DOKEZO Wauguzi Bochi hospitali kuweni na utu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Leo mida ya jioni nilikuwa Bochi hospitali, wakati nikiwa kwenye foleni ya kuingia kwa daktari ambayo tayari imeshanichosha kutokana na foleni kuwa kubwa na kucheleweshewa huduma kwa mlolongo mrefu wa kumuona daktari mara akaja mgonjwa ambaye kikawaida altakiwa kupewa huduma za haraka kwa hali aliyokuwa nayo.

Lakini cha kushangaza mgonjwa mtu mzima mwanaume alifika akiwa katika hali ya ulevi huku kabanwa sana na Pumu( kwa mujibu wa masesi na madaktari) na sauti ya kifua kupiga kelele na kupumua kwa shida sana ilitosha kabisa kujiridha kuwa maelezo ya wauguzi yaikuwa sahihi.

Lakini alifika na kutopatiwa huduma huku akibaki nje anahangaika kwenye mabenchi na wauguzi wakimwangalia na kumsema kuwa ni mlevi wanamjua kwa usumbufu wake na lugha yake mbaya ya matusi ivyo atajijua mwenyewe wao washamchoka.

Watu waliosindikiza wagonjwa wengine pamoja na wagonjwa wengine walishindwa kuvumilia na kuanza kuuliza kwa nini hapatiwi huduma ila kauli za wauguzi wa Bochi zilikuwa:-
  • Huyu mzee tunamjua anakujaga hapa kaanwa kifua ana lugha chafu.
  • Tumemwambia aende kitandani kabaki kakaa tu sisi tumfanyaje, tumbebe? Au mnataka tumfunge kamba tumuruze atajua mwenyewe.
  • Limtu lenyewe linajijua lina athma ila bado lilevu mbwa nani ahangaike na mtu kalewa, unamwambia afanye hivi anafanya vile mi siwezi
  • Nyie mnaouliza kama mna huruma naye sana muhudumieni, au mpelekeni hospitali nyingine.
  • Muhudumu mmoja akasema alikuja mwanzo akapewa huduma ya kwanza akatulizwa sasa karudi tena daktari kasema hawezi kupewa huduma nyingine
  • Mwingine akasema tushazoea kuona wagonjwa wa kila aina tena waliozidiwa hasa huyu ana nafuu mwacheni tu akitaka ataenda kitandani si anapajua wodini.
Watu walihoji akifa hapo wahudumu watasemaje? Wahudumu wale kwa jeuri wakasema kwani atakuwa wa kwanza kufa?

Haya yaikuwa majibu ya wauguzi kama 8 walikuwa wakipita na wengine kudiriki kumfata mgonjwa na kusema kwa ulevu wake na tabia zake mbaya hadi katelekezwa hapo.

Mgonjwa huyo aliendelea kupumua kwa shida huku akilia na kuomba msaada asaidiwe naye akijaribu kujisaidia kwa kuvua shati lakini hakuna muhudumu aliyejali, mgonjwa huyo alianguka chini na kuanza kutambaa huku watu wakijaribu kupiga kelele za kuwasihi wahudumu wamuhudumie ila wapi.

Baadhi walichukua simu ya mgonjwa na kuanza kuwapigia ndugu ili wafike haraka waweze kumhamisha hospitali ili kuokoa maisha maisha yake kwa kuwa mgonjwa alikuwa peke yake. Baadhi wakaanza ukutafuta boda boda kabisa ili ndugu wakifika tu waondoke naye wamuwahishe hospitali.

Huku wengine wakiendelea kupiga kelele, ndipo nesi mmoja ambaye alikuwa akitokea eneo lingine kabisa hakuwepo mwanzo alipomuona akaamua kumhudumia, akamchoma sindano palepale nje, na baada ya hapo akamchukua mgonjwa na kumuingiza chumba cha wagonjwa wa dharura japo wakati akitoa huduma nesi mmoja alisikika akisema Unajidai una huruma sana shauri yako naona huangalii kibarua chako, huruma itakuponza.

Mpaka naondoka hapo alikuwa bado yupo kule alikopelekwa ila kitendo hicho si cha kiungwana kwa mgonjwa hataka kama ana matatizo ya ulevi na kauli chafu bado alistahili kupata huduma ya kuokoa masisha yake kwanza kisha ndio wakae naye kumuonya.



 
Kama hizo statement ni za kweli basi hawakufanya utu.

Hii kazi wanatibu wezi/majambazi/walevi, ni kuvumilia tu.
 
Back
Top Bottom