Tunavyojiepusha na Matatizo Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunavyojiepusha na Matatizo Tanzania

Discussion in 'Great Thinkers' started by Kichuguu, Apr 14, 2012.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Viumbe wote hawataki matatizo. Hata wanyama wakali kama simba, hawataki matatizo katika maisha yao, ndiyo maana huchukua tahadhari sana wakati wakiwinda ili wasijejikuta katika matatizo ya namna yoyote.

  Kuna njia nyingi za kujiepusha na matatizo, zote zinaangukia katika makundi matatu kama ifuatavyo.

  (a) Njia zinazoepusha mazingira yanayokaribisha matatizo; kwa hiyo matatizo hayatokei kabisa

  (b) Njia zinazokabiliana na matatizo hayo ana kwa ana na kuhakikisha yanatoweka.

  (c) Njia zinazotuondoa kwenye mazingira yenye matatizo na kutupeleka kule ambako hakuna matatizo tukiyaacha matatizo ya awali apo hapo yalipo.


  Njia zote zina faida na hasara zake kama ifuatavyo:

  (1) Njia zinazoepusha mazingira ya matatizo zinatumia raslimali nyingi kwani zinatabiri uwezekano wa matatizo kutokea hata kama utabiri huo siyo kweli. kwa mfano inabidi mtu ajenge nyumba kwa kutumia nondo ghali ili kujiimarisha na matatizo yaletwayo na kimbunga hata kama hakutatokea kimbunga chochote kwa miaka mingisa sana. Faida zake kubwa ni kuwa njia hizo hutukinga kabisa na madhara ya matatizo hayo iwapo yakiibuka.

  (2) Njia za kukabiliana na matatizo ana kwa ana huwa pia zinatumia raslimali, na muda mwingi sana katika kukabiliana na matatizo hayo. Vile vile hakuna uhakika kama kweli kwa kutumia njia hii tunaweza kuyashinda matatizo yetu. Faida kubwa za njia hizi ni kuwa tukishakabiliana na tatizo na kulishinda, basi hata kama tatizo hilo litajirudia tena siku za mbeleni, halitakuwa na madhara kabisa kwa vile tutakuwa tunajua namna ya kulikabili.

  (3) Njia rahisi sana ya kutusalimisha na matatizo ni kuyakimbia yanapotokea. Kila yanapotokea basi sisi tunaondoka katika mazingira ya matatizo hayo na kwenda sehemu nyingine. Pamoja na kuwa njia hii haitumii raslimali nyingi, tatizo lake kubwa ni kuwa kuna matatizo mengine ambayo ni vigumu kuyakimbia. Na hata kama kuna sehemu nyingi za kukimbilia, kuna wakati tunakuwa hatuna pa kukimbilia tena.

  Je Tanzania tunatumia njia gani kukabiliana na matatizo yetu kama taifa?

  Nilipofuatilia ule mjadala kati ya Mkapa na wanazuoni wa Kigoda cha Nyerere pale mlimani kuhusu sera yake ya ubinafsishaji, na hoja zilizotolewa na Mkapa, ikanijia wazi kichwani kuwa Mkapa alikuwa anatumia hiyo njia ya tatu kukabiliana na matatizo ya mashirika ya umma. Badala ya kukabiliana na matatizo yale ana kwa ana na kujenga mazingira ya kuzuia matatizo hayo yasijirudie, yeye alikuwa anayakaimbia matatizo hayo kwa kuwasukumia watu wengine waliojulikana kama wawezekezaji.

  Leo hii Tanzania tuna matatizo ya urari wa mapato; badala ya serikali kukabiliana na tatizo hilo ana kwa ana kwa kuweka sera imara inayoihakikishia serikali mapao yake, sisi tunakimbilia pembeni na kuwaacha wafadhaili ndio wakabiliane na tatizo hilo.

  Je kwa nchi hii iliyojaa matatizo, tutaendelea kuyakimbia hadi lini? Inabidi tujifunze tena namna ya kukabiliana na matatizo hayo ana kwa ana na kuyashinda.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Du Mkuu hii ni mada inayohitaji thesis ya PhD.
  Sasa mimi nikiwa na njaa tatizo Hilo nitalikimbiaje?
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  kweli hutaweza kukimbia bali njaa yako utakabiliana nayo ana kwa ana kwa kupata msosi wa uhakika. Ndiyo maana inabidi wanasiasa wetu nao wajifunze namna ya kukabiliana na matatizo badala ya kuyakimbia na kuwasukumia wengine.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Heshima mbele Prof. Mwl Kichuguu...........Vipi kuhusu hybrid ya hizo njia tatu...........

  umenikumbusha mambo ya models za risks management...........

  Nimependa njia zako mbili za mwanzo kwani zina mtizamo wa ku-solve tatizo..............njia ya tatu kwa maoni yangu si nzuri kwani tuankimbia tatizo.......

  Fundamentally......kunapokuwepo na tatizo kunakuw ana mambo MAWILI ya kufanyika......either Ku-Manage tatizo or Kutafuta na Kutoa Solution juu ya tatizo husika..........

  Waziri Mkuu Pinda....anadai wamejaribu njia mbali mbali ili kukabiliana na mfumuko wa bei...na gharama za undeshaji serikali.......bila mafanikio!......na sasa serikali hina hali nzuri kifedha...........hivi hizi elimu tulizopata misingi yake ni ile ile au kuna elimu nyingine ni za kufikirika.........
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Umeandika sana lakini kwa ufupi ni kuwa hakuna mtu anayependa matatizo kwa namna yoyote ile. Matatizo yanakuja pale ambapo rasilimali hazitumiki vyema kukabili matatizo. Hapa tunaanzia na WATU. Wazungu nawasifu sana kwa kuepa na kukabili matatizo, japo mengine yapo nje ya uwezo wao.

  Lishe duni ni tatizo. Traffic jam ni tatizo. Mbu ni tatizo, n.k. Haya mambo yanatatulika na ndio maana wazungu wanaweza kukabiliana nayo. Sisi wabantu wenyewe ni tatizo. Sasa tatizo na tatizo vikikutana ni janga, na ndio tunayokumbana nayo daily.

  Kuna hii kitu inaitwa WHAT IF function. What if hunger, what if jam, what if torrents, what if drought, what if fuel scarcity, etc. Sasa wazungu ndio wanatuacha hapo. Hawa waasia miaka 50 iliyopita walikuwa sawa na sisi kiuchumi lakini leo kwa kutumia hii 'what if' wamefika mbali.

  Suala jingine ni kuhusiana na demand na capacity. How do we flex capacity when demand is high, and vice versa. Watu wanaongezeka lakini miundombinu ni ile ile kuanzia mabarabarani, mashuleni, vyuoni, mahospitalini, n.k. Naambiwa ukifika kwenye mabweni ya wanachuo hapo mlimani huwezi amini kinachoendelea humo ndani. Vyoo vimejaa na vinafurika vinyesi na wadudu. Mbaya zaidi ni vyoo vya kukaa. Haya ndio aina ya matatizo ya kujitakia. Chuo kina kila aina ya wasomi kuanzia wahandisi hadi wanasanaa. Kazi zao ni kukutana Nkrumah na kuandika pepa kwa donors...

  Nadhani sijatoka nje ya mada
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nadhani mwishoni utakubaliana nami tena kuwa njia za kukabiliana na mamtatizo ya aina yoyote sinaangukia katika makundi hayo matatu tu.

  Watanzania wengi pamoja na serikali yetu kwa jumla tumejengwa katika msingi wa kutumia njia ya tatu tu, na inapoonekana kuwa hatuna namna ya kuyakimbia matatizo yetu tena basi tunaishi nayo kama vile ni sehemu ya maisha yetu. Ni kutokana na hali hiyo ndiyo maana barabara ikiwa na mashimo basi tutaendelea kuitumia hadi apatikane mfadhili wa kuyaziba. Vyoo vikiharibika, kama unavyodai kwenye mabweni ya UDSM, basi ama tutaendelea kuvitumia katika hali hiyo hiyo au tutachimba choo cha shimo pembeni mahala ambapo hapakuwa pamepwangwa na mbaya zaidi tunaweza kuamua kujisadia nje hovyo hovyo hovyo tu. Tabia ya kukabiliana na matatizo yetu na kuyataua ili yasijirudiea tena (yaani njia ya pili) hatunayo.

  Vile vile watanzania hatukujengwa kujitengezea mazingira yanayotuepusha na matatizo (yaani njia ya kwanza); hatuna kitu kinachoitwa long term planning. Tunaishi kama vile dunia itakuwa hivyo hivyo na maisha yatakuwa hivyo hivyo kama yalivyo leo; hatuangalii mbali. Ni Tabia hiyo ndiyo inayotufanya tusiwe tunapanua miundo mbinu yetu. Barabara zote zinazojengwa Tanzania yetu leo hii zina lane moja tu, wakati wenzetu wanajenga barabara zenye lane tatu hadi sita. Tanzania tunajua kuwa mahitaji yetu ya umeme yameongezeka sana, badala ya kutatua hilo kwa kuongeza uwezo imara wa uzalishaji kuondokana na adha hiyo kwa miaka mingine 30 ijayo, tunakimbilia kutafuta majibu ya mkato ili ama kukimbia tatizo kwa kutumia MW100 ya kukodi kutoka DOwans au kwa kuliacha tatizo hilo litatuliwa na mwekezaji. Huko ni kushindwa kujenga mazingira ya kuzuia matatizo na vile vile kushindwa kukabiliana na matatizo yetu ana kwa ana.

  Hybrid approach iliyokuwa proposed na Ogah hapo juu, ndiyo approach inayotakiwa kufuatwa. Hao wenzetu waasia na wazungu wanachanganya njia zote tatu kwa mpigo kama recipe yao ya kuwaepusha na matatizo. Ilipotekea Mafuriko kwenye mto Mississipi, walianza kwa kuhamisha watu kuwapeleka nje ya mafuriko (njia ya tatu), baada ya hapo wakajenga ukuta wa mdoa kwa kutumia sand bags (njia ya pili), baada ya msimu wa mafuriko kuisha wamemua kujenga ukuta imara wa kuhakikisha kuwa mafuriko hayo hayatatokea tena (njia ya kwanza.) Je Tanzania tuliwahi kukabiliana na matatizo ya mfuriko kwa approach hiyo?
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe katika hayo. Na pengine tatizo ni kubwa zaidi ya hapo. Tumefikia hatua ya kutatua tatizo kwa tatizo. Mathalan tatizo ni ufinyu wa bajeti. Serikali inatoka kwenda kwa wafadhili kutafuta fungu la kufidia ufinyu wa hiyo bajeti, bila kujishughulisha kufikiri masharti yanayoambatana na hilo fungu la wafadhili. Wakati mwingine tatizo ni food security. Taifa halina chakula cha kutosha. Na huu uhaba unasababishwa pengine na ubovu wa miundombinu kwa mikoa yenye kulima chakula kutofikika kwa urahisi, matokeo yake chakula kinaozea huko ama wakulima kuuza nje ya nchi kutokana na urahisi wa kufika huko kuliko kufika dar au pwani, na uhaba wa chakula kutokea. Njia rahisi ya serikali kupambana na hili wanaagiza chakula toka nje tena, ama wanaalika wakulima wakubwa wa kizungu kuja kuhodhi mashamba makubwa kwa kisingizio cha kuzalisha chakula cha kutosha kwa taifa. Gharama ya kuagiza chakula toka nje na gharama ya kupora wananchi ardhi kubwa na kumpa mwekezaji ni kubwa kuliko kama wangeboreshewa barabara, madaraja na masoko. Kwa hiyo hapa unaona tatizo linatatuliwa kwa tatizo.
   
Loading...