Tunaomuunga Mkono Magufuli Hatufurahishwi na hizi "Distractions"

Mimi nakumbuka October 25, 2015 nchi ilipigwa na butwaa baada ya kutangazwa eti kashinda.

nchi haikuwa na furaha..mikoa yote Tanzania nzima ilikuwa kama msiba.

I highly doubt

Yes..upinzani waliweka mtu dhaifu..lakini huyu bwana hakumshinda huyo mtu dhaifu.

Na anayoyafanya sasa ni matendo dhahiri ya mtu aliyekataliwa
Mkuu nchi ilikaa karibia wiki mbili kama inamsiba, hata siku aliyoapishwa wa CCM wenyewe waliosombwa na malori kwenda uwanjani hawakuwa na furaha kabisa. Mpaka siku ile Sizonje alipoanza yale maigizo ya kutembelea Hazina na Muhimbili
 
Mbona uchumi watu hamuuzungumzii? serikali inabana private secta kama vile kuna cold war..private sector ndio zinazooajiri na kulipa kodi, private sector ni kama inauawa na awamu hii ya tano hadi watu wanatamani heri ufisadi urudi
makusanyo makubwa ya TRA wameona sio sustainable kwa hii staili, ndio maana wamepunguza mbwembwe za kutangaza. . ila hili halipewi mjadala kama hayo mengine?

Tough times ahead as govt unveils more spending cuts
KWANI WEWE HUKUJUA KUWA SEKTA BINAFSI WENGI WALIKUWA WAPIGA DEAL? KWA SASA NI UTAWALA WA HAKI WA KULIPA KODO STAHIKI NI LAZIMA SASA HAWAWEZI KUINGIA KWENYE USHINDANI KWA KUWA FAIDA YAO HAIKUWA HALALI, WAMEAMUA KUACHA KUFANYA BIASHARA! WAFANYABIASHARA WA SASA WENGI WALIKUWA WAAMINIFU TANGU KITAMBO, KWA HIYO MFUMO WA UTAWALA HUU HAUWAATHIRI KIBIASHARA! RAIS MAGUFULI AENDELEE KUKAZA ILI KUONDOA WAPIGA DEAL WOTE, WAKATAFUTE MADAMBWE KATIKA NCHI NYINGINE!
 
Hicho unachotaka ndicho Raisi Magufuli anafanya kila siku, sijui uko Tanzania ipi?
Raisi anatutaka wananchi tufanye kazi kwa bidii na tulipe kodi
Raisi anachukia Ufisadi, Rushwa, Wizi, Matumizi mabaya ya fedha za umma, Uzembe, Upotoshaji, Uchochezi na nk.
Una hakika?
 
Kwa upande wangu sikutegemea jambo lolote la ziada kutoka kwa Magufuli kwasababu akujiandaa kuwa Rais. Yeye alijaribu kea bahati nzuri/mbaya akaupata huo urais,na yeye mwenyewe alisema ali-"bip" ikapokelewa.
Kiufupi,mtu hauwezi kujaribu nafasi ya uongozi ata siku moja kwasababu unatakiwa kuandaa misingi yako ya nini unatakiwa kusimamia na serikali yako itakuaje. Leo hii hajui asimamie nini,alianza kusema atapambana na mafisadi ila mpaka sasa mahakama imejaa mabuibui amna kesi ata moja.
Akasema anataka Tanzania ya "Hapa kazi tu" mpaka sasa ajaajiri wala kuongeza mishahara,kupandisha watu vyeo. Uko sekta binafsi kila siku wanapunguza wafanyakazi.
Sasa hivi anasimamia "Tanzania ya viwanda" tujiulize unawezaje kwenda kuwa nchi ya viwanda bila ya kuwekeza kwenye elimu hasa elimu ya ufundi na kilimo? Kilimo kimetupwa halafu mtu anategemea kuwa na viwanda.
Magufuli akujiandaa kuwa Rais ndio maana anakosa msingi ya kusimamia.
Well said
 
Mzee Mwanakijiji

Hoja uliyoweka ni muhimu sana kuijadili, lakini kama unavyofahamu hoja kama hizi hakuna anayetaka kuzijadili. Kama unavyofahamu mimi sina chama lakini napenda kuona Tanzania yenye maendeleo chanya ya kutufikisha kwenye neema. Kasi anayokwenda nayo JPM nimeipenda sana, lakini hawa wapinzani uchwara wanataka kumchelewesha na yeye anayo meno makali ya kuwang'ata na watanyooka tu.

JPM ameandaa progamme yake kwa miaka kumi inayokuja, panapo majaliwa hawa wote pimbi wanaopiga kelele watakuwa wanalialia kutaka aongeze muda.
Believe me hatua ambayo atakuwa amepiga itakuwa ni aibu kubwa sana kwa marais watatu waliomtangulia na hawa ni kikwazo kikubwa sana hivi sasa. Kama wakileta fyoko asiwape marupurupu yao ambayo yanawafanya wawe na kiburi.

Hatuwezi kuwapa nchi hawa wapinzani uchwara wanaoongozwa na cartel ya wezi wa kimataifa.
Mkuu umeeleza vizuri sana, lakini hujajibu hoja za Mwanakijiji wala hujaweka hiyo mikakati ya miaka kumi ijayo ya Serikali ya JPM.

Naona nawe umeenda kulekule kwa watetezi wa kila jambo wa Serikali na kuwalaumu wapinzani kana kwamba wao ndio wanaongoza Serikali. Inatakiwa ujue tu, basically wapinzani kazi yao kuu ni 'kupinga', ndio maana wanaitwa wapinzani.

Vv
 
Mzee mwanakijiji nakupongeza kwa mada nzuri yenye fundisho na mwelekeo wa huko tunapoenda. Tatizo tulilonalo tuna Rais ambaye hakujiandaa kutuongoza na kutufanya sisi wote tukawa kitu kimoja. Nakumbuka mwanzoni mwa utawala wake aliwahi kutamka wazi kuwa yeye sio rais wa CCM, Chadema na wala chama chochote cha siasa bali ni rais wa watanzania wote. Sasa tunachokiona ni tofauti na kauli yake maana kazi anayoifanya ni kutengeneza makundi baina ya watawala na watawaliwa huku tendo hilo likichagizwa na matumizi makubwa ya vyombo vya dola kukandamiza na kukamata raia na wapinzani wa kisiasa wenye mawazo tofauti. Huku si kujenga Nchi. Kiongozi anaijenga Nchi yake kwa kufuata Ilani ya chama kilichompa ridhaa ya kuongoza bila kusahau kufuata misingi ya sheria mama iliyopo kwenye katiba. Wakati mwingine binafsi najiuliza tunaelekea wapi maana mara leo utasikia hili kesho lile hatuna uhakika wiki ijayo litajiri lipi. Mimi namuunga mkono kwenye hii vita ya ufisadi lakini inaonyesha nguvu yake imepungua kwa kuwa naye ana mazonge makubwa aliyoyafanya akiwa ujenzi na waliomzunguka wakati ule wana vidhibiti vingi ambavyo vinaweza kumuumbua (rejeeni yanayomkuta huyu sijui Daud au makonda anajua mwenyewe yy nan). Ushauri wangu ni hivi;
1. Aache kwanza siasa za chuki dhidi ya wapinzani wake maana huwezi ukajifunza jambo lolote bila kukosolewa
2. Akubali kupokea ushauri wa wataalamu kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo Nchi maana yangu hapa hawezi kujua kila kitu pamoja na kwamba yy ndiy Rais
3. Aache matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambayo ndiyo yanayoleta dhana ya yy ni dikteta
4. Uwepo mrejesho kwa wananchi ikiwa kuna masuala muhimu ya utekelezaji kwa maslahi ya Nchi
5. Na mwisho amfukuze kazi huyu Mkuu wa Mkoa wa Dsm (simtaji jina maana analijua mwenyewe) maana anaidharirisha serikali na kuonekana ya kihuni huni
 
Wapo wafanyakazi wa serikali katika proffessional levels wanataka kuacha kazi serikalini...

Naongelea engineers, advocates, specialists waende abroad ama waende private sectors....
sijakuelewa inahusiana vipi na comment yangu?
 
Unajua uzi huu ukiusoma taratibu unaweza kuona watu walivyo na hoja za maana sana katika pande zote mbili - za wale wanaompinga na wale wanaomkubali Magufuli. Ni wachache tu ambao wanaingiza siasa na hivyo wanaweka ukungu katika uzuri wa hoja za watu. Mnanipa mawazo mazuri wachangiaji wote, asanteni.
 
Hivi mwanakijiji hivi ndio wewe kweli w miaka ile?
 
KWANI WEWE HUKUJUA KUWA SEKTA BINAFSI WENGI WALIKUWA WAPIGA DEAL? KWA SASA NI UTAWALA WA HAKI WA KULIPA KODO STAHIKI NI LAZIMA SASA HAWAWEZI KUINGIA KWENYE USHINDANI KWA KUWA FAIDA YAO HAIKUWA HALALI, WAMEAMUA KUACHA KUFANYA BIASHARA! WAFANYABIASHARA WA SASA WENGI WALIKUWA WAAMINIFU TANGU KITAMBO, KWA HIYO MFUMO WA UTAWALA HUU HAUWAATHIRI KIBIASHARA! RAIS MAGUFULI AENDELEE KUKAZA ILI KUONDOA WAPIGA DEAL WOTE, WAKATAFUTE MADAMBWE KATIKA NCHI NYINGINE!

Huyu naye ni GT kweli JF ni sawa na KOKORo!
 
UKATOLIKI ulishammaliza hata ukichunguza vita vyake zamani ilikuwa kwa sababu Mkulu hakuwa MKATOLIKI na alipona Lowassa nataka kuchukua akabadili gia anagani kwenda kwa mkatoliki mwenzie
Bhana kweli huyu jamaa amebadilika sana mpaka hata mimi naamini kuna uwezakano hii ID inatumiwa na mtu mwingine sio yule wa 2010
 
kumbe Ben sa8 hajarud bado uraian lakin mwanahalisi walisema huwa anashinda vijiwe vya kahawa
Raisi Magufuli siyo Superhuman ni Binadamu kama Binadamu wengine hivyo hawezi kuwepo kila mahali na kutimiza kila hitaji la kila Binadamu, kama hamumkubali kuna njia ya kufanya hivyo nayo ni 2020 msimrudishe Ikulu, vinginevyo kaeni pembeni na mwachieni Uwanja na Timu yake wafanye yale wanayaoona yanafaa na kama mnaona ni Udikteta au huo mnaouita Utawala ya Sheria haufatwi basi Watanzania tutaamua 2020, lkn binafsi namuunga mkono Raisi Magufuli na kwanza ukiniuliza mimi hawa wanaojiita Upinzani siyo watu wa kuwachekea kabisa, ni watu wabaya, kama nikikuuliza
Ben Saanane yuko wapi? Na kwa nini hamumuongelei tena? Kwa nini mlisema Serikali yetu imemuua na kufukia maiti yake Mto Ruvu halafu leo muko kimya? Hizo shutuma zilikuwa na lengo gani? Mlitembea kwa Wazungu Ulaya kuwaambia kwamba Serikali yetu imemuua Ben Saanane, Je ninyi ni watu wazuri wa kuchekewa chekewa? Raisi Magufuli bana hapo hapo usirudi hata milimeta 1 nyuma, nchi haijengwi kwa ulele mama, Historia itakuwa hakimu!
 
Mzee mwanakijiji nakupongeza kwa mada nzuri yenye fundisho na mwelekeo wa huko tunapoenda. Tatizo tulilonalo tuna Rais ambaye hakujiandaa kutuongoza na kutufanya sisi wote tukawa kitu kimoja. Nakumbuka mwanzoni mwa utawala wake aliwahi kutamka wazi kuwa yeye sio rais wa CCM, Chadema na wala chama chochote cha siasa bali ni rais wa watanzania wote. Sasa tunachokiona ni tofauti na kauli yake maana kazi anayoifanya ni kutengeneza makundi baina ya watawala na watawaliwa huku tendo hilo likichagizwa na matumizi makubwa ya vyombo vya dola kukandamiza na kukamata raia na wapinzani wa kisiasa wenye mawazo tofauti. Huku si kujenga Nchi. Kiongozi anaijenga Nchi yake kwa kufuata Ilani ya chama kilichompa ridhaa ya kuongoza bila kusahau kufuata misingi ya sheria mama iliyopo kwenye katiba. Wakati mwingine binafsi najiuliza tunaelekea wapi maana mara leo utasikia hili kesho lile hatuna uhakika wiki ijayo litajiri lipi. Mimi namuunga mkono kwenye hii vita ya ufisadi lakini inaonyesha nguvu yake imepungua kwa kuwa naye ana mazonge makubwa aliyoyafanya akiwa ujenzi na waliomzunguka wakati ule wana vidhibiti vingi ambavyo vinaweza kumuumbua (rejeeni yanayomkuta huyu sijui Daud au makonda anajua mwenyewe yy nan). Ushauri wangu ni hivi;
1. Aache kwanza siasa za chuki dhidi ya wapinzani wake maana huwezi ukajifunza jambo lolote bila kukosolewa
2. Akubali kupokea ushauri wa wataalamu kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo Nchi maana yangu hapa hawezi kujua kila kitu pamoja na kwamba yy ndiy Rais
3. Aache matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambayo ndiyo yanayoleta dhana ya yy ni dikteta
4. Uwepo mrejesho kwa wananchi ikiwa kuna masuala muhimu ya utekelezaji kwa maslahi ya Nchi
5. Na mwisho amfukuze kazi huyu Mkuu wa Mkoa wa Dsm (simtaji jina maana analijua mwenyewe) maana anaidharirisha serikali na kuonekana ya kihuni huni
Hata wanaccm wanaisoma namba katika uwajibikaji ila wapinzani wakijenga hoja zao kwa matusi na kejeli ni lazima washitakiwe.
 
Mkuu umeeleza vizuri sana, lakini hujajibu hoja za Mwanakijiji wala hujaweka hiyo mikakati ya miaka kumi ijayo ya Serikali ya JPM.

Naona nawe umeenda kulekule kwa watetezi wa kila jambo wa Serikali na kuwalaumu wapinzani kana kwamba wao ndio wanaongoza Serikali. Inatakiwa ujue tu, basically wapinzani kazi yao kuu ni 'kupinga', ndio maana wanaitwa wapinzani.

Vv
Wapinzani kazi yao ni kupinga, hivyo ndivyo ulivyokaririshwa, beggars belief. Hivi umesoma ulichoandika.
Mikakati ya JPM inatekelezwa kwani huoni?

The alternative look stupid and in disarray.
 
Wazo Zuri, Tatizo Mkuu hana mpango wa kurasimisha maono na mipango yake,kwa kuweka mikakati ya kisheria na sera badala ya matamko kutoka moyoni.
e.g Katiba ,Sera ya viwanda,Elimu,Usalama na Mamlaka za Uteuzi
pic+magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Sielewi kwanini serikali inapojaribu kusimamia mabadiliko na nidhamu katika utumishi wa umma inajigongelea misumari yenyewe. Ninavyoona ni sawa na fundi seremala mashuhuri anayejaribu kutengeneza samani nzuri lakini haishi kujigonga nyundo vidoleni yeye mwenyewe! Anataka tuone uzuri wa samani zake ili tuzipende lakini wakati huo huo hatukosi kumuona anavyolia kila nyundo inapotua kwenye kidole ambacho angeweza kukiepuka kama angekuwa makini. Anajigonga mwenyewe kwa sababu wakati huo huo anafanya ufundi wake bado anazungumza mambo yasiyohusiana, mara ashike kitabu kusoma, mara asikilize muziki n.k kiasi kwamba anaonekana hana focus.

Binafsi ningependa sana serikali ya Magufuli ioneshe nidhamu yenyewe (self discipline) na kutulia mkazo wanachofanya(focurs) badala ya sasa ambapo hadi baadhi ya vitu hatujui vinaendelea vipi kwani mazungumzo ya kitaifa yamebakia kwenye mambo yasiyo ya msingi au ya lazima (irrelevant issues).

Kuna msemo kuwa "neno la muungwana ndio dhamana yake". Msemo huu unamaanisha tu kwamba mtu muungwana akisema neno, au akitoa ahadi fulani basi haitaji kuweka rehani kitu chochote ili kuaminika; yaani neno lake ni rehani tosha kwa yeye kupewa dhamana. Mtu muungwana anapotoa ahadi basi anaaminika kwa sababu neno lake linaaminika.

SIKUMBUKI (na nimeweka herufi kubwa kwa mkazo tu) kama Magufuli wakati anatoa ahadi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 alisema jambo lolote ambalo liliashiria kuwa ama angekuwa na ugomvi wa kudumu na wapinzani au kwamba atajaribu kuingilia au kushawishi mihimili mingine ya dola. NINACHOKUMBUKA ni kuwa aliahidi kati ya vitu vingi (hasa kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni pale Jangwani mwezi Augusti 2015) kwamba ataheshimu mawazo ya watu mbalimbali hata kama ni upinzani na kuwa ataheshimu uhuru wa mihimili mingine.

Sasa inapotokea kuwa vyombo vya dola vinahangaika sana na vitu ambavyo vinaangukia kwenye himaya ya uhuru wa maoni au mawazo inasikitisha. Nimewahi kusema hapa miaka karibu kumi sasa kwamba haki ya uhuru wa maoni na uhuru wa mawazo hailindi mawazo mazuri au yenye kufurahisha. Mawazo mazuri na yenye kufurahisha hayahitaji kulindwa; kinacholindwa ni mawazo mabaya, mabovu, ya kuudhi na wakati mwingine ya kukera kabisa. Magufuli alipokubali kutaka kugombea Urais na kusimama kugombea maana yake ni kuwa alikuwa tayari kusemwa, kukejeliwa, kufanywa kituko, kuchorwa vibaya, na hata kufikiriwa vibaya. Alikubali kwa sababu aliaminisha umma kuwa ana ngozi ngumu (tough skin). Na sisi tuliomuunga mkono na ambao bado tunamuunga mkono tunaamini ana ngozi ngumi hivyo tunaposikia ati mtu kakamatwa kwa sababu kamsema vibaya Rais, au sijui kasema jambo lenye kumkera Rais inatuudhi!

Sasa inawezekana ni watu wa chini tu ambao nao wanafikiria wanamtendea Rais hisani kwa kufuatilia watu wanasema nini juu ya serikali au nini. Hizi ni distractions! Leo hii sijui kuna kesi ngapi zinahusiana na mambo ya kipuuzi na watu wazima na akili zao kuchwa kucha wamekaa wanahangaika hadi kama ni burudani inaanza kufanya watu wasinzie. Watu gani hawachoki kutafuta kesi za kila namna, asubuhi na mchana, hadi watu kwenye mitandao wanaanza kutunga vitu vya uongo ili kuwajaza watu hofu! Juzi kuna message inatembea ati serikali inarekodi mazungumzo yote ya kwenye simu na watu wanaanza kuhofia hata kuzungumza kwenye simu, huu ni upuuzi gani?

Kama kweli Magufuli anaumia sana moyoni, anakereka kirahisi rahisi, anakwazika na kila kibaya kinachosemwa juu yake kiasi kwamba anaona wanamzuia kutekelezas wajibu wake au anaona kuwa kazi hii ni ngumu sana kwake kuifanya binafsi nina ushauri mzuri tu; Katiba imeweka utaratibu wa hiari kwa Rais akujiuzulu. Si LAZIMA awe Rais. Kwa sababu tunaomuunga mkono tunaamini yeye ni Rais ambaye Tanzania ilimhitaji sasa na tuliamini kuwa akiweka mkazo (focus) na kusimamia nidhamu (self discipline) ya serikali yake basi katika miaka hii mitano mambo makubwa yanaweza kufanywa kuliko yaliyofanywa miaka hamsini iliyopita!

Hivyo basi, ushauri wangu ni kuwa Serikali ikae chini na kujiuzuli kwanini inachekelea hizi distractions? Kwanini inazunguka zunguka kwenye mambo yasiyo na msingi badala ya kuwashawishi wananchi kwa uongozi wake kuonesha mambo makubwa yanayofanywa au yanayopangwa kufanywa?

Magufului ni lazima ahakikishe mambo yafuatayo nayatokea:

a. Kuheshimu mahakama kwa gharama zote - demokrasia na utawala wa demokrasia vinasimama au kuanguka na uhuru wa mahakama. Kama kuna viongozi wanaitwa mahakamani ni LAZIMA watii! Na binafsi hilo peke yake ni sababu tosha ya kumfukuza mtu kazi kwa kutokutii mahakama. Na Rais mwenyewe aepuke kwa nguvu zake zote undue influence ya mahakama.

b. Rais atumie ushawishi wa nguvu za hoja kuliko ushawishi wa hoja za nguvu. Watu ni lazima waone mantiki ya kinachosimamiwa kuliko hofu ya kutokukisimamia. Katika hili ni lazima Rais ajioneshe kuwa ni mtu wa tafakari na siyo mtu wa munkari. Ukali uliopo ni wa lazima na binafsi naamini kati ya vitu vilivyokosekana kwa muda mrefu ni viongozi wakali; lakini ukali hauondoi ushawishi.

c. Kesi dhidi ya wapinzani na ambazo zinaonekana ni za kisiasa zifutwe ili taifa lirejee kwenye mijadala ya kisiasa bila hofu ya kumuudhi Rais. Na labda hili litawafanya polisi wafocus na wenyewe kwenye mambo ya msingi - kama vita dhidi ya madawa ya kulevya, ufisadi n.k Sasa hivi ni kana kwamba vita dhidi ya ufisadi imeenda picnic! Magufuli aliungwa mkono na baadhi yetu kwa sababu alikuwa ni chaguo sahihi kupambana na ufisadi kwani tulijua ana uthubutu wa kuugusa ufisadi. Hadi hivi sasa kasi ya kupambana na ufisadi haijaleta matumaini sana. Na kinachosikitisha ni kuwa kesi kadhaa hadi hivi sasa zinaonekana haziendi popote kwa sabbabu hazioneshi kama zimefikiriwa vizuri na mawakili wa serikali wanatia aibu! Ni rahisi zaidi kumkamata mtu kuliko kuthibitisha kwanini umemkamata! Watu wakamatwe pale ambapo kuna uthibitisho wa uhalifu hasa lakini hizi kesi nyingine zinafanya serikali ionekane haina mawakili wabobezi au wenye ujuzi wa kusimamia kesi nzito matokeo yake tunatengeneza precendence za ajabu sana!

d. Wakati umefika kwa Magufuli kulihutubia taifa na kulishawishi (persuade) lielewe anataka kufanya nini na anafanya nini vitu hivyo. Ni hotuba ya kuliamsha taifa pia ili kila Mtanzania afanye nini katika nafasi yake. Kitu kibaya ambacho kimetokea (na nilidokeza kwenye makala yangu wiki mbili nyuma) watu wanaitegemea sana serikali hakuna moyo wa kujitolea (kwa kiasi kikubwa). Ni lazima kuamsha roho ya kujitolea katika taifa badala ya watu kusubiria serikali ifanye. Magufulia anatakiwa kuamsha roho ya ujenzi wa taifa; watu wajitolee kulijenga taifa lao kuliko kusubiria kila kitu serikali ifanye. Je, ni vitu gani Watannzania wanaweza kufanya wenyewe bila serikali kuwafanyia? hii ndio changamoto ya kiuongozi!

Kwa ufupi, tuachane na distractions na vitu vinavyopoteza mwelekeo au hata mjadala wa kitaifa. Ni muhimu serikali ioneshe ina nidhamu katika watendaji wake ikibidi hata kupangua baraza la mawaziri kwani kuna watu wanapwaya kupita kiasi sasa hadi inakera. Kama kuna jambo lolote Rais anaona haliendi sawa au linahitaji sheria ngumu ni muhimu serikali iende Bungeni na mabadiliko ya sheria ili jambo hilo lishughulikiwe kisheria.

Tunaomuunga mkono Magufuli tunataka uwajibikaji, utawala wa sheria, kuheshimu tunu za kidemokrasia, ushawishi wa hoja, kuwa makini na wenye mkazo na kuepuka kupoteza muda kwenye mambo yasiyo ya msingi. Muda uliobakia na mchache na tusipoteze nafasi kwa mambo yanayopoteza fedha za umma na muda wa wananchi kujadili mambo ya msingi.
 
Back
Top Bottom