Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hawezi kuboresha afya, elimu na huduma za jamii sababu familia yake inaishi Ubelgiji

Ndugu zangu,

''Ukweli mchungu'', hata ukimsikiliza Tundu Lissu yeye anazungumzia ''mikataba'' ''sheria'' huku waziwazi akipuuza uboreshwaji wa elimu, afya, huduma za jamii na miundombinu ya msingi. Hii si bahati mbaya, familia yake inapata huduma za afya, elimu na malazi kutoka Ubelgiji.

Leo hata huduma ya kisheria anatumia za mawakili waliopo Ulaya ni dhahiri Lissu hana mpango na Watanzania. Na hata baada ya uchaguzi atatokomea huko huko kuganga njaa.

Tutafakari kwa makini, hoja kwa hoja.
MATAGA bhana, ni dhambi kuishi Ulaya?
Hao familia zao zinazoishi hapa wamefanya nini?
Lissu alipotua uwanja ndege hata tv ya mwenyekiti wa ccm hapo ushetu ulikosa kuangalia?
Uzalendo ni kuishi nyumbani? Hao wzungu wanaoishi masaki na oysterbay, shanty town Moshi wao si wazalendo?
 
..kwanza, watoto wa TL wameondolewa nchini baada ya baba yao kunusurika kuuwawa.

..mnapaswa kujiuliza watoto hao walikuwa ktk hali gani kisaikolojia baada ya baba yao kupitia tukio kama lile.

..ukiacha watoto ambao wako nje, ndugu wengine wa TL wapo hapa Tanzani, kwa hiyo sioni kama mtoa mada ana hoja ya msingi.
 
Sasa Kama kapeleka kijijin kwake roho inakuuma Nini Kwan kule hakuna watu...
Dar ambayo kila kitu hupelekwa ina chann kikubwa !!?au watu wake ndo wanastahiri kuliko wa Lindi mtwara,chato na kwingineko... Au Kuna Sehem zinapaswa kuendelea kuliko nyingine
Akili huna
 
Narudia Lissu anadharau 'machineries' za nchi yetu Tanzania na anatudharau sisi Watanzania!
Acha wivu kama wewe uwezo na mwisho wako ni Kwa waganga wa Gambosi usidhani na wenzio ndiyo upeo wao waache wenzio wakate mawimbi, mmempiga risasi Mungu kamponya hujaridhika bado unataka alindwe na waliompiga ili mpate second chance wewe na genge lako bure kabisa.
 
Acha wivu...
Acha mkumbo na utulizine. Fikiria mustakabali chanya wa ustawi wako, wa wanaokuzunguka, wa watanzania na wa waafrika wote kwa ujumla. Mweleza Lissu aweke wazi makubaliano yote aliyofanya na watu, mashirika, ama entity yoyote ya hapa nchini na hata nchi za ng'ambo. Akifanya hivyo, fuatilia kwa makini makubaliano hayo uone kama yanabeba mustakabli chanya wa ustawi kwako,jamaa zako, watanzania na waafrika. Baada ya hapo fanya maamuzi sahihi.
===
Ha ha ha aa! mkuu hakuna namna, ni mwendo wa 'bampa' to 'bamba'.
 
Back
Top Bottom