Tunahitaji Katiba Mpya au upinzani mpya?

Hii tabia ya wana siasa kusema uongo mfululizo ikiachwa iote mizizi bila kukemewa inaweza kuja kuleta maafa makubwa sana kwa taifa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii na kujikuta watanzania wazalendo wanawekwa pembeni na mafisadi ndiyo yanashika usukani wa kuongoza nchi yetu.

Kwa kuzingatia amri ya Mungu inayotutaka kutosema uongo wala kumshuhudia jirani yako uongo basi wanasiasa wafuatao wanatakiwa kujitokeza mbele ya jamii kutubu na kuwaomba radhi watanzania kwa kuwaaminisha uongo kabla ya ghazabu za mwenyezi Mungu hazijawashukia.

1. Zitto Kabwe
Huyu alianza kwa kupinga ufufuaji wa shirika la ndege , akawatangazia watanzania kwamba ndege zinazonunuliwa na serikali ni mitumba hivyo hazitakuja kufanya kazi yoyote. Leo ndege hizo zimemaliza miaka 5 zikipiga kazi ya kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi na yeye mwenyewe Zitto Kabwe amekuwa mteja mkubwa wa ndege hizo. Je, ni lini Zito atatoka mbele ya jamii kukanusha uongo wake kwamba hizo ndege hazikuwa mitumba?

2. Tundu Lissu
Huyu alipinga serikali kuanzisha upya mazungumzo kuhusu mikataba mbalimbali ya madini iliyokuwa inanyonya nchi yetu. Lisu alijigeuza wakili wa kutetea Acacia na akawatisha watanzania kwamba watashitakiwa MIGA, cha kushangaza kampuni ya Acacia walikubali matakwa ya serikali na kuunda kampuni mpya ya Twiga iliyopelekea mapato ya madini kupanda maradufu hapa nchini. Je Lisu akatubu lini kwamba aliwadanganganya watanzania?

3. Freeman Mbowe
Huyu aliwadanganya watanzania kwamba lazima wafanye lockdown ya Corona na chanjo ya Corona lazima iwe lazima Tanzania, alifikia hatua ya kuanza kufanya mikutano kwa njia ya mtandao lakini jioni akawa anaonekana bila barakoa kwenye viwanja vya bia, je alikuwa anamdanganya nani?

4. John Heche
Huyu alipinga ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) akasema watanzania waamke hakuna kipande hata cha mita moja cha reli ya kisasa kitakachojengwa, lakini sasa kipande cha Dar -Dodoma kimeshakamilika na Heche bado hajatoka hadharani kufuta uongo wake!.

5. Nape Nnauye
Huyu alitumia kila njia kupinga ujenzi wa bawawa la kufua umeme la mwl Nyerere kwamba utaleta hatari kubwa kwa wakazi wa mikoa ya kusini, lakini ujenzi wa bwawa unaendelea na umefikia 70% lakini bado Nape hajajitoleza tena kuwafafanulia wananchi hatari walizozipata mpaka sasa kutokana na mradi huo kufikia 70%.

Kutokujitokeza kwake kuainisha hizo athari maana yake alisema uongo na hatujui alikuwa anasema uongo ili watanzania wasichimbe bwawa lao kwa faida ya nani.
 
Tunahitaji upinzani wa kweli, siyo hawa wanaoongozwa na mlamba asali Mbowe na kibaraka wa mabeberu Lissu.
 
TUNATAKA KATIBA MPYA BILA CCM kwani CCM ina Miaka 60 Madarakani bado inahangaika na Ujenzi wa MATUNDU ya VYOO
 
Kwenye list ongezea,
Rais ni mzima anachapa kazi, au mnataka kumwona kariakoo, kilichofuata unakijua.
Aliesema hayo tena msikitini unamjua,
 
Kumbuka upinzani siyo chama Bali Ni wananchi kuwa na akili na kujitambua,
Ujitaka upinzani usiwepo,inabidi uwaue wananchi wote unaki peke yako,asiwepo mtutu yoyote wa kupishana nae kimawazo.
Akili yako inawazaga kuua tu? Nazungumzia mfumo mpya wa kufanya upinzani; sio huu wa maluweluwe na danganyatoto tunaouona sasa kwenye vyama vinavyojiita kwamba ni vya upinzani.
 
Upinzani kama uliopo Russia??
Akili yako inawazaga kuua tu? Nazungumzia mfumo mpya wa kufanya upinzani; sio huu wa maluweluwe na danganyatoto tunaouona sasa kwenye vyama vinavyojiita kwamba ni vya upinzani.
 
Wananchi,watu ndiyo huwa wanatakaga na kuleta mabadiliko ya kweli siyo vyama siasa

Ova
 
Hii tabia ya wana siasa kusema uongo mfululizo ikiachwa iote mizizi bila kukemewa inaweza kuja kuleta maafa makubwa sana kwa taifa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii na kujikuta watanzania wazalendo wanawekwa pembeni na mafisadi ndiyo yanashika usukani wa kuongoza nchi yetu.

Kwa kuzingatia amri ya Mungu inayotutaka kutosema uongo wala kumshuhudia jirani yako uongo basi wanasiasa wafuatao wanatakiwa kujitokeza mbele ya jamii kutubu na kuwaomba radhi watanzania kwa kuwaaminisha uongo kabla ya ghazabu za mwenyezi Mungu hazijawashukia.

1. Zitto Kabwe
Huyu alianza kwa kupinga ufufuaji wa shirika la ndege , akawatangazia watanzania kwamba ndege zinazonunuliwa na serikali ni mitumba hivyo hazitakuja kufanya kazi yoyote. Leo ndege hizo zimemaliza miaka 5 zikipiga kazi ya kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi na yeye mwenyewe Zito Kabwe amekuwa mteja mkubwa wa ndege hizo.! Je ni lini Zito atatoka mbele ya jamii kukanusha uongo wake kwamba hizo ndege hazikuwa mitumba?

2. Tundu Lissu
Huyu alipinga serikali kuanzisha upya mazungumzo kuhusu mikataba mbalimbali ya madini iliyokuwa inanyonya nchi yetu. Lisu alijigeuza wakili wa kutetea Acacia na akawatisha watanzania kwamba watashitakiwa MIGA !, cha kushangaza kampuni ya Acacia walikubali matakwa ya serikali na kuunda kampuni mpya ya Twiga iliyopelekea mapato ya madini kupanda maradufu hapa nchini. Je Lissu akatubu lini kwamba aliwadanganganya watanzania?

3. Freeman Mbowe
Huyu aliwadanganya watanzania kwamba lazima wafanye lockdown ya Corona na chanjo ya Corona lazima iwe lazima Tanzania , alifikia hatua ya kuanza kufanya mikutano kwa njia ya mtandao lakini jioni akawa anaonekana bila barakoa kwenye viwanja vya bia. Je, alikuwa anamdanganya nani?

4. John Heche
Huyu alipinga ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) akasema watanzania waamke hakuna kipande hata cha mita moja cha reli ya kisasa kitakachojengwa,lakini sasa kipande cha Dar -Dodoma kimeshakamilika na Heche bado hajatoka hadharani kufuta uongo wake!.

5. Nape Nnauye
Huyu alitumia kila njia kupinga ujenzi wa bawawa la kufua umeme la mwl Nyerere kwamba utaleta hatari kubwa kwa wakazi wa mikoa ya kusini, lakini ujenzi wa bwawa unaendelea na umefikia 70% lakini bado Nape hajajitoleza tena kuwafafanulia wananchi hatari walizozipata mpaka sasa kutokana na mradi huo kufikia 70%. Kutokujitokeza kwake kuainisha hizo athari maana yake alisema uongo na hatujui alikuwa anasema uongo ili watanzania wasichimbe bwawa lao kwa faida ya nani.
 
Back
Top Bottom