Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Wapelekee watu Solar, Huko Bush au hata mtaani uone nani atakupangia bei...., unless otherwise unataka kutumia miundombinu ya Tanesco au unataka kusambaza miundombinu yako utuletee madhara ya kutuunguza na kutuchafulia miji
Ok, sasa excuse ya Tanzania kutokuwa na umeme wa bei nzuri, wa kutosha na kuaminika ni nini? mnataka monopoly na kazi hamuwezi na kila kitu ni visingizio tuu, mna safari ndefu sana nyie
 
Kuna mashirika ya Serikali kutokana na wajibu wake ni kama idara za Serikali. Yanatakiwa yagharamikiwe na hazina kuu. Yanafanywa mashirika ili kuweza kudhibiti matumizi na kwamba iwepo tija.

Ukitaka kugeuza TANESCO liwe la kibiashara moja kwa moja kwanza utapata muwekezaji gani? Lazima awe wa nje na atakua na nguvu gani ya kisiasa nchini? Yeye atataka faida tu na umeme ndio roho ya uchumi wa nchi.

Sisi tunamlenga nani kuhusu maendeleo? Raia wa kawaida au wawekezaji kutoka nje? Lazima umeme utakua bei mbaya kwa raia wapiga kura na ndio mfarakano utaanzia hapo.

Hii mambo ya kubinafsisha sijui asili mia 20 TANESCO ni ile ile habari ya kubinafsisha TTCL. Wajanja wakawagawia wahindi hisa za TTCL kwa bei ya bure wakati Serikali ishawekeza mabilioni. Kisha wajanja kushirikiana na wahindi wakakwapua celltel kampuni ya TTCL ya simu za mikononi.

Ikawa wahindi wameshika jikoni TTCL wakikamua hela za umma kwa ruzuku za Serikali eti ni wabia wa TTCL. Magufuli akaja kuwafukuza wahindi na kuirejesha kampuni yake ya mkononi kwa kuhakikisha serikali inapewa hisa stahiki.

Sio kila anayejidai ana uthubutu ana uwezo au nia nzuri. Mashirika kama TANESCO au TTCL sio ya kuwekwa sokoni kama njuku.

Wanaoweza kuyaendesha kwa kufikia malengo yake kwa nchi kama Tanzania hakuna. Ni watanzania gani utawashawishi kuwekeza tanesco?

Hivi unaweza mshawishi mtu awekeze kwa gereza. Gereza linaweza kua mradi wa kibiashara? ..sina hakika wala sijaona. Lakini si lazima magereza yawepo? Kuna mambo lazima yawe jukumu la serikali. Ndio maana kuna kodi.

Tukikubaliana na uhuni huu wa january na zitto akijidai mpendekezaji wa hoja tunaona yale ya TTCL na ule mradi wa umeme wa makaa kule Songwe mbeya uhuni ule wa simon group kuhusu uda na kwingine.

La kufanyika ni uongozi imara wa kisiasa usiyokua na mchezo kudhibiti mashirika makubwa ya umma kuhakikisha hakuna ubadhirifu na inakwepo tija.
Sina imani na Makamba mpaka atapoweka wazi kumiliki Kidimbwi na kwanini kajifichi nyuma ya yule dogo wa salasala,anatuficha nini?
 
Wazo la kubinafsisha tanesco achilia mbali ttcl ni wazo zuri sana kwa mtu anaethnk po+ . Ni vzur kwakua kwasasa hio unayosema kunatija kuendeshwa chni ya serikali ni Big NO. Hapa tuangalie tuu namna nzuri ya ubinafsishaji, mwekezaji sio lazima atoke nje, pia tuweke mfumo mzur wa kudhibiti wizi, uhujumu wa shirika na mfumo mzur utakao mpa bei nafuu ya units mwananchi.
Wewe unahofu tuu kwa mfumo wa sasa wa uwekezaji kuwa tunaweza kupigwa,, YES tunaweza kuibiwa but best b4 investing tufanye tafiti na uchunguzi kutoka nchi zlizoruhusu mashirika binafsi yalivowekeza Kwenye umeme apa mabarozi wanahusika sana kama watajitambua.
My take: tanesco ibaki mmiliki wa sources of energy na muuzaji wa energy hio kwa mainvestors ambao wao watafanya kazi kubwa upande wa distribution.
Hapa tenda itolewe na pia serikali isimamie vigezo na tija katika kuwanufaisha watumiaji wa mwisho.

I will only take your “my take” . Angalau!
 
Nachofaham JPM aliitoa Tanesco kutoka kwenye madeni ya mikataba yote ya kinyonyaji ikiwemo IPTL ,na Ata ewura walipo tangazaga kukubali bei ya umeme kupanda aliwatumbua sababu tayari shirika lilikua halina tena mzigo wa madeni,
Na alikua anasubiri bwawa Rufiji likamilike ili unit ya umeme ishuke Bei
Leo nimesoma mahali Tanesco imetengeneza faida ya Tsh Bil 52 ,
Sasa nini kinatafutwa!?
Inachotaka Tanesco ni utashi tu wa viongozi
 
Idea yako ya semi monopoly for serious investor wont work, na for profit hakuna ubaya na ndio kinachotakiwa haswa ili investors wawe motivated kuweka pesa zao, michezo michafu kama ENRON ipo popote pale lakini nafikiri unajua kilichowakuta baada ya hapo,monopoly ya TANESCO ndio tatizo la sekta ya umeme TZ
For Profit peleka kwenye luxury au bia na sio vitu muhimu kama nishati na afya za watu (Tukirudi America unaweza kuona kwa jinsi gani Pharmaceuticals na Insurance Companies zinawafanya watu wafe na kutokutibiwa kwa kukosa Bima)...

Unaongelea Investors wawe motivated kuweka pesa zao ? Kwa lipi hasa tunahitaji pesa zao ? Bwawa tunajenga kwa mikopo ambayo hadi watukuu watalipia, Gesi tulishaifikisha mpaka Dar huenda napo kwa madeni mpaka vitukuu..., Umeme vijijini kila mtu analipa anaponunua LUKU..., sasa hao investors waje ili wafanye nini ? (Tugawane faida ya jasho letu) au sisi tuliochumia juani waje kutusaidia kulia kivulini ?

As for ENRON Kampuni ili-file bancruptcy, watu kupoteza pesa zao, na kazi zao.... In short people;s lives were ruined (I don't think the bancruptcy was any consolation)

Unaongelea Monopoly ya Tanesco; kwahio unataka hizi baadhi ya njia zake (distribution tuwape kina Dowans na Symbion) for me badala ya kuwapa hizi kwanini hao investors wasiende huko in the middle of no where waweke miundombinu (kumbuka na hii miundombinu mimi na wewe ni stakeholders sababu tunaichangia kwenye LUKU)

As for generation mbona watu binafsi walishakuja tu kina Dowans na yaliyotupata kila Mtanzania anajua
 
Ok, sasa excuse ya Tanzania kutokuwa na umeme wa bei nzuri, wa kutosha na kuaminika ni nini? mnataka monopoly na kazi hamuwezi na kila kitu ni visingizio tuu, mna safari ndefu sana nyie
Tanesco either kwa makusudi au Bahati mbaya kuna kipindi ilikuwa inanunua umeme kwa hao wadau wako so called investors (Kina Dowans et al) na Gesi nadhani nayo sio yetu walikuwa wanauziwa..., ukiongezea na management mbovu na vyanzo vingine vya HEP kutokufanya vizuri kupelekea kutumia umeme wa diesel it was a recipe for disaster.... That was then...

Kumbuka wakati wote huo Generated Capacity ilikuwa kama 1600MW; Sasa kama tunakaribia kuongeza 2100MW nyingine tena kwa jasho kubwa la watu kupigwa Matozo na Ma - Mikopo ya kufa mtu....., kweli huu ndio wakati wa kuanza kutafuta mnunuzi ?

Ni kama wewe kuku wako ulikuwa unakataa kumuuza wakati ana magonjwa na sasa karibia anaanza kutaga na amepona eti ndio unaona umuuze, ukiulizwa kwanini eti unasema majirani wote wameuza wao....
 
Du kazi kweli kweli, haya mawazo ya kijamaa ndio yanayoturudisha nyuma. Mashirika mengi ya umma yalikufa haya kama TANESCO yameendelea kuwepo kwasababu tu yanapatiwa ruzuku serikalini ambayo ni kodi za wananchi tunalipia uzembe wote na wizi wote katika shirika hili. Dawa ya haya yote ni kilivunja shirika hili kuwa katika sehemu 3 au mbili generation and trasmission na distribution and collection of revenue. Yabinafsishwe kwa uwazi na kuzingatia sheria yunaweza kutafuta uzoefu kwenye mataifa mengine. Na kuweka vigezo vitakavyolinda maslahi ya Taifa kwa uwazi na kwa faida ya walaji. Generation ndio vital watupe ememe usio na kutetereka na penalt incase of default. mfano gas/ nuclear could be the cheapest source of power, sisi tumekimbilia water generation. Kurudi kwenye mashirika ya umma ni ngumu kumeza.
Sio kweli kwasasa tanesco inajiendesha yenyewe bila ruzuku ya serikali
 
Tanesco either kwa makusudi au Bahati mbaya kuna kipindi ilikuwa inanunua umeme kwa hao wadau wako so called investors (Kina Dowans et al) na Gesi nadhani nayo sio yetu walikuwa wanauziwa..., ukiongezea na management mbovu na vyanzo vingine vya HEP kutokufanya vizuri kupelekea kutumia umeme wa diesel it was a recipe for disaster.... That was then...

Kumbuka wakati wote huo Generated Capacity ilikuwa kama 1600MW; Sasa kama tunakaribia kuongeza 2100MW nyingine tena kwa jasho kubwa la watu kupigwa Matozo na Ma - Mikopo ya kufa mtu....., kweli huu ndio wakati wa kuanza kutafuta mnunuzi ?

Ni kama wewe kuku wako ulikuwa unakataa kumuuza wakati ana magonjwa na sasa karibia anaanza kutaga na amepona eti ndio unaona umuuze, ukiulizwa kwanini eti unasema majirani wote wameuza wao....
Wenye akili watakuelewa,lakini madalali wa Mafisadi watapinga
 
Nafahamu linauziwa.
Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ni mfano mzuri.

Songas pia ni mfano mwingine. Ila sio kila taasisi au shirika la uma ni la kubinafsisha.

Umetolea mifano ya mabank, ukatoa mfano wa kampuni ya bia.

Nikikuwekea vitu hivi Umeme,Sigara,Pombe, Na uchague bank ya kuhifadhi pesa zako bila shaka chenye thamani zaidi ni umeme hapo.

Umeme ni nguzo muhimu ya kiuchumi kwa taifa, inatakiwa iwe stable siku zote kuiruhusu ubinafsishaji ni kuruhusu mlipuko wa bei za ajabu ajabu za bidhaa, huduma na maisha kwa ujumla.

Narudia maboresho mazuri yanahitajika lakini sio ubinafsishakuna
Madeni yasiyo lipika kivipi! mbona Makamba juzi alisema wanakusanya tilioni mbili? zote zinaenda Wapi;hapa naona madarali wa Mafisadi wameisha anza kurusha ndoano.Mbona miaka 5 ya Magufuri utukusikia upuuzi huu?
 
Lakini tukiwauliza maswali rahisi tuu kama vipi huduma ya umeme under TANESCO nina uhakika hata nyie wenyewe mnajua TANESCO ni shirika la ovyo sana, umeme haupatikani kama unavyotakiwa, umeme ni bei mbaya sana, ubadhirifu ndani ya shirika, madeni yanaongezeka kila mwaka na hamna chochote kizuri kuhusu Tanesco, waliuze tuu na waruhusu sekta binafsi, serikali ijipange kuwa strong regulator
Nmewahi kaa huko ubaruku miaka ya nyuma...Hawa jamaa wa ihefu ndo walikuwa wanasambaza umeme ., Ulikuwa Bei chee na haukatikagi mzee Ila walivokuja tanesco ni msala, Tena huko Kuna mashine kubwa za mpunga Ila wanaoata wakijiskia,...tanesco wakaanzisha monopoly system na wakamtoa mchizi , jamaa akatoa waya akawaachia nguzo imara za cement tanesco Sasa anafel,

Huko njombe Kuna mbena anadhalisha umeme na anasambaza na anapiga Mia mia za kutosha tu na ananguzo zake na watu wanaenjoy maisha
 
Zito ni starter kwenye gari hivyo ujue katumwa kuwasha gari engine ikopokea yeye hana kazi tena fikiria ikipelekwa mswada bungeni wa kuuza his za tannesco utafanyaje kwenye bunge hili ndiyo maana tunataka katiba mpya,wananch tukichagua viongozi wapewe uongozi wasifanyiwe fitina naserikali kuwaapisha waliopendwa na rais.
Kama Zungu na Tozo
 
Wakati Magufuli anaonyesha kiburi cha madaraka kwa kuhujumu upinzani mlikuwa mnachekelea kuwa ccm imeimarika.

Leo wamebaki CCM wenyewe na hawataki kukosolewa, matokeo yake chain ya wapigaji inaanza kurudi ndio mnalialia.

Acha hao wahuni warudi kwenye ulaji, na wauze kila kitu kwa bei ya kutupa ili siku nyingine mjue balance of power maana yake ni nini.

Akina Januari na wahuni wenzenu uzeni hiyo TANESCO bei ya kutupwa ili mliokuwa mnafurahia siasa na chaguzi za kishenzi mjifunze.
Umemaliza!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom