Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,077
Kwa uchafu uliotokea, kwa kadiri ya report ya CAG ilivyoweka wazi, na namna baadhi ya Mawaziri walivyojitahidi kuulinda uovu huo kwa kauli na vitendo; kama Rais anauchukia uovo, Watanzania wanatarajia kupata baraza jipya la Mawaziri hivi karibuni.
Nchi hii, kama ambavyo mara nyingi, wengi wetu tumesema, inashindwa kuwa na maendeleo ya kuridhisha kwa sababu ya kukosekana uongozi thabiti maeneo mengi ya Serikali na taasisi zake. Mbaya zaidi, viongozi walio wengi, wamezifanya ofisi zao kuwa madanguro ya kuporea pesa za umma. Na wengi wao, uwezo wao wa kutenda kazi ni duni sana lakini ni mabingwa wa wizi na ufisadi. Fikiria mtu anayezalisha kidogo sana, lakini anaiba sana. Hawa watu ni hasara kubwa kwa Taifa.
Sasa ni wakati wa serikali kuongozwa na watu wanaojua kutenda kuliko wanaojua kuiba na kupiga porojo.
Viwanda, apewe mtu anayevijua viwanda, mtu mwadilifu anayezijua changamoto zinazozuia viwanda vingi kujengwa Tanzania.
Kilimo apewe mtu anayekijua kilimo. Anayezijua changamoto zake kisahihi.
Wizara zinazohusika na ujenzi wa uchumi kama vile Wizara ya Fedha, Uchumi na mipango; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Madini; Kilimo na Uvuvi; pamoja na Wizara zinazotengeneza mazingira ya kuwezesha sekta za uchumi kustawi, kama vile Wizara ya sheria; Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje; Wizara ya Maji; Wizara ya Nishati; na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, hizi zote wapewe watu ambao wanayajua maeneo hayo vizuri, na wawe wanajua uzito wa sekta hizi katika kuwezesha uchumi kukua.
Tunafahamu changamoto anayokutana nayo Rais katika kuwapata watu wanaofaa, kwa sababu katiba inamlazimisha awateua kutoka miongoni mwa wabunge, na bahati mbaya wabunge waliopo ndio hao ambao hawakuchaguliwa na wapiga kura, na wengi wao wanachojua ni kugonga tu meza na kusema NDIYOO.
Katika kuondokana na tatizo hili, wabunge wote wa kuteuliwa, wapewe uteuzi wa kufanya kazi nyingine za Serikali, halafu wajiuzulu ubunge. Rais awateua watu wenye uwezo na waadilifu kuwa wabunge, ndio washikilie Wizara zote muhimu. Hawa wabunge bandia wanaweza kupewa wizara kama za utamaduni, wanawake na watoto, na mazingira,