Tunajifunza nini kutoka Nchi ya Uingereza?

Tunajifunza nini kutoka Nchi ya Uingereza?

Sisi tumejifunza kuwa hata bunge la uingereza huwa halirushwi live masaa yote ili wananchi wachape kazi kweri-kweri na ndiyo maana hapa Tz tulifuta swala la bunge live na tunasonga mbere mabeberu wakubwa hao.
 
Huo utashi wa kujifunza upo? Bunge lilipovunjwa kuna baadhi yetu humu walipata hoja kwamba utawala wa sheria ni ndoto za mchana, nia yao ikiwa kutetea hoja zao. Sitegemei uwaone kwenye uzi huu achilia mbali kuendelea kujifunza kama walivyokuwa tayari kujifunza uhayawani wa Boris Johnson kuvunja bunge.
 
Wana jukwaa habari za majukumu ya kila siku?
Nimeona niweke mjadala huu ambao unalenga Utawala wa sheria pamoja na majukumu ya washauri wa Rais.

Mafanikio yoyote ya uchumi duniani yanategemea Utawala wa kisheria, hasa Raia kutendewa haki, Mahakama kuheshimiwa na kuwajibika.

Kwa wale wanaofuatilia Siasa za Dunia kuna mvutano wa Makosa aliyoyafanya Waziri mkuu kwa kuvunja sheria ya kuahirisha vikao vya bunge nje ya utaratibu, pili kumshauri vibaya Malkia katika uamuzi huo. Je nasi Nchi zinazoendelea tunajifunza nini kwa Nchi zilizo endelea juu ya Utawala wa kisheria, vipi washauri wa Rais wanapo kosea kumshauri Rais wanachukuliwa hatua gani?

Mwana JF mwenzangu maoni yako ni yapi?

KARIBU.
SIPANGIWI, SIJIFUNZI KWA MABEBERU. SIPANGIWI
 
Back
Top Bottom