Tundu 'Frankenstein' Lissu

Tundu 'Frankenstein' Lissu

K
Kweli kabisa mkuu,Ndugai hastahili heshima yoyote.
Uliona wapi spika akaramba miguu ya Rais hapa duniani.
Huyu Ni spika wa hovyo kabisa hapa duniani halafu fisadi.
Nimeona Tanzania spika alipokuwa Job Ndugai mzee wa kujipendekeza kwa Rais
 
Ni kweli kabisa sometime watuulize hata wengine namna ya kumsoften mpinzani wako pasipo madhara ya mwili wake ,uhai au kumpatia umaarufu.

Washukuru tu kuwa baada ya 2020 1. Atakuwa sio Rais wa nchi
2. Si mbunge wa jimbo au kuteuliwa
3. Sio rais wa TLS
Hivyo atapiga kelele huko uchochoroni tuuuuu No impact
Wakicheza vzr atakuwa kimya
 
Zile kamata kamata zisizo na kichwa wala miguu dhidi ya Tundu Lissu na zile kesi uchwara zote zilizofunguliwa dhidi yake naamini ndizo zilizompandisha chati huyo bwana katika huu utawala wa awamu ya tano.

Mara nyingi kama si zote hizo kamata kamata zilitokea baada ya yeye kutoa maneno makali dhidi ya serikali na rais.

Kuna nyakati alikuwa yupo sahihi na nyakati zingine alikuwa mzushi tu. Kwa mfano, aliposema nchi inaendeshwa kwa misingi ya kikabila na kikanda, huo ulikuwa ni uzushi tu. Zilikuwa ni propaganda tu.

Uzushi na propaganda kwenye siasa ni jambo la kawaida sana na la kutegemewa kuwepo. Mwanasiasa asiyezusha, asiyetia chumvi, na asiyepiga propaganda atakuwa kakosea fani.

Sasa mimi naamini hii serikali inafanya makosa sana katika kuwakamata na kuwafungulia mashitaka watu wanaoipinga na kuikosoa. Hizo kesi wanazofunguliwa ni vichekesho mtupu.

Katika kukosea kwao huko, naamini serikali imeunda lidubwana [monster] ambalo kuanzia sasa kwenda mbele itakuwa vigumu kulidhibiti. Lidubwana hili nalifananisha na lile lidubwana la kwenye filamu ya Frankenstein.

Lidubwana hilo ndo Tundu Lissu. Hebu fikiria haya:

Jamaa keshaonyesha kuwa haogopi kuikosoa serikali wala kumsema vibaya rais [mambo ambayo ni ya kawaida sana kwenye demokrasia na ambayo yanahimizwa kufanyika].

Uthubutu na ujasiri wake huo ndo umepelekea yeye kukamatwa kamatwa na kufunguliwa vi kesi uchwara.

Uthubutu na ujasiri huo huo ndo si ajabu umepelekea yeye kushambuliwa kwa risasi kwa lengo la kutaka kumuua. Sijui kwa uhakika ni nani anayehusika na hilo shambulio.

Sasa pata picha atapopona na kurejea tena nchini na kuendelea na harakati zake pale alipoishia!

Serikali itamfanya nini huyu mtu? Wataendelea kumsumbua na hizo kamata kamata zao na kumfungulia hivyo vi kesi uchwara mtu ambaye tayari ana huruma za umma kwa ujumla wake kutokana na yale yaliyomtokea?

Sioni utamkamataje na kumfunga mtu ambaye kanusurika kuuwawa namna ile. Akili yangu inaniambia hata dhamiri yako, kama ni safi, basi itakusuta tu.

Hakika hii serikali ya awamu ya tano ilibugi stepu katika namna ya kumkabili Lissu na sasa amekuwa lidubwana ambaye anaweza asidhibitike tena.

Ni muda tu ndo utaotueleza.....
Hatimaye muda ndio unaongea Sasa.
 
Hivi wewe unadhani kuwa kiongozi wa Juu ndio kuwa na busara? Hivi Ndugai Ana busara gani na nanhii naye Ana busara gani,anashinda mwaka mzima anaongea matusi tu jukwaani na mabarabarani.
Lissu anaongea ukweli mtupu.
Mtazoea tu,najua hamkuzoea.
Nilitegemea jibu kama hilo kwa kuwa niliamini, na ukathibitisha, kuwa unawakilisha kundi (lugha ya matusi) la wasiojua maana ya busara.
 
Tatizo hao unowaita viongozi wa juu, wewe unawachukulia kama miungu fulani inayotakiwa kutukuzwa.

Kwenye nchi zilizoendelea hao watu wanachukuliwa kama watumishi wa umma, hivyo wako subjected to demands of their people

Hayo uliyosema ni kweli. Je, ni sahihi kukebehi binadamu mwenzio, kwa mila za kiafrika? Au ndiyo itikadi ya chama chake? Je, akipata madaraka itakuaje?
 
Hayo uliyosema ni kweli. Je, ni sahihi kukebehi binadamu mwenzio, kwa mila za kiafrika? Au ndiyo itikadi ya chama chake? Je, akipata madaraka itakuaje?
Mchuma janga hula na wa kwao, hao ccm unaowatetea wangekuwa hawapendi kejeli wasingekuwa na utamaduni wa kuwakejeli wapinzani wao

Ila kwa kuwa wao wakiongozwa na mwenyekiti (Rais) huwa wanakejeli wenzao, acha na wao wakejeliwe.

Hili game gumu mwaka huu.
 
Daah watu wamefukua kaburi ila nyani uliona mbali, na kweli karejea na anaendeleza alipoishia, moto anauwasha kweli kweli

All in all Lissu ni mwanaume wa shoka, mwamba kweli kweli ni jasiri sana, sikutarajia kama angerejea Tanzania ya Magufuli isitoshe na ujasiri ule ule kama hakuna kilichomkuta uko nyuma

Kuna siku Lissu alikamatwa akapelekwa Central, kipindi hicho Lissu alikua na makesi kibao, wandishi wakamuliza Mkewe kuhusu misimamo ya Lissu kwamba ndio inam'cost, mkewe akajibu huyu ndio Lissu anayemfaham toka ujanani wao, akaendelea akasema siku Lissu akibadilika akapiga magoti kwa watawala yeye atakua wa kwanza kudai talaka, nilishangaa kauli ile ya mkewe
Hahahaha!!! Kumbe yule mama naye mwamba sana!
 
Kwanza kabisa huyo jamaa siyo wa kurudi leo wala kesho na hata akirudi kila kitu kwisha habari yake, kuna kiwango cha risaisi ambazo mwili wa Binadamu unaweza kuhimili, kupigwa risasi zote hizo siyo mchezo, huyo kwanza hata akifanya press conf. mtu akibamiza mlango tu kwa bahati mbaya atazimia atafikiri ni hitman wamemjia tena,

Kama ulishawahi kupigwa risasi au hata kukoswa tu unaweza kuelewa ninachomaanisha, hivyo ukiniuliza mimi huyo Tundu Lisu ndiyo basi tena its over, kwani sidhani hata kama ataweza kutembea tena, achilia bali hata tu kuinuka, atabakia jina tu kwa wafuasi wake kama vile Marando &Co., kwa kifupi they fvcked the guy up forever man, whoever shot him!
Mkuu Tundu Lissu anakusalimia sana, na anakutakia usiku mwema.
 
Mchuma janga hula na wa kwao, hao ccm unaowatetea wangekuwa hawapendi kejeli wasingekuwa na utamaduni wa kuwakejeli wapinzani wao

Ila kwa kuwa wao wakiongozwa na mwenyekiti (Rais) huwa wanakejeli wenzao, acha na wao wakejeliwe.

Hili game gumu mwaka huu.
Game la mwaka huu limeanzia mitandaoni na litaishia mitandaoni kama yalivyo mapenzi ya mitandaoni.

Nje ya mitandao hali ni tofauti kabisa. Nafasi finyu CHADEMA kilikuwa nayo kinachafuliwa na mteule wake wa Urais. Mikusanyiko ya watu (nyomi) imemwondoa kwenye busara za kiuongozi na kuwa mzee wa kijiweni wa MIPASHO. Anacheza ngoma ya Magufuli pasipo kujitambua
 
Dah!

CCM nadhani mna majuto mengi sana!

Maana mmeumba dubwana [sisemi hivyo kwa ubaya] ambalo halidhibitiki tena.

Sasa hivi hata kumkamata na kumfungulia vi kesi uchwara hamuwezi tena.

Mkuu, nakuhakikishia Lisu anajaribu kuchangamsha genge tu, kitu ambacho ni kizuri sana kwa afya ya democrasia

Lakini hawezi kupata zaidi ya 20%
 
Mkuu, nakuhakikishia Lisu anajaribu kuchangamsha genge tu, kitu ambacho ni kizuri sana kwa afya ya democrasia

Lakini hawezi kupata zaidi ya 20%
Hilo la kupata hata 20% sina uhakika nalo kwa sababu hatuna tume huru ya uchaguzi.

Hivyo ni vigumu kusema atapata kiasi gani cha kura.

Ila binafsi naamini kabisa kama uwanja wa mapambano ungekuwa uko sawa, basi Lissu angeshinda huu uchaguzi by a landslide.
 
Mkuu Ngabu!! Kwa ninavyoona uchaguzi uwe huru au usiwe huru Lissu anaenda kumshinda magufuli vibaya sana!! Sioni mtumishi wa umma kwenye sekta yeyote iwe vyombo vya ulinzi na usalama au taasisi za serikali ambayo consciousness yake itamwambia ambebe magufuli dhidi ya Lissu. Sijaona
 
Kipi Lisu kinamfanya amshinde Magu? Kuzunguka kwenye mitaa kadhaa hapa dar?
 
Objectively speaking, Lissu ni presidential candidate mzuri sana.

Ana uwezo mkubwa wa kuelezea changamoto zinazowakabili watu.

Lakini bado sioni ni jinsi gani anaweza kukivuka kizingiti cha tume ya uchaguzi isiyo huru....
 
Hilo la kupata hata 20% sina uhakika nalo kwa sababu hatuna tume huru ya uchaguzi.

Hivyo ni vigumu kusema atapata kiasi gani cha kura.

Ila binafsi naamini kabisa kama uwanja wa mapambano ungekuwa uko sawa, basi Lissu angeshinda huu uchaguzi by a landslide.
Mkuu, hata kura zihesabiwe hadharani Lisu hashindi!

Sijui mnaosema Lisu anashinda mnakuwa mko mitaa gani yani
 
Kipi Lisu kinamfanya amshinde Magu? Kuzunguka kwenye mitaa kadhaa hapa dar?
Lissu anapendwa, Lissu anakubalika. Akili yake, sera zake na maono yake juu ya a Tanzania si ya kawaida.
kubwa zaidi ni exposure yake anayoitumia kwenye mazingira yetu inamuweka mbali zaidi kwenye kukubalika dhidi ya wagombea wote!

Mbaya zaidi matendo ya Magufuli dhidi yake Lissu na Chama chake Lissu bila kusahau dhidi ya wafanyakazi, wakulima, vijana na wafanyabiashara inamfanya pia Lissu kuwa hazuiliki vyovyote vile!
 
Back
Top Bottom