Tundu Lissu akishinda urais, mikopo na hasa misaada, itaongezeka kutoka kwa Wahisani wa Maendeleo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,035
144,388
Huu ndio utabiri wangu kuwa,Lissu akishinda uraisi na kutangazwa mshindi kwa mbinde au vinginevyo, nchi wahisani na wadau wengine wa maendeleo wataongeza misaada na mikopo yao kwa nchi yetu na inaweza kuongezeka hata mara mbili.

Ni imani yangu wanatoa mikopo na misaada kwa sasa kwasababu tu wanaamini wana wajibu huo kibinadamu ila hawapendezwi na mambo yanayoendelea hivi sasa hapa nchini kama vile uminyaji wa demokrasia, uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari , utekaji, mauji,unyanyasaji wa wapinzani,n.k.

Misaada na mikopo itatolewa kwa haraka zaidi kuliko ilivyo sasa na mingi itatolewa kwa asilimia mia moja kulingana na ahadi zitazotolewa

Kama nchi inaahidi kutoa dola milioni moja ndani ya mwaka fulani wa fedha,mpaka mwaka husika unaishi ,watakuwa wametoa kiasi chote walichoahidi tofauti na ilivyo sasa kwa baadhi ya ahadi za wahisani kutotimizwa ahadi zao kwa asilimia mia moja

Ukweli mchungu ni kuwa, siku tukiondokana na huu utawala,watakuwa na moyo wa kutoa zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.

Kingine ni Lissu kupokea mialiko mingi ya kiserikali ya kutembelea nchi nyingi za Ulaya na Marekani.

Time will tell.
 
Sasa yule kichaa nani anampa nchi na wewe embu kuwa serious

Si bora hata apewe mnyika mara 1000
 
Huyo ni wakala wa CIA, hatuwezi kuuza nchi, amekimbilia kwa bwana zake na ndio wanamfadhili kuishi ulaya
 
Back
Top Bottom