Tundu 'Frankenstein' Lissu

Tundu 'Frankenstein' Lissu

Objectively speaking, Lissu ni presidential candidate mzuri sana.

Ana uwezo mkubwa wa kuelezea changamoto zinazowakabili watu.

Lakini bado sioni ni jinsi gani anaweza kukivuka kizingiti cha tume ya uchaguzi isiyo huru....
Kuna jambo ninaliona kwenye kona ya kipekee sana. Kina sehemu mbaya sana Tume itaenda kubanwa na endapo ikitokea tu watu wakakubaliana na Lissu Tume itamnawa Jiwe
 
Nyani Ngabu,

..hata wasingempiga risasi, bado TL angewapa shida.

..ukweli ni kwamba, he is more talented, knowledgeable, and informed, than Jpm.

..TL akizungumza akiwa ametulia unaona kwamba there is potential to be tapped.

..anachokosa TL ni wasaidizi na washauri wa kumpiga msasa.
 
Ana uwezo mkubwa wa kuelezea changamoto zinazowakabili watu
Nadhani unampaka Lissu mafuta kwa mgogo wa chupa!!! Anaelezea changamoto zipi...hizi alizowaambia watanzania wanaoishi Kilimanjaro kuwa siku hizi hawana madaraka, ila akiwa rais atarudisha madaraka kwa wananchi kama ilivyokuwa enzi za mkoloni!? Nyani Ngabu, angalia hiyo chupa unayotumia kumpaka mafuta ni ya kioo na imepasuaka, Utamchana Lissu ngozi iwe kesi!!!
 
Zile kamata kamata zisizo na kichwa wala miguu dhidi ya Tundu Lissu na zile kesi uchwara zote zilizofunguliwa dhidi yake naamini ndizo zilizompandisha chati huyo bwana katika huu utawala wa awamu ya tano.

Mara nyingi kama si zote hizo kamata kamata zilitokea baada ya yeye kutoa maneno makali dhidi ya serikali na Rais.

Kuna nyakati alikuwa yupo sahihi na nyakati zingine alikuwa mzushi tu. Kwa mfano, aliposema nchi inaendeshwa kwa misingi ya kikabila na kikanda, huo ulikuwa ni uzushi tu. Zilikuwa ni propaganda tu.

Uzushi na propaganda kwenye siasa ni jambo la kawaida sana na la kutegemewa kuwepo. Mwanasiasa asiyezusha, asiyetia chumvi na asiyepiga propaganda atakuwa kakosea fani.

Sasa mimi naamini hii serikali inafanya makosa sana katika kuwakamata na kuwafungulia mashitaka watu wanaoipinga na kuikosoa. Hizo kesi wanazofunguliwa ni vichekesho mtupu.

Katika kukosea kwao huko, naamini serikali imeunda lidubwana [monster] ambalo kuanzia sasa kwenda mbele itakuwa vigumu kulidhibiti. Lidubwana hili nalifananisha na lile lidubwana la kwenye filamu ya Frankenstein.

Lidubwana hilo ndo Tundu Lissu. Hebu fikiria haya:

Jamaa keshaonyesha kuwa haogopi kuikosoa serikali wala kumsema vibaya Rais [mambo ambayo ni ya kawaida sana kwenye demokrasia na ambayo yanahimizwa kufanyika].

Uthubutu na ujasiri wake huo ndio umepelekea yeye kukamatwa kamatwa na kufunguliwa vikesi uchwara.

Uthubutu na ujasiri huo huo ndo si ajabu umepelekea yeye kushambuliwa kwa risasi kwa lengo la kutaka kumuua. Sijui kwa uhakika ni nani anayehusika na hilo shambulio.

Sasa pata picha atapopona na kurejea tena nchini na kuendelea na harakati zake pale alipoishia!

Serikali itamfanya nini huyu mtu? Wataendelea kumsumbua na hizo kamata kamata zao na kumfungulia hivyo vi kesi uchwara mtu ambaye tayari ana huruma za umma kwa ujumla wake kutokana na yale yaliyomtokea?

Sioni utamkamataje na kumfunga mtu ambaye kanusurika kuuwawa namna ile. Akili yangu inaniambia hata dhamiri yako, kama ni safi, basi itakusuta tu.

Hakika hii serikali ya awamu ya tano ilibugi stepu katika namna ya kumkabili Lissu na sasa amekuwa lidubwana ambaye anaweza asidhibitike tena.

Ni muda tu ndo utaotueleza.....
Binafsi namkubali magufuri kwa kuboresha miundombinu, barabara ya kwenda kwetu kakonko-kasulu km 180 ipo kwenye ujenzi. Hivyo nimetangaza mara kadhaa kura yangu ni magufuri na familia yangu na wale wanaonitegemea nawashawishi wampigie kura JPM.

Lakini nikitafakari
1. Umuhimu wa katiba mpya
2. Lisu anavyo nyanyaswa kila kona. Kuna mahali ma dc wamejaribu kumpiga mawe, serngeti akazuiwa kupita maeneo muhimu, ukerewe kivuko kikaondoshwa wkt zilibaki dk 15 tu na nafasi zilikuwepo.
3. Kuzuiwa kufanya kampeni na tume
4. Wagombea wa upinzani kuengeliwa huku wa ccm wote wamepitishwa.
5. Kesi za kijinga alizo funguliwa
6. Maofisa wa polisi kuonesha u ccm wao(Shana-r.i.h, Kigondo, ocd hai, na wote walioleta figisu za kijinga

Frankly, natamani nimchague Lissu asaidie kuweka misingi ya democracy nchini. Hawa ma Rc, DC, ded wanakaa na kupanga kuipitisha ccm, nachukizwa sana. Mambo haya hayana budi kukomeshwa.

Lkn jpm namkubali. Nina utata hakika

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kwa nini hizo kura zisihesabiwe hadharani?
Kanuni ya tume haisemi hivyo.

Ni kweli ccm inabana vyama pinzani kitu ambacho hata chadema wangefanya hivyo hivyo lakini Lisu hana kura za kumfanya awe rais
 
Nyani Ngabu,

..hata wasingempiga risasi, bado TL angewapa shida.

..ukweli ni kwamba, he is more talented, knowledgeable, and informed, than Jpm.

..TL akizungumza akiwa ametulia unaona kwamba there is potential to be tapped.

..anachokosa TL ni wasaidizi na washauri wa kumpiga msasa.
Ni kweli.

Ila pia ku survive risasi 16 [au ni 32?] kumemuweka kwenye level ya kipekee.
 
Kanuni ya tume haisemi hivyo.

Ni kweli ccm inabana vyama pinzani kitu ambacho hata chadema wangefanya hivyo hivyo lakini Lisu hana kura za kumfanya awe rais
Hajasema hajui kanuni za tume hazisemi ivo!! Swali kama mnajiamini basi kura zihesabiwe hadharani
 
Kaishia kuwa mpiga ramli tu saivi. Yote aliyowai kuyasema humu yamekuwa ndivyo sivyo alafu anadai watu tumuamini Eti Lissu hawezi shinda!!! Huyu kilaza kachanganyikiwa mbaya. Lissu amemfanya arukwe na akili
Mkuu kuniita mimi kilaza hakuondoi ukweli kwamba Lisu hata pata hata 20% ya kura zote!

Baada ya oktoba hii tutarudi hapa. Mungu atupe uhai
 
Hajasema hajui kanuni za tume hazisemi ivo!! Swali kama mnajiamini basi kura zihesabiwe hadharani
Ili kumridhisha Lisu kama kashindwa kihalali?

Siku nyingine si atakuja aseme kura zikahesabiwe nyumbani kwake?
 
Dah!

CCM nadhani mna majuto mengi sana!

Maana mmeumba dubwana [sisemi hivyo kwa ubaya] ambalo halidhibitiki tena.

Sasa hivi hata kumkamata na kumfungulia vi kesi uchwara hamuwezi tena.

Tangu uolewe huko umekuwa boga haswaa
 
Acha visingizio.

..binafsi nasikitishwa sana na utendaji wa tume.

..kuna vikwazo vingi sana kwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi.

..nilitegemea Tume iwawezeshe na iwe msaada na siyo kikwazo kwa wale wote wanaotafuta nafasi za uwakilishi.

..na kwa bahati mbaya vikwazo na vihunzi hivyo vinawaathiri wapinzani, huku wana-ccm wakipeta.

..kupitishwa na tume kugombea ni shida. kampeni ni shida. kupiga na kuhesabu kura pia ni shida.
 
Back
Top Bottom