Tunaposheherekea miaka takribani 50 ya uhuru wa Tanganyika, tunajivunia nini?

Je, uhuru tulioupata mwaka 1961 umetusaidia kujikwamua na maadui watatu?

  • Ndiyo

    Votes: 1 6.7%
  • Hapana

    Votes: 14 93.3%

  • Total voters
    15
We have made a lot of progress since independence. Roads, airports, ports, hospitals, railways and universities have been built.
Education has been for decades offered for free.
We have witnessed the massive influx of foreign investments.
Mushrooming of tv and radio stations, and newspapers as well.
The economy has been growing at a very steady rate making it among the fastest growing in subsaharan Africa.
Music and enternainment industry has been growing and thus, new generation of local artists (Bongo flavor)
Telecom sector has made a lot of progress, making Tz a lucrative market for cellular phones, 2nd only to South Africa in the continent.
Tourism is booming.
Real estate is booming, though i suspect it will go bust in the next few years.
Kilimo kwanza, MDG, Saccos, and so many things.
So we are not in the dark
 
on coming holiday ya kusherehekea 49 yrs of uhuru kuna baadhi ya watu wanadai eti bado ni nch changa! mi nashindwa kuelewa tanzania ni nchi changa au watu wake ndo wanafikra changa!
 
i cant blieve ninachokiona! yani for this yrs bado tuna tatizo la umeme na maji! haswa hili la maji yani gas wameitoa kilwa mpaka dar lakini just kutoa maji from rufiji water bed inawashinda mpaka some pple wamakufa kiu places like kisarawe
 
Ndugu wana JF kwanza napenda kuwashukuru kwa michango mizuri na ya msingi sana katika kuleta mabadiliko ya kweli katika kumkomboa mtanzania.Lakini pamoja na hayo yote naomba kuuliza swali lifuatalo:" hivi hata baada ya miaka 49 ya uhuru bado watanzania tupo gizani?"Ndugu zangu watanzania bado hutuwezi kuona kinachoendelea katika nchi yetu hii.Kwa mfano leo hii watanzania wanafurahia net za bure zilizogawiwa hivi karibuni,hivi nyuma ya pazia la net hizi za bure kuna nini?Nakumbuka aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA DR.W.Slaa akiwa kwenye kampeni mkoani Kagera mjini Bukoba alitoa kauli ifuatayo" Rais Kikweti anapokuwa ktk ziara nje ya nchi wakati wa kurudi akiwa hewani kwenye ndege anapishana wenzake nao wakiwa hewani kwenye ndege wakati yeye anarudi na NET kwenye ndege wenzake wanarudi kwao DHAHABU kutoka kwake"

Naomba tusiwe tunakubali vitu bila kujiuliza nyuma kuna kitu kimejificha matokeo yake tunapewa net halafu wao wanabeba rasirimali zetu kama madini(URANIUM,GOLD etc).Naomba watanzania tufunguke macho nchi hii yetu ndio maana Mungu ametupa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
MAGEUZI YA KATIBA NI LAZIMA.

Tanganyika haijapata uhuru wake, ndiyo tupo kwenye harakati za kudai uhuru wetu, na kupatikana kwake ni mpaka chadema iingie madarakani.
Uhuru tulionao ni wakutembea barabarani, na kulala kitandani, pamoja na uhuru wa kuzaana kama wanyama.
Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Afrika.
 
Habari za asubuhi wapendwa wanaJF, Hivi punde nimeamka nikiwa salama namshuruku Mungu kwa nijaalia kuiona siku ya leo. Lakini nina masikitiko makubwa jamaa wamechukua umeme wao na sikuwahi kupiga pasi. Inamaana leo nitasherekea sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika bila umeme.
 
Na siku tutakayopata uhuru,wahindi na waarabu pamoja na ccm yenu mtakiona cha mtema kuni
 
Hata hivyo tujipongeze mkuu tumezaa sana kipindi cha uhuru tulikuwa 11m sasa tunakaribia 42m.
 
LEO tunaadhimisha miaka 49 ya Uhuru tukiwa na jambo moja kubwa la kujivunia ambalo ni umoja wa taifa letu. Umoja wetu ulisukwa katika misingi ya kujenga taifa moja lisilokuwa na matabaka, ukabila wala udini, lakini kidogo kidogo misingi hiyo ikaanza kukiukwa, kwa kuanzia na kuwapo kwa matabaka ya walio nacho na wasio nacho. Pengo baina ya masikini na matajiri likawa kubwa, hapo ndipo watu wakaanza kuhoji kulikoni? Ule ukabila na umajimbo uliokuwa ukipigwa vita mara baada ya uhuru, sasa unaibuka kwa kasi kubwa. Udini nao umeanza kujenga mizizi yake taratibu.

SWALI JE UHURU WETU NA SIFA YETU YA TANZANIA YA AMANI UTADUMU TENA...?
 
Najarabu kuangalia S. Africa, Botswana na kwingineko ambako uhuru ulichelewa naona tofauti kubwa ya kimaendeleo ya miundo mbinu, Afya, Elimu, na maendeleo binafsi namaanisha ya mifukoni na mengine kibao inanitosha kabisa kuamini kuwa uhuru wetu wa miaka 49 hauna maana kwa nilio wakuta walioko na hata kwa watoto wetu pia kama tutakuwa tunaendelea kwa mtindo huu tulio nao hapa Tanzania na baadhi ya nchi za kiafrica.

Nina maswali mengi ambayo ni tata sana

Je ni kweli hatukuwa tumekomaa kuweza kujitawala na uhuru wetu?

Je ni kweli hatuna rasilimali za kutosha kuweza kusogea mbele kimaendeleo?

Je ni kweli matumizi yote tunayoyafanya kwenye serikali zetu ni muhimu na yanaendana na hali zetu?

Je ni kweli bado hatujaelimika vya kutosha kuweza kuacha makosa yetu yaliyopiata na tujirekebishe?

Je ni kweli kwa nchi ambayo ina ardhi yenye rutuba ya kutosha na ya pili kwa ufugaji barani Africa kuna ulazima mtanzania kuishi chini ya dola moja kwa siku?

Kama tulitawaliwa na Mwingereza na kuiga mambo mengi kutoka kwao hivi ni vigumu sana kuitumia japo katiba yao (copy & paste) tutoke hapa tulipo?

Hivi ni lazima kuwa na magari katika serikali yetu ya gharama kubwa na matumizi makubwa ya mafuta ambayo sidhani hata nchi matajiri kama wanayatumia

Nina maswali mengi sana ambayo siwezi kupata majibu yake kwa nchi ambayo ni ya tatu kwa kuwa rasimali za asili baada ya Congo DRC. Na Angola ambao wao wana kisingizio cha vita!

Najiona mtumwa kwenye nchi yangu hasa nikiona mtu anakodisha toroli kubebea mgonjwa kumpeleka hospitali mjini na wengine kujifungulia njiani.

Tumekuwa kama mtoto mdogo wa miaka 4 aliyekabidhiwa gari abebe abiria kutoka Dar kwenda Mwanza huku akiamini analiendesha vizuri na hataki kukosololewa wala kuelekezwa au kumpisha mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na uwezo zaidi yake.

Ninauona utumwa mkubwa na matabaka ya ajabu katika nchi hii huku tunajifariji kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na bora tukae hivi na amani yetu ya utumwani maana tuliyowanyang'anya wakoloni tumewarudishia kwa njia ya kuwaita wawekezaji kwa njia nyingine na hawa wa sasa ni wabaya sana maana hawajengi nchi zaidi ni kuhamisha mali zilizoko kwa kushirikiana na viongozi wa serikali.

WANAJAMII NAOMBENI MCHANGO WENU SIONI MAANA YA UHURU KWANGU.
 
tena mkoloni huyu mweusi ni mbaya sana hana hata huruma na ndugu zake weusi maana anahakikisha anakubana kila kona halafu hakuletei maendelo wala hajengi nchi utafikiri sio nchi yake, inasikitisha sana kuwa na watu wasio na huruma na nchi
 
Bora wakoloni na babu zetu walikuwa wanaipenda tanganyika kuliko "sisi" tunavyoitenda nchi hii.

Babu zetu wanambiwa walikuwa "wajinga" kwa kubadilisha Goroli na almasi. wao walihitaji mawe yaliyochongwa vuzuri au kuwa na sura nzuri kwa ajili ya kuchezea bao, kwao ambao hawakuliona darasa, bao ndicho walichokuwa wakihitaji.

Leo watu wetu wenye shahada zao Lukuki wanavutia wawekezaji wa madini ambao baada ya kuingia nchini wanatupatia vyandarua!

Ukiwaangalia watawala wetu wa sasa, unasema bora, wakoloni!. Pale Mwadui walipogundua almasi, serikali wakoloni ilikuwa na hisa ya asilimia 51 na mwekezaji ambaye ndiye aliyetoa mtaji n.k aliachiwa asilimia zilizobaki. nauliza swali kati ya watawala wetu wa sasa na wakoloni nani aliipenda nchi hii?

Je Treni aliyoiacha mkoloni mwaka 1961 iko katika hali gani, watawala wetu wa sasa wanaipenda nchi hii kuliko wakoloni au wakoloni waipenda kuliko wao
 
ndo maana tukawa maskini, na tutaendelea kuwa maskini. kwasababu hata mawazo yetu ni ya kimaskini..hivi kuadhimisha siku ya uhuru ni kushabikia gwaride, au ni kuangalia jinsi wanajeshi wanavyopiga miguu uku jasho likiwatoka..
nilitegemea siku ya leo vyomba vya habari vingekuwa vinatoa mstakabadhi wa nchi hii yenye ufisadi, kutoa fikra zao kuhusu katiba mpya.. eti kila mtu anasimulia, mizinga 21 inapigwaa..AIBUU..

siku za nyuma, nilikua naangalia maadhimisho ya siku ya uhuru INDIA.
kila mtu alikuwa anangelea mwenendo mzima wa taifa lao, hasa kwenye sector ya ajira na elimu.
vyombo vya habari vilitilia msisitizo sana swala la elimu in-relation na miaka yao ya uhuru. na kuibana serikali iongelee maswala hayo muhimu.
leo hii india wanaongelea nishati ya nyukilia, ambayo itawezesha nchi kupata umeme wa kutosha.
lakini sisi miaka 49 ya uhuru, vyomba vya habari vinaongelea gwaride, wakati hiko kitu kinafanywa kila mwaka...AIBUu
 
Bora wakoloni na babu zetu walikuwa wanaipenda tanganyika kuliko "sisi" tunavyoitenda nchi hii.

Babu zetu wanambiwa walikuwa "wajinga" kwa kubadilisha Goroli na almasi. wao walihitaji mawe yaliyochongwa vuzuri au kuwa na sura nzuri kwa ajili ya kuchezea bao, kwao ambao hawakuliona darasa, bao ndicho walichokuwa wakihitaji.

Leo watu wetu wenye shahada zao Lukuki wanavutia wawekezaji wa madini ambao baada ya kuingia nchini wanatupatia vyandarua!

Ukiwaangalia watawala wetu wa sasa, unasema bora, wakoloni!. Pale Mwadui walipogundua almasi, serikali wakoloni ilikuwa na hisa ya asilimia 51 na mwekezaji ambaye ndiye aliyetoa mtaji n.k aliachiwa asilimia zilizobaki. nauliza swali kati ya watawala wetu wa sasa na wakoloni nani aliipenda nchi hii?

Je Treni aliyoiacha mkoloni mwaka 1961 iko katika hali gani, watawala wetu wa sasa wanaipenda nchi hii kuliko wakoloni au wakoloni waipenda kuliko wao
Tatizo wakoloni wa sasa hawafanyi unyonyaji endelevu wanachoangalia ni kuchota leo hajiulizi kesho mwanaye atachota nini ?
 
Wakoloni waliomo CCM ni wabaya kuliko mjerumani aliyetuchapa kiboko. Je huyu anayeiba rasilimali zote, si ni mbaya zaidi?
 
hizi ndo aibu za TZ..
eti mtangazaji anajisifia sio lazima kwenda cHINA kujifunza Kiduku.
kweli hii nchi ya aibu
 
mi nilihisi hii ndo fursa kuwaelimisha wa-TZ kuhusu muktabadhi wa nchi yao.
sio kuwaambia maana ya mizinga 21, hivyo vitu vimepitwa na wakati, kwenye kizazi hiki cha utandawazi
 
Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni mwaka 1961! Toka pale mwalimu Nyerere alitangaza vita dhidi ya maadui watatu wakubwa: Ujinga, Umaskini na maradhi. Leo sisi baada ya miaka 49 tunapigana na maadui wakubwa wanne: Ujinga, Umaskini, Maradhi na Rushwa! Tutafakari kama huu uhuru tuliopata toka kwa mkoloni yule umetusaidia kuboresha maisha ya Watanganganyika au Watanzania wote. AU Uhuru ule ulikuwa ni kumtoa mkoloni mweupe na kumwingiza mkoloni mweusi. Hii inasema hivi kwa kuwa lengo kubwa la mkoloni lilikuwa kutunyonya na kunufaisha nchi yake Uingereza. Mweusi mwezetu anajinufaisha mwenyewe na tumbolake na familia yake. Mwalimu Nyerere aliwahi kuandikia mawaziri wake wote kuwaonya juu ya "ujiko" kwa kuwa na misafara mikubwa isiyo na maana maana hiyo inamaliza mali za wananchi! Je, leo misafara vipi! Baba, mama, na watoto- wote misafara mikubwa- wananchi kazi yao kupiga makofi.
Watu wanaona hayo yote lakini wanaogopa maana wanataka kupalilia kibarua chao! Kweli Watanzania tubadilike ili tuone matunda ya uhuru wetu.
 
Back
Top Bottom