Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba amshukia vikali Tundu Lissu, ahoji kuweka pingamizi kwa wagombea wawili ilhali wote wamefata maelekezo ya Tume

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Mgombea Urais wa CUF, Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lissu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera, Amani, Maendeleo na Demokrasia ya Nchi yetu.

Prof. Lipumba amehoji sababu za Lissu kumuwekea pingamizi kwenye tume ya uchaguzi eti kisa tu amefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi!! Lipumba amehoji asipofuata maelekezo ya tume ya uchaguzi afuate maelekezo ya nani?? Pia amehoji wagombea wote wa urais mwaka huu wamefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi akiwemo Membe, iweje awawekee pingamizi wagombea wawili tu?

Hali hiyo imemsikitisha sana Lipumba na kuwaasa watanzania kutokumchagua Lissu kwani ameonyesha udikteta wa kuminya demokrasia mapema sana.

Mwenyekiti wa chama Cha wananchi (CUF) ambae pia ni mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof Ibrahim Lipumba amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisipewe madaraka kwani hakina sifa ya wanakuongoza nchi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama icho ikiwa ni siku moja baada ya kuona taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Tundu Lissu kumuekea pingamizi kwa Tume ya uchaguzi (NEC) la kumtaka asigombee kwa kile kichodaiwa amefuata malekezo ya tume hiyo na tume kulitupilia mbali pingamizi hilo.

Amesema kuwa, chama Cha CHADEMA kinapaswa kijitafakari kwa Mgombea waliemsimamisha inawezekana baada ya kupata ajali amepoteza matatizo ya akili kwani hoja alizozitoa tume ya uchaguzi dhidi yake hazina mashiko.

“Sisi tunasimama kusimamia Demokrasia lakini Cha ajabu CHADEMA kinaniwekea pingamizi, hii ni dhahiri hoja zangu hawaziwezi kwa nini waniekee pingamizi mimi”amesema Prof Lipumba.

Ameongeza kuwa”Kama CHADEMA wapo vizuri katika uchaguzi mkuu basi washindane kwa hoja na sio kuweka pingamizi zisizo na maana kwani hii haijengi demokrasia ya kweli”amesema

Hata hivyo amesema kuwa, Tundu Lissu amekufa kisiasa hivyo anatafuta sababu ya kiki ili aanze upya katika ulimwengu wa siasa,anaona njia inayofaa ni kuleta taharuki kwa wanachama wa CUF.

Aidha amesema kuwa tume ya uchaguzi ilifanya kazi yake vizuri kwa kuvishirikisha vyama vya siasa kwa kuwaita viongozi wa kwavyama ajili ya kuwapa elimu, na kujadili maadili ya uchaguzi, kutokana na Tundu lissu kutokuepo nchini ndio maana haelewi yanayoendelea Tanzania.

“Naweza kusema Tundu Lissu amekurupuka tu kwani wakati tunapewa semina yeye hakuepo hata hao CHADEMA hawakumshauri ndio maana ameanza kuongea ovyo au baada ya kuumia ndio anatafuta huruma kwa wananchi”amesema


DarMpya.com

 
Mgombea urais wa Cuf ,Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lisu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera ,amani , maendeleo na democrasia ya nchi yetu...

Yale yale ya 2015 kwa kumuita Mhe Lowassa fisadi halafu kakimbilia Rwanda kutaliiiii! CUF, ACT Wazalendo, TLP, NCCR, ADC, CHAUMA, UPD, TADEA, hawapati mbunge hata mmoja Tanzania Bara na Chadema hawapati mbunge hata mmoja Tanzania Visiwani!! Act Wazalendo watapata wabunge wanne tu Visiwani! Procrastination. hiyo.
 
Lisu amefanya makosa sana, kitendo tu cha kumtaja Lipumba kimefanya watu wajue kuwa hata Lipumba anagombea urais.
Kumbe ulikuwa unaona ni sawa watu kutokujua kuwa hadi Lipumba nae anagombea urais ila hauoni sawa vyombo vya habari vinavyompotezea Lissu!
 
Mgombea urais wa Cuf ,Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lisu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera ,amani , maendeleo na democrasia ya nchi yetu...
Profesa Lipumbaaaa katika ubora wake
 
Mbona Lissu alisema wazi kuna wengine kaamua kutowawekea mapingamizi?
Kwanini hakuweka kama wote walifanya kosa moja. Nyie jamaa Lisu wenu kawashikia akili yaani you are not using your brain kabisa
Mahaba yanawafanya mnakuwa fools. jamaa kakosea kuweka mapingamizi ambayo actually hayana mantiki
 
Kumbe ulikuwa unaona ni sawa watu kutokujua kuwa hadi Lipumba nae anagombea urais ila hauoni sawa vyombo vya habari vinavyompotezea Lissu!

Lissu ni kama moto, hata usipouona utasikia harufu yake. Huyo Lisu hata asipotangazwa na chombo chochote cha habari humu nchini, bado habari zake watu watazitafuta.

Mpaka sasa Tundu Lisu hapewi covarage na vyombo rasmi vya habari, na hata akipewa ni zile negative, lakini ndio mwenye mvuto automatically kwa watu.

Huo ndio ukweli usiopingika. Huyo Lipumba acha tu kupewa covarage na vyombo vya habari, hata awe mtangazaji kwenye media zote au mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hana mvuto tena.
 
Back
Top Bottom