Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kinachofanywa na mpenzi wako ni kwaajili ya mpenzi wake wa zamani

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kinachofanywa na mpenzi wako ni kwa ajili ya mpenzi wake wa zamani, mahusiano hayadumu siku hizi kwasababu tunawapata watu wanaowapenda na kuwakumbuka watu wao wa zamani, tunakabiliwa na ukosefu wa amani ambao hatukuusababisha sisi.

Tunachumbiana na kuwa kwenye mapenzi na watu ambao wanataka kuwaonesha watu wao wa zamani kuwa wana uwezo wa kuishi bila wao, ni ukweli uliowazi kuwa tupo na watu ambao wanataka kuwaonesha watu wao wa zamani kuwa wana furaha kuliko wao, in short tunashughurika na ku uunda moyo ambao hatukuuvunja sisi, wanapima mapenzi waliyokuwa wanapewa zamani na unayompa wewe, kifupi tunapigana vita nyingi bila kujua.
 
Mbona mimi ni tofauti kwa sababu:-

Tukiachana naendelea na maisha yangu, sitaanza kukuchunguza unaendeleaje, uko na furaha au mahusiano yako yanaendeleaje hii kazi mimi binafsi kwa upande wangu imenishinda yan hua naanza moja, sitakutafya wala sitakufatilia popote pale iwe mitandaoni iwe mtaani

Sio kwamba kuna muda memories hazitanijia vile tulivyokua tunaishi lakini ukweli wa moyo wangu hua najiambia he is no longer yours focus na mambo yako na inafanya kaz vizur kabisa

Tukiachana s kua siumii au skua nakupenda nina ile saut huniambia hakupangiwa kuwa wako kubali maamuzi utapata kilicho bora na najikuta nina amani kweli na maisha yanasonga

Najiuliza huu ugumu wa kuwasahau ma ex wenu mnautoa wapi??

Mkishaachana kubalini ndani ya mioyo yenu na akili zenu huyo mtu si wako tena yakubali hayo maamuzi
 
Shida ipo kwa wanawake akipata jimbo jipya basi control ni wapenzi wa zamani. Raha yoyote inaanza na wewe mwenyewe.
 
Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kinachofanywa na mpenzi wako ni kwa ajili ya mpenzi wake wa zamani, mahusiano hayadumu siku izi kwasababu tunawapata watu wanaowapenda na kuwakumbuka watu wao wa zamani, tunakabiliwa na ukosefu wa amani ambao hatukuusababisha sisi, tunachumbiana na kuwa kwenye mapenzi na watu ambao wanataka kuwaonesha watu wao wa zamani kuwa wana uwezo wa kuishi bila wao, ni ukweli uliowazi kuwa tupo na watu ambao wanataka kuwaonesha watu wao wa zamani kuwa wana furaha kuliko wao, in short tunashughurika na ku uunda moyo ambao hatukuuvunja sisi, wanapima mapenzi waliyokuwa wanapewa zamani na unayompa wewe, kifupi tunapigana vita nyingi bila kujua......
Ni vyema umelitambua hilo. Sasa ebu tupe solution yake basi
 
mimi kwa sasa nimeolewa, na sijawahi kujihusisha kuwaza kama na yeye ana mtu ana mzuzua huko nje bora napewa basic needs inatosha na kamwe siwez mchunguza

mimi kwa sasa nimeolewa, na sijawahi kujihusisha kuwaza kama na yeye ana mtu ana mzuzua huko nje bora napewa basic needs inatosha na kamwe siwez mchunguza
Kwa mwanamke hiyo mbona hamna jipya. Women look for the security that money provides na sio love.
 
kwa mwanamke hiyo mbona hamna jipya. Women look for the security that money provides na sio love.
Duh nilichomaanisha hakuna ndoa njema bila upendo,kuthaminiana, kusameheana, kuheshimiana, kuaminiana na mume kusimamia majukumu yake kama baba na kichwa cha familia hizo basic needs sijamaanisha hela hata hayo nimetaja kwangu ni basic needs na kikubwa mahitaj ya kimwili, sipo kwenye ndoa ili tu nionekane nimeolewa au nimefuata kitu fulani sababu najua kuna siku kitakosekana bas na ndoa itaanza kuyumba, kamwe siangalii pesa sababu najua zinatafutwa hivo tutazitafuta pamoja
 
Mbona mimi ni tofauti kwa sababu:-

Tukiachana naendelea na maisha yangu, sitaanza kukuchunguza unaendeleaje, uko na furaha au mahusiano yako yanaendeleaje hii kazi mimi binafsi kwa upande wangu imenishinda yan hua naanza moja, sitakutafya wala sitakufatilia popote pale iwe mitandaoni iwe mtaani
Dada hapo kwenye kupata kilichobora sio mara zote huwa ni kweli, unaweza achana na mtu lakini usipate aliyebora kama yeye.

So usijifariji na inspirational quotes kwamba ukiachana na mtu utapata aliyebora zaidi yake unaweza usipate aliyebora for the rest of your life japo najua huwezi confess hili
 
Dada hapo kwenye kupata kilichobora sio mara zote huwa ni kweli, unaweza achana na mtu lakini usipate aliyebora kama yeye.

So usijifariji na inspirational quotes kwamba ukiachana na mtu utapata aliyebora zaidi yake unaweza usipate aliyebora for the rest of your life japo najua huwezi confess hili
Sikia nikueleze, unapoanza mahusiano na mtu ni wazi kuna muda unaona kabisa hapa nimefika, na kama binadam hatufanani kimawazo wala mtazamo, mimi sijawah kujifariji ila ntakueleza jambo

Mpaka mnaamua mnaachana ni kwamba hamuwez kuwa pamoja tena na kila mtu kuendelea na maisha yake s ndio, sasa tumeachana nianze tena kucompare ex na alieopo inahusu?? kisa tu kamzidi sehem?? skia rafiki ni ngumu sana kuniamini lakini Mungu anaiona nafsi yangu hata huo ujinga wa kusema ex amemzidi sehem alieopo sijawah kuufanya, sijawah kukwama popote nikamtafta ex anisaidie, sjawah kuwasiliana na ex yoyote yule baada ya kuachana huyu ni mimi na najivunia kwa hili

Wewe kama huwez bas usilazimishe kila mtu asiweze kama wewe. na kila mtu ana namna yake alivyojipangia hivyo usilazimishe sana nifit kwenye namna yako
 
Dada hapo kwenye kupata kilichobora sio mara zote huwa ni kweli, unaweza achana na mtu lakini usipate aliyebora kama yeye.

So usijifariji na inspirational quotes kwamba ukiachana na mtu utapata aliyebora zaidi yake unaweza usipate aliyebora for the rest of your life japo najua huwezi confess hili
Na kuna wakati unaweza ukampata aliyebora zaidi ya wote ila ujinga wako kichwani ukakudanganya ukaanza kung'ang'ania mahusiano ya zamani, hapo ndo wengi wameharibu hata ndoa zao kwa ujinga kama huo!
 
sikia nikueleze, unapoanza mahusiano na mtu ni wazi kuna muda unaona kabisa hapa nimefika, na kama binadam hatufanani kimawazo wala mtazamo, mimi sijawah kujifariji ila ntakueleza jambo

mpaka mnaamua mnaachana ni kwamba hamuwez kuwa pamoja tena na kila mtu kuendelea na maisha yake s ndio, sasa tumeachana nianze tena kucompare ex na alieopo inahusu?? kisa tu kamzidi sehem?? skia rafiki ni ngumu sana kuniamini lakini Mungu anaiona nafsi yangu hata huo ujinga wa kusema ex amemzidi sehem alieopo sijawah kuufanya, sijawah kukwama popote nikamtafta ex anisaidie, sjawah kuwasiliana na ex yoyote yule baada ya kuachana huyu ni mimi na najivunia kwa hili


wewe kama huwez bas usilazimishe kila mtu asiweze kama wewe. na kila mtu ana namna yake alivyojipangia hivyo usilazimishe sana nifit kwenye namna yako
Natamani wanawake wengi wangeliona hili, wajinga wengine wanaharibu ndoa zao kwa kuendekeza ujinga ujinga tu!
 
Natamani wanawake wengi wangeliona hili, wajinga wengine wanaharibu ndoa zao kwa kuendekeza ujinga ujinga tu!
Unajua hata kimaisha unapoamka huwezi kuwaza jana ilishapita hiyo lazima uwaze siku uliopo na siku zinazokuja kama uzima utajaaliwa, sasa imagine mmeachana halaf bado una hold on na ex atakufikisha wapi??

Ukianza kuwaza mambo yaliyopita huwez kusonga mbele sababu kuna muda utatamani uishi hizo nyakat ukarekebishe palipo na makosa kitu ambacho hakiwezekani ni kukubali na kukubali kujifunza kutokana na makosa

Na shida mtu ukiongea ya moyoni watu wanaona unafake kitu ambacho s cha kweli mimi hivi ndio naishi na si kwamba sina ex walikuwepo na ukiniuliza wanaendeleaje jibu ni sijui na wala sitaki kujua sababu kila mtu ana maisha yake
 
Wakuu habari zenu kwanza!!! Nami nimeona nichangie kidogo kwenye uzi huu kama ifuatavyo; Ni ukweli usiopingikaa kuwa watu wengi wameoa||wameolewa na watu wasio wa machaguo yao na ndio maana hata leo hii ukiwauliza wanandoa kama wangepewa nafasi ya pili kuoa||kuolewa na watu hao hao_Je,wangemchagua mtu huyo huyo tena??

Nafikiri wengi majibu tunayajua yangekuwaje!!!! Maisha yako ni matokeo ya machaguo yako,hivyo basi katika kuchagua jitahidi sana UCHAGUE yule wa SIZE yako hata kama nae alikuwa na size yake lakini ikampwaya__Ipo hivi ukiona HUYO MTU UMEMSHINDWA WEWE haimaanishi WOTE WATAMSHINDWA,kwani huyo uliyemshindwa wewe kuna WENGINE WANAMWEZA!!!! Nawatakia siku njema...
 
Back
Top Bottom