Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000


Asha Mkwizu Hauli akipelekwa Mahakamani


R. v. Asha Mkwizu Hauli
, Crim Sessions Case No 3 of 1984 (DSM) (unreported).


Mnamo tarehe 19 Novemba , 1983 mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwanahamisi Happiness Senzota alikwenda katika kituo cha Polisi cha Salender Bridge. Alipofika pale kituoni alikutana na askari wa upelelezi aliyejulikana kwa jina la Haruna Masumai ambapo alitoa malalamiko yake kwamba mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Asha Mkwizu ametishia kumdhuru.

Mpelelezi huyo alifanya mawasiliano na mtuhumiwa na ilipofika tena tarehe 21 Novemba wote wawili mlalamikaji Happiness Senzota na mtuhumiwa Asha Mkwizu walifika kituoni hapo kama walivyoelekezwa na askari huyo wa upelelezi. Na kutokana na maelezo yao ndipo askari huyo alipogundua kwamba Happpiness alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa Asha Mkwizu aliyetajwa kwa jina la Dr. Hauli. Baada ya kuchukua maelezo yao aliwaambia waende lakini waje tarehe 22 Novemba 1983 ambayo ilikuwa ni siku inayofuata.

Kwa mujibu wa house boy wa Asha Mkwizu aliyejulikana kwa jina la Musa James, alidai kwamba mnamo tarehe hiyo ya 22 Novemba 1983, bosi wake Asha Mkwizu alimtuma kwenda kununua mkaa, baada ya yeye Musa kuandaa chai na kumwagia maji katika bustani ambapo alidai pia kuona shimo la urefu wa kama futi tatu kwenda na chini upana wa futi tatu na nusu hapo bustanini. Musa alitakiwa kwenda kununua mkaa Kariakoo na alitakiwa na Asha asirudi kabla ya saa sita mchana. Na baada ya kutoa maelekezo hayo Asha Mkwizu, aliondoka kwenda kituo cha Polisi cha Salender Bridge kama walivyotakiwa na askari wa upelelezi wa kituo hicho.

Walifika hapo kituoni kukutana na askari wa upelelezi Harun. Lakini askari huyo aliwaambia kwamba asingeweza kusikiliza shauri lao kwa sababu Dr. Hauli hayupo nchini kwa hiyo wasubiri mpaka hapo atakaporudi, ndipo wazungumzie shauri lao na kupatiwa muafaka. Askari huyo wa upelelezi aliwasihi wasije wakadhuriana wakati wanamsubiri Dr. Hauli. Baada ya kuwaonya Happiness ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka na baada ya dakika 10 Asha Mkwizu naye akaondoka. Huo ndio ulikuwa mwisho wa Mwanahamisi Happiness Senzota kuonekana akiwa hai.

Kwa mujibu wa House boy wa Asha Mkwizu, alidai kwamba alirudi kutoka Kariakoo kununua mkaa na alipofika nyumbani alimkuta mdogo wake Dr. Hauli aitwae Robson Hauli akiwa hapo nyumbani, alimkuta bosi wake Asha pia akiwa hapo nyumbani. Asha alimwambia Musa aandae ndizi kwa ajili ya watoto, lakini Musa alishangaa kuona damu pale sebuleni na ilikuwa ni damu nyingi. Asha alimwambia Musa kwamba amejiumiza na alimtaka asafishe ile damu pale sebuleni na kule bafuni pia ambapo damu ilikuwa imeganda ukutani. Mnamo tarehe 24 Novemba 1983, Asha alimweleza Musa, "Nimemmaliza adui yangu"

Musa alipomuuliza ni nani huyo adui yake aliyemmaliza, Asha alimjibu kuwa ni Happiness Senzota. Asha aliendelea kumweleza Musa kwamba amemuua Happiness na kumzika katika eneo la hapo nyumbani, lakini alikataa kumuonyesha Musa mahali alipouzika mwili huo. Mnamo 27 Novemba, 1983, Musa alikwenda kuripoti jambo lile Polisi ingawa alionywa na Asha kwamba atunze siri hiyo na asije akamweleza mtu yeyote kuhusu jambo hilo. Baada ya Musa kuripoti Polisi, Asha alikamatwa na baada ya kuhojiwa alionyesha mahali alipouzika mwili wa Happiness.

Polisi waliufukua mwili huo na baada ya uchunguzi wa awali ilithibitishwa kwamba mwili ule ulikuwa ni wa Mwanahamisi Happiness Senzota. Uchunguzi zaidi ulionyesha kwamba ule mwili ulikuwa na majeraha matatu, jeraha moja katika mkono wa kushoto, na majeraha mawili yalikutwa kichwani, moja likiwa kubwa kwa upana wa sm 5 likiwa na kina kirefu kiasi cha kufumua ubongo. Hili jeraha ndilo lililoelezwa Na Daktari kusababisha kifo cha Happiness Senzota.

Mnamo 29 November 1983 SSP Gewe alimhoji mtuhumiwa na baadae mlinzi wa amani naye alimhoji mtuhumiwa huyo, ambapo maelezo hayo yalitumika kama ushahidi pale mahakamani dhidi yake.Kesi hii ni ya mwaka 1983 ya Asha Mkwizu Hauli, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Mwanahamisi Happiness Senzota hapo mnamo tarehe 22 Novemba 1983 nyumbani kwake katika mtaa wa Lugalo Upanga. Kosa hilo la Kuuwa kwa kukusudia (Murder) limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu (Penal Code) kifungu cha 196.

Kesi ilisikilizwa katika mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Jaji A. Bahati akisaidiwa na Wazee wa Baraza waliojulikana kwa majina ya Bi. Mwasabuli Ali na mwenzie aliyejulikana kwa jina moja la Mzee Kikoti.Upande wa mashtaka katika kesi hii waliita jumla ya mashahidi 14. Hapakuwa na ubishi wowote kwamba, Mwanahamisi Happiness Senzota amefariki na amefariki kwa kuuawa akiwa mikononi mwa Asha Mkwizu Hauli. Mtuhumiwa mwenyewe alikiri kumuua Happiness kwa kumpiga na chuma kizito kichwani ambacho kililetwa pale mahakamani kama ushahidi. Pia mtuhumiwa alikiri kwamba, kutokana na kumpiga Happiness ikawa ndio sababu ya kifo chake.

Matokeo ya uchunguzi wa daktari (Post Mortem) ulibainisha kwamba kifo cha Happiness kilitokana na kupasuka kwa fuvu la kichwa na kupelekea athari kubwa katika ubongo.Mwendesha mashtaka alibainisha pale mahakamani kwamba mtuhumiwa alimuua Happiness baada ya kumshawishi afuatane naye hadi nyumbani kwake na baada ya kumuua aliuchoma mwili wa marehemu moto na kisha kuuzika katika bustani yake na baadae kuondoa ushahidi ili kuficha mauaji hayo. Ili kuthibitisha ukweli wa tuhuma hizo mwendesha mashtaka alileta mashahidi na pia alileta vielelezo pale mahakamani.

Mtuhumiwa utetezi wake ulikuwa kwamba, Marehemu Happiness alimkashifu kupita kiasi wakati alipokuwa hapo nyumbani kwake kiasi kwamba alipatwa na hasira kali zilizopitiliza na kumpiga na kipande cha chuma kichwani mara moja. Katika maelezo yake wakati anahojiwa, Asha alitoa maelezo marefu kuhusiana na maisha yake na matatizo yake ya ndoa na Dr. Hauli. Aliendelea kueleza jinsi alivyokuja kugundua kuhusu mahusiano aliyokuwa nayo Happiness na Mumewe na jinsi alivyokuwa akipelekwa na Polisi na Happiness mara kwa mara kujibu tuhuma kwamba alikuwa akimtishia kumdhuru yeye Happiness.

Asha alidai kwamba mnamo hiyo tarehe 22 Novemba alikwenda tena Polisi kama alivyoelekezwa, baada ya swala lao kuahirishwa siku moja iliyopita. Alipofika pale alimkuta Happiness tayari ameshafika. Lakini askari huyo aliwaambia kwamba asingeweza kusikiliza shauri lao kwa sababu Dr. Hauli hayupo nchini kwa hiyo wasubiri mpaka hapo atakaporudi, ndipo wazungumzie shauri lao na kupatiwa muafaka. Askari huyo wa upelelezi aliwasihi wasije wakadhuriana wakati wanamsubiri Dr. Hauli. Baada ya kuwaonya happiness ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka na baada ya dakika 10 na yeye aliondoka na alimkuta Happiness akiwa kasimama kwenye taa za kuongozea magari pale Salender Bridge akiwa anasubiri kuvuka. Walivuka pamoja upande wa pili ilipo Hoteli ya Palm Beach. Ndipo Asha alipomuaga Happiness na kumtaka amfikishie salaam zake kwa mkuu wa shule anakofanyia kazi yeye Happiness aliyemtaja kwa jina la Mwalimu Mpanda.

Lakini Happiness akadai kwamba haendi shule. Lakini pia akamwambia Asha kwamba anajisikia njaa na anahitaji kitu cha kula. Asha alimweleza kwamba kwa muda ule hakuna huduma pale katika Hoteli ya Palm Beach kwani ilikuwa ni saa nne asubuhi. Happiness alimuuliza ni wapi anaweza kupata duka la vinywaji baridi na ndipo Asha akamjibu kuwa jirani na anapoishi kuna kioski kinauza vinywaji baridi na kuku wa kukaanga. Happiness alisema ni vyema akioneshwa hicho kioski. Walikubaliana waende pamoja ili baadae yeye Happines awahi kwa dada yake ambaye ilikuwa ampeleke kwa Dr. Mvungi kwa matibabu.

Kwa maelezo hayo Asha alionekana kukwepa hoja kumshawishi Happiness ili wafuatane nyumbani kwake kama alivyonukuliwa katika maelezo ya awali wakati akihojiwa na Polisi. Asha alidai kwamba alikuwa hayuko katika hali nzuri wakati anahojiwa na SSP Gewe na hakusomewa maelezo yake na badala yak alitakiwa kuweka sahihi yake katika sehemu zote zilizowekwa X.

Asha aliendelea kueleza kwamba walifika nyumbani na kumkaribisha Happiness hapo nyumbani kwake ambapo alitoka kwenda kununua chupa mbili za bia na chupa moja cocacola. Alichanganya bia na cocacola kwenye glasi akiwa jikoni kwa sababu Happiness alitaka achanganyiwe vivyaji hivyo kwa mtindo huo. Walikunywa pamoja vinywaji hivyo pamoja na ndizi. Wakati huo walikuwa wakizungumza pamoja. Asha alimweleza Happiness ni kwa jinsi gani wote wawili walivyo na mnasaba na Dr. Mvungi. Na hapo ndipo Happiness aliposema Dr. Hauli ni wake na hawezi kumwacha mpaka kufa.

Baadae aliomba aonyeshwe kilipo choo, ambapo alioonyeshwa. Wakati Asha anaosha glasi hapo jikoni, Happiness alifika hapo jikoni na wakati ananawa mikono yake akaanza kumkashifu yeye Asha kwa kumwambia, "Hivi kwa nini unanifuata fuata wewe kizee, huna thamani tena na umeshakwisha, na umgumba. Kama mumeo angekuwa anakuthamini angekufungia wewe na wanao kuja kupitisa usiku kwangu?" Asha akamwambia, "Happiness, wewe ni kama mwanangu, huwezi kunitusi kiasi hicho." Ndipo Happiness akamwambia Asha kwa kipare, "Chebakie ni Kushoshorwa hena mzuti na vichaa." Maneno hayo yalitafsiriwa kama, "Kilichobaki ni wewe kupata mtu wa kukutia vidole mkunduni."

Na baada kusema hivyo Happiness alimsukuma Asha ambapo shubaka la zana likaangua mguuni mwa Asha, wakati asha anaondoa shubaka lile mguuni mwake, Happiness alimfuata Asha pale alipo na ndipo alipookota kipande cha chuma na kumpiga nacho. Mara aliona damu nyingi ikivuja na alijaribu kumpa huduma ya kwanza lakini haikuwezekana, Happiness Alifariki. Kuhusu kuuchoma moto mwili wa marehemu kabla ya kuuzika mtuhumiwa alidai kwamba tukio hilo lilitokea kama bahati mbaya.Mtuhumiwa alikanusha kumwambia house boy wake Musa kuwa asirudi nyumbani mpaka saa sita mchana. Anachojua ni kumweleza Musa kwamba awe makini asije akakamatwa na Polisi kama mzururaji kwa sababu hakuwa na kitambulisho.

Pia alikanusha madai ya Musa aliyowaeleza Polisi kwamba yeye Asha alichimba shimo kwenye bustani kabla ya kumuua Happiness, madai mengine aliyokanusha ni kuhusu kumweleza Musa kwamba amemuua adui yake. Alisema alimweleza Musa kwamba kuna tukio limetokea kwa bahati mbaya na amemuua mtu na kumzika katika bustani na alimuonyesha Musa kaburi alipomzikia Happiness. Asha aliieleza mahakama kwamba kama angekuwa na dhamira ya kumuua Happiness basi angemuua kwa sumu kwa sababu yeye kama Muuguuzi anajua sumu za aina nyingi ambazo angaweza kuzitumia.

Alimalizia kwa kusema kwamba anafahamu kuwa ndugu zake na mumewe Dr. Hauli walikuwa wanataka yeye Dr. Hauli aoe mke mwingine kutoka katika kabila lake na amekuwa akisikia tetesi kwamaba anatakiwa kurudishwa kwa wazazi wake na mumewe.Mtuhumiwa alifanyiwa usaili kwa muda mrefu kutokana na maelezo yake na alidai kwamba yeye ni mkubwa kwa umri na na kimo zaidi ya Marehemu. Kuhusiana na maelezo ya Musa alidai kwamba Musa anaweza kudanganya kwa sababu ametokea Kusini kama ilivyo mumewe Dr. Hauli.

Pia alitaja idadi ya mahawara aliokuwa nao mumewe wakiwemo wanawake wa wazungu.Alipoulizwa na Mahakama kwa nini mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha matatu wakati alidai kwamba alimpiga marehemu kwa pigo moja tu, Asha alijibu kwamba, alimpiga marehemu kwa kile chuma mara moja katika mkono wake na wakati anaanguka alijigonga sakafuni kwa kishindo na ndio akaumia.Akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa wazee wa baraza mtuhumiwa huyo alisema. Mtu akikupeleka Polisi hawezi kuwa rafiki yako, lakini yeye binafsi hakuwa akimchukia marehemu, na hata alipokuja kugundua kuwa marehemu alikuwa na uhusiano na mumewe hakuwa na kinyongo naye.
Alipoulizwa kwa nini katika mahojiano yake na Polisi na pia mlinzi wa Amani hakueleza lile tusi alilotukanwa kwa Kipare na marehemu.

Asha alijibu kwamba, Polisi walimwambia hawahitaji maneno mengi na ingawa alilitaja tusi hilo lakini Polisi hawakuliandika katika maelezo yake. Pia Polisi walimwambia aeleze kwa mlinzi wa Amani yale yote alivyowaeleza bila kuongeza kitu.
Katika kesi hiyo kulikuwa na mashahidi watatu wa mtuhumiwa ambao ni Yahaya Mkwizu, kaka yake mtuhumiwa, Benson Hauli, baba mkwe wa mtuhumiwa, na Dr. Rugeyamu mtaalamu wa magonywa ya akili (Consultant Psychiatrist)Shahidi wa kwanza aliieleza mahakama kuhusu kikao kilichokaa kwa Dr. Hauli na kuamua mtuhumiwa arudishwe kwa wazazi wake.

Dr. Rugeyamu alitoa ushahidi kuhusu vipimo alivyomfanyia mtuhumiwa baada ya tukio lile la kuua ili kujua kama alikuwa na matatizo ya akili wakati alipokuwa akitekeleza mauaji hayo. Dr. Rugeyamu aligundua kwamba mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili ambayo kwa kawaida hutokana na matatizo ya ndoa na pia alikuwa na msongo wa mawazo (Depression) kutokana na matatizo ya kifamilia aliyokuwa nayo. Dr. Rugeyamu alikamilisha ripoti yake kwa kubainisha kwamba yote hiyo ilitokana na kile alichokiita kuondokewa kwa hali ya ubinadamu (diminished responcibility).

Wakimtetea mtuhumiwa katika kesi hiyo pale mahakamani mawakili wa mshitakiwa (Counsels) wote kwa pamoja walikuwa na hoja ya kumtetea mtuhumiwa. Akimtetea mtuhumiwa, mmoja wa mawakili hao (Counsel) aliibua dhana ya Hasira ziliopindukia (Defence of Provocation) na aliungana na ripoti ya daktati wa magonjwa ya akili Dr. Rugeyamu ambayo ilikuwa ndio kielelezo cha tatu (Exibhit 3) pale mahakamani ambacho kilibainisha kwamba mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili wakati akitekeleza mauaji hayo, na aliendelea kusema kwamba ni hali hiyo ndiyo iliyosababisha mtuhumiwa kushindwa kuzuia hasira zake. Wakili huyo alitoa mifano ya kesi kadhaa ambazo zinakubaliana na nadharia ile.

Aliitaka mahakama kukubali kwamba mtuhumiwa alipatwa na hasira zilizopindukia baada ya kukashifiwa kupita kiasi na marehemu na ndio sababu ya kufanya kile alichofanya.Akijibu hoja hio mwanasheria wa serikali alisema mtuhumiwa alimshawishi marehemu aende naye nyumbani kwake ili aweze kumuua na hiyo dhana ya kukasirishwa kupindukia (Provocation) haiwezi kupewa nafasi katika kesi ile.Alirejea ushahidi uliotolewa na mashahidi pale mahakamni hususan ushahidi uliotolewa na Musa ili kupinga dhana hiyo ya kukasirishwa kupindukia.Mwanasheria huyo alisema, na hapa nanukuu,
"Napenda kujumusha maelezo yangu mbele ya wazee wa baraza kwamba sheria inasemaje kuhususiana na dhana ya kukasirishwa kupindukia (Provocation) kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 202 cha kanuni ya adhabu kwa kutofautisha na kifungu cha sheria cha 192 cha kanuni ya adhabu cha mwaka 1945.

Ningependa pia kuwaeleza wazee wa baraza nafasi ya sheria kuhusiana na dhana ya kuondokewa kwa hali ya ubinadamu (diminished responsibility) kwa mujibu wa sheria zetu hapa nchini....... I understood the point that in provocation the test used was that of a reasonable of ordinary man, hence an objective test rather than a subjective test."
Mwisho wa kunukuu.

Mzee wa baraza wa kwanza Bi. Mwasabuli Ali hakukubaliana ushahidi wa dhana ya kukasirishwa kupindukia (provocation) na aliridhia ushahidi wa kwamba mtuhumiwa alipanga kumuua marehemu na alisema mshitakiwa anayo hatia ya kuua kwa kukusudia. Pia mzee wa baraza wa pili mzee Kikoti alikubaliana na mwenzie.

Kesi hiyo iliisha kusikilizwa kwake, na mnamo tarehe October 2, 1985, na Mheshimiwa Jaji A. Bahati alisoma hukumu ya kesi hiyo.

Akisoma hukumu hiyo muheshimiwa Jaji A Bahati alisema, na hapa namnukuu, "Sasa nitafanya majumuisho na kuweka maoni yangu katika kesi hii. Ni wazi kwamba hakuna ubishi kuwa Mwanahamisi Happiness Senzota amekufa, na amekufa akiwa mikononi mwa mtuhumiwa Asha Mkwizu Hauli. Na ni dhahiri kuna ushahidi wa kuthibitisha hilo. Kwa hiyo basi ni ukweli kwamba Mwanahamisi happiness Senzota amekufa na kifo chake kilitokana na kuuliwa kikatili na mtuhumiwa. Kilichopo ndani ya shauri na tunachokizingatia katika shauri hili na kutolea maamuzi ni kuangalia kama je mtuhumiwa alimuua marehemu kwa thamira ovu au la." Mwisho wa kunukuu...............

Jaji Bahati alielezea ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao ulioanisha matukio yaliyofuatana ili kuthibitisha kwamba mtuhumiwa alikuwa amedhamiria kwa makusudi kabisa kumuua marehemu, kuanzia maandalizi ya kaburi lililochimbwa katika bustani kwa ajili ya kumzika marehemu baada ya kumuua na kitendo cha mtuhumiwa kumuonya house boy wake Musa, kwamba asirudi kutoka huko alikomtuma kabla ya saa sita mchana, ili apate muda wa kuuwa na kuzika mwili wa marehemu. Pia kulikuwa na kitendo cha mtuhumiwa kumshawishi au kumlaghai marehemu ili aende nyumbani kwa kwake yeye mtuhumiwa mtaa wa Lugalo, Upanga na baadae huduma ya vinywaji na kitendo cha kukashifiwa na marehemu ambacho kilipelekea kuuawa kwake. Pamoja na hayo pia kulikuwa na kitendo cha mtuhumiwa kuuchoma moto mwili wa marehemu na kisha kuuzika ikiwa ni pamoja na kusafisha nyumba ili kuondoa ushahidi. Pia kulikuwa na taarifa kwa Musa kwamba ameshammaliza adui yake na onyo kwa Musa kwamba asije akamwambia mtu yeyote.Upande wa mashtaka ulikuwa na hoja kwamba hata kama marehemu alikuwa amemkashifu kupita kiasi mtuhumiwa, lakini bado jambo hilo haliwezi kumkera mtu mzima kufikia kufanya kitendo kama alichofanya mtuhumiwa.

Mahakama ilirejea kifungu cha sheria cha 202 kuhusiana na dhana ya kukasirishwa kupindukia (Provocation). Hata hivyo mheshimiwa Jaji Bahati alisema atarejea kwenye kanuni ya adhabu baadae.Akizungumzia utetezi wa mawakili wa mtuhumiwa Mheshimiwa Jaji Bahati alisema. Namnukuu,"Upande wa utetezi kwa upande mwingine umekataa kukubaliana na ushahidi uliotolewa dhidi ya mtuhumiwa kwamba alikuwa amepanga kwa makusudi kabisa kumuua marehemu, na badala yake walikuja na madai ya mtuhumiwa kukasirishwa kupindukia (Provocation)"

Kisha Mheshimiwa Jaji Bahati akaendelea,
"nimekuwa nikiwaza sana kuhusu kesi hii, na nimefikia kuamini kwamba hakukuwa na swala la kukasirishwa kupindukia katika kesi hii, na ningependa kuungana na wazee wa baraza kwamba hakukuwa na swala la kuchokozwa katika kesi hii." Mwisho wa kunukuu.Mheshimiwa Jaji alitoa sababu za kuamini hivyo kama ifuatavyo, kwanza ilikuwa ni maelezo ya mtuhumiwa (Extra Judicial) ambayo yalichukuliwa pale mahakamani kama ni ushahidi wa sita (Exhibit P6) katika kesi hiyo, ambapo mtuhumiwa alimuomba marehemu wafuatane hadi nyumbani kwake ambapo angempatia vinywaji na baadae hela ya taxi. "Je kitendo hiki tukiiteje kama si kushawishi au kulaghai?" Alihoji Mheshimiwa Jaji Bahati, kisha akaendelea..

"Pia katika utetezi wake mtuhumiwa alidai kwamba kitendo cha kushawishi au kulaghai kama ilivyoandikwa katika maelezo yake Polisi ambao ni ushahidi wa tano (Exhibit P5) kuhusiana na swala hilo la kumshawishi marehemu, mtuhumiwa alidai kwamba Polisi ambaye ni shahidi wa 10 (PW 10) aliongeza maneno ambayo hayakutoka kinywani mwake, lakini wakati huo huo, mtuhumiwa hakukanusha madai hayo katika maelezo yake hapa mahakamani kama yalivyonukuliwa katika ushahidi wa sita (Exhibit P6)."

Mheshimiwa Jaji alikubaliana na maelezo ya Polisi kwamba ni ya ukweli kwa sababu Polisi huyo aliyemhoji mtuhumiwa ni mtu mkubwa na kwa nafasi yake hawezi kuandika kitu ambacho hakikutamkwa na mtuhumiwa na badala aliandika kile kilichosemwa na mtuhumiwa na alimsomea maelezo yote kama alivyomnukuu na mtuhumiwa akaweka sahihi.Akizungumzia juu ya ushahidi huo wa mtuhumiwa kupanga mauaji, Mheshimiwa Jaji Bahati alizungumzia juu ya ushahidi wa house boy wa mtuhumiwa. Kama alivyoileleza mahakama.Mheshimiwa Jaji alisema. "Lakini katika maelezo yake, Mtuhumiwa alipinga maelezo ya Musa akidai ameidanganya mahakama. Kwa mujibu wa mtuhumiwa alidai kwamba Mtuhumiwa alisema ushahidi wa Musa sio wa kweli kwa sababu, Musa ametoka eneo moja na Dr. Hauli na pia aliogopa kwamba angedhaniwa kuwa yeye Musa ndiye aliyemuuwa marehemu. Pia alibainisha kwamba hakuwa na mahusiano mazuri na Musa."

Jaji Bahati akizungumzia madai hayo alidai kwamba, maelezo ya Musa hayamshawishi kuamini kwamba ni muongo. Na hata majibu yake wakati akihojiwa pale mahakamani hayakuonyesha kwamba ni muongo. Alichokiona yeye ni kwamba, Musa alikuwa ni shahidi aliyesema ukweli.Mheshimiwa Jaji alisema kwamba haoni sababu ya Musa kudanganya dhidi ya mtuhumiwa, kwani ni sawa na mtu kudanganya dhidi ya rafiki yake kama ilivyo katika kesi hii, bila sababu ya msingi. Na ndio sababu akakubaliana na ushahidi wa Musa kwamba ni wa ukweli.Alithibitisha madai ya upande wa mashtaka kwamba mtuhumiwa alipanga kumuua marehemu kama ilivyonukuliwa katika maelezo yake wakati akihojiwa na Polisi, Mheshimiwa Jaji Bahati alinukuu maelezo hayo kama ifuatavyo:

"hapo ghadhabu zilinishika na kwa ghafla nilichukua lichuma fulani fupi ambayo (sic) ilikuwa karibu na mlango wa jiko aliko huyo Manahamisi Happiness Senzota na kumpiga nacho kichwani akiw amesimama kwa nyuma, hapo nilimwona ameanguka chini nilimpiga tenakichwani kwa kutumia hicho hicho chuma ambapo pia ilimpata (sic) sehemu ya mkono.................."

Upande wa utetezi ulidai kwamba SSP Gewe aliongeza hicho kipengele ili kesi hii imuwezesha kupanda cheo. Jaji Bahati hakukubaliana na maoni hayo.Pia Jaji Bahati alizungumzia ushahidi wa Daktari aliyemfanyia mtuhumiwa vipimo ili kubaini kama mtuhumiwa alikuwa amerukwa na akili wakati akitekeleza mauaji hayo. lengo lilikuwa ni kupinga ile dhana ya kukasirishwa kupindukia (Provocation) kama alivyodai mtuhumiwa. na hapa alinukuu maelezo ya mtuhumiwa kama alivyoeleza katika maelezo yake Polisi:

"........Nilifanya mauaji hayo kwa sababu ya hasira nyingi tokana na marehemu kutaka kuvunja nyumba yangu."Mheshimiwa Jaji alisema kwamba maelezo hayo yanathibitisha kuwa mtuhumiwa alipanga kumuua marehemu ili kulipiza kisasi kama alivyonukuliwa na Polisi.Kilichofuata baada ya mauaji hayo, pia ni muhimu ili kuthibitisha kwamba mauaji yalikuwa ni ya kupangwa. Hapa chini ni maelezo ya mtuhumiwa wakati akihojiwa nna Polisi:

"......... Nilimburuza hadi bafuni ambapo nilichukua mafuta ya taa na kumwaga katika shuka niliyomfunika nayo na kuwasha kibiritiambapo mmoto ulilipuka na kumchoma marehemu sehemu kadhaa za mwili (sic). Na madhumuni yangu ni kwamba akauke damu isizidi utoka..............niliingia ndani na kuiweka maiti ndani ya jamvina kuiviringisha shuka ya kitandani. Niliiburuza maiti toka ndani hadi kwenye shimo hiyo (sic) na kuitumbukiza.

Maelezo hayo yaliendelea kwamba mtuhumiwa alifanya usafi ili kuficha ushahidi na kisha alienda kazini na kufanya kazi kama kawada na kisha kurejea nyumbani saa nne usiku.Pia Mheshimiwa Jaji alizungumzia maoni ya mzee wa baraza Bi Mwasabuli Ali. Kwa mujibu wa maoni yake Bi Mwasabuli alisema kwamba, haamini kuwa marehemu ambaye alimshitaki mtuhumiwa anaweza kumuomba mtuhumiwa amwelekeze mahali panapouzwa vinywaji baridi. Alisema, haamini kwamba marehemu ambaye sio mgeni hapa jijini Dar asiwe anajua mahali panapouzwa vinywaji baridi. Bi Mwasabuli alisema pia haamini kwamba marehemu anaweza kumkashifu mtuhumiwa wakati akiwa hapo nyumbani kwa mtuhumiwa. Alikataa kukubaliana na dhana kukasirishwa kwa sababu kama mtuhumiwa alikuwa amekasirishwa kupita kiasi (Provoked) asingeweza kuuburuza mwili hadi bafuni, kuuchoma moto na baadae kuuzika akiwa peke yake, na pia kumwambia house boy wake, "Nimemuua mbaya wangu."

Pia Bi Mwasabuli alishangaa iweje mtuhumiwa amudu kwenda kazini na kufanya kazi kama kawaida kama vile hakuna kilichotokea.Kwa upande wa Mzee wa baraza wa pili mzee Kikoti pia alikubaliana na maelezo ya mwenzie. Mheshimiwa Jaji alikubaliana na maelezo hayo ya wazee wa baraza kwamba mauaji hayo yalikuwa hayana maana nyingine isipokuwa dhamira ovu. Mheshimiwa Jaji aliendelea kusema kwamba ingawa mtuhumiwa anadai alipatwa na hasira zilizopitiliza (Provoked) lakini yeye hakubaliani na utetezi huo kwa sababu ushahidi uliotolewa hapo mahakamani hauoneshi kukubaliana na dhana hiyo.

Ili kuweka uwiano Mheshimiwa Jaji alitolea mfano kesi kati ya Jamhuri na Stephano Aloys ya mwaka 1972 HCD n. 199. Jaji aliendelea kusema kwamba, mpaka hapo mashtaka ya kuua kwa kukusudia (Murder) dhidi ya mtuhumiwa yamethibitishwa pasi na shaka yoyote, kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 200 cha kanuni ya adhabu.Hata hivyo Jaji alieleza kwa kirefu juu ya dhana ya kuondokewa kwa hali ya ubinadamu (diminishing responsibility). Akizungumzia dhana hiyo alitolea mfano kesi ya mwaka 1978 ya Jamhuri dhidi ya Agnes Doris Liundi (Unrepoted), Mheshimiwa Jaji Makame J. Alirejea kesi ya Uingereza ya R.v. Julia Everton ambapo sheria hiyo kwa kule Uingereza inayo nafasi, ambapo mtuhumiwa aliwekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka mitatu.Mheshimiwa Jaji aliendelea kusema kwamba, kwa Tanzania hatuna sheria hiyo, na itakuwa ni kinyume na taaluma yake kwenda nje ya mipaka yake.

Kisha akaendelea.......Kwa heshima na taadhima ninakubaliana na mtazamo wa hapo juu na hata mahakama ya rufaa ya Tanzania katika rufaa ya kesi kama hiyo No. 82 ya 1978 (Haijaripotiwa) inakubaliana na hitimisho la mheshimiwa Jaji katika hilo. Na hivi ndivyo mahakama ya rufaa ilivyosema:

"Inawezekana haswa, kwa kweli kwamba sheria yetu katika suala la kurukwa na akili (Insanity) limepitwa na wakati na ni la kizamani. Katika ushahidi wa Dr. Haule amesema kwamba katika uchunguzi wa kisasa, utofauti kati ya kurukwa na akili na kuondokewa kwa hali ya ubinadamu mkamilifu (diminished responsibility) lipo chini ya mjadala mkubwa kwa sababu halikubaliki. Bunge kwa hekima yake linaweza likataka kurekebisha matawi husika ya sheria na kuyaleta ama kuyaongeza katika mstari utakaoenda sambamba na taaluma za kisasa za kitabibu juu ya suala husika. Na katika nguvu nyingine kimahakama ikiwemo mojawapo hata ya Afrika Mashariki iwe inafanya hivyo. Lakini kama sheria ilivyo tupo katika mchango wa mawazo kuona Mheshimiwa Jaji ameelekea katika hitimisho sahihi"

Huu ulikuwa ni mtazamo wa mahakama ya rufaa.

Katika mahakama ya rufaa ilizingatia rufaa ya kesi ya Agnes Liundi, katika maelezo yake katika kesi hiyo Mheshimiwa Jaji Bahati alikiri kwamba hayatofautiani sana na kesi iliyo mbele yake. Kwa kesi ya Agness Liundi ni kwamba alikuwa ameteswa sana na mumewe kiasi cha kuamua kujiuwa na kuwauwa wanae wote. Siku hiyo ya tukio Agness alinunua sumu pamoja na Juice ya Orange Squash ambapo aliwapa watoto wake wanywe na yeye pia kunywa sumu hiyo. Watoto watatu walifariki lakini yeye na mtoto wake mmoja waliokolewa na madaktari. Katika kesi hiyo mawakili wa utetezi walikuja na hoja ya uwendawazimu (Insanity) wakati mtuhumiwa akitenda kosa hilo lakini mahakama kuu haikuafiki hoja hiyo. Pia kulikuwa na jaribio la kuleta au kuingiza hoja nyingine ya kupoteza hali ya kibinadamu (diminished responsibility,) hoja ambayo pia ilikataliwa na mahakama kuu.

Mheshimiwa Jaji Bahati alikataa kuikubali hoja hiyo ya kupoteza hali ya kibinadamu (diminished responsibility) kama utetezi katika kesi hiyo ya Asha Mkwizu kama ilivyokataliwa katika kesi ya Agnes Liundi.

Kutokana na tafiti za Mheshimiwa Jaji hapakuwa na kipengele chochote cha sheria kinachoeleza juu ya kukasirishwa. Baada ya kukataliwa kwa maelezo ya mtuhumiwa yanayohusu kutukanwa, Mheshimiwa Jaji hakuona umuhimu wa kuhusisha vipengele vya sheria ya kanuni ya adhabu na makosa ya jinai vya 201 na 202 kuhusiana na kukasirishwa. Hapakuwa na umuhimu wa kuoanisha hayo.

Katika hitimisho Mheshimiwa Jaji alisema:

Nimeridhika na tuhuma za mauaji ya kukusudia zimethibitishwa pasi na shaka yoyote, kwa hiyo basi, mtuhumiwa amepatikana na hatia ya kuuwa kwa kukusudia na ninamhukumu kulingana na sheria kama ifuatavyo;

Mahakama - Hukumu iliwasilishwa mbele ya mahakama ikishuhudiwa na mtuhumiwa, wasaidizi wa mahakama na wazeewa baraza.

Mshitaka - Sina la kusema.

Jopo la mahakimu – Hatuna la kusema.

Mtuhumiwa – Sina la kusema ila nilichosema ni kweli, naiomba mahakama inipunguzie adhabu kwa sababu ya matatizo yote haya, nina mzazi mzee sana na afya yangu ni dhaifu, nimefanyiwa operesheni mbalimbali, ninasumbuliwa na kibofu cha mkojo na uti wa mgongo.

Hukumu - "Kwa mujibu wa sheria kuna hukumu moja tu kwa makosa ya kuuwa kwa kukusudia, nayo ni adhabu ya kunyongwa hadi kifo. Alichosema mtuhumiwa katika kesi hii, kinaweza kumsaidia kwa hatua nyingine na si kwa mahakama hii. Kwa hiyo basi, nakuhukumu wewe Asha Mkwizu Hauli adhabu ya kifo kwa kunyongwa"

Haki ya mtuhumiwa kukata rufaa iko wazi.

Jaji A. Bahati

2/10/1985
 

Attachments

TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
21,844
1,250
Mkuu mbona unafungua vidonda aisee??? wako wapi hawa wanawake wawili??

Pia tukumbuke kwamba katika kesi zote mbili wanaume ndio chanzo cha shida zote kutokana na tamaa zetu za mwili, na kwa upande mwingine kesi ya Asha inasikitisha zaidi kwani kwa namna moja adue wa mwanamke ni mwanamke ambaye anaonekana alishakua comfortable kabisa na hali ya kuwa competitor

IT HURTS TO SAY THE LEAST, AND I FEEL SORRY FOR THE TWO WOMEN
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
Wana JF wenzangu na wasomaji wa JF, kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba nitarejea kesi za Afika Mashariki na leo nimekuja na kesi hii iliyovuma sana miaka ya 80.

Kesi hii nimeipata kwa ushirikiano wa maktaba ya mahakama kuu, na bado naendelea kutafuta kesi nyingine ambazo nitakuwa naziweka hapa kwa kadiri muda utakavyoniruhusu.

Naomba sana ushirikiano wenu, ili tuweze kukusanya kumbukumbu hizi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

NB: Nipo tayari kupokea maoni, kukosolewa au kuelimishwa, pale ambapo nitakuwa nimekosea, maana mimi sio mtaalamu wa sheria na wala sijawahi kusoma sheria.
 
Mbu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,738
1,500
...mzee Mtambuzi, ....dahhh, asante.
hiyo kesi ya mama Haule imetokea nyuma ya nyumba
yetu.....

F.y.i.... Prof Haule alikuwa daktari mtaalamu bingwa wa
magonjwa ya akili....yaani kama namuona na ndevu zake.
Halafu Happy na Mussa aka Moses...mnh...
mpo wapi aisee?
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
21,844
1,250
Mtambuzi, unaweza kuandika kitabu kizuri sana cha review ya imact ya mahusiano mabaya na athari kisheria na kisaikolojia... hizi cases zitatusaidia ku-cement athari mkuu. Nakumbuka nilikua primary, and i had to go stendi ya basi kumnunulia baba magazeti enzi hizo tulikua tunayapata kwa foleni na kugombania, ili tu asome hii kesi ya mkwizu....

I am touched!!
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
Mbu;

Mkuu naamini utakuwa na mengi ya kusimulia..........
Hebu tupe dondoo ya kile kilichotokea hasa, maana mie nimerejea zaidi kile kilichotokea katika kesi husikam pale mahakamani, lakini wewe unaweza kuwa na zile za mitaani zaidi, wakati tukio hilo lilipotokea................
 
Last edited by a moderator:
Mbu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,738
1,500
MTM;

...nadhani mama Haule alifungwa "maisha"....30yrs? ...yupo uraiani sasa, au...sina uhakika,
nyumba ikachukuliwa na jeshi..na watoto wakahama nchi kama sikosei...
mama Liundi no comment....inauma sana aiseee....

.....kesi hizi zimenikumbusha Sarah Martin Simbaulanga pia na ule wizi wa ' vijisenti'
Miaka hiyo Sokoine, Nyerere, na Kawawa wakiendesha inji hii...
 
Last edited by a moderator:
S

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,904
2,000
Mtambuzi:

Asante sana kwa uchambuzi wa kesi hii. Inatoa funzo kwa kada mbali mbali. Je, kulipuwa na rufaa yoyote kuhusu hili? Na, Kama ilikuwepo, Je nini yalikuwa matokeo yake? Je, huyu mama yupo wapi sasa?

Wasalaam,

Shadow.
 
maishapopote

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
2,234
2,000
so iliishaje mkuu? alinyongwa?
 
Mbu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,738
1,500
Mkuu naamini utakuwa na mengi ya kusimulia..........
Hebu tupe dondoo ya kile kilichotokea hasa, maana mie nimerejea zaidi kile kilichotokea katika kesi husikam pale mahakamani, lakini wewe unaweza kuwa na zile za mitaani zaidi, wakati tukio hilo lilipotokea................
....hapana, ushahidi wa mahakamani ndio wa kuaminika zaidi, umefanyiwa uchunguzi...
ila kiukweli....mama Asha was a devouted wife...mwenye heshima na kuheshimika mtaani.

Sisi wanaume kiukweli tunamaruweruwe ambayo mwanamke asipokuwa na akili timamu ya
kuamua mapema, anaweza kuua....

Kumbuka, miaka hiyo kuomba au kupewa talaka ilikuwa kama taboo...
Kesi zote mbili zilihusisha kina baba waliokuwa " vichwa" na wanaoheshimika
kwenye jamii...Ingawa kumbe majumbani they had long suffering wives...
 
KIKUNGU

KIKUNGU

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
853
195
Mtambuzi asante sana,umenikumbusha mbali sana,nilikuwa ndio niko primary school,i was struggling with reading as a subject then na kichwa changu killikuwa mgado kidogo kwani dadaangu alikuwa comfortable kwenye kusoma na mimi nilikuwa nahagaika kweli basi katika kujitutumua niklikuwa nasubiri baada ya dingi kutoka kazini na magazeti ya uhuru na Mzalendo weekend nilikuwa nasoma magazeti ndipo nilikuja kukutana na hii kesi.It was very interesting then ukiwa bado mdogo kusoma vitu kama hivyo.

Na asante sana kwa huu uamuzi wako wa kutuletea "KUTOKA MAKTABA"kwani itawapa picha wale vijana wa 90's na 2000's kupata angalau yaliyo jili then.Ombi langu kubwa naomba usiache "KU-SERIALISE" kesi ya uhaini ya kina FATHER TOM,kama inawezekana.Hii kesi ilinipaga hamu ya kuwa Mwanasheria hasa kutokana na yule Wakili wa kihindi(sikumbuki jina) alivyo kuwa anawachachafya wakili wa serikali kina Massaba na wenzie,lakini baadae nikaangukia kuwa "mbeba makalai" (PROCUREMENT SPECIALIST)kama watani zetu Wahasibu walivyokuwa wanatuita.

Mungu akubariki sana
 
Cantalisia

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,227
1,195
Dah!story tamuuuuuuuuuuuu,hata haichoshi kusoma,
Kiukweli imenigusa aisee,
Miaka hiyo ndio nilikua bado nanyonya hata sikua naelewa chochote humu dunia lol!
Nimejifunza kuwa makini tu na hawa wanaume,kwan usipoangalia unaweza kujigarimu kwa ajili ya mapenz yenu alafu ukaishia jela na kumwacha mwezio anadunda mtaan kwa raha zake!!!
Asante baba,japo nataman ufatilie na kujua hata ya huyu mama na musa pia!
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
MTM;

Wazo lako la kuandika kitabu ni zuri, ngoja nilifanyie kazi, ila muda unabana kweli..............
 
MERCIFUL

MERCIFUL

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
2,230
2,000
INASIKITISHA!! Natumaini watoto wameweza kusonga mbele kimaisha na Mungu amewajalia kuliweka hili nyuma yao...
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,211
2,000
huyo dada kifo kakitafuta isee...yaani mumewe amchukulie, kwake aende kula ndizi..na kumtusi juu!!!!!!!!

ila nashangaa kwa nini hakumuua mume ambaye ndo dr. pendapenda.... kamuua mwanamke mwenzie ambae nae somehow ni victim....
 
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
Mtambuzi,

Nadhani hii kesi ni nzuri sana ya kutufundisha kama jamii, kwamba lazima tufike mahali tutambue ni kwa kiasi gani wakati mwingine udhaifu wetu wanaume unasababisha maafa kwa watu wengine.

Mkuu kama ukiweza kuziweka hizi kesi kwenye kijarida ama kitabu itapendeza zaidi, ingawa najua ni gharama kubwa sana kufikia hatua hiyo.

Jambo lililonishangaza sana katika kesi hii ni uthubutu wa happines kwenda nyumbani kwa asha huku akitambua kwamba anamchukulia mume wake, hata kama asha ndiye alimshawishi bila shaka happines naye hakufikiria vizuri sana, ama alikuwa anamchukulia poa "mke" mwenzie?
 
Top Bottom