Tunahitaji chama kipya?

Tunahitaji chama kipya?

Huu ni mwanzo.....kama marekani waliwahi kupigana wao kwa wao lengo likiwa ni kurudisha umoja na utii wa sheria.....basi nasi tusikate tamaa. Hawa akina chenge, makamba, lowasa, chiligati na wenzao muda si mrefu they will be dying.
 
TUanzishe chama cha Kibepari, mlengo wa kibepari na mfumo wa uchumi wa kibepari kama vile vyama vilivyoko Scandinavia/Nordic!
 
Huu ni mwanzo.....kama marekani waliwahi kupigana wao kwa wao lengo likiwa ni kurudisha umoja na utii wa sheria.....basi nasi tusikate tamaa. Hawa akina chenge, makamba, lowasa, chiligati na wenzao muda si mrefu they will be dying.

Huwa hawafi mapema hao watu!, sentensi yako ni ya kuwa umekata tamaa, na kilichobaki unawaombe kufa tu, yaani kwa vile sio mchawi, kama ungekuwa mchawi ungeshawaroga

Nadhani uchaguzi wa chadema ulikwisha salama na kambi zote mbili zilivunjwa siku hiyo kwa ajili ya kuleta mshikamano kwenye chama. Nadhani tusikae tuna quote mambo ya nyuma kila chama kina matatizo yake.

Je hayo makambi hayatatokea in near future?? guaranteed?

Hii topic ni nzuri.
mjj amelenga pazuri.
kuunda chama kipya itatuchukua muda mrefu kutarua matatizo ya nchii hii. tuwasaidie hawa viongozi wa vyama vilivyopo katika uteuzi mzuri wa kiongozi wa kitaifa (Rais) ambaye ana sifa zote ambazo sisi wananchi tunazi afiki. na ana maadili mema ya kiungozi na hasa mkali kwa tukio lolote linalokwenda kinyume na matakwa ya wananchi (adhabu iwepo pale pale kwa mtuhumu huyu). naamini candidates hao wapo. support ni muhimu sana baada ya kupatikana mtu huyu. natuanze kumfikiri sasa. Mimi nitaanza na dr slaa sisna mrengo wowote wa kichama. kama kuna mtu wa kunikosoa na anikosoe sasa.

Wako wanaojiamim kuwa wana uwezo na mawazo mazuri, lakini je watapata nafasi kwenye hivi vyama vya kifamilia na ukoo?
 
Mkulu Mwanakijiji, heshima mbele sana;-

- Haya nimeyasema sana hapa JF, kwamba dawa ni kuanza upya na ninashukuru kwamba finally umeliona hili kama lilivyo, kwamba tunahitaji kuanza upya. Kwa maoni yangu ni kwamba vyama vyote vya siasa nchini in one way or another vina spirit ya CCM ndani yake, hatuwezi kwenda popote wala kupata mabadiliko yanayotakiwa, na hivi vyama.

- Ni miaka karibu 15 sasa toka tuingie kwenye siasa za vyama vingi, matokeo hayaridhishi ukilinganisha na nchi zingine majirani ambao tulianza pamoja mabadiliko, CUF na Chadema, sio siri wamejitahidi sana lakini it is too little na ni too low to show for, huku the time is running out.

Wakati ni huu wa kuanza upya! I mean tunahitaji chama kipya very badly regardless ya its immediate effect kwa taifa, lakini ni lazima tuwaamshe wananchi kwa kuwaanika wazi hawa wanafiki kwamba wote wanafanana, kazi kupeana per-day za kusafiri nje na kamati uchwara za bunge huku wakidai serikali haina pesa, nonsense!

Respect.

Field Marshall Es!
 
I wish hicho chama kipya kiibuke leo leo......but hold on.....? Nani atakuwa behind that chama na kusimamia mazuri hayo unayoyasema? Watanzania waliowengi sasa hivi wamekata tamaa kabisa na siasa....to them ni bora liende!

Look uchaguzi wa juzi, very few walijiandikisha na kupiga kura jana......kwa mfano Dar es Salaam yote..only 500,000 people ndio waliojiandikisha kupiga kura.....out of more than 5,000,000 people! kati ya hao pengine hata 200,000 hawakufika kupiga kura, ask yourself why?

Yes, we badly need that chama kipya......lakini utaingia na strategy ipi to win the mass, na kubadili idealogy za watz walio wengi? Tutafanya nini kuamsha ari ya kisiasa kwa Watanzania ambayo siku hadi siku inakufa /potea?
 
Kwa mnaosema tuanzishe chama kipya maswali yangu yako pale pale na sijajibiwa bado. Tukumbuke kuwa lengo letu liwe quality ya vyama na kamwe si quantity.

At the risk of coming off as immodest, I quote myself.

Kabla ya kuanzisha chama kipya, kama kinataka kuwa cha maana, inabidi waanzilishi wajiulize maswali yafuatayo.

1. Kuna haja ya chama kipya?
2. Vyama vilivyopo haviwezi kukidhi mahitaji?
3. Kuna tofauti gani ya kimsingi kati ya vyama vilivyopo na hiki kipya?
4. Ni kwa vipi chama hiki kipya kitajizuia kurudia makosa ya vyama vilivyopo?
5. Chama hiki kipya kitachangia nini kipya?

Tusije kuhangaika kuanzisha chama kipya halafu kikaja kuwa carbon copy ya vilivyopo sasa.
Tusije kuanzisha chama kipya wakati tunachohitaji hasa ni mabadiliko ya kikatiba
Tusije kuanzisha chama kipya wakati hatujawaelimisha wananchi wetu juu ya umunimu wa elimu ya uraia.
Tusije kuanzisha chama kipya bila kujua tunataka kuleta mabadiliko gani na kwa nini vyama vilivyopo haviwezi kufanya kazi hii.
 
Tatizo sio wananchi. tatizo ni vyama havijapata viongozi sahihi....mwaka 1995, upinzani chini ya mrema ulifanikiwa kushinda asilimia43 ya kura za urais, asilimia 40 za kura za ubunge...kumbukeni hii ilikuwa miaka3 tu tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe...na labda kwa taarifa tu ni kwamba jijiji la Dar es Salaam, upinzani ulishinda majimbo yote saba, serikali ikafuta uchaguzi....viongozi wa upinzani wasiendekeze lawama kuwa wananchi hawataki mabadiliko..NO. wananchi wako tayari, tatizo ni viongozi wa upinzani bado wanasua mno...hatujapata mtu wa kuvaa viatu vya mrema wa 1995...tukimpata, wananchi sio tatizo mwanakijiji....
 
95 wananchi walikuwa na moto wa vyama vingi, kwa sababu ndiyo kwanza vilikuwa vimeruhusiwa. Na wapinzani walikuwa hawajapata muda wa kufanya makosa na kujionyesha kwamba na wao ni fallible kama CCM.

Kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele ndivyo upinzani unavyozidi kukosa nguvu (bara). i would say kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele ndivyo wananchi wanafunguka macho kuhusu mapungufu ya vyama vyote, including CCM.

Tatizo, hii scenario ni nzuri kwa CCM kwa sababu wananchi wanaonekana kusema "Ni bora chama kibaya chenye national presence na uzoefu kuliko chama kibaya kilicho kichanga kisicho uzoefu na kukosa national presence"

Hii ndiyo sababu pekee CCM inapeta mpaka leo, hatuna upinzani.Wakija wapinzani wa nguvu CCM inaondoka within 5 years.

Tatizo wapinzani wa nguvu hawawezi kuja katika system yetu ya sasa ambayo CCM inacontrol kila kitu, mpaka tume ya uchaguzi.

Ndiyo maana mimi nataka tujiulize sana kabla ya kuanzisha chama, je tunahitaji zaidi chama kipya (ambacho kitaface challenges hizi hizi) au tunahitaji zaidi institutional changes kama mabadiliko ya katiba na elimu ya uraia kwa watu?
 
Mkulu Bluray, with all due respect:-

- Tunahitaji chama kipya ambacho condition ya kujiunga itakuwa ni pamoja na kutowahi kushiriki kwenye siasa za taifa in the past, Rawlings aliwakusanya wanasiasa wote muhimu wa zamani na kuwatwanga risasi kule beach, leo Ghana ni numero uno na uongozi bora,

- Sisi hatuwapigi risasi ila hatuwataki kujiunga nasi, lengo la kwanza liwe ni kuwaamusha wananchi wa Tanzania, ambao sio siri wapo usingizini sana na kinachoendelea na taifa lao.

- Ni lazima wananchi waamushwe kwanza, the rest baadaye! Na yes tunahitaji chama kipya chenye wanachama wenye mawazo mapya na solutions kwa matatizo ya taifa letu.

Respect.

FMEs!
 
Lengo la kuanzisha chama kipya ni nini, Kama lengo ni 2010, nadhani sio wakati muafaka. Mnadhani na huu mgawanyiko wa chama tawala msajili wa vyama atathubutu kusajili chama kipya???? Hawezi kamwe. Sheria zibadilishwe ikiwamo sheria ya vyama vya siasa.
 
Mkulu Bluray, with all due respect:-

- Tunahitaji chama kipya ambacho condition ya kujiunga itakuwa ni pamoja na kutowahi kushiriki kwenye siasa za taifa in the past, Rawlings aliwakusanya wanasiasa wote muhimu wa zamani na kuwatwanga risasi kule beach, leo Ghana ni numero uno na uongozi bora,

- Sisi hatuwapigi risasi ila hatuwataki kujiunga nasi, lengo la kwanza liwe ni kuwaamusha wananchi wa Tanzania, ambao sio siri wapo usingizini sana na kinachoendelea na taifa lao.

- Ni lazima wananchi waamushwe kwanza, the rest baadaye! Na yes tunahitaji chama kipya chenye wanachama wenye mawazo mapya na solutions kwa matatizo ya taifa letu.

Respect.

FMEs!

MKuu sauti ya umeme,
Maneno makubwa haya, umegusa kabisa kwenye mzizi wa fitna. Kuna baadhi ya watu wamekuwepo kwenye siasa toka mkoloni anaondoka na mpaka leo wapo. Wamevuruga nchi na wanendelea kuvuruga nchi na hawataki kuachia madaraka. Sitaki kutaja majina yao.
Hatua aliyochukua Jerry Rawlings pamoja na kuwa inaoekana ni ya kishenzi ni hatua positive na effective. If we have to extricate ourselves from this mess, a few hundred people have to be eliminated from political life. Hii haikwepeki, huweze kusema unaserikali mpya Tanzania au chama kipya kikiwa kina operate under the shadow of mafisadi, no way.
Akitokea messiah na akifanya hilo, tunaweza kuanza kupiga hatua otherwise, we can notmove forward as a nation.
 
Mimi nadhani tunahitaji viongozi wazuri na si watawala wala chama tawala. Na hii tunaweza kufanya tu kama watu tutapiga kura na kuelimisha jamii juu ya uongozi bora na kiongozi bora. Vyama vya TZ zina sera nzuri sana. Tatizo ni jamii kutoa tamko kuwa tutamchagua anayefaa. Lakini pia siyo wote wanaojitokeza wanafaa, wengi wa wanaochaguliwa ndiyo wanaonekana angalau wanafaa. Basi vijana tujitokeze tugombee nyadhifa mbalimbali. Tuache kusemasema tu na wakati sisi wenyewe hatupo tayari kuomba ridhaa ya kuongoza hata mtaa. Maendeleo yako mtaani, barabara nzuri mtaani ni barabara nzuri TZ. Ukiangalia uongozi wa mtaa wamejitokeza wengi vikongwe sasa hawa ndiyo wanajukumu la kuwaweka madiwani, wabunge, na rais madarakani, kwani kura zote ni za vitongoji na mitaa....
 
Nadhani hakuna haja ya kuanzisha chama kingine bali kuna haja ya kufuta vyama vyote vya siasa.......haya mambo ya vyama ni kuiga tamaduni zisizo na tija. Tunaweza kufuta vyama na kuwa na serikali makini walau kwa muda ili utaalamu ufanye kazi badala ya siasa kuwa kila kitu. Tukishafikia mahali watu wamebadilika kifikra na kutambua uzalendo na umuhimu wao katika kujenga taifa ndio tunaweza kuamua ni mfumo upi unafaa kuongoza taifa letu.
 
Hata mukaanzisha chama gani sijuwi lakini serikali hamupati tanzania.

Ikiwa nyinyi ndio wasomi lakini bado CCM hamujaijuwa au sijuwi munababaisha tu.

CCM Haina Shida Ya KURA ya mtu YOYOTE wao wanatume ya U C H A G U Z I B A S I ikiwa mutaweza kufahamu hapo basi chama chengine kinahitajika vyenginevyo endeleeni kubwabwaja tu.
 
Usitegemee toka kwa NDIVYO TULIVYO.... Ukiweza kuelewa Wadanganyika na jinsi wanavyofikiria mkuu wangu chukua glass ya maji kunywa upoze koo. Ni swala ambalo haliwezekani na ndio maana tumekuwa hapa.

Kwanini umekata tamaa hivyo? Sivyo tulivyo; mabadiliko hayaji mara moja kama nguvu ya soda. Inahitaji determination na patience. Lakini kila jambo lina mwanzo na mwanzo ndo kama huo wa Mwanakijiji katoa wazo litazaa tamaa tamaa itakua na kuzaa uhalisia. Hata kama hatutaki mazingira yatatulazimisha kutaka kama mambo yataenda jinsi yalivyo basi naona muda si mrefu hii itakua si ndoto bali kitu halisi.
 
Mkulu Mwanakijiji, heshima mbele sana;-

- Haya nimeyasema sana hapa JF, kwamba dawa ni kuanza upya na ninashukuru kwamba finally umeliona hili kama lilivyo, kwamba tunahitaji kuanza upya. Kwa maoni yangu ni kwamba vyama vyote vya siasa nchini in one way or another vina spirit ya CCM ndani yake, hatuwezi kwenda popote wala kupata mabadiliko yanayotakiwa, na hivi vyama.

- Ni miaka karibu 15 sasa toka tuingie kwenye siasa za vyama vingi, matokeo hayaridhishi ukilinganisha na nchi zingine majirani ambao tulianza pamoja mabadiliko, CUF na Chadema, sio siri wamejitahidi sana lakini it is too little na ni too low to show for, huku the time is running out.

Wakati ni huu wa kuanza upya! I mean tunahitaji chama kipya very badly regardless ya its immediate effect kwa taifa, lakini ni lazima tuwaamshe wananchi kwa kuwaanika wazi hawa wanafiki kwamba wote wanafanana, kazi kupeana per-day za kusafiri nje na kamati uchwara za bunge huku wakidai serikali haina pesa, nonsense!

Respect.

Field Marshall Es!

Wewe si mwanachama wakudumu au? hahaaaaaaa nimefurahi kusikia umeokoka kisiasa. Sasa karibu nje ya chama ili tupange mikakati ya kuwakomboa vijana wenzetu na vyama vilivyozeeka. Njia rahisi nikuunganisha nguvu ya vijana wa taifa hili ambao mimi naona ndiyo watakao liokoa taifa hili na hivyo vya wazee tuwaache navyo waendelee kutupa changamoto huku sisi tukijipanga kuwaondoa taratibu pamoja na sera zao za ambazo nazo zimezeeka.
 
Chama hicho kitakusanya ndani yake baadhi ya vipaji vya hali ya juu ktk siasa zetu. It is just a matter of time.
 
mimi nadhani tunahitaji WANASIASA WAPYA!kwamba we get rid of the whole existing politicians,we start over
 
Mwana KJJ,
Labda ungeuliza kama tunahitaji watanzania wapya (kizazi tofauti na hiki)watakaokuwa wanachama wa vyama vya siasa! Upuuzi unaotokea hapa petu Dar unatia kichefuchefu! Mageuzi mara zote yanaanzia jijini, lkn kwetu ni vijijini. Wengi wetu ni wanafiki tu, tunapenda kusikia fulani katenda jambo lkn ushiriki wetu SIFURI. Ungetegemea Dar kushindwa japo kufikisha viti 80 vya upinzani serikali za mitaa?

Kwamba wagombe wote wa upinzani ni makapi na mandondocha? kwamba waliokuwa wanachagulika wote walienguliwa? kwamba wananchi hawakupata fursa ya kusikia wagombea tofauti na wa ccm?

Mwana wa nyani alimuliza ***** amuonyeshe mpaka la shamba lao la mahindi; mama alimpa jibu jepesi tu "Kula mwanangu, wenyewe watakauja kuweka mpaka". Huenda tunasubiri wajukuu wa watoto wetu kujaweka mpaka, ila sisi hatuna nafasi wala hayatuhusu. Ni aibu kubwa na inakatisha tamaa kiasi cha kutisha hasa kwa wale waliojitoa kwa hali na mali kuona hali ya mtanzania inabadilika kuiendea neema!
 
Chama hicho kitakusanya ndani yake baadhi ya vipaji vya hali ya juu ktk siasa zetu. It is just a matter of time.

Mwanakijiji,

Tatizo tuna address superficialities za vipaji and so on (personalities) wakati matatizo yetu yako katika institutional level.

Tunatibu TB kwa Cofta!

Sehemu inayotaka mabadiliko ya katiba, sisi tunataka kuanzisha chama chenye "dream team" ambayo huenda hata isifocus kwenye kuumaliza ukiritimba wa CCM uliokuwa constitutionalized.

Yale maswali yangu pale juu bado yanasimama, naona wote tuna beat around the bush, kabla ya kujibu maswali haya tunaweza kuzunguka kwenye vicious cycle of mediocrity tu.

Tunaanzisha chama kipya

Tunatafuta wanachama na viongozi

Kwa vile CCM ndiyo inagawa ruzuku na kimsingi Tanzania ni nchi ya chama kimoja CCM inaendelea kufustrate vyama vyote vya upinzani.

Migogoro inaanza kwenye chama kipya.

Watu wanaona ni wale wale tu.

Tunaanzisha chama kingine

Meanwhile CCM wanaendelea kupeta huku wakijisifia how democratic our country is, with all these new parties being formed every year.

Tunahitaji institutional changes, tunahitaji kupunguza nguvu za rais, tunahitaji tume huru ya uchaguzi, tunahitaji mabadiliko ya katiba, tunahitaji elimu ya uraia kwa wananchi, tunahitaji rule of law.Chama kipya kitajengwa vipi ili kiweze ku address haya yote in a way ambayo haiwezekani katika vyama vilivyopo? In other words, upya wake utakuwa nini?

Tusije kuleta chama kipya katika jina lakini kuanzia sera, format mpaka watu ni old wine in a new bottle.
 
Back
Top Bottom