Tundu Lissu apinga uamuzi wa Spika kuwataka Wabunge watoro kurejesha posho na kutolipwa mshahara

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,274

===
Kufuataia sakata la Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Ndugai kuwataka Wabunge watoro wa vikao vya Bunge kurejesha posho na kutolipwa mishahara yao Mh. Tundu Lissu atoa neno lake.


Lissu ameanza kwa kuhoji kuwa je Wabunge hao wa Chadema wanaotakiwa kurejesha hizo pesa waliomba fomu za malipo hayo wanayodaiwa?

Aisha, Lissu anaeleza Wabunge wa Chadema wamemweleza kuwa wao hawakuomba fomu za kuingiziwa malipo ya posho bungeni isipokuwa baada ya uongozi wa Bunge kusikia rai ya Wabunge wa Chadema kutokuingia Bungeni wakapeleka pesa kwenye akaunti zao. Katika hili lisu anahoji je ni wizi wa aina gani?

Aidha, jambo la pili Lissu amesema "kama wabunge hao wangekuwa wamejaza hizo fomu na pesa zikalipwa kwenye akaunti zao likatokea janga, ikatokea dharura kama hii, kuna wabunge watatu wamekufa, wabunge wengine wapo hospitali au wametengwa wanaumwa Corona au kuna Corona Bungeni; Kama kuna dharura ya aina hii, Wabunge wakasema hatuendi kwenye vikao kwa sababu tunaogopa kuambukiza au kuambukizwa Corona tunataka tupimwe kwanza".

Lissu anahoji, “Hii habari ya wizi inatoka wapi? Inaanzia wapi kwa Mbunge anayesema kwamba mimi nataka nipimwe nionekane kama niko salama na nataka wenzangu wapimwe waonekane kama wapo salama ili tusiambukizane haya maafa ambayo kila mtu anakubali yanaua. Hii habari ya wabunge kuitwa wezi ni ya kijinga, hakuna Mbunge aliyeiba pesa, hakuna Mbunge mtoro”

Tatu, Lissu amesema kuwa “Spika amesema kwamba hawatalipwa mshahara kwa sababu ni wezi au kwa sababu wamechukua pesa za vikao na wamekimbia bunge hawatalipwa mshahara wa mwezi huu.” Naomba twende kwenye sharia za Tanzania, kwenye sharia za nchi yetu, utaratibu wa malipo ya mishahara ya Wabunge upo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na vilevile upo kwenye sheia za uendeshaji wa bunge na tatu upo katika kanuni za kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anaongeza kuwa “Sheria ya haki, kinga na madaraka ya bunge inazunguzia masuala mengine ya haki za wabunge, haizungumzii mishahara yao”. “Kwahiyo, tukitaka kuijua haki za malipo ya pesa za Wabunge tunaangalia kwenye Katiba, Tunaangalia kwenye sharia ya uendeshaji wa bunge tunaangalia kwenye kanuni za kudumu za uendeshaji wa Bunge. Hivyo, msimamo wa kisheria ni kwamba haki, mshahara na posho za kibunge unalipwa kwa mbunge yeyote yule ilimradi ni Mbunge”.

“Sasa kwenye kanuni za kudumu za Bunge kuna mazingira ambayo Mbunge anaweza akakatwa mshahara na posho zake za kibunge, Kanuni za kibunge zimeweka uwezekano huo; Na kanuni hizo zinasema Mbunge atakatwa nusu ya mshahara wake na nusu ya posho za kibunge endapo tu atasimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kama adhabu iliyotolewa na Bunge kwa kosa alilolifanya ndani ya vikao vya Bunge”.

Wabunge wetu wengi mmeshuhudia katika miaka ya hivi karibuni wamesimamishwa kuhudhuria vikao, Wote ambao wameadhibiwa namna hii wamekuwa wakikatwa nusu ya mshahara na posho za kibunge kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge, hayo ndiyo mazingira pekee ambayo Mbunge wa Tanzania anaweza asilipwe mshahara na posho zake za kibunge na sio kwamba halipwi kabisa, analipwa nusu ya mshahara na posho zake za kubunge” Lakini inakuwa hivyo endapo tu mbunge huyo amepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vya bunge”

“Sasa hiki kinachosemwa kuwa hawatalipwa kwasbabu ya utoro, kwa sababu ya kitu kinachoitwa wizi sijui hizi ni hoja za kijinga. Na kama kuna maamuzi yanafanyika ya kutokuwalipa mishahara yao kwa sababu ya hoja hizi za kijinga yatakuwa ni maamuzi ya kijinga, yatakuwa ni maamuzi ya kinyume cha sharia, yatakuwa ni maamuzi yale yale ambayo tumeyazoea katika bunge la Spika Ndugai na katika Tanzania ya Magufuli”.

“Bunge lisilozingatia sheria, Serikali isiyozingatia sharia, Bunge lisilojali kanuni za kudumu za bunge na Serikali isiyojali katiba wala sharia za nchi” Kwahiyo kama wanazuiliwa mishahara, sio kwa sababu wametenda kosa lolote la kuzuiliwa mishahara ila kwa sababu tunaishi katika Serikali ambayo haijali katiba wala sharia za nchi na bunge linaendeshwa na Spika maybe alishasahau kabisa kwamba kuna kanuni za kudumu za bunge zinazopaswa kumuongoza”

“Tuna Bunge ambalo spika wake anapokea maagizo ya wazi wazi ya kutoka kwa Raisi wa Jamhuri wa Muungano na ni Rais Magufuli aliyesemwa wasilipwe. Kwa hiyo kama hawalipwi sio kwa sababu wamekosa, ni kwa sababu kuna mtu nje ya Bunge ndiye anayeongoza bune wakati aliye ndajni ya Bunge anakaa kwenye kiti cha ni mpokea maagizo na shuruti kuoka nje, kwa maana nyingine ni kibaraka wa hao wanaomuongoza”

Aidha kuhusu suala la Wabunge hao kuripoti kituo cha polisi Lisu amesisitiza kuwa hoja hizo ni za kijinga, Amesema kuwa “Kama tutakuwa na jeshi la polisi la namna hii tutakuwa na jeshi ambalo limesahau wajibu wake wa kulinda sharia za nchi.

Lisu anahitimisha kwa kusistiza kuwa katika yote yaliyofanyika hakuna kosa la wizi, utoro au kusa la kwenda kituo cha polisi.

KUELEWA ZAIDI KUHUSU JAMBO HILI SOMA HAPA
- Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110 - JamiiForums
 
Msisahau wakati ule Zitto alivyofukuzwa Chadema aliendelea kukaa bungeni. Acheni double standards Sky Eclat
Mkuu kawadanganye ukoo wenu, zitto alikwenda kuweka court injection ya kuzuiwa kuvuliwa uwanachama mpaka shauri lilipokwisha mahakamani, hatukuona spika Wa bunge Anne makinda akimkingia kifua Zitto, kama anavyofanya spika Ndugai.
 
Mkuu kawadanganye ukoo wenu, zitto alikwenda kuweka court injection ya kuzuiwa kuvuliwa uwanachama mpaka shauri lilipokwisha mahakamani, hatukuona spika Wa bunge Anne makinda akimkingia kifua zitto, kama anavyofanya spika ndugai.
Spika anadai hana taarifa, it’s their word against his. Wakati wa lala salama lazima uvumilivu utumike
 
Boris alileta story za herd immunity maara paap kalazwa mwenyewe ICU kwa Corona mpk Leo haongelei tena mambo ya Herd Immunity an BL

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Unadhani nchi zinazoanza kulegeza masharti ya lockdown wakati idadi ya wanaombukizwa ikiongezeka wanalenga nini!?

Ukumbuke haijapatikana chanjo na tiba wanazoziamini kwenye nchi hizo. Binafsi nadhani wanalenga herd immunity tu!
 
Back
Top Bottom