Tunaitoaje CCM madarakani?

Tunaitoaje CCM madarakani?

Kuna sababu nyingi ambazo zinakifanya CCM iendelee kutawala hata miaka 40 ijayo. Nazo ni kama ifuatavyo.
1. Uoga wa watz. Yaan hawajazoea mambo ya vita na mshike mshike. Tofauti na nchi zingn kam za kiarabu
2. Ubinafsi na njaa. Kila mmoja anajijali na hutamani apate peke yake. Akishapata husahau wengne. Ndo maana utawaona watu kama Kitila Mkumbo, polepole, Mwita, etc
3. Ujinga na umaskini. Hivi vyote vinarandana. Mtu mjinga mara nyingi niaskini. Hatambui haki zake, na mustakabali mzima wa maisha yake. Na hajui chanzo cha matatizo yake. Akiambiwa kua tz bila ccm itakua na vita huamini hivo. Na umaskin hupelekea watu kujipendekeza na kua wasaliti.
4. Unafiki na kujipendekeza. Hii ndo kansa inayotutafuna. Apataye cheo husahau. Na hata wananchi waitwao wanyonge wanaonyesha unafiki wa wazi kwa kuimba ngojera za kusifu nana pia wakiwa ni watu wa kujikomba kwa wakubwa angalau aweze kupata mli na cheo.
5. Matabaka, utengano na udini. Hivi vinashbiana kwa ukaribu. Ukiskia huyu alieko madarakani kama ni dini flan basi atapigiwa makofi wakijinadi kua na sisi tumepata raisi. Huwez pata suppprt na kam ni kura atapta.
6. Ukabila na ukanda. Hii inaelekeana na no 5 ingawa utofauti wake ni pale unaposkia huyu katokea kanda flani na ni kabila flan. So utakuta anapifiwa kura na watu wengi wa kabila lake, regardless yy ni chama chake.
7. Upinzani dhaifu wenye unafiki ndan ake. Juzi CHADEMA wakaitiaha press kwenda kujitetea sakata la gari la CAG badili ya kujadili ubadhilifu uliobainishwa na CAG. Mtazame aliekua mgombea wa ACT 2015 alivokubali matokeo haraka ili apate cheo.

Mambo ni meng mda ni mchache

Hivyo vitu hapo juu vitayafanya madiliko ya kweli yachelewe kwa miongo kadhaa mbele mpaka pale kila mmoja atachoka na kunena kwa lugha moja, na hata pale ambapo mawe nayo yatachoka na kujiunga kwenye unenaji. Hapo mbuyu utaangushwa. Ila sio leo.
 
Kujadili kuitoa Ccm Mamlakani ni sawa na kuchezea Amani kwenye Tundu la choo
Mkuu kwenye Hilo nnakubaliana na wewe kabisa, so far hakana chama kilicho taasisi imara(kisicho endeashwa mtu au kikundi kidogo Cha watu)......
Ila pia histori inaonyesha hakuna chama kilichoweza hodhi madarakana milele,pia binadamu hawatabiribi ipo siku wanaweza wakapiga kura Kama wehu(Bila tafakakari makini)au hata wakaandamana (mfano Ni mingi mno,misri, Zimbabwe,Tunisia,aljeria, etc) CCM ikatupwa inje...Kwa kuwa hatuwahiwi kuindaa nchi yetu pendwa kuongozwa na chama tofauti taifa letu litarudi nyuma kimaendeleo for year (angalia hiyo mifano,misri Na Libya wakalibia kufisha 10 years Mambo yajakaa sasa Wala hayana dalili)...

Katiba pendekezwa ya warioba ingekuwa mwanzo mzuri Sana wa kuanza kuindaa nchi na taifa(kupunguza madarakani ya Raisi,kuimarisha kwa taasisi zingine,na kutoruhusu muingiliano wa kimadaraka bunge serikali na mahakama), ile siku hiyo itakapofika (hatakama hispofika itachukua miaka) taifa na nchi isiyumbe......

Zimbabwe, Juzi TU miaka michache nyuma tulikuwa tunasikia kuwa wazimbabwe wanapenda na anaobwa Kama shujaa wa taifa Hilo, japo katokea mlango wa nyuma ila taifa lile linapita kipindi kigumu Sana sahivi....
 
Kuna sababu nyingi ambazo zinakifanya CCM iendelee kutawala hata miaka 40 ijayo. Nazo ni kama ifuatavyo.
1. Uoga wa watz. Yaan hawajazoea mambo ya vita na mshike mshike. Tofauti na nchi zingn kam za kiarabu
2. Ubinafsi na njaa. Kila mmoja anajijali na hutamani apate peke yake. Akishapata husahau wengne. Ndo maana utawaona watu kama Kitila Mkumbo, polepole, Mwita, etc
3. Ujinga na umaskini. Hivi vyote vinarandana. Mtu mjinga mara nyingi niaskini. Hatambui haki zake, na mustakabali mzima wa maisha yake. Na hajui chanzo cha matatizo yake. Akiambiwa kua tz bila ccm itakua na vita huamini hivo. Na umaskin hupelekea watu kujipendekeza na kua wasaliti.
4. Unafiki na kujipendekeza. Hii ndo kansa inayotutafuna. Apataye cheo husahau. Na hata wananchi waitwao wanyonge wanaonyesha unafiki wa wazi kwa kuimba ngojera za kusifu nana pia wakiwa ni watu wa kujikomba kwa wakubwa angalau aweze kupata mli na cheo.
5. Matabaka, utengano na udini. Hivi vinashbiana kwa ukaribu. Ukiskia huyu alieko madarakani kama ni dini flan basi atapigiwa makofi wakijinadi kua na sisi tumepata raisi. Huwez pata suppprt na kam ni kura atapta.
6. Ukabila na ukanda. Hii inaelekeana na no 5 ingawa utofauti wake ni pale unaposkia huyu katokea kanda flani na ni kabila flan. So utakuta anapifiwa kura na watu wengi wa kabila lake, regardless yy ni chama chake.
7. Upinzani dhaifu wenye unafiki ndan ake. Juzi CHADEMA wakaitiaha press kwenda kujitetea sakata la gari la CAG badili ya kujadili ubadhilifu uliobainishwa na CAG. Mtazame aliekua mgombea wa ACT 2015 alivokubali matokeo haraka ili apate cheo.

Mambo ni meng mda ni mchache

Hivyo vitu hapo juu vitayafanya madiliko ya kweli yachelewe kwa miongo kadhaa mbele mpaka pale kila mmoja atachoka na kunena kwa lugha moja, na hata pale ambapo mawe nayo yatachoka na kujiunga kwenye unenaji. Hapo mbuyu utaangushwa. Ila sio leo.
Kuna watu wengi tu wamechoka kamanda
 
Mbowe ni agent wa ccm.

Je ewe bavichaa una uwezo wa kumtoa mbowe?
 
Wadau kwema?
Hivi wadau sisi kama binadamu wa karne ya 21 tumekubali kabisa CCM watutawale miaka 30+?Ujanja woteee tulio nao tumefeli miaka yote hiii? Kwanza naamini humu JF wapinzani ni wengi kuliko CCM, tunashindwa nini?
OK, kuna jibu moja ambalo liko popular miaka yote eti vijijini watu wengi hawajasoma wanajua bado nyerere anatawala na CCM yake,nakwambia si kweli.Nimezunguka vijiji vingi tena interior haswa wanajua Mbowe ni nani na Magufuli ni nani.
The main problem iko hapa:UCHAGUZI tunaibiwa.Tusipo kuwa makini tutakuwa ruled na CCM for another 30 years!tutakuwa ni watu wa kulalamika kimya kimya miaka yote hiii? Tazama leo tumepigwa nakos za uso huko Arumeru tumetulia tu as if we are in the 20th century. Damn!
Ajitokeze mtu hapa atuambie tunashindaje 2020 maana tunatofautiana kimawazo.Tuchukue hata awamu moja tukifeli basi warudi CCM.Ninachoamini mimi nchi ya kidemokrasia inayotawaliwa kwa miaka zaidi ya 30 na chama kimoja maana yake watu wa nchi hiyo bado ni wafungwa hawajawahi kuwa "nje ya box".
Unafikiri ni kwa nini wananchi wa marekani wanajiamini nchini kwao? Sababu wanajua mtawala atakapoleta ujinga atatoka for sure regardless of his /her political party.
Angalia sisi tulivyo waoga ni kwa sababu hatujawahi kuwajibisha utawala kwa kuweka madarakani chama kingine.Ikitokea hii utaona namna watanzania watakavyo kuwa confident.Tumekata tamaa, tumekata tamaa.Majuzi nilikuwa naongea na group la jamaa zangu fulani wanasema hata ufanyaje sa hv huwezi kubadili siasa ya CCM.
Ikishindikana kwa njia ya kura tunaweza kufanyaje? Wasomi tuambieni.Fikiria chama cha upinzani kimechukua nchi mizizi yote ya CCM toka 1970s hadi leo itakavyo wakost CCM kuing'oa kumsafishia ofisi mpinzani, CCM wakifikiria hilo wanachanganyikiwa ndio maana wanatumia nguvu kubwa.
Hivi sisi tuliopo JF,twitter, Facebook, Instagram, whatsapp etc hatuwezi kuwa chachu kwa wengine?
Ni aibu kwa kweli 30yrs+ bado tuko na chama kimoja?China wanaweza kuwa na justification ingawa ni chama kimoja leo ni second world economy.Tanzania ni economy ya ngapi? Mtu aliyekufa mwaka 80 akifufuka leo anamkuta CCM bado yupo.Tuna tabaka la vijana wengi waliosoma kuliko miaka mingine yote, tunafeli wapi? Tutafute muarobaini. Nipe mawazo yako alafu niambie hapa wewe ni MPINZANI au CCM niweke kura yako.
Tumechoka na CCM.
Muarubaini ni katiba mpya na tume huru
 
tutaitoa kwa kuzungusha mikono eti mabadiliko, shenzy kabisa
 
Ukitaka kukitoa Chama cha Mapinduzi madarakani mumtoe kwanza Mbowe pale kwenye Uenyekiti wake maana na yeye amekaa sana pale,Obviously miaka inaenda na hana nia hata ya kuachia madaraka na wengine waongoze!
 
kuitoa CCM madarakani ni ngumu kwasababu;
1.upinzani wao kwa wao hawana umoja
2.hawajitangazi mfano ukienda vijijini chama cha upinzani ambacho kinajulikana labda ni chadema vingine hola
3.hawana mipango mikakati endelevu wapo wapo tu wanasubiri CCM waongee wao wa crush

sababu zipo nyingi hizo ni baadhi tu nisije nikawapa zote mkashinda ilihali bado ni wachanga kwenye siasa
 
Huko kote ulipotaja kuna nini wamekipata baada ya hayo Mapinduzi?

Libya wanachinjana kama Mbuzi Kule Vingunguti
Kule Egypt Al Sisi anapeleka mswaada Bungeni atawale Mpaka 2030 n.k
Ni kweli mkuu, wanachinjana kwasabubu Libya haikujiandaa,mfano kuwa na taasisi imara Kama jeshi,polisi,mahakama, na zingine zote za kawaida za kiserikali ambozo zitaweza heshimu na kulinda katiba na mamlaka halali Kama Raisi Bila kujali anatoka chama kipi, haki kwa wote(kusiwe na mtu aliyeko juu ya sheria).......

Na kwa bahati mbaya muda muda badilika hivyo na binadamu pia(mabadiliko hayapukiki kimaana hiyo) na huwa na athari zote nzuri (+) na mbaya (-).

Hivyo basi namna nzuri ya kukabiliana na mabadiliko Ni kujiandaa hii hupunguza athari HASI bindi yatokeapo, ila KUPINGA na KUBISHA na KUJI APIZA kuwa mabadiliko hayawezi kutokea ilihaji siku hazigandi miaka inakimbia watu wanazaliwa,wanakuwa,wanazeeka, mahitaji yanabadilika, technolijia inakuwa, NIKUJIDANGANYA...........
 
Wadau kwema?
Hivi wadau sisi kama binadamu wa karne ya 21 tumekubali kabisa CCM watutawale miaka 30+?Ujanja woteee tulio nao tumefeli miaka yote hiii? Kwanza naamini humu JF wapinzani ni wengi kuliko CCM, tunashindwa nini?
OK, kuna jibu moja ambalo liko popular miaka yote eti vijijini watu wengi hawajasoma wanajua bado nyerere anatawala na CCM yake,nakwambia si kweli.Nimezunguka vijiji vingi tena interior haswa wanajua Mbowe ni nani na Magufuli ni nani.
The main problem iko hapa:UCHAGUZI tunaibiwa.Tusipo kuwa makini tutakuwa ruled na CCM for another 30 years!tutakuwa ni watu wa kulalamika kimya kimya miaka yote hiii? Tazama leo tumepigwa nakos za uso huko Arumeru tumetulia tu as if we are in the 20th century. Damn!
Ajitokeze mtu hapa atuambie tunashindaje 2020 maana tunatofautiana kimawazo.Tuchukue hata awamu moja tukifeli basi warudi CCM.Ninachoamini mimi nchi ya kidemokrasia inayotawaliwa kwa miaka zaidi ya 30 na chama kimoja maana yake watu wa nchi hiyo bado ni wafungwa hawajawahi kuwa "nje ya box".
Unafikiri ni kwa nini wananchi wa marekani wanajiamini nchini kwao? Sababu wanajua mtawala atakapoleta ujinga atatoka for sure regardless of his /her political party.
Angalia sisi tulivyo waoga ni kwa sababu hatujawahi kuwajibisha utawala kwa kuweka madarakani chama kingine.Ikitokea hii utaona namna watanzania watakavyo kuwa confident.Tumekata tamaa, tumekata tamaa.Majuzi nilikuwa naongea na group la jamaa zangu fulani wanasema hata ufanyaje sa hv huwezi kubadili siasa ya CCM.
Ikishindikana kwa njia ya kura tunaweza kufanyaje? Wasomi tuambieni.Fikiria chama cha upinzani kimechukua nchi mizizi yote ya CCM toka 1970s hadi leo itakavyo wakost CCM kuing'oa kumsafishia ofisi mpinzani, CCM wakifikiria hilo wanachanganyikiwa ndio maana wanatumia nguvu kubwa.
Hivi sisi tuliopo JF,twitter, Facebook, Instagram, whatsapp etc hatuwezi kuwa chachu kwa wengine?
Ni aibu kwa kweli 30yrs+ bado tuko na chama kimoja?China wanaweza kuwa na justification ingawa ni chama kimoja leo ni second world economy.Tanzania ni economy ya ngapi? Mtu aliyekufa mwaka 80 akifufuka leo anamkuta CCM bado yupo.Tuna tabaka la vijana wengi waliosoma kuliko miaka mingine yote, tunafeli wapi? Tutafute muarobaini. Nipe mawazo yako alafu niambie hapa wewe ni MPINZANI au CCM niweke kura yako.
Tumechoka na CCM.
Mimi nashauri tuachane na kupiga kura kabisa kwa sababu kura zetu hazina thamani hata mukiandisha wa Milioni 20 na wakapiga kura watu 1000 na ccm wakapewa 600 kati ya hizo 1000 wataambiwa wwshinda kwa 60%.
Hebu Kumbukeni 2015 walisajiliwa wapiga kura karibu milioni 20.Waliopiga kura ni milioni 12 ,na Magu kashinda kwa kura milioni 8 hivi hii ni haki gani mil 12 wamekukataa na mil.8 tuu ndo wamekukubali hamuoni kuwa haya wengi haizingatiwi? .Sasa mimi naona mfano 2020 wasajili milioni 10 mpaka 12 kisha wapige kura Millioni 4_5 tuu. 2025 wasajili mil.2 na wapige kura laki 5_8 .Tuende mwendo huu mpaka wabakie wapiga kura ni jamaa wa wagombea tuu.YAANI TUFANYE UCHAGUZI USIWE KITU CHA MAANA KABISA ,IWE NI MGOMO BARIDI.WATAELEWA LUGHA HII KAMA ALIVYOELEWA NYERERE. YEYE UCHAGUZI WAKE WA NDIO NA HAPANA WA MWISHO 1980 NADHANI ALIPATA KURA LAKI NNE AU TANO.HAPO ALISHAKOSWAKOSWA KUPINDULIWA MARA 4 ,ALIACHIA NGAZI NA KUNGATUKA.
ila tukubali kuvumilia.na.tusikubali.ushawishi wa chama chochote kile kwani uhalisia ccm hawatokipachama.chochote kutawla.SASA SISI TUNAFANYWA MABOYA TUU.BORA TUSUSE.
 
Muarubaini ni katiba mpya na tume huru
Hvi wewe unaweza kukata tawi la mti huku ukiwa umekaa kwenye hilo tawi la juu kabisa? Moja ya nguzo kubwa inayoiweka CCM madarakani si police kama watu wengi wanadhani. Nguvu kubwa inayoiweka CCM madarakani ni Katiba yetu ya sasa. Inampa rais wa JMT madaraka mengi na makubwa sana na rais ni mwenyekiti wa CCM na pia huwa ni mgombea wa kiti cha urais. Sasa wewe unadhani huyo rais na mwenyekiti wa chama atakuwa tayari kubadili katiba ya nchi ambayo kimsingi ndiyo inampa hiyo nguvu ya ushindi wa kuendelea kuwa madarakani? CHINI YA SERIKALI YA CCM HAKUNA KATIBA MPYA! NI KUZIBA TU VIRAKA KAMA KUTATOKEA TOBO AMBALO LINAWAHUSU NA KUHATARISHA MASILAHI YA CHAMA NA SERIKALI.
 
Dunia inaenda kasi sana. Walioccm wengi wanajua kwamba kuwepo kwao na kuwepo kwa ccm madarakani kunawahakikishia urahisi wa maisha katika nchi hii corrupt..
Wajanja na wanaweza kufanya mengi kulinda nafasi ya chama.

Hata wapinzani wanaona ccm wana nafasi za kufaidika na mfumo corrupt na hivyo wao ndo maana wanaponda tu na hawana mbadala.

Ccm wanaelewa trick za kisiasa na wanaenda na upepo. Huu udhaifu wa ccm ndo umetufikisha hapa. Tunacheza danadana na kuridhishana na hadithi. Kwa nguvu ya chama waliyonayo wangeweza kutengeneza dira ya nchi hii miaka 200 baadaye tukaenda hivyo. Sasa hatujielewi

CCM wanajua watu wanaofanya kazi na kula jasho lao huwezi kuwavuruga kirahisi. Wameacha mifumo ya dili, katika nyanja zote za jamii yetu imestawi kiasi kwamba watu hawaoni ugumu wa maisha.

Kuwatoa tunahitaji ugumu ukolee watu wawe na sababu ya kuwatoa. Akiendelea hivi miaka mitatu ijayo kutakuwa na mtaji wa watu wakutosha kuanza kutikisa kibiriti.
 
Kwani kuna amani Tanzania tangu lini? Amani ya majizi yanayopiga trillions kila mwaka? Amani ya majizi yanayodhulumu wakulima wa korosho zaidi ya 350 billions zao? Amani ya kuteka, kutesa, kubambikia kesi na hata kuuwa wanaotumia haki yao ya kikatiba kama raia au Wabunge? Acha kuandika pumba!

Kule Tripoli Libya wakati wa Ghadafi walikuwa wakiambiwa issue za amani walikuwa wana kejeli kama wewe sasa hivi Shughuli wanaipata
 
Mimi nashauri tuachane na kupiga kura kabisa kwa sababu kura zetu hazina thamani hata mukiandisha wa Milioni 20 na wakapiga kura watu 1000 na ccm wakapewa 600 kati ya hizo 1000 wataambiwa wwshinda kwa 60%.
Hebu Kumbukeni 2015 walisajiliwa wapiga kura karibu milioni 20.Waliopiga kura ni milioni 12 ,na Magu kashinda kwa kura milioni 8 hivi hii ni haki gani mil 12 wamekukataa na mil.8 tuu ndo wamekukubali hamuoni kuwa haya wengi haizingatiwi? .Sasa mimi naona mfano 2020 wasajili milioni 10 mpaka 12 kisha wapige kura Millioni 4_5 tuu. 2025 wasajili mil.2 na wapige kura laki 5_8 .Tuende mwendo huu mpaka wabakie wapiga kura ni jamaa wa wagombea tuu.YAANI TUFANYE UCHAGUZI USIWE KITU CHA MAANA KABISA ,IWE NI MGOMO BARIDI.WATAELEWA LUGHA HII KAMA ALIVYOELEWA NYERERE. YEYE UCHAGUZI WAKE WA NDIO NA HAPANA WA MWISHO 1980 NADHANI ALIPATA KURA LAKI NNE AU TANO.HAPO ALISHAKOSWAKOSWA KUPINDULIWA MARA 4 ,ALIACHIA NGAZI NA KUNGATUKA.
ila tukubali kuvumilia.na.tusikubali.ushawishi wa chama chochote kile kwani uhalisia ccm hawatokipachama.chochote kutawla.SASA SISI TUNAFANYWA MABOYA TUU.BORA TUSUSE.
Jiulize kwa nini inakuwa hivyo chanzo ni nini hasa. Kama utapata jibu basi anzia hapo kutafuta njia mbadala!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom