Tunaposheherekea miaka takribani 50 ya uhuru wa Tanganyika, tunajivunia nini?

Je, uhuru tulioupata mwaka 1961 umetusaidia kujikwamua na maadui watatu?

  • Ndiyo

    Votes: 1 6.7%
  • Hapana

    Votes: 14 93.3%

  • Total voters
    15
ndo maana tukawa maskini, na tutaendelea kuwa maskini. kwasababu hata mawazo yetu ni ya kimaskini..hivi kuadhimisha siku ya uhuru ni kushabikia gwaride, au ni kuangalia jinsi wanajeshi wanavyopiga miguu uku jasho likiwatoka..
nilitegemea siku ya leo vyomba vya habari vingekuwa vinatoa mstakabadhi wa nchi hii yenye ufisadi, kutoa fikra zao kuhusu katiba mpya.. eti kila mtu anasimulia, mizinga 21 inapigwaa..AIBUU..

siku za nyuma, nilikua naangalia maadhimisho ya siku ya uhuru INDIA.
kila mtu alikuwa anangelea mwenendo mzima wa taifa lao, hasa kwenye sector ya ajira na elimu.
vyombo vya habari vilitilia msisitizo sana swala la elimu in-relation na miaka yao ya uhuru. na kuibana serikali iongelee maswala hayo muhimu.
leo hii india wanaongelea nishati ya nyukilia, ambayo itawezesha nchi kupata umeme wa kutosha.
lakini sisi miaka 49 ya uhuru, vyomba vya habari vinaongelea gwaride, wakati hiko kitu kinafanywa kila mwaka...AIBUu
tunaonyesha ulinzi wetu na jeshi letu lilivyoimala ili tusivamiwe na wabaya wa ccm! wanaotaka chama chetu kielekee kubaya!
na umeme tunakumbuka kuwa NI ANASA KUTUMIA UMEME!
MAJI ya nini wakati mtachota mitoni!
ELIMU hahahaha mnataka mtutoe madarakani eeeh!
 
Uhuru ule ulikuwa ni kumtoa mkoloni mweupe na kumwingiza mkoloni mweusi-NDIVO NINAVYO MMI
 
Hizi sherehe tangu nilipoacha mambo ya chipkizi early eighties siyajui tena!
 
Najarabu kuangalia S. Africa, Botswana na kwingineko ambako uhuru ulichelewa naona tofauti kubwa ya kimaendeleo ya miundo mbinu, Afya, Elimu, na maendeleo binafsi namaanisha ya mifukoni na mengine kibao inanitosha kabisa kuamini kuwa uhuru wetu wa miaka 49 hauna maana kwa nilio wakuta walioko na hata kwa watoto wetu pia kama tutakuwa tunaendelea kwa mtindo huu tulio nao hapa Tanzania na baadhi ya nchi za kiafrica.

Nina maswali mengi ambayo ni tata sana

Je ni kweli hatukuwa tumekomaa kuweza kujitawala na uhuru wetu?

Je ni kweli hatuna rasilimali za kutosha kuweza kusogea mbele kimaendeleo?

Je ni kweli matumizi yote tunayoyafanya kwenye serikali zetu ni muhimu na yanaendana na hali zetu?

Je ni kweli bado hatujaelimika vya kutosha kuweza kuacha makosa yetu yaliyopiata na tujirekebishe?

Je ni kweli kwa nchi ambayo ina ardhi yenye rutuba ya kutosha na ya pili kwa ufugaji barani Africa kuna ulazima mtanzania kuishi chini ya dola moja kwa siku?

Kama tulitawaliwa na Mwingereza na kuiga mambo mengi kutoka kwao hivi ni vigumu sana kuitumia japo katiba yao (copy & paste) tutoke hapa tulipo?

Hivi ni lazima kuwa na magari katika serikali yetu ya gharama kubwa na matumizi makubwa ya mafuta ambayo sidhani hata nchi matajiri kama wanayatumia

Nina maswali mengi sana ambayo siwezi kupata majibu yake kwa nchi ambayo ni ya tatu kwa kuwa rasimali za asili baada ya Congo DRC. Na Angola ambao wao wana kisingizio cha vita!

Najiona mtumwa kwenye nchi yangu hasa nikiona mtu anakodisha toroli kubebea mgonjwa kumpeleka hospitali mjini na wengine kujifungulia njiani.

Tumekuwa kama mtoto mdogo wa miaka 4 aliyekabidhiwa gari abebe abiria kutoka Dar kwenda Mwanza huku akiamini analiendesha vizuri na hataki kukosololewa wala kuelekezwa au kumpisha mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na uwezo zaidi yake.

Ninauona utumwa mkubwa na matabaka ya ajabu katika nchi hii huku tunajifariji kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na bora tukae hivi na amani yetu ya utumwani maana tuliyowanyang'anya wakoloni tumewarudishia kwa njia ya kuwaita wawekezaji kwa njia nyingine na hawa wa sasa ni wabaya sana maana hawajengi nchi zaidi ni kuhamisha mali zilizoko kwa kushirikiana na viongozi wa serikali.

WANAJAMII NAOMBENI MCHANGO WENU SIONI MAANA YA UHURU KWANGU.

Pole sana ndugu yangu,I understand your concern.Lakini we have never been free after all. Napenda uelewe kwamba wewe sasa hivi ni mtumwa wa hiari na utumwa huu ni mbaya kwa vile hujui kuwa ni mtumwa.Hata leo wakikuambia you are free hutawaelewa because after all you do not know that you are a slave.Wanatumia soft power badala ya physical power kutuingiza mkenge.Tunafanya wanayotaka kwa kutumia indocrination ( TV,the Internet etc.) and mind control techniques.The space is full of satellites for this work.Tunajidanganya kwamba what we do ni mawazo yetu lakini actually ni mawazo yao.We are actually their zombies.This is the truth and frightening truth indeed.
 
jamaa ana smile tu pale mbele km wa tz hawana shida. mwalim wangu wa english form 1 alijuwa ni mmarekani akiitwa miss claire, tarehe km ya jana yaani tar 8 alikuja na bendera ya tz na marekani akijua kwa vile tar tisa ni mapumziko basi atleast tar 8 wanafunzi na walimu wangekuja na bendera ya nchi kuonesha uzalendo lkn hakuna ht mbongo mmoja aliyekuja na angalau na bendera ya tz akiwauliza walimu wanamjibu eti huruhusiwi kuwa na bendera ya taifa wakati ule akazidi kuchanganyikiwa, sana sana alichoshangaa ni watu eti wako happy kupumzika kazi akasema africa will remain poor forever. tarehe yenyewe ya uhuru akipita barabarani akashangaa haoni ht bendera zikipepea watu wakamwambia viongozi ndo wanaoufaidi huo uhuru na sio mlalahoi.
 
tunaonyesha ulinzi wetu na jeshi letu lilivyoimala ili tusivamiwe na wabaya wa ccm! wanaotaka chama chetu kielekee kubaya!
na umeme tunakumbuka kuwa NI ANASA KUTUMIA UMEME!
MAJI ya nini wakati mtachota mitoni!
ELIMU hahahaha mnataka mtutoe madarakani eeeh!

Hahahahaha nimeipenda hiyo mkuu!
 
Maana ya uhuru haipo tena, gap ya walio nacho na wasionacho imeongezeka sana na matokeo yake imekuwa ni udhaifu mkubwa kwa kutoa huduma katika elimu, afya na huduma zingine za jamii. Siku hii ilikuwa muhimu kutafakari hayo yote na kujiuliza kama tumepiga hatua ama la. Pengine ingetulazimu kuomboleza badala ya kusherehekea.
 
WANA JAMII
Tuna utafsirije UHURU huu TANGANYIKA, kiuchumi,kimaisha na kimaendeleo? Maana mie siuelewi kabisa tunacho elezwa kila kukicha ni Amani na Utulivu ndio basi.........?
 
hii yote ni kudhiirisha akuna tulichopata cha kujivunia zaidi ya gwaride na vjana wa alaiki kila mwaka jambo hlo hlo tu hii ni aibu yao wenyenyewe mafisadi
 
Sahihisho NI UHURU WA TANGANYIKA SIYO UHURU WA TANZANIA.

Tanganyika huru ilikuwa ya maziwa na asali elimu bure, afya bure, maisha nafuu (mfano kilo ya sukari chini ya senti 75 yaani 0.75 ya shilingi).

Hakukuwa na na neno ufisadi; uchumi ulikuwa bora angalau hadi 1972. Uliweza kusafiri na shirika reli nchi nzima ukitumia mabasi na reli ya TRC. Kuliibuka Wahujumu uchumi na walishughulikiwa (Na Marehemu Sokoine). Kulikuwa na Azimio la Arusha ambayo ni Dira ya Utanzania (tangabyika)

Kulikuwa na Jeshi la Kujenga Taifa lililokuwa chuo cha uzalendo, ukakamavu, ujasiri nk.

Mwalimu Nyerere alikuwa anaweza kuwakemea Marekani kwa maslahi ya watu wanaoonewa hadi akawaingiza China UN. Tulikuwa ngome ya wapigania uhuru dunia nzima.

Machozi yananilengalenga kwa tunu iliyopotea ni muhimu kukumbuka siku ya uhuru. Maisha mabovu na huria kwa kila Mtanzania.
 
Katika kumbukumbu zangu,TZ hamna popote panapoonesha ilishawahi kupata uhuru.Uhuru ulikua wa Tanganyika,kwa maana hiyo uhuru wa 9/12/1961 ni wa Tanganyika na sio Tanzania,ieleweke hivyo.Zanziba wao wajanja ikifika siku ya Mapinduzi wanaadimisha kivyao,ila watanganyika hawana chao.Kama kuna mtu anabisha atueleze hapa Tanzania ilipatikana baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar,sasa je uhuru huo ulipatikana wapi na kutoka kwa nani?
 
Katika kumbukumbu zangu,TZ hamna popote panapoonesha ilishawahi kupata uhuru.Uhuru ulikua wa Tanganyika,kwa maana hiyo uhuru wa 9/12/1961 ni wa Tanganyika na sio Tanzania,ieleweke hivyo.Zanziba wao wajanja ikifika siku ya Mapinduzi wanaadimisha kivyao,ila watanganyika hawana chao.Kama kuna mtu anabisha atueleze hapa Tanzania ilipatikana baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar,sasa je uhuru huo ulipatikana wapi na kutoka kwa nani?
 
Sioni tatizo hapo, kwani kuna aliedai kuwa leo ni uhuru wa Tanzania? huyo atakua anamchokoza Mtumishi Mtikila
 
Zanzibar ilipata Uhuru wake December 10, 1963 na ilikua mwanachama wa UN pia wakati huo baadae ndio yalitokea hayo mapinduzi na baada ya hapo muungano uliozaa Tanzania. Si sahihi kusema Desemba 9 ni uhuru wa Tanzania.
 
Tanganyika haijawahikupata uhuru, tulimfukuza mkoloni mzungu akaja mkoloni mweusi ndio mbaya kuliko mzungu. mkoloni mweusi anaua kila kitu mpaka maisha ya watu wa kawaida, hajengi ni muharibufu kuliko mkoloni mweupe. Bora tungezidi kutawaliwa na mkoloni mweupe kuliko mweusi mwizi, mmbabe, hana elimu ya kufikiria, mpumbavu, muonevu na kila kitu anajua yeye. je lini watanganyika tutapata Uhuru wetu au ndio tutatawaliwa na hawajingajinga mpaka lini?
 
Nilikuwa naangalia TBC kipindi maalumu kinachoonesha tulikotoka ambapo hata msimuliaji anasikika akieleza kuhusu our past. Kwamba Tanzania ndio ilikuwa mzalishaji mkuu wa Viko duniani. Maelezo haya yamenitisha sana na kujikuta nikijiuliza, hivi kwa sasa tuko wapi? Where are we?
 
Back
Top Bottom