COMOTANG
JF-Expert Member
- Jan 6, 2021
- 2,131
- 1,808
Yap
Yap
- Tanganyika ndio nchi iliyopata uhuru wake, 9 Desemba, 1961. 1964 Tanganyika ikaungana na Zanzibar kwa muungano wa union wa nchi mbili kuwa nchi moja, hivyo tulipoungana, tuliitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina la Tanzania lilikuja mwezi September 1964.
- Ile siku tunaungana, utaifa wa Jamhuri ya Tanganyika (sovereignty) na utaifa wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zote zilikwisha, na kuwa sio nchi tena, hiyo sovereignty ilikabidhiwa kwa nchi mpya ya Tanganyika na Zanzibar.
- Tanzania nayo pia ilipitishwa rasmi kule UN kama Taifa huru, la Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mnamo tarehe 14 May, 1964 kufuatia kuwasilishwa kwa taarifa rasmi ya maandishi, Note Verbale toka kwa Balozi wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa, wakati huo, Chief Arasto Mang'enya na kuitambulisha United Republic of Tanganyika and Zanzibar. Wakati huo, jina la Tanzania halijaanza kutumika. Mwezi June Balozi Mang'enya aliteuliwa rasmi kuwa balozi wa kudumu wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar kwenye Umoja wa Mataifa, na mwezi September ndipo akawasilisha rasmi hati zake za utambulisho na jina rasmi la United Republic of Tanzania kuwasilishwa UN.
- Nchi ikiishapoteza sovereignty inakuwa sio nchi tena, hivyo baada ya kupatikana jina la Tanzania, jina la Tanganyika likafutwa, likafa, likazikwa. Eneo la iliyokuwa Tanganyika sasa ndio Tanzania Bara, na iliyokuwa Zanzibar iliendelea kuitwa Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar kwa jina ila sio nchi.
- Sasa kwa vile Tanganyika haipo, tunaposhereherekea uhuru ni kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika, ila inayosherekewa ni shrehe ya Tanzania iliyopo na sio maadhimisho ya sherehe ya uhuru wa Tanzania, kumbukumbu ndio ya Tanganyika lakini maadhimisho ni ya Tanzania.
Wakati huo kulikuwa na German East Africa siyo Tanganyika. Tanganyika ilianza rasmi na ilikuwa chini ya Waingereza kutokana na League of Nations Mandate ya 1920. Nyerere aliitupa chooni kama kinyesi halafu akai flashi Tanganyika mwaka 1964.Kiukweli somo la historia linahitajika kwa wenzetu wengi humu. Haujui kuwa mipaka mingi ya bara letu la Afrika imewekwa na wakoloni baada ya ule mkutano wa Berlin wa mwaka 1884?. Katafute historia ya pre colonial Africa kabla ya ujio wa wakoloni, ndipo urejee hapa.
P
Ni kweli Tanzania haijawahi kupata uhuru, iliyopata uhuru ilikuwa ni Tanganyika chini ya chama cha TANU.Kwanza kabisa nchi bado haijapata uhuru. Tupo chini ya mkoloni mwingine anaitwa CCM. Tukijikomboa kutoka kwa huyu ndiyo tutaanza kuhesabu miaka ya uhuru
Kwahyo waziri mkuu sio wa muunganoHUNA AKILISawa Ni Uhuru wa Tanganyika mgeni rasmi anatakiwa kuwa waziri mkuu Kassim Majaliwa sababu Uhuru wa nchi hizi mbili sio Jambo la muungano .Raisi wa muungano hayamhusu .Yeye anatakiwa kuwa mgeni rasmi sherehe ya muungano tu na sio sherehe ya Uhuru wa Tanganyika au Zanzibar
Una hoja
Tanganyika ndyo Tanzania bara ya sasa, shida ulikua chooni wakati wenzio wanasoma historyDuuh tarehe 9/12/1961 nchi gani ilipata uhuru Tanganyika au Tanzania?
Unaposema Tanganyika doesn't exit labda kichwani mwako, uko shule mlenda kusomea ujinga
Kwahiyo Tanzania ilipata uhuru 1961??? Hebu jiongeze kiakili.Tanganyika Nyerere aliiflashi chooni mwaka 1964. Haipo tena. Angalia kwenye Atlas leo, Tanganyika haipo tena, angalia Google maps huoni Tanganyika.
Ccm ndo ilipata Uhuru, Tanzania bado. Ccm ikitokea wakaja kutolewa madarakani huo ndo Uhuru kamili wa TanzaniaMbona mnatuchanyanya hivi mkisema Miaka 60 ya UHURU wa TANZANIA mnakusudia hii Tanzania iliyozaliwa 64 au kuna nyengine?
Hivi waandishi wa habari na wanasiasa mnaosema UHURU WA TANZANIA hivi kweli hamjui historia yenu? Kwanini munainyanyapaa TANGANYIKA kiasi hiki?
Historia itabakia ni historia tuu hata mkitumia nguvu kiasi gani kuipotosha
Au Mimi ndio sifahamu haya mambo? Kama NI hivyo nielewesheni ni Tanzania gani iliyopata UHURU 1961?
Ni haya tu
Kiutendaji sio wa muungano Ni wa Tanzania bara tu.Shughuli zake hazigusi Zanzibar Hana sauti kuleKwahyo waziri mkuu sio wa muunganoHUNA AKILI
Tanzania haikuwahi kupata uhuru hivyo hakuna mantiki ya kusheherekea kumbukumbu ya uhuru wake.Tunaadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania, japo iliyopata uhuru ni Tanganyika. Kwa vile Tanganyika doesn't exist anymore, kilichopo ni Tanzania.
P
Uko sahihi kabisa.Kiutendaji sio wa muungano Ni wa Tanzania bara tu.Shughuli zake hazigusi Zanzibar Hana sauti kule
Hawezi mfokea au mfanyie chochote mkuu wa Mkoa au wilaya wa Zanzibar
Huyo ndie kiongozi wetu wa Tanganyika
Tanzania ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, wakati huo ikiitwa Tanganyika, hivyo tunavyosherehekea, tunafanya mambo mawili, jambo la kwanza ni kumbukizi, kumbukizi ni kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika. Jambo la pili ni kusherehekea, tunasherehekea siku ya uhuru wa Tanzania Bara, kwa kivupi Tanzania.Kabisaaa brother Pascal?? Uhuru wa Tanzania Ni Miaka 60???
Kwani Tanzania ilipata Uhuru lini?
Unapaswa kufahamu kuwa hakuna nchi inaitwa Tanzania bara, na haijawahi kutokea hiyo nchi hapa duniani. Tanzania bara sio nchi ni neno tu la kuelezea eneo la nchi kavu katika jamhuri ya muungano. Hivyo hatuwezi kusheherekea uhuru wa nchi ambayo haikuwahi kuwepo na haipo popote.Ni Uhuru wa Tanzania bara
Jina lilibadlishwa kisheria kuwa Tanzania Kama wewe unavyoweza badili jina tukasema Leo birthday ya Juma jina lako jipya baada ya kuslimu ukubwani na kubadili jina la asili la Chapombe na kuitwa Juma badala ya kuendelea nalo jina la Chapombe msikitini
Ni Uhuru wa Tanzania bara
Ila Zanzibar huwa hawataki Hilo wao huadhimisha uhuru.wa Zanzibar sio wa Tanzania visiwani!
Linatakiwa kuongeza neno bara nyuma kuwa ni uhuru wa Tanzania bara
All the facts are right, ni katika kuelimishana, baada ya Tanzania kuwa ni jina la nchi mpya iliyoundwa mwaka 1964, baada ya muungano, then nchi ya Tanganyika, ambayo haikuwahi kubadili jina, ilikwenda wapi?. Kwa faida yako na wengine kama wewe, baada ya Muungano, nchi iliyokuwa Tanganyika, ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara, na nchi iliyokuwa Zanzibar ilibadili jina na kuwa Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Nchi hizi zote mbili zinatumia majina ya kifupi kwa Tanzania Bara kuitwa Tanzania na Tanzania Zanzibar kuitwa Zanzibar, ila the official name ya Tanzania kama nchi inaitwa JMT.Tanganyika haikuwahi kubadilishwa jina ili iitwe Tanzania, bali Tanzania ni jina la nchi mpya iliyoundwa mwaka 1964.
Pascal Mayalla huo uhuru wa Tanzania ulitokeaje mwaka 1961 wakati nchi ya Tanzania iliundwa 1964?Tanzania ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, wakati huo ikiitwa Tanganyika, hivyo tunavyosherehekea, tunafanya mambo mawili, jambo la kwanza ni kumbukizi, kumbukizi ni kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika. Jambo la pili ni kusherehekea, tunasherehekea siku ya uhuru wa Tanzania Bara, kwa kivupi Tanzania.
P
Mkuu Zanzibar-ASP , ni mambo ya kuelimishana tuu,Pascal Mayalla huo uhuru wa Tanzania ulitokeaje mwaka 1961 wakati nchi ya Tanzania iliundwa 1964?
Pili, nchi ya Tanganyika haikuwahi kubadilishwa jina kuwa nchi ya Tanzania au Tanzania bara.
Mpaka leo hii, historia zote rasmi za waingereza zinatamka kuwa, taifa la uingereza liliacha Tanganyika kuwa nchi huru mwaka 1961.
Tusilazimishe Tanganyika kuwa ndio Tanzania.
Mmmh!All the facts are right, ni katika kuelimishana, baada ya Tanzania kuwa ni jina la nchi mpya iliyoundwa mwaka 1964, baada ya muungano, then nchi ya Tanganyika, ambayo haikuwahi kubadili jina, ilikwenda wapi?. Kwa faida yako na wengine kama wewe, baada ya Muungano, nchi iliyokuwa Tanganyika, ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara, na nchi iliyokuwa Zanzibar ilibadili jina na kuwa Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Nchi hizi zote mbili zinatumia majina ya kifupi kwa Tanzania Bara kuitwa Tanzania na Tanzania Zanzibar kuitwa Zanzibar, ila the official name ya Tanzania kama nchi inaitwa JMT.
P
ZANZIBAR haipo mahututi na kila leo inazidi kuwa strong kuliko Jana kikazi kipya ni kiazi cha kuhoji hamuezi kutuletea Stori za kina karumeMmmh!
Lazima hapo nitofautiane na wewe.
Nature ya muungano wa nchi mbili tuliofanya 1964, ulipelekea mambo matatu tu.
1. Kuundwa kwa taifa moja jipya lililopewa jina jipya la Tanzania. (Hivyo Tanzania ni nchi mpya na jina jipya).
2. Kuundwa kwa serikali mbili ndani ya taifa moja la Tanzania (yaani serikali ya muungano na serikali ya Zanzibar)
3. Kufa kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar AU Kuendelea kuwepo (kihistoria) kwa nchi za Tanganyika na Zanzibar mbili zilizokufa!
Kwa kifupi sana Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 ili kuunda nchi mpya ya Tanzania, iliziua nchi zote mbili, Tanganyika ilizikwa siku ile ile na Zanzibar japokuwa nayo ilikufa siku ile lakini ikagoma kuzikwa, na mara kadhaa imepambana kufufuka (na ikafanikiwa!) japokuwa iko mahututi.