Tunajifunza nini kutoka Nchi ya Uingereza?

Tunajifunza nini kutoka Nchi ya Uingereza?

Utawala wa sheria ndio njia pekee ya kutukwamua hapa tulipo. Kila anayepata dhamana ya uongozi akijua kwamba akifanya makosa mda wowote sheria inamwadhifu, basi uwajibikaji utakuwa mkubwa sana.
 
Kaka hoja yako naiunga mkono 100%. Kuwepo na washauri wa President wanao tambulika kisheria, pia kama wapo sheria iwatambue na pia sheria iwabane pindi wanapotoa ushauri wa hovyo, hii itasaidia sana kwenye maswala mazima ya Nchi.
Washauri kwa wenzetu wanajulikana na wanalipwa na kuapishwa ikibidi
sisi hata hao washauri hatuwajui achilia mbali kujua wanashauri nini
wenzetu mikutano yote ya viongozi iko documented kunamtu anaandika kila neno
hata ukishauri pumba uweze julikana hata kushtakiwa
 
Wana jukwaa habari za majukumu ya kila siku?
Nimeona niweke mjadala huu ambao unalenga Utawala wa sheria pamoja na majukumu ya washauri wa Rais.

Mafanikio yoyote ya uchumi duniani yanategemea Utawala wa kisheria, hasa Raia kutendewa haki, Mahakama kuheshimiwa na kuwajibika.

Kwa wale wanaofuatilia Siasa za Dunia kuna mvutano wa Makosa aliyoyafanya Waziri mkuu kwa kuvunja sheria ya kuahirisha vikao vya bunge nje ya utaratibu, pili kumshauri vibaya Malkia katika uamuzi huo. Je nasi Nchi zinazoendelea tunajifunza nini kwa Nchi zilizo endelea juu ya Utawala wa kisheria, vipi washauri wa Rais wanapo kosea kumshauri Rais wanachukuliwa hatua gani?

Mwana JF mwenzangu maoni yako ni yapi?

KARIBU.
Jiwe anaingilia mihimili mingine hvyo aache mara moja kwakua anavunja katiba
 
Wana jukwaa habari za majukumu ya kila siku?
Nimeona niweke mjadala huu ambao unalenga Utawala wa sheria pamoja na majukumu ya washauri wa Rais.

Mafanikio yoyote ya uchumi duniani yanategemea Utawala wa kisheria, hasa Raia kutendewa haki, Mahakama kuheshimiwa na kuwajibika.

Kwa wale wanaofuatilia Siasa za Dunia kuna mvutano wa Makosa aliyoyafanya Waziri mkuu kwa kuvunja sheria ya kuahirisha vikao vya bunge nje ya utaratibu, pili kumshauri vibaya Malkia katika uamuzi huo. Je nasi Nchi zinazoendelea tunajifunza nini kwa Nchi zilizo endelea juu ya Utawala wa kisheria, vipi washauri wa Rais wanapo kosea kumshauri Rais wanachukuliwa hatua gani?

Mwana JF mwenzangu maoni yako ni yapi?

KARIBU.
Hao walishapata maendeleo ,sisi tunatafuta maendeleo.wao wanakula matunda ya maendeleo sisi ndiyo kwanza tunatafuta maendeleo. Kwa hiyo huwezi kujilinganisha na hao !!two different things!!

Hivi tukiamua kumfanya rais wetu mpendwa kuwa mfalme wa Tanzania si inaweza kuwa nzuri??mbona uingeleza wana malkia na waziri mkuu na nchi inasonga mbele
 
Washauri kwa wenzetu wanajulikana na wanalipwa na kuapishwa ikibidi
sisi hata hao washauri hatuwajui achilia mbali kujua wanashauri nini
wenzetu mikutano yote ya viongozi iko documented kunamtu anaandika kila neno
hata ukishauri pumba uweze julikana hata kushtakiwa
Issue ya Simu kati ya Trump na Rais wa Ukraine imesababisha Trump atoe script nzima ya walichoongea bila kuondoa neno lolote lile. Maana yake maongezi yote huandikwa. Naona washauri wake wamemshauri afanye hivyo
 
Tumejifunza jinsi wenzetu wanavyoheshimu katiba, majaji walivyo huru, jinsi majaji wanavyofuata sheria na katiba katika maamuzi yao. Tumejifunza mihimili inavyofanya kazi bila kuingiliwa na uliojichimbia zaidi. Tumejifunza kuwa jaji matupa na wenzie anafanana nao ni janga kwa taifa.
 
Mahakama imetoa uamuzi kuwa waziri mkuu alikosea kusimamisha bunge na kumshauri vibaya malkia. Hivyo bunge litaendelea tena Jumatano. Waziri mkuu ametakiwa kujiuzulu baada ya uamuzi huo. Huku kwetu ukimshitaki waziri mkuu au rais unafutwa uwakili.

Kwa mfano ingekuwa ni nchi ya utawala wa sheria maneno ya juzi ya rais eti mafisadi wakikiri na kurudisha pesa waachiwe, angeshafunguliwa kesi kwa kuingilia mahakama na kuvunja katiba hivyo angetakiwa kujiuzulu.

Yaani rais alipopiga marufuku mikutano na maandamano ya kisiasa ingekuwa kule sasa hivi angekuwa mtaani hana kazi. Lakini huku kwetu rais ni Mungu wa nchi yuko juu ya sheria!
Wana jukwaa habari za majukumu ya kila siku?
Nimeona niweke mjadala huu ambao unalenga Utawala wa sheria pamoja na majukumu ya washauri wa Rais.

Mafanikio yoyote ya uchumi duniani yanategemea Utawala wa kisheria, hasa Raia kutendewa haki, Mahakama kuheshimiwa na kuwajibika.

Kwa wale wanaofuatilia Siasa za Dunia kuna mvutano wa Makosa aliyoyafanya Waziri mkuu kwa kuvunja sheria ya kuahirisha vikao vya bunge nje ya utaratibu, pili kumshauri vibaya Malkia katika uamuzi huo. Je nasi Nchi zinazoendelea tunajifunza nini kwa Nchi zilizo endelea juu ya Utawala wa kisheria, vipi washauri wa Rais wanapo kosea kumshauri Rais wanachukuliwa hatua gani?

Mwana JF mwenzangu maoni yako ni yapi?

KARIBU.
 
Wana jukwaa habari za majukumu ya kila siku?
Nimeona niweke mjadala huu ambao unalenga Utawala wa sheria pamoja na majukumu ya washauri wa Rais.

Mafanikio yoyote ya uchumi duniani yanategemea Utawala wa kisheria, hasa Raia kutendewa haki, Mahakama kuheshimiwa na kuwajibika.

Kwa wale wanaofuatilia Siasa za Dunia kuna mvutano wa Makosa aliyoyafanya Waziri mkuu kwa kuvunja sheria ya kuahirisha vikao vya bunge nje ya utaratibu, pili kumshauri vibaya Malkia katika uamuzi huo. Je nasi Nchi zinazoendelea tunajifunza nini kwa Nchi zilizo endelea juu ya Utawala wa kisheria, vipi washauri wa Rais wanapo kosea kumshauri Rais wanachukuliwa hatua gani?

Mwana JF mwenzangu maoni yako ni yapi?

KARIBU.
Unategemea mtu aliyevunja sheria kupata nafasi aliyo nayo aishemu?
 
Mkuu tofautisha Uingereza (au Marekani) na akina Tanzania...
Huku wananchi wote wanalazimika kumtukuza Mtukufu Rais kiasi cha kuamini kuwa yeye hafanyagi makosa wala halali usingizi kama binadamu wa kawaida...
Huku Rais ni alfa na omega! Anauwezo wa kufunga na kufungua kadri impendezavyo...
Na cha ajabu wengi watampigia makofi au kuandamana kumpa sapoti kama makauzu au mazwazwa!
 
Kwani kabla ya wazungu kuja kuiba mali zetu babu zetu walikuwa hawana dawa? Acha kuendekeza ukoloni... Babu zetu walikuwa wana dawa zote kwa taarifa yako ila wamewabrain wash watu kama nyie kufikiri bila msaada hamuwezi kuishi. Jitambue kaka
Kuiba Mali zetu zipi hizo madini?mbona hata sasa mkoloni mweusi anatuibia kupitia mikataba mibovu kila kukicha na inafichwa hata bungeni haifiki.
 
Mwana JF mwenzangu maoni yako ni yapi?
Ni kwamba kutokana na hali tuliyonayo nchini sasa, kila mtu anatakiwa aje ajifunze kwetu.
Hata mashirika ya kimataifa, kama WHO, huoni tunawawekea ngumu, hata katika jambo ambalo kwa kweli halistahili kabisa kulifanyia ubishi wowote!
 
Je kuna mshauri yyte amewahi kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kumshauri President vibaya?
LOoo, washauri wenyewe wanapigana vikumbo kusikiliza wanayetakiwa kumshauri anasema nini..., sasa hapo sijui ni nani hasa 'mshauri'; kama umenielewa ninachokisema hapa.

Chukulia mfano wa Mwantunu Mwalimu na ugonjwa unaofichwa..., unadhani anao uwezo wa kushauri lolote nje ya matakwa anayojua anayo mkuu wake? Matokeo yake ndio hayo tunayoyaona, ya kujiumauma, na kuficha hata yasiyostahili kufichwa!
 
F9EAC18E-9154-4A98-85CE-0C9897D84696.jpeg


Chezea wanasiasa kwa fitna na unafiki mpira washaanza kumrushia Attorney General ndiye alieshauri PM hakuna sheria atakayovunja katika maamuzi yake.

Na document za ushauri washarusha kuonyesha PM hakukurupuka tu.

Kama ni kujifunza hii ndio maana ya doctorine of separation of power kati serikari, bunge na mahakama; kwenye checks hakuna mtu kufanya mambo asiyo na mamlaka nayo kisheria.
 
Kwani kabla ya wazungu kuja kuiba mali zetu babu zetu walikuwa hawana dawa? Acha kuendekeza ukoloni... Babu zetu walikuwa wana dawa zote kwa taarifa yako ila wamewabrain wash watu kama nyie kufikiri bila msaada hamuwezi kuishi. Jitambue kaka
Mkuu mpaka leo viongozi wetu Afrika wanatibiwa ughaibuni na wengine wanafia huko,bado tuna vifo vingi vinavyo sababishwa na magonjwa yanayotibika.
Ebu funguka hizo dawa zilienda wapi au nazo ziliibwa na mabeberu?.
 
Tanzania tuna mihimili mitatu ya serikali ambayo hiyo kila mhimili unajitegemea katika kuendesha shughuli zake bila kuingilia muhimili mwingine.

Hata kama mhimili mmoja unaonyesha mapungufu mhilimi mwingine hauwezi kuuingilia

Tumeshuhudia mahakama ya juu kabisa ya Uingereza ikitengua uamuzi wa waziri mkuu Boris Johnson kusitisha bunge kujadili maswala ya Brexit ili apate urahisi wa kuitoa Uingereza katika EU.

Mahakama kuu ya Tanzania imesema haiwezi kuingilia suala kati ya lissu na bunge sababu bunge ni taasisi inayojitegemea.

Watanzania tutakimbilia wapi katika kudai haki au demokrasia kwenye suala ambalo linahusu mihimili hii mitatu . Je uamuzi kuhusu suala la lissu ulikuwa Political motivated.

Kama majaji wa Uingereza walisema kusitisha bunge kujadili suala la brexit ni kuwanyima wabunge haki yao ya msingi katika demokrasia kujadili brexit

Leo hii ni LISSU , kesho litatokea suala jingine, je mahakama utapiga chenga ,only time will tell us
 
Back
Top Bottom