ZILLAHENDER MPEMA
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 2,055
- 4,241
Kwa jinsi hiyo mikataba ilivyoandaliwa na inavoikaba Serikali zoezi la kuijadili upya ni kizungumkuti. Labda wanasheria wangeshauri kitaalam nchi itajiondoa vipi kwenye shimo hilo la mikataba mibovu bila kukiuka haki za wahusika kama zilivyoainishwa ndani ya mikataba hiyo.
Andiko limeainisha na limetoa mfano wa Rais wa Bolivia Evo Morales namna alivyofanikiwa kuzuia ujangiri wa kiuchumi nchini mwake,Magufuli alipaswa kufanya aliyoyafanya Evo kabla hajakimbilia "kuteka"mali za watu wanazozimiliki kihalali kabisa.Kwa mujibu wa mikataba yetu iliyosainiwa na Masultani Mangungo wa kizazi kipya chini ya awamu ya 3-4,mchanga huo ni mali ya mwekezaji,kuzuia mali ya mtu ni utekaji na hilo litapelekea Mwenye Mali kudai fidia.
.............................................................
Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.