Tunahitaji Katiba Mpya au upinzani mpya?

Bikirajohola

JF-Expert Member
Jun 11, 2022
356
632
Hii tabia ya wana siasa kusema uongo mfululizo ikiachwa iote mizizi bila kukemewa inaweza kuja kuleta maafa makubwa sana kwa taifa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii na kujikuta watanzania wazalendo wanawekwa pembeni na mafisadi ndiyo yanashika usukani wa kuongoza nchi yetu.

Kwa kuzingatia amri ya Mungu inayotutaka kutosema uongo wala kumshuhudia jirani yako uongo basi wanasiasa wafuatao wanatakiwa kujitokeza mbele ya jamii kutubu na kuwaomba radhi watanzania kwa kuwaaminisha uongo kabla ya ghazabu za mwenyezi Mungu hazijawashukia.

1. Zito Kabwe

Huyu alianza kwa kupinga ufufuaji wa shirika la ndege, akawatangazia watanzania kwamba ndege zinazonunuliwa na serikali ni mitumba hivyo hazitakuja kufanya kazi yoyote. Leo ndege hizo zimemaliza miaka 5 zikipiga kazi ya kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi na yeye mwenyewe Zito Kabwe amekuwa mteja mkubwa wa ndege hizo! Je, ni lini Zito atatoka mbele ya jamii kukanusha uongo wake kwamba hizo ndege hazikuwa mitumba?

2. Tundu Lissu
Huyu alipinga serikali kuanzisha upya mazungumzo kuhusu mikataba mbalimbali ya madini iliyokuwa inanyonya nchi yetu. Lisu alijigeuza wakili wa kutetea Acacia na akawatisha watanzania kwamba watashitakiwa MIGA !, cha kushangaza kampuni ya Acacia walikubali matakwa ya serikali na kuunda kampuni mpya ya Twiga iliyopelekea mapato ya madini kupanda maradufu hapa nchini. Je Lisu akatubu lini kwamba aliwadanganganya Watanzania?

3. Freeman Mbowe
Huyu aliwadanganya watanzania kwamba lazima wafanye lockdown ya Corona na chanjo ya Corona lazima iwe lazima Tanzania , alifikia hatua ya kuanza kufanya mikutano kwa njia ya mtandao lakini jioni akawa anaonekana bila barakoa kwenye viwanja vya bia, je alikuwa anamdanganya nani?

4. John Heche
Huyu alipinga ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) akasema watanzania waamke hakuna kipande hata cha mita moja cha reli ya kisasa kitakachojengwa,lakini sasa kipande cha Dar -Dodoma kimeshakamilika na Heche bado hajatoka hadharani kufuta uongo wake!

5. Nape Nnauye
Huyu alitumia kila njia kupinga ujenzi wa bawawa la kufua umeme la mwl Nyerere kwamba utaleta hatari kubwa kwa wakazi wa mikoa ya kusini, lakini ujenzi wa bwawa unaendelea na umefikia 70% lakini bado Nape hajajitoleza tena kuwafafanulia wananchi hatari walizozipata mpaka sasa kutokana na mradi huo kufikia 70%. Kutokujitokeza kwake kuainisha hizo athari maana yake alisema uongo na hatujui alikuwa anasema uongo ili watanzania wasichimbe bwawa lao kwa faida ya nani.
 
Kasimu alidai magu ni mzima anaendelea na majukumu yake kumbe mtu ameshakufa, uongo mwingine akasema watu bilioni tatu wameshuhudia mazishi ya magu, juzi akadai hakuna mapigano yaliyotokea huko kwa loliondo kwa maasai ila kifo cha askari na picha za majeruhi vimemuumbua, huyu jamaa anastahili tuzo ya uongo.
 
Sawa
 
Mbona hujamuandika Mungu wako dikteta Uchwara aliye ahidi laptop kwa kila mwalimu na laki tano kwa kila Kijiji? Magufuli alikuwa anasema maendeleo hayana Vyamaa lakini akawa anaua na kutesa wapinzani na kuwagiza wakurugenzi wasiwatangaze wapinzani ikiwa wameshindwa uchaguzi mbona hukumuweka?
 
Akina Mdee wako bungeni sababu ya utawala bora wa Magufuli, aliwaweka pembeni mahawara wa viongozi wa chadema
 
Back
Top Bottom