Tunaomba zianzishwe kamati za maadili hospitali zote kubwa kama ilivyo Mloganzila

wangwafi

Senior Member
May 21, 2020
141
70
Ni mara kwa mara tumekuwa tukiona malalamiko mengi ya wagonjwa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la maadili katika sekta hii ya afya; isitoshe mengi tumeyaona ya kusikitisha kama wenzetu wagonjwa wanvyotendewa na watendaji huko katika hospitali.

Ni juzi tu nilikuwa Ocean Road kuna mgonjwa alifika pale akwa hajapata huduma kwa siku nne zote na kila akimuita nesi anakuja anamuambia utahudumiwa mbona mlalamishi, mgonjwa uvumilivu ukamshinda akachukua simu yake akapiga kwa kiongozi wa hiyo hospitali kumuelezea anavyoumwa na kuwa huduma hapati na kumuelezea kuwa nilikuwa namueleza nesi fulani anisadie nipate huduma.

Baada kufikisha yale malalamiko kwa mkuu, nesi alikuja akiwa mbogo na kumuambia mgonjwa wewe si umeenda kumilalamikia kwa boss sasa utanikoma. Siku ya pili yake wamekuja jopo la madaktari watatu wakamwambia kwa kuwa huna hela ya vipimo na matibabu tunaomba uende ukatafute fedha halafu uje kwa kweli inasikitisha mgonjwa wa saratani akaondoka na sijui nadhani alienda kufa kwa hali aliyokuwa nayo.
 
Back
Top Bottom