwananchi wa kawaida hana uwezo wa kuingiza umeme ndani ya nyumba kwa sababu anatakiwa alipie gharama za nguzo ambazo ziko juu sana kutokana na mzigo mkubwa wa madeni ilionao TANESCO ambayo wanayabeba Watanzania kupitia gharama za umeme," aliongeza.

  Mnyika aliwataka wananchi kutafakari kwa makini na kubaini ukweli kuhusu kutofautiana kwa Kamati Kuu ya CCM na UVCCM juu ya ulipwaji wa fidia hiyo ya Dowans na kubainisha kwamba mgongano huo ni wa kimaslahi ndani ya chama hicho hasa ikizingatiwa kuwa ni mgogoro unaokitafuna kwa kipindi hiki.

  "Mwaka 2006, tulifanya kongamano la Vijana wa CHADEMA, mimi nilizungumzia hoja ya kampuni ya Richmond ambayo ndiyo iliyozaa Dowans kuwa ilikuwa ni kampuni ya kitapeli, haikustahili kuingia nayo mkataba wa kuzalisha umeme, UVCCM hao hao waliibuka na kubeza hoja hiyo, leo wao ndio wanataka waonekane kama hoja hiyo ni ya kwao, wananchi waangalie wachuje mbivu na mbichi ni zipi," alisema Mnyika.
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Bunge likipitisha hii hoja Pinda hana kibarua kwa sababu ufisadi mkubwa upo na unaendelea kushamiri ndani ya ofisi yake ya Waziri Mkuu...............
   
 18. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Shime waTanzania Ukombozi Umekaribia!
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Hoja hii ya Mnyika haina mashiko hata chembe msingi wa kuwalipa au kutowalipa DOWANS ni sheria tu na wala siyo vipaumbele vya wepi wanastahili kufikiriwa gawiwo la kitaifa................................................

  Mnyika anapaswa ajikite zaidi katika kuchambua uhalali wa madai ya DOWANS kisheria ili aweze kulisaidia taifa hili kwenda mbele au kubaki hapo lilipo au hata kurudi nyuma kimaendeleo............................Malipo ya DOWANS yankinzana na sheria za nchi na hiyo ndiyo sababu ya kukataa kuyalipa na kushinikiza serikali kwenda mahakamani kuhoji TUZO ya kitapeli ambayo DOWANS walipewa
   
 20. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huo ni mwanzo tu yatafumuliwa mengi. keep it up TL
   
Loading...