Tunaonewa sana

Tunaonewa sana

Nimewahi pia kuwaza hivi
Mungu na shetani ni nguvu pinzani
Sisi pia ni chakula chao

Mungu ameumba binadamu (amepanda mazao) tunapokufa tukiwa wema roho zetu zinaungana na Mungu yani ndiyo chakula sasa anapata nguvu zaidi ndiyo maana tunaimizwa wema tumpendeze Mungu

Shetani ni muharibifu wa mazao tukifa katika maovu tunamfaidisha shetani au tunakuwa chakula chake anapata nguvu zaidi ambazo ni pinzani kwa Mungu
 
Nadhani mleta mada anataka tuchambue ..kwamba ..baada ya kuwa tumejua sisi ni mifugo so kipi kifanyike?nadhani anataka tumcontorl mungu na shetani ...yani binadamu awe na nguvu zaidi kumshinda mungu na shetani...

Nadhani anataka kuweka point ya tunafanyaje ili tuwe na nguvu zaidi ya mungu na shetani?
itabidi tule tunda lingine hakuna namna
 
Hata hao wanaona pia
tapatalk_316291206_720x629.jpg
 
Habari zenu mifugo ya Mungu na Shetani? Naona mnazidi kusukuma siku mkingoja kuliwa tu.

Nimegundua kitu kuwa kila kinachofugwa huwa akiruhususiwi kujua dhima na dhamira ya yule aliyekifuga.

Yaani ni hivi binadamu hata afanye nini hatoweza kujua dhamira na dhima ya yeye kufugwa hapa duniani.

Kama ilivyo kwa kuku na ng'ombe, hata wafanye nini hawatoweza kamwe kujua dhamira na dhima ya wao kufugwa na binadamu.

Ebu fikiria Kuku, ng'ombe na mbuzi wanatuchukuliaje sisi binadamu?

Wanatuona sisi ni msaada mkubwa sana kwao, kwani tunawapa msaada mkubwa sana. Ikiwepo sehemu ya kulala, tunawapa chakula, tunawatibu magonjwa. Wanaamini bila ya sisi wao si lolote wala chochote. Kwani tunawaepusha na majanga mbalimbali ikiwepo kuliwa na paka, mbwa n.k.

Kama wewe unavyoamini Mungu ni msaada mkubwa sana kwako na yeye ndiye mwanzo na mwisho kwako. Kwasababu tu anakupa uhai, anakupa riziki, anakuponya magonjwa ukiumwa na anakuepusha na majanga mbalimbali.

Kama ilivyofungwa akili ya kuku na ng'ombe juu ya dhamira kuu ya wao kufugwa na binadamu hivyo ndivyo ilivyofungwa akili ya binadamu kujua dhima kuu ya kwanini wapo hapa duniani.

Na siku binadamu akijua kwanini yupo hapa duniani ndiyo utakuwa mwisho wake wa kumwabudu Mungu na ataingia mgogoro mkubwa sana na Mungu uliojaa visasa . Ebu fikilia siku mifugo yako ikipewa utambuzi kwamba umeifuga ili uichinje tu au uiuze. Najua unajua nini kitakachotokea.

Wazee nawaambia ukweli sisi ni mifugo tu tunaoliwa na Mungu au na Shetani. Dhima kuu ya sisi kuwepo hapa duniani ni kuwa kitoweo cha Mungu au Shetani. Ndiyo maana tupo tupo tu bila mwelekeo wowote. Achana na story za kwenye biblia ni saundi tupu.

Kubisha ruksa kwani hata kuku anaweza akabisha huwa haliwi na binadamu.

Tunaonewa sana.
Kuna mawazo ni fact kasoro kiingereza" najua uta shangaa Una jua kwanini?
jf wengi huamini hili wazo nikweli pindi tu mwandishi atakapo andika kakiingereza

Basi hapo ataone kama ni mtu wa maana na kaongea Cha maana
Hata akiandika pumba
usishangae nikwasababu wengi Wana amini katika elimu sio kipaji au vipaji

Najua wengi watakukashifu mkuu Ila haya ni mawazo huru nje ya mawazo ya kuaminishwa na kukalilishwa

Mpaka sasa Kuna watu Wana amini kwamba mtawala wa dunia ni mwanadamu no more., Lakini Mimi siamini katika Hilo

wakati naona watu Wana wehuka kwa majini na mapepo na Wana saidiwa nawatu wenye uwezo ulio zaidi ya uwezo wa kibinadamu
je Bado utaniambia wanadam tuna itawara dunia na viumbe vyote vilivyomo?
Tusiishi kwa kukalilishwa tujaribu kufikiri nje ya elimu tuliyo pewa
Na tusionane wajinga mtu kufikilia nje ya ukalili wetu
Kwani kufikiri hakuna mipaka
 
Nadhani mleta mada anataka tuchambue ..kwamba ..baada ya kuwa tumejua sisi ni mifugo so kipi kifanyike?nadhani anataka tumcontorl mungu na shetani ...yani binadamu awe na nguvu zaidi kumshinda mungu na shetani...

Nadhani anataka kuweka point ya tunafanyaje ili tuwe na nguvu zaidi ya mungu na shetani?
Yes! au ana maana je hakuna namna nyingine ya kuishi kinyume nahivi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom