Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Public Discourse II
Na. M. M. Mwanakijiji
Nilikuwa nazungumza na Mkulu mmoja wa idara siku chache zilizopita alisema kitu fulani ambacho wakati huo hakikunisumbua kichwa hadi sekunde chache zilizopita. Alikuwa anaulizia vitu fulani fulani kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake mpya ambavyo angeweza kuagiza kutoka hapa au Uchina (mwenyewe alipenda vya hapa US).
Kutokana na mazungumzo hayo nikaulizia (katika kutosheleza udadisi wangu tu) kuwa kwani samani zake za ofisi amenunua wapi? Alicheka kidogo na kuniambia kuwa ziliagizwa toka Uarabuni (sijui kijiji gani); Katika kutaka kujua zaidi nikamuuliza na mazulia mmeyapata kutoka Magereza (lile Gereza la Maweni Tanga walikuwa wanatengeneza mazulia mazuri tu na kulikuwa/kipo kiwanda cha mazuria) akacheka tena kunishangaa na kusema Mazuria mazuri siku hizi yanatoka Omani huko na Qatar ingawa yeye alikokuwa mwanzoni (kabla ya wadhifa mpya) waliagiza ya kwao toka China huko huko.
Tukaendelea na mazungumzo mengine hadi hivi punde:
Hivi Maofisi ya serikali yanaagiza vitu gani nje ambavyo vingeweza kabisa kupatikana nchini katika ubora mzuri na kwa bei nafuu na hivyo kuchangia katika kutoa ajira, huduma na kukua kwa uchumi? Je kuna kitu chochote cha ofisini ambacho hakiwezi kupatikana Tanzania hadi twende nje? Hofu yangu ni kuwa tusipoangalia tutakuta tunaagiza hata watumishi kutoka nje na viongozi kutoka nje huku wenyewe tukiona fahari kwamba tunatumia vitu vya "ng'ambo"!
On the other hand, labda uzee umeanza kuniingia kwa kasi!!