Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,514
- 122,879
Unakumbuka chopa 5 kata 3?
Unaweza kuniambia nini kilitokea mpaka usemi huo ukatokea?
Hivi kwanini tunajidanganya hata nafsi zetu?
Lisu hapati zaidi ya 20% ya kura.
Achilia mbali wabunge ambao mkifikisha 15 mshukuru Mungu
Kwani wakati huo wa chips tatu kata tatu tume ilikuwa huru? Kwanza unakumbuka ratio ya kura za wakati ule? Na unajua kipi kilitokea uchaguzi wa 2015? Inaonekana hujui siasa ndio maana unaangalia aliyetangazwa mshindi tu, bila kupima ushindi ulikuwa wa marafiki kiasi gani.
Ngoja nikupe mfano mrahisi wa mpira. Kabla ya Liverpool kuchukua ubingwa msimu huu, msimu uliopita walishindwa na Manchester City kwa point moja. Ila walianza msimu huu kwa nguvu ile ile hadi kuwa bingwa, huku wakiwaacha Mancity kwa zaidi ya point15+. Lazima ujue kusoma alama za nyakati, hiyo mifano yako ya zamani haina nafasi kwa sasa maana mazingira sio static na kuna mambo mengi sana yamebadilika. Kama wapinzani wamefanyiwa hujuma zote ndani ya hii miaka mitano na bado kwa sasa wana hamasa, utakuwa mwendawazimu kujisifia huku mifumo yote ya uchaguzi ikikubeba bila sababu za msingi.
Kutokana na hujuma dhidi ya cdm ndani ya hii miaka mitano, na kile alichofanya Magufuli, na propaganda zote chafu dhidi ya Lisu achia mbali shambulio lake, ilitakiwa apate watu wa idadi ya mikutano ya Hashimu Rungwe, sio hicho kinachoendelea. Kama uchaguzi utafanyika kwa utashi wa Magufuli, Lisu hata hizo 20% hafikishi, na wabunge au madiwani hata kufikia watano itakuwa maajabu. Ila sio kwa uchaguzi kwa maana ya kura halali.