Tunaposheherekea miaka takribani 50 ya uhuru wa Tanganyika, tunajivunia nini?

Je, uhuru tulioupata mwaka 1961 umetusaidia kujikwamua na maadui watatu?

  • Ndiyo

    Votes: 1 6.7%
  • Hapana

    Votes: 14 93.3%

  • Total voters
    15
LEO tunapoadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika, Watanzania wa kada mbalimbaliwanakitazama kipindi hicho kwa namna tofauti, kamawanavyoeleza katika mahojiano haya yaliyofanywa na Elias Msuya. Naomba basi tuanglie nini hawa watanzania wenzetu maoni yao
Frank Moyo
NDANI ya miaka 51 ya uhuru, kuna mambo mengi ya maendeleo yamefanyika. Kwamfano, kuna ajira nyingi, rasmi na zisizokuwa rasmi, zimejitokeza. Wakati huuvijana wengi tumejiajiri kwenye usafiri wa bajaj, hii inasaidia kujikimukimaisha.
Siyo kwamba tunapata fedha nyingi, lakini tunaweza kujikimu tu kimaisha.
Hata hivyo naweza kusema kuwa bado nchi yetu haijaendelea kamazilivyo nchi za wenzetu. Wenzetu wana treni zinazopita chini ya ardhi, wanabarabara za angani (flyovers). Sisi bado reli na barabara ni zile zile tu.

Nashauri Serikali iwaangalie na wananchiwalio katika ajira zisizo rasmi kwa kuwa ndiyo wengi kuliko watumishi wa ummana wafanyakazi walio katika sekta rasmi.
Serikali pia iimarishe miundombinu kama relina barabara ili kuongeza maendeleo.

Japhet Kanyika
SAWA tumepata uhuru, lakini ni wa maneno tu. Hakuna uwajibikaji wa kweli wakuleta maendeleo.

Kwa mfano elimu yetu tangu tumepatauhuru bado haijazaa matunda katika jamii. Watanzania wengi hawana elimu yakuwawezesha kueleza kero zao, ukilinganisha na raia wa Kenya ambaowanajua haki zao kwetu bado.
Utakuta mtu hajui hata haki zake au anashindwa kueleza shida yake, mwishoanabaki na umasikini wake.

Kwa upande mwingine, ukiangalia maeneoya vijijini, vijana wengi wamejiajiri kwenye biashara ya bodaboda, lakinihawana mafunzo ya kutosha ya biashara hiyo.
Isitoshe Serikali inaweka ukiritimba kwa vijana, mfano kijana akihitaji leseniambayo gharama yake ni Sh40, 000 tu, atazungushwa hadi anajikuta ametoa Sh200,000.

Kwa upande wa kilimo, mimi ni mkulimanatoka wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Wakulima wengi hawana elimu yakilimo, matokeo yake wanalima mashamba makubwa bila utaalamu, hivyo kuishiakupata mazao kiduchu. Wanatumia nguvu na fedha nyingi lakini hakuna cha zaidiwanachopata.
Nashauri Serikali iwekeze kwenye elimu ili wananchi wajikwamue kiuchumi.

David William
MIAKA 51 ya uhuru, bado hatuna la kujivunia kwa sababu vijana wengi hatunaajira. Ukiacha vijana waliosoma hadi vyuo vikuu, lakini wengi wetu hatuna chakufanya, tumebaki na umasikini mtupu.

Mimi ni mwanamichezo na nimechezea timuza Kombaini ya Makuburi na Simba ‘B’, lakini nimeshindwa kuendelea kwa sababuya mazingira magumu. Sina uwezo wa kujikimu kimaisha wala kujikita kikamilifukwenye michezo.
Hilo ndiotatizo linalotukumba sisi vijana. Naamini kabisa kwa kipaji changu hiki chamichezo ningefika mbali, lakini kwa umasikini huu nimeshindwa.

Serikali haina mkakati wowote wakutukwamua vijana, ndiyo maana sioni faida za kusheherekea uhuru.
Kwa sasa najishughulisha na biashara ya taxi ili kujikimu kimaisha hata kama ndoto yangu ya kuwa mwanamichezo imepotea.

Naishauri Serikali iwekeze kwenyemichezo kwa kutambua vipaji vya vijana na kuviendeleza. Waanzishe shule za sokana michezo mingine.
Huko ndiko tutakapotokea, siyo lazima vijana wote tukae ofisini, hata hukumitaani tunaweza kujikwamua. Kwa nchi za wenzetu wanamichezo wanalipwa vizurikuliko hata maofisa wa Serikali.

Saleh Mpiga
NI kweli katika miaka hii 51 ya uhuru kuna mafanikio mengi yaliyopatikana.Uchumi umekua, kilimo kimeimarika, barabara zimejengwa na miundombinu mingine,ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Lakini bado kuna tatizo la ajira kwavijana. Wengi hatuna ajira tunaishi maisha ya kubahatisha. Kibaya zaidi hatavijana waliosoma vyuo vikuu hawana ajira.
Chanzo cha tatizo hili ni utandawazi ambapo raia wa mataifa mengine wanakuja nakuchukua ajira zetu. Ukifuatilia utaona elimu zao ziko juu, sisi tunaishi kwaujanja tu.
Tatizo jingine liko kwa viongozi wetu ambao wamekalia kujilimbikizia mali kulikokujali maslahi ya umma. Wananchi wengi wanataabika kwa umasikini lakini waowanafaidi kwa maisha ya anasa.

Ally Juma
KWA kweli mimi bado sijaona matunda ya uhuru, ikiwa hadi leo, wakulima vijijiniwanakosa hata matreka ya kulimia.

Serikali imeshindwa kupeleka matrektaili kuwasaidia wakulima, matokeo yake wanalima kwa kubahatisha tu na bei zavyakula zinakuwa juu kwa sababu kilimo hakijaboreshwa.
Mimi nimetokea Mzumbe, Morogoro ambako nilikuwa mkulima. Kule matrektayanamilikiwa na watu wachache. Mbunge wetu alikuwa na matrekta yake ambayohayakuwa yakitumia na wananchi wote.

Tunashindwa kuelewa kwa nini Serikali isipeleke matrekta hayokwa Serikali za vijiji ili wananchi wachangie tu gharama za mafuta. Lakini kwahali ya sasa mkulima atapata wapi fedha za kukodi trekta ili alime?
Hiyo ndiyo sababu ya vijana wengikukimbilia mijini kutafuta vibarua. Ni tatizo la kitaifa.
Mimi sasa nimejiajiri kama dereva wa taxi.Tumeunda umoja na tuna mfuko wetu tunaokusanya fedha kwa ajili ya kukopeshana.Ila bado tunatafuta mfadhili wa kutuongeza mtaji, ili tupate mikopo yamaendeleo. Huo ndiyo ukombozi kwa vijana wasio na mitaji.
Naishauri Serikali iwekeze kwa vijana ili kuleta maendeleo ya kweli.

Zainab Kapoma
MAFANIKIO yaliyopatikana kwa miaka 51 ya uhuru kwa kweli yananichanganya.Hakuna kitu kinachoniuma kama vijana wetuwanaosoma hadi vyuo vikuu kukosa ajira, eti kwa sababu tu hawana uzoefu.Atapataje uzoefu wakati ndiyo katokea shule?

Wazee wanang’ang’ania madarakani huku vijana wakisotea ajira kwamuda mrefu. Watu wamekuwa madarakani tangu tupate uhuru lakini wamo tu. Sana sana wanawaachia watoto wao, huku vijana wengi wenye sifa wakisota tu.
Ndiyo maana nasema sioni mafanikio ya uhuru. Labda hilo treni waliloleta hapo juzi, kwa sababu tumekuwa wakwanza kwa Afrika Mashariki na kati kuwa na treni la abira jijini Dar es Salaam.
Lakini nashauri kuwepo kwa utaratibu kwa vijana wenye elimukupewa ajira haraka, siyo kwa watoto wa vigogo peke yao.

Nawasilisha!!
 
Binafsi naona cha kujivunia hapa ni safari za Kikwete na ujinga wetu wa kukubali kudanganywa kila kukicha kuwa sie ni wapole na wapenda amani kwani tunaibiwa na viongozi huku tukifurahi.
 
tulichofanikiwa ni nidhamu ya woga tuliyokubalishwa na serikali bado waTanzania tumo ndani ya ukoloni
Kwanini tuliweza kumpeleka mkoloni mzungu mpaka lego na UN tushindwe eti kumshitaki Raisi alietoka hapa Tanzania? Bado tunatawaliwa Raisi ni mfalme haezi kushitakiwa kwa kosa lolote akiwa madarakani na baada ya madaraka
Ndio tumekuta tunarudi nyuma kila siku kwani hakuna uwajibikaji, hakuna nchi ambayo unachaguliwa mbunge masikini baada ya miaka mitano unakuwa tajiri kama Tanzania
Maendeleo tutayasikia kwenye redio tena sio ile ya mkulima
 
Ndugu Mtoa mada nashukura sana kwa mada nzuri sana uliyoitoa hapa jamvini tuichambue tupike mwanye kuila na ale na asiyetaka kula atuachie wenye meno tuile. Kwa sisi Watanganyika ambao nchi yetu ilifariki miaka miwili na miezi mnne baada ya kuzaliwa jambo kubwa tunalojivunia si lingine ila ni kwamba TUNASHUKURU WALIOFANYA HIVYO KUIUA TANGANYIKA WALITUACHIA UHAI WETU. Siku moja wakati niishi Buguruni maeneo fulani nilishuhudia jamaa mmoja akikabwa na vibaka wakimuamuru awape pesa, wakiwa wanafanya hivyo walikuwa wamemkaba shingo kisha akalalamika sana, kibaka mmoja akamwambia mkabaji legeza kidogo mkono. Yule jamaa akawaambia "KILA KITU CHUKUENI NIACHIENI ROHO YANGU"

Hiki ndicho ninachoweza kusema kwamba NASI WATANGANYIKA TUNASHUKURU SANA KWA KUACHIWA ROHO ZETU HAI.

TUNAHITAJI MABADILIKO AMBAYO NCHI HII INATAKIWA KURUDI KATIKA UPYA WAKE KISERA.
SERA MAMA NI AZIMIO LA ARUSHA TU.
 
Nimesoma maoni wa wana JF humu wengi wao hawajui history ya Tanzania,, uhuru wa tanganyika wanaita tanzania, labda munipe hoje ya uhuru wa tanzania ilipata mwaka gani ?

mi najua kuna jamuhuri ya muungano wa tanzania, ambao ni tanganyika na zanzibar 1964 na tanzania ilikuja mwaka 1977 kikatiba inavyotambulika kimagumashi.

Neno Muungano kwa english ni union , na tanzania ni jina la union au muungano, leo hii zanzibar wakichukua mbao zao ambazo zimo ndania ya Tanzania Tan -Tanganyika , Zan - zanzibar ,ia wanasema ni kiburudisho tu kama wimbo..

Jiulize zanzibar wakichukua Zan yao uhuru wa tanzania mtajivunia wapi ? Ni aibu kwanu shame on you guys.

Musipoteze history ya nchi yenu Tanganyika,kama viongozi wanaficha kuwa Tanganyika ndio Tanzania basi watamke wazi ili wazanzibari wafahamu, ni sawa zaire kuita kongo.
 
Back
Top Bottom