Tunapotaka kutumia nguvu kubwa Kupindua Meza kwa Kaizer Chiefs FC je, tunaoenda kukutana nao Semi Finals tutawaweza?

Hiyo Al Ahly ni mpya au ni ile Simba walicheza nayo group stage.Mnawaza kwa kutumia nini?

Yani mentality ya mitanzania mingi Ni ya kimaskini Sana, Unyonge, kutojiamini,watu wasio na malengo.Kila kitu sisi hatuwezi,kila kitu sisi bado sana.

Sijawahi kujua mnatumia nini kuwaza.
Swali la kwanza la msingi, uliangalia mechi ya Al ahly na mamelody ilivyopigwa au unakuja kuharisha hapa? Sasa hao Al ahly unaowana ni wanyonge wanaenda hadi fainali, wakati sisi tunaishia hapa hapa robo
 
Muwekeze nguvu zaidi Azam fc, hawa atleast wataleta ushindani kimataifa na watafika mbali. Lakini mkiendelea na usimba na uyanga mtakua mnaishia makundi.. ..

🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Najua kuanzia sasa nguvu Kubwa ya Kupindua Meza (kwa Fitna za nje ya Uwanja) zitaanza Kutumika ili Kuwafunga Kaizer Chiefs FC Wikiendi ijayo huku tukidanganywa sana kuhusu uwezo wa Timu yetu na Kuaminishwa mno na Kauli Mbiu za Kibabe za Kuujaza Uwanja ili Mapato yapatikane wakati wenye Kuujua vyema Mpira tumeshajua kuwa Safari yetu kwa Msimu huu ndiyo imefikia Tamati hapa na kwa wengi huu ni Ukweli Mchungu.

Kwa nilivyozitizama Klabu Kubwa Tatu ambazo nimehisi huenda Simba SC ikakutana nazo kama itabahatika Kupindua Meza kwa Kaizer Chiefs FC huenda huko mbele tukaja Kufungwa hata Goli 13 na mojawapo ya hizo Timu kwani zina uwezo mkubwa sana na Wachezaji wa Daraja la Juu ambao kwa Simba SC yetu ni Maji marefu kweli kweli Kushindana ( Kupambana ) nao.

Jana nimewatizama Wydad Casablanca, Esperance du Tunis na Mamelodi Sundowns (ambao Wote hawa ni African Soccer Giants kwa sasa ) ambao najua kama Simba SC itakutana na Mmoja wapo katika CAF CL Semi Finals kuna Hatari ya Kupokea Kipigo Kitakatifu (cha Kishalubela) zaidi ya tulichokipokea Jana pale Soccer City FNB Stadium Johannesburg Afrika Kusini kutoka kwa Kaizer Chiefs FC.

Ushauri wangu wa bure tu kwa Simba SC (ambao najua utawaudhi Wapuuzi, Wanafiki na Washamba kadhaa) ni kwamba Simba SC tusitumie Nguvu Kubwa Kupindua Matokeo bali tuitumie tu hiyo Mechi kama sehemu ya Kujifunza zaidi na kupata Uzoefu ili basi Msimu ujao tukiingia tuwe tumejidhatiti vya Kutosha kwa Kufika mbali Kimashindano.

Kwa Kikosi cha sasa cha Simba SC Kulazimisha kufika Nusu Fainali ya CAF CL na kukutana na hao Giants Watatu niliowataja hapo juu ( ambao uwezo wao ni maradufu ya Kaizer Chiefs FC waliotuadhibu Kikatili jana ) ni Kujitafutia tu Aibu nyingine na tuzidi Kuchekwa na Watani zetu wakubwa Yanga SC ( japo na Wao Timu yao hivi sasa ni kama tu Mgonjwa anayekaribia Kukata Roho ) katika Kuwania Ubingwa wa VPL ambao kuna uwezekano mkubwa wasiupate kwa miaka kadhaa mpaka wakijirekebisha Kiufundi na Timu yao pamoja na Uongozi wao mzima.

Nimefurahi kumsikia Mwekezaji Mo Dewji akisema kuwa amehairisha Kununua Magari yake Mawili aina ya Ferrari na Rolls Royce ili astarehe nayo na ajikite Kuisaidia zaidi Klabu yake pendwa ya Simba SC.

Nami GENTAMYCINE namshauri Mwekezaji Mo Dewji kwamba kama kweli kapania kuachana na Starehe ya Kuyanunua hayo Magari ili aisaidie Simba SC namuomba hizo Pesa azitumie Kusajilia Wachezaji wakubwa, mahiri na wa Kiwango cha Kimataifa na Kimashindano hasa ili tukicheza tena Champions League Msimu ujao lengo letu lisiwe tena kufika Robo au Nusu bali liwe ni Kufika Fainali na kubeba Kombe kabisa la Afrika kwa mara ya Kwanza.

Binafsi kwa Kikosi cha Simba SC cha sasa ( ambacho si cha Kucheza Nusu Fainali ya CAF CL ) kutokana na kuwa na Mapungufu makubwa hasa ya Kiufundi hata tukiishia hapa Robo Fainali kwa kutolewa jumla na Kaizer Chiefs FC Wikiendi ijayo bado nitajiona nimejitahidi na Kukazia katika Lengo na kamwe sitochukia au kujisikia vibaya kwani nitakuwa nimetolewa katika hatua nzuri ya Kimashindano na Timu Bora pia kwa bara la Afrika.

Timu ikirejea Kesho Watafutwe haraka Wataalam wa Saikolojia ili wawajenge upya Wachezaji wetu na warudi katika hali zao kwani kwa Jicho langu Kali la Kisaikolojia leo katika recovery session yao pale Kambini Afrika Kusini nimeona almost 95% ya Wachezaji wa Simba SC wamekuwa affected psychologically hivyo kama hawatopata thorough counseling huenda Timu ikapoteza kwa margin kubwa zaidi ya Goli zile Nne ( 4 ) za Jana.

Mpira wa sasa ni wa Kisayansi zaidi hivyo nasi tubadilike na tuacheni na huu Upuuzi Upuuzi wetu wa mambo ya Kiswahili ya nje ya Uwanja ( sijui Kuroga sana na Kupulizia mno Dawa 4-4-2 Vyumbani ) hayatatusaidia lolote na sana sana tutazidi Kuharibikiwa tu na kuonena ni Wapumbavu wa Kiwango kisichovumilika tena katika hii dunia ya Kisasa yenye kuhitaji Fikra, Ubunifu na Mipango thabiti yenye Mikakati endelevu.
Kama Simba anafuzu nusu fainali, anaenda kukutana na Wydad Casablanca au Mc Algers.

Ni lazima.
 
Mchezo wa mpira ni saikolojia, alimradi tu muwe na timu bora inayoweza kucheza na kupata matokeo!
Matokeo ilopata Simba hatua ya makundi sio ya kubahatisha kwanini hatua ya robo fainali tushindwe? Ofcoz we can!
 
Mkuu usiwe kama mtoto wa darasa la 7 anayewaza mtihani wa form four! Hakuna haja ya kucomplicate mambo hebu twende na ule msemo wa Lowassa kwamba Tutalivuka daraja tutakapolifikia!
 
GENTAMYCINE:

Hongera sana kwa andiko lako zuri mkuu.
Kwanza ni hatua kubwa sana kwa Simba Sc kufika hapo lakini pia tusiishie tu kushinda ni lazima tujifunze kwa hivi vilabu vikubwa namna na jinsi ya wao wanavyobrand hizi timu.

Nilijaribu kuwafatilia #Amakhosi4Life namna na jinsi timu yao ilivyokuwa branded inakuonesha kabisa hii timu ni klabu ya pili kwa utajiri Afrika tuna haja sasa ya MO badala ya kufikiria kujizawadia vitu ambavyo ni maisha yake binafsi kuliangalia hilo na asituaminishe na mafanikio ya muda mfupi.

Huwezi ukakuta Stan Kroenke Arsenal haijafanya vizuri na akaanza kuongelea maisha yake binafsi. Huu ni ukweli ambao hausemwi Simba kabla yakucheza inakuwa na mashabiki wengi akipoteza makosa yanaonekana.
 
We utakuwa yanga yaani unaibeza team ambayo imefika QF na kusema hamna kitu. We boya kweli. Kufika QF unaona kitu chepesi....ushabiki wa kindezi tuacheni kisa unajua kutype keyboard ya simu yako. Simba knawachezj wazuri...kukosea plan ya kucheza na kaizer ndo manenooo weeee. Mlitubez sana group stage. Simba inazid kukua kama hujui. Punguza unafiki
 
Mchezo wa mpira ni saikolojia, alimradi tu muwe na timu bora inayoweza kucheza na kupata matokeo!
Matokeo ilopata Simba hatua ya makundi sio ya kubahatisha kwanini hatua ya robo fainali tushindwe? Ofcoz we can!

Timu inayoongoza ligi imefungwa goli 4 na timu inayoshika nafasi ya 11 😄 kwa maana mmekutana na vibonde na vikawapiga 4G.. ..je wangekutana na wydad, Belouizdad au mc algiers si wangepigwa hata 10!!!

Haujawahi kuvuta bangi ujanani
 
Kama Simba anafuzu nusu fainali, anaenda kukutana na Wydad Casablanca au Mc Algers.

Ni lazima.
Sasa unadhani kwa hawa Giants wa Kiarabu tutapita Mkuu kwa aina ya Beki zetu nyoro nyoro Kapombe, Hussein, Wawa na Onyango?
 
Timu inayoongoza ligi imefungwa goli 4 na timu inayoshika nafasi ya 11 😄 kwa maana mmekutana na vibonde na vikawapiga 4G.. ..je wangekutana na wydad, Belouizdad au mc algiers si wangepigwa hata 10!!!

🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
Nimetahadharisha hili Kiufundi kabisa nimeishia Kulaumiwa, Kuchukiwa na kuambiwa Mimi ni Yanga SC huku nikifananishwa na Michael Wambura na Shaffih Dauda huku huko nyuma pia nikifananishwa na Haji Manara, Nape Nnauye na Masoud Kipanya.
 
We utakuwa yanga yaani unaibeza team ambayo imefika QF na kusema hamna kitu. We boya kweli. Kufika QF unaona kitu chepesi....ushabiki wa kindezi tuacheni kisa unajua kutype keyboard ya simu yako. Simba knawachezj wazuri...kukosea plan ya kucheza na kaizer ndo manenooo weeee. Mlitubez sana group stage. Simba inazid kukua kama hujui. Punguza unafiki
Naijua Simba SC kuliko Pumbavu Mmoja Wewe na nimejitolea na hadi kuhatarisha Maisha yangu ili kuipa Mafanikio Simba SC yako hiyo sawa? Huna ulijualo kuhusiana na Simba SC na acha kunipotezea pia muda wangu kwani Wewe si wa Level yangu Kujadiliana Masuala ya Simba SC na Soka la Tanzania na hata la Ulaya vile vile sawa?
 
Mkuu usiwe kama mtoto wa darasa la 7 anayewaza mtihani wa form four! Hakuna haja ya kucomplicate mambo hebu twende na ule msemo wa Lowassa kwamba Tutalivuka daraja tutakapolifikia!
Sina Fikra za Kiuswahili na Kipumbavu kama ulizonazo ( mlizonazo ) Mashabiki wengi wa Simba SC.
 
Mchezo wa mpira ni saikolojia, alimradi tu muwe na timu bora inayoweza kucheza na kupata matokeo!
Matokeo ilopata Simba hatua ya makundi sio ya kubahatisha kwanini hatua ya robo fainali tushindwe? Ofcoz we can!
Saikolojia huwa inaenda na Quality hebu acheni Kunichosha na uwezo wenu mdogo wa Akili ( Kufikiri ) tafadhalini sawa?

Yaani umefungwa Goli zile Nne ( 4 ) Kiufundi na kutokana na Ubora mkubwa wa Wachezaji ghali wa Kaizer Chiefs FC ambayo imewekeza kweli kweli leo unakuja kuniambia Upuuzi wako wa Simba SC Kushinda kwa Kigezo cha Saikolojia.
 
Back
Top Bottom