Tunamsaidiaje Irene? Kanyimwa talaka na mumewe, kesi Jumatatu mahakamani

carlos raull

New Member
Dec 28, 2016
4
45
Anaomba ushauri wa kisheria; bwana Yesaya alifunga ndoa na mwanadada Iren miaka 4 iliyopita, ndoa yao ilidumu kwa miaka 2 tu kisha mwanamke akaondoka baada ya kutoridhiswa na tabia za mumewe, hususan kunywa pombe kupita kias, uvutaj wa sigara ulioptilza n.k, baadae alimuomba TARAKA take ili awe huru mume akakataa, Iren akampata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, mwisho akapata ujauzito, akarudi nyumbani kujiangalizia ndipo alipokutana na mume Yesaya, yesaya akapeleka kesi kituo kidogo cha polisi kumshtaki Irene kwa kubeba ujauzito angali na mke wake halali. Tunamsaidiaje Iren?
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,003
2,000
Hivi "spelling" kwa lugha yetu wenyewe mbona ni shida sana? "TARAKA" kweli! ama unamaanisha talaka?
Mambo ya talaka ambayo ni madai na vituo vya polisi, wapi na wapi?
Kesi kama hizo ni za mahakamani moja kwa moja na siyo polisi.
Hakuna sheria yoyote inayolazimisha ndoa, bali huwa ni usuluhisho tu na ikishindikana, ndoa hiyo hubatilishwa kisheria.
Mnaweza msigombane, lakini mmoja akamchoka mwenzie, hiyo ni sababu tosha ya kuachana, maana ndoa ni mkataba wa hiari wa "me" na "ke" kuishi pamoja. Na kiunganishi kikubwa ni upendo. Upendo unapokosekana ni halali ndoa hiyo kubatilishwa ili kila mtu afuate 50 zake, ili mradi kwa kufuata sheria.
 
ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,436
2,000
kwenda nje ya ndoa (uzinzi) tayari ni jambo mojawapo linaloweza kuvunja ndoa!
huyo mama,amwache jamaa aende anakotaka,kesi ikifika mahakamani mama anaweza akapress kuwa anampenda huyo mwanaume wa nje,na hivyo kupelekea ndoa kuvunjwa'
kwani ukiacha uzinzi,kupata gonjwa la ngono/ukimwi,kushindwa kufanya tendo la ndoa,kupata ukichaa na kutoonekana katika ndoa kwa miaka mitano na zaidi kutokana na kufungwa jela au vyovyote ni hoja zinazoweza ibatilisha ndoa!
labda swali la msingi:huyo mwanaume uko mahakamani anaenda kudai nini?talaka au fidia?
hati ya mashitaka inasemaje?
 
jojojo

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
926
500

Wewe asingebeba mimba ndani ya ndoa, alipoona tabia ya mme imekuwa mbaya angeomba talaka. Sio kukimbia huko ni sawa na huyo aliyemtia mimba ameharibu ndoa halali. Huenda huo ulevi ulisababishwa na matatizo ya mwanamke, kutokea kwa huyo aliyemtia mimba. Alipe kwanza ugoni huyo mwanaume aliye tia mimba, unaingia kwenye ndoa huku bado unatamani nje.
 
Fraeda

Member
Dec 28, 2016
21
75
kupata mimba nje ya ndoa teyari ameshajipa talaka mwenyewe kilichobaki ni kwenda mahakamani kukamilisha taratibu.
 
dareda

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
222
500
Hapa ushauri unashindikana kidogo kutokana na mkanganyiko flani uliojitokeza, kwanza me kwenda polisi kushtaki eti mkewe kapewa mimba is that a criminal case?? Sina hakika kama kweli polisi waliweza kufungua shauri la namna hiyo Abadan, pili hoja zilizopelekea yy kuondoka kwa mumewe n hoja dhaifu sana na kimsingi hazina mashiko ya kuvunja ndoa na kikubwa kinachojidhihirisha hapa n kwamba huyo mwanamke alikua na mahusiano mengine ndo yaliyopelekea wafike hapo walipofika......... All n all huyo Iren n mzinzi period
 
KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,525
2,000
Ndoa za siku hizi....zinafungwa usoni tu kwa msukumo wa mali na vitu vingine lakini sio moyoni......

Ndio maana ndoa zimegeuka vifungo au magereza ya mateso badala ya kuwa ni muunganiko wa furaha amani na upendo.......

Wengi hawafurahii maisha ya ndoa zao....isipokuwa wanaishi kwa uvumilivu huku mioyo yao ikiwaka moto kwa huzuni na karaha.......

Wachache wenye kushindwa kuhimiri maumivu ya mateso hayo ya kujitakia....hudai taraka ili wawe huru huku jamii ikiwashangaa.....bila ya kujua siri zote za mtungi anayezijua ni kata.......
Na wanaogopa lawama za watu na macho mabaya ya ndugu na jamaaa....wameamua kujikaza kisabuni ndani beseni la maji huku wakiteketea......

NB; BE EXTRA CAREFUL WITH YOUR CHOICES.....
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Anaomba ushauri wa kisheria; bwana Yesaya alifunga ndoa na mwanadada Iren miaka 4 iliyopita, ndoa yao ilidumu kwa miaka 2 tu kisha mwanamke akaondoka baada ya kutoridhiswa na tabia za mumewe, hususan kunywa pombe kupita kias, uvutaj wa sigara ulioptilza n.k, baadae alimuomba TARAKA take ili awe huru mume akakataa, Iren akampata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, mwisho akapata ujauzito, akarudi nyumbani kujiangalizia ndipo alipokutana na mume Yesaya, yesaya akapeleka kesi kituo kidogo cha polisi kumshtaki Irene kwa kubeba ujauzito angali na mke wake halali. Tunamsaidiaje Iren?
= talaka

Kiswahili ni lugha yako ya taifa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
carlos raull

New Member
Dec 28, 2016
4
45
kwenda nje ya ndoa (uzinzi) tayari ni jambo mojawapo linaloweza kuvunja ndoa!
huyo mama,amwache jamaa aende anakotaka,kesi ikifika mahakamani mama anaweza akapress kuwa anampenda huyo mwanaume wa nje,na hivyo kupelekea ndoa kuvunjwa'
kwani ukiacha uzinzi,kupata gonjwa la ngono/ukimwi,kushindwa kufanya tendo la ndoa,kupata ukichaa na kutoonekana katika ndoa kwa miaka mitano na zaidi kutokana na kufungwa jela au vyovyote ni hoja zinazoweza ibatilisha ndoa!
labda swali la msingi:huyo mwanaume uko mahakamani anaenda kudai nini?talaka au fidia?
hati ya mashitaka inasemaje?
Kwa ufup jamaa bado anampenda mkewe japo wamengana kwa zaid ya miaka 2 na talaka asitoe, lakin kilicho mpeleka mahakaman ni kutaka kurudiana na mkewe na mwamke hayuko tayar ana nae, kwahiyo Mume ameamua ku2mia nguvu ya pesa kupenyeza lupia kwa mkuu wa kituo,wakili pamoja hakimu, imebainika imetolewa kama milion 10 hiv ili mwanamke sheria imbane alipe fidia kwa kubeba ujauzito nje ya ndoa na arudi kwa mumewe kwan bado n mke halal. Kama ilivyo ada; watanzania tuliokua weng sheria za kutulinda wenyewe hatuzjui, na ndio maana tunaburuzwa,
 
Mwanyasi

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,895
2,000
Anaomba ushauri wa kisheria; bwana Yesaya alifunga ndoa na mwanadada Iren miaka 4 iliyopita, ndoa yao ilidumu kwa miaka 2 tu kisha mwanamke akaondoka baada ya kutoridhiswa na tabia za mumewe, hususan kunywa pombe kupita kias, uvutaj wa sigara ulioptilza n.k, baadae alimuomba TARAKA take ili awe huru mume akakataa, Iren akampata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, mwisho akapata ujauzito, akarudi nyumbani kujiangalizia ndipo alipokutana na mume Yesaya, yesaya akapeleka kesi kituo kidogo cha polisi kumshtaki Irene kwa kubeba ujauzito angali na mke wake halali. Tunamsaidiaje Iren?
Wewe ndio unataka kumuoa huyo Irene?
Kwani hajui ndoa ni kuvumiliana?
Nitamshauri akiwa anatoka kwako
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,003
2,000
Wewe ndio unataka kumuoa huyo Irene?
Kwani hajui ndoa ni kuvumiliana?
Nitamshauri akiwa anatoka kwako
Pointi ama kichwa cha habari kinachozungumzwa hapa ni kwamba " tumsaideje Irene, ndiyo tunachojadili sasa. Irene kaolewa muda mfupi, kumchoka mmewe na kuomba talaka,lakini mwanaume kakataa.
Matokeo yake kabebwa na mwanaume mwingine na kutiwa mimba. Pia hataki kurejeleana na huyo mme wake wa ndoa.
Mustakabali wa Irene hapa ni nini?
Ndiyo nikasema kwamba? Hakuna ndoa ya kulazimishana. Kama usuluhisho umeshindikana, kinachofuata ni talaka inayotolewa mahakamani tu. Bila kujali ni upande upi utakao peleka shauri hilo mahakamani.
Lakini kwa maudhui ya mada hii ni kwamba Irene aende mahakamani kudai talaka yake, asiende kwa mme wake kudai talaka.
Huyo mme ataitwa mahakamani kusikiliza madai ya talaka ya mke wake na mwishowe, mahakama itatoa hukumu ya haki kumaliza kadhia iliyopo kwenye mafungamano ya wawili hao.
 
kioju

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
804
250
kwenda nje ya ndoa (uzinzi) tayari ni jambo mojawapo linaloweza kuvunja ndoa!
huyo mama,amwache jamaa aende anakotaka,kesi ikifika mahakamani mama anaweza akapress kuwa anampenda huyo mwanaume wa nje,na hivyo kupelekea ndoa kuvunjwa'
kwani ukiacha uzinzi,kupata gonjwa la ngono/ukimwi,kushindwa kufanya tendo la ndoa,kupata ukichaa na kutoonekana katika ndoa kwa miaka mitano na zaidi kutokana na kufungwa jela au vyovyote ni hoja zinazoweza ibatilisha ndoa!
labda swali la msingi:huyo mwanaume uko mahakamani anaenda kudai nini?talaka au fidia?
hati ya mashitaka inasemaje?
Hill la uzinzi ni mpaka mume apeleke malalamiko mahakaman na kuomba talaka, lakin hili ni kinyume chake, kifupi hakuna sabab ya msingi ya kuvunja ndoa hapo, ulevi anaosema hapo kama kero hizo zinaitwa rabsha ktk ndoa hazizuii kuwepo kwa ndoa labda kama huyo mume anampiga na kumdhalilisha hapo sawa ila hizi sabab alizotaja hapo, soon asaidiweje hapo labda aendelee kuchepuka tu mpaka mume akasirike ampe talaka
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,249
2,000
Kwa ufup jamaa bado anampenda mkewe japo wamengana kwa zaid ya miaka 2 na talaka asitoe, lakin kilicho mpeleka mahakaman ni kutaka kurudiana na mkewe na mwamke hayuko tayar ana nae, kwahiyo Mume ameamua ku2mia nguvu ya pesa kupenyeza lupia kwa mkuu wa kituo,wakili pamoja hakimu, imebainika imetolewa kama milion 10 hiv ili mwanamke sheria imbane alipe fidia kwa kubeba ujauzito nje ya ndoa na arudi kwa mumewe kwan bado n mke halal. Kama ilivyo ada; watanzania tuliokua weng sheria za kutulinda wenyewe hatuzjui, na ndio maana tunaburuzwa,
Huyo Yesaya ni mjinga....

Hiyo hela bora angeenda rehab anaacha pombe na sigara chenji awekeze na kutafuta mwanamke atakayempenda kwa dhati

Sent from my SM-N910H using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom