Tunapotaka kutumia nguvu kubwa Kupindua Meza kwa Kaizer Chiefs FC je, tunaoenda kukutana nao Semi Finals tutawaweza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,697
109,125
Najua kuanzia sasa nguvu Kubwa ya Kupindua Meza (kwa Fitna za nje ya Uwanja) zitaanza Kutumika ili Kuwafunga Kaizer Chiefs FC Wikiendi ijayo huku tukidanganywa sana kuhusu uwezo wa Timu yetu na Kuaminishwa mno na Kauli Mbiu za Kibabe za Kuujaza Uwanja ili Mapato yapatikane wakati wenye Kuujua vyema Mpira tumeshajua kuwa Safari yetu kwa Msimu huu ndiyo imefikia Tamati hapa na kwa wengi huu ni Ukweli Mchungu.

Kwa nilivyozitizama Klabu Kubwa Tatu ambazo nimehisi huenda Simba SC ikakutana nazo kama itabahatika Kupindua Meza kwa Kaizer Chiefs FC huenda huko mbele tukaja Kufungwa hata Goli 13 na mojawapo ya hizo Timu kwani zina uwezo mkubwa sana na Wachezaji wa Daraja la Juu ambao kwa Simba SC yetu ni Maji marefu kweli kweli Kushindana ( Kupambana ) nao.

Jana nimewatizama Wydad Casablanca, Esperance du Tunis na Mamelodi Sundowns (ambao Wote hawa ni African Soccer Giants kwa sasa ) ambao najua kama Simba SC itakutana na Mmoja wapo katika CAF CL Semi Finals kuna Hatari ya Kupokea Kipigo Kitakatifu (cha Kishalubela) zaidi ya tulichokipokea Jana pale Soccer City FNB Stadium Johannesburg Afrika Kusini kutoka kwa Kaizer Chiefs FC.

Ushauri wangu wa bure tu kwa Simba SC (ambao najua utawaudhi Wapuuzi, Wanafiki na Washamba kadhaa) ni kwamba Simba SC tusitumie Nguvu Kubwa Kupindua Matokeo bali tuitumie tu hiyo Mechi kama sehemu ya Kujifunza zaidi na kupata Uzoefu ili basi Msimu ujao tukiingia tuwe tumejidhatiti vya Kutosha kwa Kufika mbali Kimashindano.

Kwa Kikosi cha sasa cha Simba SC Kulazimisha kufika Nusu Fainali ya CAF CL na kukutana na hao Giants Watatu niliowataja hapo juu ( ambao uwezo wao ni maradufu ya Kaizer Chiefs FC waliotuadhibu Kikatili jana ) ni Kujitafutia tu Aibu nyingine na tuzidi Kuchekwa na Watani zetu wakubwa Yanga SC ( japo na Wao Timu yao hivi sasa ni kama tu Mgonjwa anayekaribia Kukata Roho ) katika Kuwania Ubingwa wa VPL ambao kuna uwezekano mkubwa wasiupate kwa miaka kadhaa mpaka wakijirekebisha Kiufundi na Timu yao pamoja na Uongozi wao mzima.

Nimefurahi kumsikia Mwekezaji Mo Dewji akisema kuwa amehairisha Kununua Magari yake Mawili aina ya Ferrari na Rolls Royce ili astarehe nayo na ajikite Kuisaidia zaidi Klabu yake pendwa ya Simba SC.

Nami GENTAMYCINE namshauri Mwekezaji Mo Dewji kwamba kama kweli kapania kuachana na Starehe ya Kuyanunua hayo Magari ili aisaidie Simba SC namuomba hizo Pesa azitumie Kusajilia Wachezaji wakubwa, mahiri na wa Kiwango cha Kimataifa na Kimashindano hasa ili tukicheza tena Champions League Msimu ujao lengo letu lisiwe tena kufika Robo au Nusu bali liwe ni Kufika Fainali na kubeba Kombe kabisa la Afrika kwa mara ya Kwanza.

Binafsi kwa Kikosi cha Simba SC cha sasa ( ambacho si cha Kucheza Nusu Fainali ya CAF CL ) kutokana na kuwa na Mapungufu makubwa hasa ya Kiufundi hata tukiishia hapa Robo Fainali kwa kutolewa jumla na Kaizer Chiefs FC Wikiendi ijayo bado nitajiona nimejitahidi na Kukazia katika Lengo na kamwe sitochukia au kujisikia vibaya kwani nitakuwa nimetolewa katika hatua nzuri ya Kimashindano na Timu Bora pia kwa bara la Afrika.

Timu ikirejea Kesho Watafutwe haraka Wataalam wa Saikolojia ili wawajenge upya Wachezaji wetu na warudi katika hali zao kwani kwa Jicho langu Kali la Kisaikolojia leo katika recovery session yao pale Kambini Afrika Kusini nimeona almost 95% ya Wachezaji wa Simba SC wamekuwa affected psychologically hivyo kama hawatopata thorough counseling huenda Timu ikapoteza kwa margin kubwa zaidi ya Goli zile Nne ( 4 ) za Jana.

Mpira wa sasa ni wa Kisayansi zaidi hivyo nasi tubadilike na tuacheni na huu Upuuzi Upuuzi wetu wa mambo ya Kiswahili ya nje ya Uwanja ( sijui Kuroga sana na Kupulizia mno Dawa 4-4-2 Vyumbani ) hayatatusaidia lolote na sana sana tutazidi Kuharibikiwa tu na kuonena ni Wapumbavu wa Kiwango kisichovumilika tena katika hii dunia ya Kisasa yenye kuhitaji Fikra, Ubunifu na Mipango thabiti yenye Mikakati endelevu.
 
chezeni hata mbili kabla ya kukutana na kaizer chiefs ili wachezaji wapate fitness.
Una Akili sawa sawa Wewe? Mechi ni Jumamosi hii ijayo na Timu inaingia leo Jumatatu itachezaje hizo Mechi Mbili wakati hata Kanuni tu za FIFA zinasema Timu inatakiwa ipishane Kucheza Mechi zake kila baada ya Saa 72?

Muwe mnachangia kwa kutumia Akili sometimes kwani mnakera na kuchosha pia. Na kama unajua hujui Masuala ya Mpira ni vyema ukaacha tu Kushadadia na ukachangia Upopoma mtupu tu.
 
Hata timu tunayopaswa kukutana nayo nusu fainal hujui ni ipi unaunganisha tim zote af bado unaumtushaur?
Nakushaur rud kafanye utafit upya watakaokutana nusu final wanajulikana tayali
Hatukutanu na Mamelod nusu ndg
Pumbavu hivi nimetaja Mamelodi Sundowns tu pekee? Sijazitaja na Wydad Casablanca pamoja na Esperance du Tunis?

Na nimezitaja hizi Timu Tatu baada ya Kuangalia Mechi za Semi Finals CL zilivyopangwa na CAF na iwe isiwe Simba SC ikiingia itakutana na mojawapo ya hizo Timu.

Huna ukijuacho hivyo kuwa Msomaji tu.
 
Ina maana Simba hawachezi mechi yeyote mpaka warud
iane?
Kwa muendelezo ule ule wa Kudekezwa na TFF haitacheza Mchezo wowote wa VPL ili wajiandae na Mechi hiyo ya marudiano Wikiendi ijayo huku Wakiroga sana, Wakiuroga Uwanja na wakianza Kupulizia Dawa ( 4-4-2 ) Vyumbani ili Wapindue Meza na Lengo la Kufuzu CAF CL Semi Finals litimie.
 
Kwa stairi hii Simba Wana wakati mgumu Sana hawana sehem ya kujisahihisha
 
Hata timu tunayopaswa kukutana nayo nusu fainal hujui ni ipi unaunganisha tim zote af bado unaumtushaur?
Nakushaur rud kafanye utafit upya watakaokutana nusu final wanajulikana tayali
Hatukutanu na Mamelod nusu ndg
Duuu sasa ni bora mngekutana na Mamelod kuliko hao wengine. Amini hii!
 
We jamaa ni mnafiki, toka mashindano yaanze umekuwa ukiitabiria vibaya Simba, ulitoa maneno kama hayo baada ya mechi ya vita na al ahly lakini vita walikuja wakapigwa nne, pia sielewi kwanini unangangania uchawi inaelekea ndio tabia zako
Sasa kama umeshajua na unajua Mimi ni Mnafiki na siitakii Mema Simba SC kwanini huwa unapoteza muda wako Kunisoma hapa JamiiForums na hata Kuchangia Threads zangu pia?

Kuamini Uchawi ( Njia Mbadala ) ni tatizo? Kuna Uchawi wa Faida na wa Hasara kwa Mwanadamu au kutokana na Upumbavu wako wa Kurithishwa na waliohangaika Kukuleta duniani hujui?

Kama Uchawi ni mbaya inakuwaje katika Mafunzo ya Ukomandoo Cuba, Israel na China ( bila kusahau katika nchi zote za Afrika ) kuna Kipengele cha Utumiaji wa Ndumba ( Uchawi ) kwa recruits wa Kozi hii / hiyo?

Kinachowasumbueni baadhi ya Mashabiki Wapumbavu ( Fools ) wa Simba SC wakiongozwa na Wewe Kinara Wao Mkuu mnataka ( mnapenda ) Mtu akiwa ni Shabiki wa Simba SC basi awe tu anatetea Upuuzi na anaisifia ila asiwe ( asithubutu ) Kuikosoa.

Sina Unafiki na Upumbavu huo na tena huenda GENTAMYCINE nikawa ndiyo Mshabiki mzuri wa Simba SC kuliko Wewe ( Nyie ) Wapuuzi wachache na ndiyo maana huwa napenda Kukosoa, Kushauri na Kutahadharisha ili Timu ipate Maendeleo.

Na nazidi Kukujaza Hasira tena kwa Kukuhakikishia kuwa Kiufundi ( hasa nilivyoiona Simba SC na Uchezaji wa Kaizer Chiefs FC ) kwa 99.9% tumeshatoka tayari, ila kwa Bahati na Fitna ya Kupulizia Dawa ( 4-4-2 ) Vyumbani na katika Basi litakalowabeba Simba SC inaweza Kupindua Meza na ikaifunga Kaizer Chiefs FC hata Goli 5 au 6 Wikiendi ijayo.

Ninapenda Kuchukiwa na Wapumbavu.
 
Wewe si ndio unaenda kupuliza dawa, ungekuwa karibu ningekugecha
 
Duuu sasa ni bora mngekutana na Mamelod kuliko hao wengine. Amini hii!
Mkuu tena tusiombe kabisa kukutana na hawa Mamelodi Sundowns kwani kwa Uchezaji wao, Ubora wao na Uwezo mkubwa wa Wachezaji wao tukikutana nao tunafungwa kati ya Magoli 9 na hata 10.

Ukirudi huko kwa akina Wydad Casablanca na Esperance du Tunis ambao kama Simba SC tutabahatika Kupindua Meza Wikiendi ijayo tutakutana nao ndiyo huenda tukapata Dhahama Kubwa zaidi kuliko tuliyoipata Juzi kwa Kaizer Chiefs FC.

Naomba GENTAMYCINE hapa nieleweke vizuri tu kuwa siidharau wala siichukii Simba SC yangu ila kwa Jicho langu la Kiufundi nimegundua Timu yetu ( Simba SC ) haina Kikosi Kilichokomaa Kucheza Hatua ya Nusu Fainali ( ambako ndiko Kugumu zaidi ) lakini ina Kikosi cha kutufikisha hapa Robo Fainali tulipofikia na tunapoenda kuishia.

Na tukitolewa hatua hii na Kaizer Chiefs FC sasa iwe Changamoto Kwetu ( hasa kwa Mwekezaji Mo Dewji ) ya Kusajili Wachezaji wakubwa, mahiri, washindani na wa kutufikisha si tu Nusu Fainali tulipokulenga bali wa Kutufikisha kabisa Fainali ya CAF CL na Simba SC tubebe Kombe ( Ubingwa ) kabisa.

Lazima tuambiane Ukweli na tuvumilie.
 
Genta kama Genta! Umewashauri vizuri! Ila tatizo linaanzia kwa "spika ya timu" anajimwambafy sana kiasi kwamba wachezaji wakiingia uwanjani wanajiona wameshashinda!
Na hapo ndipo tatizo kubwa lilipo Mkuu.
 
Wewe si ndio unaenda kupuliza dawa, ungekuwa karibu ningekugecha
Nimeshariki Kuifanyia Umafia Simba SC yangu ili ishinde katika Mechi ile ya Ismailia FC, Yanga SC ( zile Goli 5 tulizowafunga ) na ile ya Nkana FC tena nikiwa na Waandamizi wako akina Nkamia na Kassim Dewji ( KD ) ambazo zote tulipata Matokeo japo kwa Ismailia FC Mvua Kubwa ilituharibia.

Naijua Simba SC yako ( yenu ) kuliko Wewe na Oya Oya ( Washamba na Wapuuzi ) Wenzako na nikiwa naikosoa siyo kwamba naichukia bali naioenda ila Wewe Mnafiki unataka tu usikie nikiisema kwa mazuri ili nikuridhishe ( niwaridhisheni ) mfurahi. Bahati mbaya sana GENTAMYCINE sipo hivyo na ni bora mnichukie ila Ukweli Mchungu niwape na uwaingieni vilivyo.
 
Inaelekea wewe ni.mwezi mchanga siku nyingine unakuwa na pointi ila siku nyingine unaharibu kabisa rudi kwenu ukafanyiwe tambiko
 
Back
Top Bottom