Mkuu kuanza kuhangaika kumtoa mbowe sasa hivi ni kuwapa points tu CCM, cha muhimu nani tumpe kura zetu 2020 Lissu, Zitto?
Mbowe 2020 ataharibu zaidi kuliko alivyoharibu 2015 atatoa maamuzi ya kubadili gia baharini na Chombo kitazama kabisa.
Mana kilibadili gia angani kikaangukia Baharini , bado kinatapatapa baharini.
Akiendelea 2020 atabadili gia baharini na kuzamisha kabisa Chadema.
Hakuna Mtu mwenye akili Timamu atakayepigania kura za Chadema kwa ajili ya Fisadi.
Bora Twende na ACT Chadema ikae makumbusho na Mbowe.
Hata Jimboni kwake na kanda ya Kaskazini imelemaa kabisa kwa sababu ya Ulemavu na udhaifu wa Mbowe kisiasa.
Zile amamsha amsha za Dr. Slaa ziko wapi!
Mbowe hajiulizi tu kuwa ni kwa nini watu wanataka urais na Chama apewe Lisu aliyeko Hospitalni wakati yeye yupo na ni Mzima was afya. Watu wanatamani Mgonjwa aje hata kesho apewe Chama na Nchi.
Tafsiri yake watu kama taifa sio Chadema pekee wamemchoka sana Mbowe.
Kuna siku Mbowe aliteleza akataja neno demokrasia kwenye Tamko la vyama juu ya kesi waliyofungua ya kupinga sheria ya Msajili.
Alibabaika sana namna ya kulikwepa hilo neno Demokrasia.
Tafuta Clip yake umfuatilie. Usione kuwa tunampinga na hata kumchukia sana Mbowe sio kwa sababu ya Uenyekiti tu Bali kwa dhamira yake Mbaya iliyopo moyoni Mwake.
Huwezi kujenga Chama kwa misingi ya uongo,udikteta,ukabila,udini,vitisho, hasira, hujuma kwa vyama vingine tena vichanga kabisa halafu ukategemea kuwa watakuunga mkono.
Demokrasia ikishamiri ndani ya Chadema hakika na kuambia hata CCM itapukutika, na vyama vingine vitaona mahali pa kukimbilia.
Hivi Zito yupi atakayeiunga mkono Chadema chini ya Mbowe aliyetengeneza kila aina ya hila ili afukuzwe bila huruma ndani ya Chama alichokipigania kwa UDI na uvumba akijua iko Siku atakipeleka mbele zaidi.
Nakumbuka Kwenye kampeni za uchaguzi kule Tabora Zito alivyokua anawanyima usingizi CCM kwa nyomi ya vijana huku akichoma T-shirt za CCM.
Zito ana Nyota ya kung' aa sana kuliko Mbowe anayefuga midevu ya bangi mm... e z.ke.
Mbowe haaminiki kama alimsababishia Mtatiro kukosa Ubunge na wakalikosa wote hakika 2020 kila Chama kitakua na mgombea wake sio kuungana na kuiachia Chadema na Chadema Chini ya Mbowe hata kubali kuwaachia wengini mana wote ni wachanga.
Lisu asikubali kupoteza Muda wake kugombea Urais Chini ya Mwenyekiti Mbowe kwa kuwa atapoteza Ubunge wake huku Mwenzake akipiga hela kutokana na Uenyekiti wa Chama na Ubunge na Msemaji wa kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Mbowe aache utapeli tujenge nchi kwa kujenga imani ya Chama kwa wapiga kura.
Mbowe akae pembeni aone Chama kikijengwa na wenye nia njema.
Tajiri kamwe hajawahi kuwapigania Maskini. Ukiona hivyo ujue kuna Faida ameiona.
Nchi hii ni Lazima vyama hivi viongozwe na watu waliotoka from ziro to hiro kama Magufuli, Zito, Lisu,Mnyika ,Juma Mwalim, n.k. Lakini sio kuongozwa na mzaliwa wa masaki asiyejua shida za watanzania zaidi ya kuwaza ufahari na Kuponda Ruzuku na wanawake.
Bora CCM iendelee miaka 1000 kuliko Chadema Chini ya Mbowe tutajuta sana mana nchi itaendeshwa anavyotaka yeye bila hofu yoyote na mauaji yatakua makubwa sana kwa wale asiowapenda. Mbowe Ni mtu hatari kwa usalama wa wanyonge kuliko kitu chochote unachokijua duniani.