Libya
JF-Expert Member
- Nov 11, 2016
- 783
- 1,918
===========
Tundu Lissu amewataka wanachama wasishangilie sana kwani wanatarajia mapingamizi hivyo wasubiri kesho mpaka saa kumi kuona hali itavyokuwa.
Tundu Lissu: Sio wao peke yako wanaojua kuandika mapingamizi na sisi tunajua hivyo usiku huu nitaangalia kitu gani tunacho ambacho tunaweza tukafanya ambacho sheria za uchaguzi zinaturuhusu, na sisi tunaweza tukaweka mapingamizi.
Kama kuna mtu anafikiria sisi tutakuwa wajibu mashtaka tu, wafikirie mara mbili. Mwisho nawaombeni, kesho ni siku muhimu kuliko leo. Kwa sisi tusiokuwa na serikali, mapolisi, tusiokuwa na watu wa kutulinda, tunahitaji nguvu ya umma, tunahitaji wingi wenu.
Nawaombeni sana mhamasishane mji huu na miji ya jirani na yeyote anayeweza kuwa Dodoma awe Dodoma ili kesho tuwe wengi zaidi tuone mpaka kufikia saa kumi jioni itakuwaje.