Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

Maridhiano ya kitaifa kupitia tume maalumu yangelazimisha wote walioifisidi nchi,ilaghai nchi,ifitini nchi,Walioingia mikataba ya ulaghai,Mikataba mibovu,waliotengeneza mikataba ya kimangungo..

Tume ingewalazimisha waungame,watubu na kukiri madudu walioyafanya na siri zote zenye kusababisha umaskini,mateso,unyonyaji na uharamia wa rasilimali za taifa Tanzania...
 
Wanaomtetea JPM leo wanalazimika kuzibadili ID zao au kuwa wachunguliaji hapa JF ACACIA watakapoibwaga serikali mahakamani na watanzania kutumia kodi zetu kulipa fidia badala ya kuinua uchumi wetu.
Ubabe autumia kwa mama Jesca sio kwenye mikataba na sheria.
 
Ukimsoma vizuri Lissu ametoa suluhisho ambalo kama Taifa linaweza likafanya,hivyo pamoja na kumlaumu Rais Magufuli kwa kutoa angalizo,ametoa na SULUHISHO.

Soma paragraph yake ya Mwisho
Tangu lini wewe ukapingana na lissu???
 
kama tuna jeuri ya kukiuka mikataba tuanze na kuiweka adharani...maana nasikia kuna kipengere kinapiga marufuku kufanya hivyo...maana sasa tunachangia tusichokijua...ila hilo la kushitakiwa kwenye mahakama za mabepari ni given....tatizo jamaa wako smart kuliko sisi...na waliotuwakilisha kwenye hii mikataba walitanguliza matumbo yao...

Nadhani badala yake tungeanza na hawa walio saini hii mikataba...watueleze walitumia reasoning gani?!
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Mkuu ushauri upo na kumponda vyote vipo. Sasa hapo mkulu achague kile kizuri cha hovyo anaacha.
 
we litundu ulilipwa sh.ngapi kutangaza ile njaa uchwara.
njoo huku songea tukupe mahindi ukalishe kwenu .wewe kazi yako kupiga uwongo tu kwenu hakuna maendeleo yoyote domo kubwa kuliko masikio.
hivi lisu amewahi kufnya nini kwa nchi hii chenye mashiko,
ney tenda haki ,imba .kunawatu wamedanganya kuna mvua ya kununua thailand.
kunawatu watengeneza njaa feki
 
Mchanga kama kutetesi una dhahabu na wala si makinikia kama makubaliano yalivyo! Unataka uruhusiwe mchanga usafirishwe ushahidi utapata wapi?? Hebu tumieni akili kidogo basi..
Hiyo akili kidogo ingetumika wakati wa kuingia hiyo mikataba mibovu. Sasa hivi inatakiwa akili kubwa kurekebisha hiyo mikataba. Tukienda kichwa kichwa tutaula wa chuya.
 
wanapokea waliokuwa wanawaponda kisa wana hela. chadema bana ukiwa na hela tu mzee safii huyo mpe nchi mchaga kala hela akawapa dada zake viti maalumu
Kama hata mambo ya wazi hivi naona ni mweupe hivi sasa mnajiunga ktk mitandao ya kijamii kuonyesha ulofa wenu au mnatafuta kitu gani JF?
 
Kwani kazi ya wanasheria wa wizara ya nishati na madini ni ipi?na kazi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni ipi?ni kazi kubwa kumshauri mtu asiye kua tayari kushauliwa.maana na kama ni mikataba ya madini imo ofisini mwa pr muhongo .
 
Mkuu soma hii thread uelewe. Ni funzo hata kwetu tunaoshinda kwenye mitandao kumponda au kumtetea JPM kwenye hili suala bila uelewa. Tusome tujifunze; ku attack mtu badala ya hoja imeshaonyesha haitusaidii kamwe mkuu.
Ni kweli mkuu, baadhi ya watu hawaangalii tena hoja, wanaangalia nani kaandika wanaanza kupambana naye badala ya kupambana na hoja kwa hoja. Inasikitisha sana.
 
Mh Tundu Lissu, keep your mouth shut. You are wasting your time. Tangu lini hilo kundi la akina haambiliki linasikiliza ushauri kutoka kwako na wale wenzako? Hukumbuki wakati ule mikataba hii inasainiwa wewe na wenzako mlipokuwa mnapigia kelele kuhusu mikataba hiyo mibovu mliambiwa wachochezi, na tena wakaambia watanzania kwamba mna lengo la kuleta vita???? shut up your mouth already....waache waliolikoroga walinywe wenyewe.
 
wewe ukituliza ubongounaweza hata mshauli rais.
ila kwa domo lako bovu lisilo na staha ,hata mimi diwezi kukusikiliza hata uje na point.
we msomi uchwars ebu toa udhauri kwa staha.
we unafikiri kuongea ovyo ndio kiki?
 
Tangu lini wewe ukapingana na lissu???

Napingana na Lissu pale anapokosea,ameeleza vizuri tu na sioni shida kama mawazo yake yakafanyiwa kazi.

Sina ubaguzi wa Kiitikadi aliyekuwa kwenye haki nampa haki yake.
 
Back
Top Bottom