Tunahitaji kamusi yetu ya maendeleo wala si msamiati wa ulaya' ili kujikomboa weusi wa Africa

Mar 31, 2018
27
16
Wazungu, wa Asia hawa wezi watuhujumu sana Waafrica...biashara huria, ukoloni , utumwa, na ubeberu mambo leo ni matone tu katika bahari...! sio Ulaya wala Asia: Adidu rejea ya maendeleo wala ustaarabu...ni sisi wenyewe kujikubali kama tulivyo...
Nani Malaika wa kumhukumu Ndg; Magufuli?
Karibuni ndugu lakini kumbuka swali haliangalii tu eneo la lugha au isimu na fasihi yake bali eneo zima la maendeleo katika uzoefu wa mtazamo wetu wenyewe, inachosha kasumba ya wengi kufanya Ulaya na Asia kuwa adidu rejea ya maendeleo ya Africa....Ajabu ndio wamekuwa mabingwa wa kutukosoa na kutuagiza ya kufanya
Lakini wanasahau wao ndio walio koroga maendeleo na ustaarabu wetu uliodumu zaidi ya miaka 10,000 kabla ya kuziwa kristo...kwa kifupi na kubaliana na Ncha ya Mkukina et al' kwamba mstaarabu asilia mtu mweusi...Donald Trump kanawia uso kopo la uwani
 
Mi naanza na kuuliza msamiati wa neno hili hapa chini la Kiingereza kama lipo ktk lugha ya Kiswahili linalohusu tabia ya kibaolojia kuwa na harakati za kimaisha wakati wa usiku tu:

nocturnal
 
Wazungu, wa Asia hawa wezi watuhujumu sana Waafrica...biashara huria, ukoloni , utumwa, na ubeberu mambo leo ni matone tu katika bahari...! sio Ulaya wala Asia: Adidu rejea ya maendeleo wala ustaarabu...ni sisi wenyewe kujikubalu kama tulivyo...
Nani Malaika wa kumhukumu magufuli?
Umeupa kazi ubongo wako wa kufikiri sawasawa? Kwa hiyo we huoni chochote? Yaani wewe mambo yako sawa hakuna tatizo lolote?
 
Racist
 
Umeupa kazi ubongo wako wa kufikiri sawasawa? Kwa hiyo we huoni chochote? Yaani wewe mambo yako sawa hakuna tatizo lolote?
Yaliwahi kuwa sawa lini? Na yako sawasawa wapi? Kila mtu ataijenga nyumbake mwenyewe' kila nyumba haikosi upungufu wake...nyumba kamilifu na stadi labda kaburi..
 
Kwa uhusiano gani na mada husika?

Swali zuri, mojawapo ya kuonesha unaweza kujikwamua kifikra na kuwa na msamiati wa 'maendeleo' kwa mtazamo wa 'weusi' ni kuwa na lugha ya 'weusi' iliyoshiba/ sheheni maneno ya kisayansi, teknolojia, utabibu, sanaa n.k .

Hii haijalishi hata kama maneno yametoholewa / kukopwa toka lugha za Asia na Europa kuja ktk lugha ya 'weusi' ili uweze kuishawishi jamii inayokuzunguka kwa ufasaha kuwa wanaweza kufanya maendeleo kwa mtazamo wa ndani na siyo wa kuiga toka nje.
 
Dhima ya Kiswahili katika Usomaji kuelekea Umajumui wa Kiafrika........ 74
Dhima ya Lugha ya Mawasiliano katika Jamii: Kiswahili na Mkakati wa Usomaji kuelekea Umajumui wa Kiafrika.
Aldin K. Mutembei
Ikisiri
Dhima ya lugha ya mawasiliano imejadiliwa na wanazuoni kadhaa. Wengi wameiangalia kama yenye kuongelea masuala ya jamii inamochipuka wakiihusisha na fasihi, au ile yenye kutumia lugha za picha au kitaswira katika kuumba maana iliyokusudiwa. Makala hii inalenga mambo mawili yamsingi.

Mosi, ni kuangalia dhima ya lugha ya mawasiliano katika baadhi ya kazi za kifasihi zinazovuka mipaka ya jamii zinamochipuka na pili, ni kuiangalia ikiwa lugha hii inao uwezo wa
kutabiri yale yatakayokuja. Katika lengo la pili, makala inakwenda hatua moja zaidi na kuangalia ikiwa suala la Umajumui wa Kiafrika linaweza kujengwa na namna ya usomaji chanya wa kazi za kifasihi. Kwa hiyo, makala inajadili dhana ya “usomaji” kwa maana pana zaidi ya kuangalia
maandishi na kupata maana. Katika mjadala wa vipengele hivyo, makala hii itatumia nadharia ya Thieta ya Walalahoi (Theatre of the Oppressed) kwa mujibu wa mawazo ya Boal (2008). Mawazo ya Boal, ndiyo yatakayotuongoza kufafanua maana ya “usomaji” kwa mujibu wa makala hii.

Makala
inaonesha kuwa Umajumui wa Kiafrika unaweza kujengwa na kuimarishwa kupitia katika usomaji wa kazi za kifasihi wenye kulenga ukombozi. Mawasiliano katika lugha ya Kiswahili na baadhi ya kazi za Kifasihi za Kiswahili yanatolewa kama mfano wenye kuweza kutumika katika kujenga Umajumui wa Kiafrika.
 
Swali zuri, mojawapo ya kuonesha unaweza kujikwamua kifikra na kuwa na msamiati wa 'maendeleo' kwa mtazamo wa 'weusi' ni kuwa na lugha ya 'weusi' iliyoshiba/ sheheni maneno ya kisayansi, teknolojia, utabibu, sanaa n.k .

Hii haijalishi hata kama maneno yametoholewa / kukopwa toka lugha za Asia na Europa kuja ktk lugha ya 'weusi' ili uweze kuishawishi jamii inayokuzunguka kwa ufasaha kuwa wanaweza kufanya maendeleo kwa mtazamo wa ndani na siyo wa kuiga toka nje.
Asante
 
Mi naanza na kuuliza msamiati wa neno hili hapa chini la Kiingereza kama lipo ktk lugha ya Kiswahili linalohusu tabia ya kibaolojia kuwa na harakati za kimaisha wakati wa usiku tu:

nocturnal
Nimekuelewa, lakini si hoja ya msingi, ni jambo la kawaida katika isimu ya lugha baadhi ya msamiati na maana zake kutokuwepo katika lugha nyingine ama kutoholewa kutoka lugha nyingine kwa mfano niambie neno Shangazi kwa kiingereza....? Tupambane na hali sambamba na mazingira yetu sio kutengenezewa hali na mazingira bandia....
 
Tuliletewa fikra za waafrika kujikana kwanza na inavyoonesha ni kana kwamba tulilambishwa na "yamini". So sad indeed.
Hakika hatuko kwa ajili ya nafsi zetu wenyewe
Tunatawaliwa kiujanja mno kupitia akili ama mfumo mawazo....in other words we are working for them
 
Back
Top Bottom