Tundu Lissu ashinda Urais wa Chama cha wanasheria nchini (TLS) kwa kupata 88% ya kura

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
--Kwa Ufupi--

Wakili msomi Mhe. Tundu Lissu ameshinda Urais wa Chama cha wanasheria nchini (TLS) kwa kupata kura 1,411 kati ya kura 1,682 zilizopigwa, sawa na ushindi wa 88% ya kura zote.

Katika mawasiliano na Lissu amethibitisha ushindi huo na kusema kwa kifupi "Nimeshinda Urais TLS, ushindi huu uende kwa watanzania wote, na kwa wote mlioonewa ambao mpo mahabusu na magerezani".

President: Tundu Lissu.
Vice President: Godwin Ngwilimi
HT: Magai

List of Council Members.
1. Jeremiah Mtobesya
2. Gida Lambaji
3. Hussein Mtembwa
4. Aisha Sinda
5. Steven Axweso
6. David Shilatu
7. Daniel Bushele.

-----Jinsi zoezi zima la Uchaguzi wa TLS lilivyokuwa-----
Ni asubuhi iliyo njema kabisa ndani ya Jiji la Arusha Mjini hali ya utuvuli na amani imetawala ambapo siku ya leo mawakili wasomi wataandika historia mpya kwa kuchagua viongozi wapya wa Tanganyika Law Society (TLS )

Jana baada wagombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Tanganyika Law Society kujieleza na kuomba kura. Zoezi la kupiga litafanyika siku ya leo Jumamosi kuanzia majira ya Saa 06.00 hadi saa tatu baada ya hapo zoezi la kupiga kura kukamilika matokeo ya uchaguzi yatatangazwa rasmi.

Wagombea nafasi ya Uraisi wa TLS
1. VICTORIA MANDARI
2. FRANCIS STOLLA
3. LAU KEGO MASHA ambaye amejitoa jana kumsapoti Tundu Lissu.
4. GODWIN MWAPONGO
5. TUNDU LISSU

Tuwe pamoja kuwaletea yote yanayojiri kutoka ukumbini Arusha International Conference Centre (AICC).

==========

--UPDATES--

Mawakili wameshaanza kuwasili ukumbini. Baada ya mawakili wote kuwasili ukumbini kura zitapigwa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu asubuhi.

Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi wa AICC ukaguzi mkubwa sana unafanyika huwezi kuingia kama huna kitambulisho bado mawakili wanaingia kwa ajili ya zoezi la kupiga kura.

Zoezi la kupiga kura bado linaendea mawakili wanaendelea kupiga kura za kumchagua Raisi wa Tanganyika Law Society. (TLS) . Linatarajiwa kumalizika Saa 4:00 asubuhi leo.

Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika mchakato wa kuanza kuhesabu kura unaanza.
Zoezi la kupiga kura limeshaanza kumalizika.

Kupiga kura kumemalizika sasa hivi ni zoezi na kuhesabu kura linaendelea mpaka saa nane mchana mshindi atatangazwa.

Mawakala wakiwa wamebeba kura kuzipeleka sehemu maalumu ya kuhesabu.

Uchaguzi wa TLS kwasasa umefikia hatua ya tatu ya kuhesabia kura!

Tayari mawakala wameingia ndani ya vyumba vya kuhesabia kura. Vyumba hivi ni vinne cha kwanza ni cha uraisi, makamu wa Raisi, mhasibu na wajumbe wa baraza.

Mawakala: Uraisi Wakili msomi Kaunda na makamu wa raisi ni John Malya.

Inategemewa mpaka saa nane matokeo yatakuwa tayari!

Mawakili wamerudi ndani ya ukumbi wa Simba Hall AICC tayari kusubiria matokeo
Bado muda mfupi matokeo yatatolewa yote.

*Nafasi ya Makamu wa Raisi wa TLS Godwin Mwapongo ameshinda.
*Nafasi ya urais Tundu Lissu ameshinda kwa asilimia 88.


Zoezi la upigaji kura TLS limeanza tangu Saa 1:00 asubuhi na linatarajiwa kumalizika Saa 4:00 asubuhi ya leo.
 
Naskia Jecha Salum Jecha alifika usiku jijini Arusha na ndege ya kukodi!

Mi nilikuwa siifahamu kabisa TLS kabla ya Tundu Lissu, leo hii usiku wa manane naifuatilia TLS. Lissu akishinda uraisi wa TLS ajiandae kwa vita kubwa 2020, watanzania tumuweke pale juu agombee uraisi dhidi ya asiyejaribiwa. Itakuwa ni kati ya asiyeshindwa na asiyejaribiwa. Patamu hapo
 
tmp_18850-IMG-20170318-WA0030-47762517.jpg

Mhe Tundu Antiphas Lissu akiwa mke wake Wakili Alicia Lissu baada ya kuwasili ukumbini AICC Jijini Arusha kushiriki kwenye uchaguzi wa Uraisi Tanganyika Law Society.
 
Back
Top Bottom