Kesi ya Mary Kay LeTourneau: Mwalimu aliyembaka mwanafunzi wake wa miaka 13 na kuzaa naye…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Mary Kay LeTourneau: Mwalimu aliyembaka mwanafunzi wake wa miaka 13 na kuzaa naye…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 26, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mary Kay LeTourneau

  [​IMG]
  Mtoto Vili Fualaau

  [​IMG]
  Mary Kay LeTourneau na Mtoto Vili Fualaau walipofunga ndoa

  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]
  Vili Fualaau na wanae Audrey mkubwa na Geogia Alexis

  Mary Kay LeTourneau alikuwa na umri wa miaka 35 na mama wa watoto wanne wakati huo. Alikuwa ni mwalimu anayeheshimika sana katika mji wa Burien ulioko katika jimbo la Washington. Mnamo October 1996 alipatwa na mkasa ambao ulibadilisha historia yake yote.

  Alikuwa na ujauzito wa miezi miwili na ujauzito huo haukuwa ni wa mumewe. Kibaya zaidi ujauzito huo ulikuwa ni wa mwanafunzi wake, mtoto wa miaka 13 aitwae Vili Fualaau ambaye alikuwa anamfundisha tangu akiwa darasa la pili katika shule ya Shorewood. Akiwa ni mwanamke wa kikatoliki, hakutaka kabisa kuitoa mimba hiyo na kwa sababu ya toauti ya asili kati yake na mwanafunzi wake kulikuwa hakuna uwezekano wa mumewe kukubali kuwa mtoto ni wake pale atakapozaliwa. Lakini pamoja na mtihani huo uliokuwa ukimkabili mbele yake, lakini hakusita kuonyesha mapenzi makubwa kwa mwanafunzi huyo aliyempa mimba na hakutaka kabisa kuitoa mimba hiyo.

  Mbali na mwanafunzi huyo, Mary hakuwa na mtu mwingine ambaye angeweza kumshirikisha katika siri yake hiyo, na alijua dhahiri kwamba bado kitambo kidogo, kila kitu kitakuwa peupe. Hata hivyo siri ikafichuka mapema sana kuliko alivyotarajia. Mnamo Novemba 1996, mume wa wake, aitwae Steve LeTourneau aliyekuwa na umri wa miaka 35 wakati huo, alifuma furushi la barua za mapenzi zilizotumwa na mwanafunzi huyo kwa mkewe.

  Ukweli ni kwamba Steve alijenga wasiwasi muda mrefu juu ya ukaribu uliokuwepo kati ya mkewe na mwanafunzi yule. Lakini katu hakufikiria au kuhisi kwamba ukaribu ule ungeweza kuwa ni wa kimapenzi. Baada ya kuzifuma barua hizo alikwenda nyumbani kwa wazazi wa mtoto yule na kumdadisi kuhusiana na barua zile alizokuwa akimwandikia mkewe. Mtoto yule alikiri kwamba ni kweli alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwalimu wake kwa miezi kadhaa sasa, na alikiri kwamba anampenda sana mwalimu wake huyo, na yeye, yaani mwalimu wake anampenda pia. Alimweleza mume wa mwalimu huyo kwamba, walikuwa wamenunuliana pete na pia akaweka bayana kwamba Mwalimu huyo ana ujauzito wake na wanatarajia kupata mtoto.

  Steve alimuonya yule mtoto kukaa mbali na mkewe kisha akarudi nyumbani kwake ili kukabiliana na mkewe. Mkewe hakusika kukiri kuwa na uhusiano na mtoto yule na pia kuwa na ujauzito wake. Kuanzia hapo siri ikawa ishajulikana kwa mtu watatu, yaani yeye mwalimu Mary, mwanafunzi wake ambaye ndiye mhusika wa ujauzito ule na mumewe.

  Steve alikaa na siri ile kwa miezi kadhaa kabla hajamweleza mmoja wa ndugu zake. Ndugu huyo alitoa ripoti kwenye kituo cha kulinda haki za watoto pamoja na mamlaka ya elimu ya mji huo, lakini hakuishia hapo alifikisha habari hiyo Polisi ambapo Mwalimu Mary alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake hadi kubeba ujauzito.

  Hata hivyo aliachiwa kwa dhamana na kesi yake kuahirisha ili kupisha ajifungue. Hatimaye Mwalimu Mary alijifungua mtoto wa kike aliyemwita Audrey mnamo Mei 1997, wakati huo akiwa nje kwa dhamana akisubiri kusomewa hukumu.

  Huo ukawa ndio mwanzo wa mikosi kumuandama kwani alisimamishwa kazi yake ya ualimu katika shule aliyokuwa akifundisha. Na mumewe naye alimuacha kwa talaka na kuondoka jimboni humo na kwenda kusikojulikana akiondoka na watoto wake wanne. Huku jukumu la malezi ya mtoto aliyezaliwa akiachiwa mama wa mtoto aliyempa mimba.

  Pamoja na kukiri kwamba alichokifanya ni kosa, lakini pia hakuonekana kujutia kosa hilo na badala yake alikuwa akijaribu kuhalalisha kosa alilolifanya. Aliwaeleza askari wa upelelezi jinsi alivyokutana na mtoto huyo aliyempa ujauzito wakati akiwa darasa la pili na jinsi alivyopata shauku ya kuwa naye karibu kiasi cha kumtofautisha na watoto wenzie. "Kulikuwa na kuheshimiana kati yangu na mwanafunzi yule, na pia hisia za kuwa karibu ziliibuka katika mioyo yetu. Ni kama aina ya hisia za mtu na kaka au dada yake, hisia ambazo katu haziondoki moyoni. Lakini sikuelewa hisia hizo zilikuwa na maana gani. Niliwaza kwamba siku moja itokee amuoe binti yangu. Lakini alipofika darasa la sita akawa ni rafiki yangu mkubwa, tukawa tunatembea pamoja na kufurahia kila jambo pamoja."

  "Siku moja majira ya joto ya mwaka 1996." Aliendelea kusema mwalimu huyo akiwaeleza askari wa upelelezi. "Mwanafunzi huyu alinishangaza sana pale aliponiletea pete ambayo alinivalisha kidoleni mwangu kama ishara ya urafiki wetu, ishara hii iliwasha moto wetu wa mapenzi na baada ya siku chache tukaanza kufanya mapenzi."

  Kama ingekuwa ni jambo lisilomhusisha mtoto wa miaka 13, wala lisingewaumiza vichwa askari wa upelelezi, kwani wangelichukulia kama jambo la mtu kutoka nje ya ndoa, lakini waendesha mashitaka hawakuwa na la zaidi bali kuendelelea na kesi hiyo.

  "Simsikitikii kabisa mama huyu" alisema Florence Wolfe mtaalamu wa ushauri nasaha kwa watu walioathirika na ubakaji anayefanya kazi katika kituo cha Northwest Treatment Association kituo ambacho kiko katika mji wa Seattle. "Mwanamke anayefanya mapenzi na mtoto, kosa hilo linaweza lisipewe uzito unaostahili kwa sababu ni jambo geni katika jamii, lakini bado ni jambo linaloshangaza. Watoto wengi wa kiume wenye umri wa miaka 13 tayari wameshabalehe na wanajitambua. Lakini hilo halihalalishi mwanamke wa miaka 35 kufanya mapenzi na mtoto wa miaka 13, je mtoto wa miaka 13, ana uwezo gani wa kushiriki mapenzi na mwanamke wa miaka 35?"

  Mnamo Agosti 7, 1997, wakati kesi yake ikiunguruma katika mahakama kuu ya mkoa wa King, jimboni Washington, Mary Kay LeTourneau alionekana kuwa na huzuni wakati akisomewa mashitaka. Baada ya kusomewa mashitaka hayo wala hakukanusha alikiri mashitaka moja kwa moja.

  Mheshimiwa Jaji Linda Lau aliagiza apelekwe rumande mpaka Agosti 29, 1997 atakaposomewa hukumu.

  "Haya si maamuzi yalioyofikiwa haraka au dakika za mwisho." Alisema wakili aliyekuwa akimtetea mwalimu huyo, David Gehrke kuhusiana na mteja wake kukiri makosa. "Anajutia makosa yake kwa uchungu mkubwa, alikuwa ni mwanafunzi wake aliyevutiwa naye, kama sisi ambavyo tunaweza kuvutiwa na waalimu wetu wa kike. Alifanya kosa kubwa, lakini kama mjuavyo hakuna mwanadamu aliye mkamilifu, wote huwa tunafanya makosa. Ni mwalimu mzuri ambaye ameghafilika na kufanya kosa kubwa."

  Kwa mujibu wa sheria ya jimbo la Washington, kesi ya ubakaji hukumu yake ni kati ya miaka mitano na nusu au saba na nusu. Baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo, mwendesha mashitaka Dan Donohoe alisema kwamba, ofisi yake itapendekeza hukumu kulingana na maelekezo ya hukumu za makosa hayo kwa mujibu wa sheria. Lakini wakili wa mshitakiwa David Gehrke alikuwa na mtazamo tofauti. "Inategemea iwapo anastahili kupewa ushauri nasaha." Wakili huyo alisema hayo akilenga hukumu maalum kwa watu wanaopatikana na hatia ya ubakaji ambapo hupewa nafasi ya kupatiwa ushauri nasaha kwa matumaini kwamba hawatorudia tena kufanya kosa hilo. hukumu ya watu hao ni kifungo cha miezi sita jela ambapo wakimaliza wanatakiwa kufanyiwa ushauri nasaha.

  Baada ya mkewe waliyeachana kukiri kosa hilo Steve LeTourneau alizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza akiwa katika nyumba yake mpya jimboni Alaska. "Ninachotaka ni yeye kupewa msaada." Alisema mumewe huyo. "yule hakuwa Mary Poppins kama wengi walivyomjua." Alisema bado anampenda mwanafunzi yule, ni ujinga……….., hakika ni ujinga sijapa kuona, kama anadhani ningeweza kukubali ujinga ule ufanyike mbele ya wanangu, labda ingekuwa niwe nimekufa…"

  Steve ambaye ndiye aliyekuwa mwangalizi wa watoto wao wanne waliowapata katika maisha yao ya ndoa waliokuwa na umri wa miaka mitatu hadi kumi na mbili aliongeza kusema kwa uchungu. "Kijana wetu mkubwa amekuwa na wakati mgumu sana, amekuwa na hasira kupita kiasi na anaona kama dunia haijamtendea haki. Ingawa anampenda sana mama yake lakini anajua alichokifanya ni kosa. Ni kama wampigwa kofi usoni mwao."

  LeTourneau alikumbuka siku moja aliporudi nyumbani kutoka kazini na kumkuta mkewe akiwa amelala kwenye sofa na huyo mwanafunzi wake. "Sikutilia mashaka hali ile." Alisema. "Baadae nikaja kufuma lundo la barua zilizotumwa kwa mke wangu na huyo mwanfunzi wake, moyo ulinilipuka kwa mshtuko, nilichanganyikiwa."

  Alipoulizwa na wandishi wa habari kwa nini hakuripoti katika mamlaka zinazohusika, mara moja baada ya kujua ukweli. LeTourneau alijibu: "ni rahisi sana kuongea kuliko kutenda, kuamua tu ghafla kumpeleka mke wako mliyenzaa naye watoto wanne polisi, ni jambo lisilowezekana kirahisi."

  Baada ya hukumu yake kuahirishwa mara kadhaa Mary Kay LeTourneau, hatimaye hukumu yake ilisomwa rasmi hapo mnamo Novemba 13, 1997, mbele ya Mheshimiwa jaji Linda Lau Johnson. Wakili aliyekuwa akimtetea mshitakiwa David Gehrke alimuomba mheshimiwa Jaji Linda Lau ampe adhabu maalum inayohusiana na makosa hayo ya ubakaji. Wakili huyo alisoma barua iliyoandikwa na mama wa mwanfunzi aliyempa mimba mwalimu wake mbele ya mahakama hiyo. Katika barua hiyo mama huyo aliiomba Mahakama imuonee huruma mwalimu huyo kwani mpaka sasa amesha adhibiwa vya kutosha, na iwapo atafungwa mwanae ambaye ndiye muhusika wa katika kesi hiyo hatajisikia vizuri kusikia mwalimu wake na mzazi mwenzake kafungwa kwa sababu yake.

  Wakili huyo aliendelea kuiambia mahakama kwamba mama huyo ameshaadhibiwa vya kutosha kwani amempoteza mume na watoto wake wanne, amepoteza nyumba, taaluma yake, kazi yake na pia heshima yake kwa jamii.

  Hata hivyo mwendesha mashitaka alimtaka muheshmiwa Jaji amhukumu Mwalimi Mary kwa mujibu wa sheria inavyotaka kwani ameshapoteza sifa ya kufanyiwa ushauri nasaha kwa kosa la kubaka, kutokana na umri wake. "Huyu ni mama mtu mzima ambaye amembaka mwanafunzi wake wa miaka 13..!" Alisema mwendesha mashitaka Lisa Johnson, "Na bado haonyeshi kujutia makosa yake……" Alimalizia kusema mwendesha mashitaka huyo.

  Wakili aliyekuwa akimtetea mwalimu huyo David Gehrke alisema kwamba, ni kweli mteja wake alikuwa anajua kuwa anachokifanya ni kosa na kinyume na maadili ya kazi yake, lakini hiyo ilitokana na hali yake kiafya. Wakili huyo alidai kwamba Mwalimu Mary alikuwa anasumbuliwa na tatizo linalofahamika kama Hypomania. Wakili huyo aliendelelea kusema kwamba, ingawa kitendo alichofanya ni kosa, lakini hakikuwa na madhara makubwa, kama makosa mengine ya ubakaji yanavyokuwa, kwa sababu hata mtoto mwenyewe alishiriki kikamilifu kushawishi uhusiano huo uwepo na hakuwaki kulalamika wala kuonyesha dalili kwamba aliathirika kutokana na ushusiano wake na mwalimu wake.

  Mary Kay LeTourneau alimkumbatia wakili wake pamoja na mama wa mtoto aliyezaa naye mara baada ya Mheshimiwa Jaji kusoma hukumu. Katika hukumu yake Mheshimiwa Jaji Linda Lau, hakukubaliana na pendekezo la upande wa mshitaka la kutaka Mwalimu huyo ahukumiwe kifungo cha miaka sita jela na badala yake akamhukumu kifungo cha miezi 6 gerezani zikiwemo siku 100 ambazo tayari alikwishakaa jela akisubiri hukumu yake. Jaji huyo alisema kwamba mtuhumiwa sio tishio kwa jamii hivyo haoni sababu ya kukubaliana na hukumu ya miaka sita gerezani kama iliyopendekezwa na waendesha mashitaka.

  Hata hivyo baada ya kumaliza kifungo chake gerezani mwezi mmoja baadae, Polisi waliona gari likiwa limepaki kusini mwa jiji la Seattle huku taa zikiwa zinawaka, ilikuwa ni majira ya saa 9:00 usiku, na walipolisogelea walimkuta mwalimu Mary Kay LeTourneau akiwa na mwanafunzi wake Vili Fualaau. Kutokana na kosa hilo alihukumiwa kifungo cha miaka saba na nusu gerezani hapo mnamo Februari 6, 1998.

  La kushangaza wakati akiwa gerezani, mwalimu huyo kupitia kwa wakili wake alithibitisha kwamba anao ujauzito mwingine na baba wa mtoto huyo ni yule yule mwanafunzi wake Vili Fualaau. Mnamo Octoba 1998 akiwa gerezani alijifungua mtoto wa kike tena akamwita Georgia Alexis na kufanya awe amezaa watoto sita kwa ujumla hawa wawili wa mwisho akiwa amezaa na mwanafunzi wake

  Mnamo Agosti 4, 2004 aliachiwa kutoka gerezani kwa mpango maalum wa kutumikia jamii. Baada ya kuachiwa kutoka Gerezani Vili Fualaau ambaye alikuwa na umri wa miaka 21 wakati huo, aliomba mahakama iondoe zuio lililowekwa la mwalimu Mary kuwa mbali na yeye. Siku chache baadae zuio hilo lilondolewa.

  Mary Kay LeTourneau na Vili Fualaau walifunga ndoa rasmi hapo mnamo May 2005 katika mji wa Seattle na kuanza maisha mapya kama mke na mume.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya ni Ijumaa nyingine tena leo...
  Hili ni onyo kwa wale wanaopenda Viserengeti Boys, Sheria ipo na inafanya kazi...........LOL
   
 3. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kunyongwa tu, yani ndio maana nahisi sikua mwanasheria, ninge hukumu sana adhabu ya kifo kwa kesi za mna hizi, wala nisingekua napoteza mda aw kumsikiliza mshitakiwa.....:cheer2::fencing::shut-mouth:
   
 4. Reserved

  Reserved Content Manager Staff Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 750
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mhhh Mtambuzi huyo dogo alipenda mama mtu mzima aise
  Mbona mama atazeeka na kumuacha dogo akiwa na afya yake
  Kweli duniani kuna mambo aise
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Aisee hii kesi ina vituko sana! Duuuu 13-35?
  Hila ingekuwa kwa nchi kama yetu wala kuingekuwa na case hapo! Lakini ingekuwa mwana ume wa miaka 35 ammempa binti wa miaka 13 ange juta!

  Duuu huyu mwalimu na mwana funzi wake si mchezo full vituko wao ni mimba juu ya mimba!

  Ila mwalimu kakosa maadili kabisa maana amesha muharibu huyo mtoto!

  Na yale mambo ya kumkabidhi mtoto wako kwa mwalimu fulan nayo yana changia!
   
 6. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Duh!
  Dogo Katisha,Yaani Kumfanya Mama Mtu Mzima Kuhasi Familia Yake!!?

  Mtambuzi We Balaaaa....Kwa Mastori Matamu!
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi hii hi balaa
  Mama mtu mzima na kiserengeti boy mpaka kupata mimba mara mbili na kuja kuoana kabis a
  Kweli mama aliamua liwalo na liwe
  Ila kijana ataachwa akiwa rijali mama atakuwa mtu mzima kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  si kila kosa lina adhabu ya kifo na wala maamuzi au hukumu si maamuzi ya mtu mmoja!

  Hivi ingekuwa Tz kesi ya namna hii unafikiri ingefika mahakamani?
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh kisa cha kusisimua kweli binafsi leo utanishangaa sana Mtambuzi Mahakama haikumtendea haki Mary Kay yamkini wengefungwa wote na kiserengeti boy chake nisingekasirika hata kidogo.Hili nifunzo kubwa kwa wakina mama wanaopenda viserengeti boy wazee tuko kwanini mnakimbilia viserengeti boy.

  Umenikumbusha mbali sana unajua kipindi nikiwa mdogo aliletwa beki tatu toka Iringa akawa ananifundisha mambo ya kikubwa wakati wazazi wamekwenda mzigoni siku moja Baba akarejea nyumbani kabla ya muda uliozoeleka akatukuta tunaendeleza libeneke mweh nakwambia kesho yake jioni beki tatu akarejeshwa kwao ha ha ha.Sijui Mama na Baba walinifikiriaje wakati huo ha ha ha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. S

  SicheKi Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu bado utasikia kelele za 'HAKI SAWA', usawa hapo uko wapi?
   
 11. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kila afanyae kosa adhabu yake ni kunyongwa tuuuu....
   
 12. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  pamoja sana mkuu Mtambuzi....eid Mubaraak
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hii nayo kali
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Duh mimi mwalimu wangu wa BTP kipindi hicho alinikosa kosa
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hili huwa nawambia watu kila siku...sijui kwa nini baadhi hawataki kuamni kuwa wanawake na wanaume wana biology ambazo zinatofautiana sana...

  After 20 years...dogo atakuwa 33.....bado anadai sana wakati huo mama ni 55.....Hana tena haja na mambo ya mapenzi....

  Hata sijui wataishije hao watu....bahati yao huko kwao maduka yamejaa maplastic....ila lolote linaweeza kuwakuta!!

  Ahsante sana Mtambuzi kwa story!

  Babu DC!!
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mweh mweh dogo alianza mapemaaaaaaa,
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA huyu alichelewa, mie nilianza na miaka 6..........!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Gunda66

  Gunda66 JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Ki ukweli hyo mtoto alimpenda mwalimu wake,,, yaan alimpa mimba ya kwanza thn ya pili na bado akasubiria mwalimu amalze kifungo chake cha miaka saba(7) na bdo akamwoa!!! sisiti kusema kwamba lilikuwa ni Penzi la dhati kwa hawa wote wawili

  but kiukweli imenishangaza,,, Mtambuzi Asante kwa kisa kngne tena!!!
   
 19. k

  kisilo Senior Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeipenda maana imeka kama comedy.
   
 20. h

  hacena JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  kwa mujibu wa sheria za Tanzania sio kosa kwa mtoto chini wa miaka 18 wa kiume kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa miaka 20 na kuendelea, sheria ya kujamiiana ya Tz inatamka male person na a girl under
   
Loading...