Tunapopangiana kula

Tunapopangiana kula

Duh umetaja vyakula ambavyo bibi yangu kila uchao ndo alikuwa anapika (Kiburu na Ngararimu).Kwa uhalisi huwezi kupanga ratiba ya( chakula cha usiku) hata kwenye mafundisho ya ndoa tuliambiwa yaani ni hapo hapo unapojisikia ilimradi pawe ni mahali salama,hadhi na usiri.Popote iwe bafuni panafaa na mie huwa nachapa tu ikitokea babu anadai kuonana na bibi(Mkeku).Ilo suala ni body emotions zaidi kuliko akili nashinwa kujua kwanini bwana kaka amwabie bi-dada maneno.Ila akijaribu tu ku-practise ameliwa wewe mwambie bi-dada ANIDIPU nije nipige DEIWAKA yaani nimshikie gari kwa muda wakati tunamsu biri dereva/konda aliyeajiriwa kwa kazi hiyo. nyambaf yeye analeta style za kuambiwa na akili za kushikiwa...

nimependa huu ushauri wako maaana ni three kama sio two in one.
1. umerefer thread 1 ilosema "kufanya mapenzi maeneo hatarishi" kama sikosei ambapo mengi yalisemwa so naona na wewe pia uliweka kwenye consideration.
2. umeweka na disadvantages za hiyo ratiba.
3. umeweka na solution kabisa na wewe ukiwa ndio instrument ya hiyo solution (kuomba deiwaka)
haya mkuu all the best ila usije ukagonga ukuta tu.
 
Mambo ya shake well before use hayo....!!!!!!

Lakini pamoja na ubunifu mnaodai unaboresha tendo hilo mbona kila uchao linawakinai wanandoa na kukimbilia nje?
Kulikoni?
Hhahah Eiyer, kuna evidence kuwa kila atokaye ni kwa sababu amekinai alicho nacho? Ana uhakika gani kuwa akikfuatacho nje kitakuwa mswano? Wala wengine ni hulka tu, anafanya safari za Vasco Da Gama au Livingstone.....................
 
Last edited by a moderator:
Hhahah Eiyer, kuna evidence kuwa kila atokaye ni kwa sababu amekinai alicho nacho? Ana uhakika gani kuwa akikfuatacho nje kitakuwa mswano? Wala wengine ni hulka tu, anafanya safari za Vasco Da Gama au Livingstone.....................

Mama,sijasema kila atokae amekinai bana

Nimesema mbona wapo wanaojituma lakini watu wanakinai na kukimbilia nje

Kile cha nje sina uhakika kuwa ni mswano ila ni katika harakati ya kutafuta ridhiko tu

Hapo kwa Vasco Da Gama sina la kuongeza kwakuwa wapo wa aina hiyo pia

Lakini mapenzi na upendo ni kama hauna mwenyewe siku hizi
Hakuna cha masikini au tajiri
Wote tunalia kilio kimoja tu

Tena wakati mwingine sisi masikini ndio angalau tunayafaidi kuliko wale walio na mali na mipesa
Wale nao wanakua na matatizo mengi sana
Unaweza kunieleza kinachowasibu hao wenye hela na wanalia mapenzi wakati sisi tunaamini ukiwa na hela unayafaidi zaidi mapenzi?

Na hawa kukinau kwao ni zaidi sana,kwanini?
 
Kichwa cha chini hakina mda wa kufuata ratb, mpk kujamba mnaweza kupeana masharti
 
Nilikuja kuelezwa hili na dada mmoja ambae nieafiki yangu kama na mimi nalijua hili

Ni kwamba huyu dada mume wake amemuambia kuwa kuanzia jana hawatakuwa wanakutana kimwili bila ya kuwa na ratiba maalum,yaani kama vile ambavyo wanaweza kupanga ratiba ya chakula yaani leo tunakula ngararimu na ijumaa tutakula kiburu basi itakuwa hivyo na kwenye suala la unjumba

Dada huyu ameniambia kuwa hali hiyo haipendi na kwa kuwa ananiheshimu ameamua kuniambia hayo ili kama na mimi nakubaliana nalo ama la

Ki ukweli mimi nilimuambia jambo hilo sidhani kama linafaa kwa kuwa kwa mtazamo wangu wa harakaharaka ni kwamba kulipanga kutalifanya liwe linabore hivi

Kitendo cha kujua kesho nitakula kiburu kunakifanya chakula hicho kipoteze ule "utam" wake wa asili

Nilimueleza umuhimu wa kuliongelea hilo suala kwa upole na mumewe na ajitahidi sana kutokuonesha hasira kwani anahisi mumewe amekuwa na nyumba ndogo

Sasa hebu niambieni nyie mnalionaje suala hili la kupanga ratiba je ni jema au halifai?
Nisingependa tumjadili huyo jamaa kwakuwa sio lengo langu kuleta mada hapa
Lengo langu ni kujaribu kulitazama hili suala la kupanga ratiba ya unyumba kama linafaa ama halifai!

Karibuni nyote......!!!!!!!

mambo ya ratiba tena?

huyo jamaa ni ticha nini!!

aisee sie twaenda kwa counter attack bwana!!

huyo jamaa anatakiwa aundiwe tume!!!!!

si bure, ana lake limemganda!!!
 
Mambo ya shake well before use hayo....!!!!!!

Lakini pamoja na ubunifu mnaodai unaboresha tendo hilo mbona kila uchao linawakinai wanandoa na kukimbilia nje?
Kulikoni?

Wakati mwingine nahis uvumilivu haupo na penzi la dhati kati ya wahusko halipo, kama penzi la kutoka moyon linakuwepo hata kama utapikiwa makande ndio iwe sababu ya wewe kukimbia nyumbani na kwenda kula kwa jiran, utajitahidi kuongea ili diet iwe inabadilishwa
 
mambo ya ratiba tena?

huyo jamaa ni ticha nini!!

aisee sie twaenda kwa counter attack bwana!!

huyo jamaa anatakiwa aundiwe tume!!!!!

si bure, ana lake limemganda!!!

Counter atack?
........LOL!

Umenichekesha sana leo!
 
Wakati mwingine nahis uvumilivu haupo na penzi la dhati kati ya wahusko halipo, kama penzi la kutoka moyon linakuwepo hata kama utapikiwa makande ndio iwe sababu ya wewe kukimbia nyumbani na kwenda kula kwa jiran, utajitahidi kuongea ili diet iwe inabadilishwa

Uko kwenye ndoa?
 
Ha,ha,ha,ha,ha,haaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa unakuwa umechoa na kitu gani?

Ofisi mkuu na majukumu mengine ya kimaisha bila kusahau mimi ni mke na mama pia. Majina yote hayo yanakuja na majukumu yake
 
Back
Top Bottom