Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

Binafsi sioni kosa la Lissu, ameeleza ni nini Rais alipaswa kufanya kabla ya kuzuia mchanga kusafirishwa.. Magufuli ana nia nzuri lakini njia anazotumia zinaweza zikaliingizia taifa hasara zaidi badala ya faida kwa sababu ya mikataba iliyoingiwa na serikali zilizopita na wawekezaji hawa..
Tusiwe mashabiki wa watu, tuwe mashabiki wa ukweli.. Tanzania ni yetu sote
Magufuli hana nia nzuri yyte, magufuli anataka muda wote ajiweke juu kisiasa na kutaka kujiona kuwa yeye anajua Kila kitu, huyo huyo hajui lolote na hakubali kusikiliza ushauri wa wataalamu, huyu atakuja kuiacha nchi haitamaniki
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Mkuu soma hii thread uelewe. Ni funzo hata kwetu tunaoshinda kwenye mitandao kumponda au kumtetea JPM kwenye hili suala bila uelewa. Tusome tujifunze; ku attack mtu badala ya hoja imeshaonyesha haitusaidii kamwe mkuu.
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
Rudi darasani ukajifunza maana ya mikataba, mkataba hata ungekuwa kandamizi upande mmoja, Lakini pande zote zimesaini ni mkataba,
 
Unaelewa kinacho jadiliwa hapa?
Mkuu moja ya matatizo yanayosumbua serikali na nchi hii ni watu kutojadili issues. JPM alilisema pia. Nilitegemea mtu kama huyu anamsema lisu, asome na akosoe hoja. Ajifunze hii saga ya udongo lakini kinyume chake anakataa kusoma na hapohapo analeta majungu. Hatutajenga nchi hii kwa staili hii. Hoja ya Lissu ni fikirishi; ni msaada kwa wafanya maamuzi. Sioni shida hapa unless kuwe na hoja tofauti.
 
Tatizo ni kwamba mkulu anadili na matawi badala ya mizizi, kuna mambo mengine anafanya kufurahisha tu watu lakini watu haohao baadae wanaanza kumkosoa na hii yote ni kwasababu hasikilizi ushauri kwa kuogopa sifa zitaenda kwa mshauri
Mkuu ni kweli Rais anahangaika na kuzima moshi badala ya moto unaotoa moshi. Hapa ni lazima tuchimbue mizizi yote ndipo matawi yakauke. Hapa ni kuitazama mikataba yote bungeni na ijadiliwe kwa kina hatutaki tena neno siri kwenye mikataba ya nchi yetu. Tujue mbichi na mbivu sio kujidondoshea sahihi tu utadhani una tia sahihi kwenye vitambulisho vya shule.
 
Kuna sehemu nilimskia Prezidaa akidai kuwa kwenye huo mchanga kuna dhahabu na amewataka wataalamu wa jiolojia kuchunguza huo mchanga ndio maana kazuia. Mbona hili hawalizungumzii au mi nilisikia vibaya?. Je kuchanganya dhahabu na huo mchanga ni part ya mkataba?
Mchanga unakuwa na kiasi kidogo cha dhahabu na madini mengine! Mbona haya mambo tumeyajadili sana kwa muda mrefu? Mlikuwa wapi?
 
Huo muda unapozuia kinyume na mkataba kwa ajili ya kufuata tetesi za WASAKAKIKI , taifa lijishtakiwa nakudaiwa fidia ndio Tanzania itakuwa imepata FAIDA ?
 
Mchanga kama kutetesi una dhahabu na wala si makinikia kama makubaliano yalivyo! Unataka uruhusiwe mchanga usafirishwe ushahidi utapata wapi?? Hebu tumieni akili kidogo basi..
Naona hujamwellewa Lissu. Mkuu, nakushauri usome tena.
 
Kuna sehemu nilimskia Prezidaa akidai kuwa kwenye huo mchanga kuna dhahabu na amewataka wataalamu wa jiolojia kuchunguza huo mchanga ndio maana kazuia. Mbona hili hawalizungumzii au mi nilisikia vibaya?. Je kuchanganya dhahabu na huo mchanga ni part ya mkataba?
Hizo ni fix tu!! Ili kuleta attention tu, ila baada ya muda c mrefu ukweli utajulikana tu na tutakuwa tumeshaumia
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
Hakuna hata ujualo, unaandika kwa hisia za kipuuzi bila kusoma kitu ukaelewa! Poor you
 
Binafsi huwa naogopa kitu kinaitwa mkataba wa kisheria. Maana nikikukmbuka kamkataba kale ka Msowero kati ya Chief Mangungo na Karl peters nabakiaga naogopa sana. lakini washauri wake wa sheria wanafanya nini . KABUDI , MASajU jamani msaidieni kama hataki jiuzuluni haraka
 
Ushauri mzuri kama Mh Rais atauzingatia kwa sasa. Wazungu waliowengi ni wezi sana na wanatumia ulafi na upumbavu wa viongozi wetu kututia umaskini. Rais tumia busara na hekima kututoa hapa vinginevyo tutaingia matatani. Yaani kwenye madini hapa ndipo napowachukia sana Marais waliopita kwani mikataba waliokuwa wanasaini kama kina Mangungu wa Msovero ndiyo inatutesa sasa. Mungu tuhurumie madini yetu wanayafaidi wageni kazi kweli kweli.
Mkuu ni kweli kabisa kuwa kwenye madini tumeshapigwa sana lakini ndio maana kuna mikataba!! Huwezi kukurupuka tu na kujifanya nina ibiwa uanze kuleta fujo kwani si kuna utaratibu wa jinsi ya kujinasua japo ni mgumu lakini kuliko kuleta hizi sarakasi??
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
wanapokea waliokuwa wanawaponda kisa wana hela. chadema bana ukiwa na hela tu mzee safii huyo mpe nchi mchaga kala hela akawapa dada zake viti maalumu
 
Binafsi sioni kosa la Lissu, ameeleza ni nini Rais alipaswa kufanya kabla ya kuzuia mchanga kusafirishwa.. Magufuli ana nia nzuri lakini njia anazotumia zinaweza zikaliingizia taifa hasara zaidi badala ya faida kwa sababu ya mikataba iliyoingiwa na serikali zilizopita na wawekezaji hawa..
Tusiwe mashabiki wa watu, tuwe mashabiki wa ukweli.. Tanzania ni yetu sote
Magufuli hana nia njema na taifa hili.

Ameokota dodo mnazini basi kazuzuuuuuka!! hadi anatia huruma.
 
Back
Top Bottom