Tumtengeneze Mwigulu kuwa Rais bora ajae

Tumtengeneze Mwigulu kuwa Rais bora ajae

Bila katiba mpya tutakuwa na viongozi ambao wana tamaduni za kimasikini kama Mwigulu mpaka leo yeye kalimbikiza mabilioni kama waziri wakati anao wawakilisha wana nyumba za matope mpaka leo !!!! Yeye ananunua nyumba kwa $2M huko masaki kila siku. Nchi itaendelea kuwa masikini kama tuna watu vilaza kama huyu mchangiaji. Katiba mpya pekee ndiyo itatutoa hapa
Porojo hizo, hakuna eliejuu ya sheria kwa mujibu wa Katiba yetu. kama kweli ushahidi wa ufisadi wake unao kwanini huendi mahakamani akamatwe mara moja? jf ni mahakama?. Tuache porojo za kudhaniahdhania tu.
 
Mbona Jpm alimtimua, amekuja kumrejesha sa100 ?


View: https://youtu.be/VYEGJmWxOoo?si=LEQPgtYvGfuIPRZT

Aliyemwita mwizi asitwambie sisi, aende mahakamani tuone kama sio chuki tu dhidi yake. Ni kama wale wehu waliokuwa wanajifanya ni wanasheria nguli lakini hawampeleki Abduli mahakamani kwa ufisadi wake anaotufanyia watanzania; hawampeleki mahakamani Rostam Azizi kwa ufisadi wake. wanadhani watanzania hawana akili kwa kiasi hicho. Mpumbavu mmoja anatuambia eti mtu wa gesi ya kupikia ulipaswa kuuzwa Tsh 2000 tu, hata chupa ya bia haiuzwi hivyo, pakiti ya singara ni zaidi ya tsh 2000.
 
Asikwambie mtu, kuna watu wa makabila na madhehebu fulanifulani walijichimbia kwenye bandari zetu wakituhujumu utadhani mali yao. hata ufanye panguapangua ya namna gani pale bandari hawaondoki. Kilio hiki cha bandari sio cha burebure kabisa. Ni ulaji, upigaji na upendeleo uliovurugwavurugwa pale na ujio wa DP world.

Duu!! eti wangetumia mabomu ya machozi na maji ya washawasha, una akili timamu wewe? Watu waliotaka kuingia Ikulu kwa nguvu walizuiwa kwa nguvu na watu waliotaka kubakia Ikulu pia. Survival for the fittest. Ni mwehu tu atakaeamini kuwa yale yalikuwa maandamano tu ya amani, tena mwehu kabisa. Yalikuwa ni maandamano ya kutoka wapi kuelekea wapi kudai nini?, nani alikuwa anapelekewa ujumbe wa maandamano yale?. Waandamaji walikusudia kuharibu nini na nini ili ujumbe wao uonekane umefika kule walikotaka ufike?

Akili yako inaongozwa na mange Kimambi wewe. Akili ambayo inashindwa kutofautisha maandamano na mapinduzi, mali ya umma na mali ya Samia, mali ya serikali na mali ya watu binafsi, mali ya umma na mali ya CCM. Eti watu kama hao tuwakabidhi nchi, over my dead body!!!!
Swali moja nawauliza hao wanaharakati, ingetokea wale vijana wakaingia ikulu na kuchukua utawala wa nchi tungezisikia hizi kelele za Samia kustahili kushtakiwa ICC?.
 
Ninaweza nikahisi lengo la swali / hoja pendekezwa yako; ila umesahau sana kuwa kwa kuandika hivyo ni kama kumtuma mtu akaonje maji ya bahari mtwara, mafia, Dar, Tanga, Pemba, Zanzibar nk na unatazamia majibu yafanane kwa kuwa yote ni bahari ya hindi. Kua uyaone!!
 
Mbona Jpm alimtimua, amekuja kumrejesha sa100 ?


View: https://youtu.be/VYEGJmWxOoo?si=LEQPgtYvGfuIPRZT

Mambo ya kipumbavu haya kama wale waliokuwa wakidhani mabasi ya Esther ni mali ya Mwigulu wakayachoma moto.

Hata Ahmed Salim alipoonekana ana sifa na nguvu za kushinda kiti cha urais alizushiwa eti ana ndugu zake ni mageneral wa jeshi huko Oman. Wajinga tu ndio wataamini upumbavu kama huu ambao watu hawaendi mahakani kuthibitishwa.
 
Ninaweza nikahisi lengo la swali / hoja pendekezwa yako; ila umesahau sana kuwa kwa kuandika hivyo ni kama kumtuma mtu akaonje maji ya bahari mtwara, mafia, Dar, Tanga, Pemba, Zanzibar nk na unatazamia majibu yafanane kwa kuwa yote ni bahari ya hindi. Kua uyaone!!
Maoni na hoja ya mtu haipigwi rungu; njoo na hoja yako kupinga hoja. Mwl. Nyerere alituambia mtu mnaedhani anafaa kuwa kiongozi wa nchi lazima watu wapate muda mrefu kumjadili kabla ya kuwa kiongozi. Mimi haya ni maoni yangu mimi kwakuwa nami ni mtanzania ambae nilikuwepo kwenye awamu zote hata hii, ingawa awamu ya kwanza sikuifaidi vizuri maana iliisha nikiwa sekondari. Hata wewe unaweza kuwa rais maana ni mtanzania, lakini nadhani huwezi kuwa rais mzuri kuliko Mwigulu.
 
waliokuwa wakidhani mabasi ya Esther ni mali ya Mwigulu wakayachoma moto.
Watu wana ushahidi broo
Hata Ahmed Salim alipoonekana ana sifa na nguvu za kushinda kiti cha urais alizushiwa eti ana ndugu zake ni mageneral wa jeshi huko Oman.
Ni mjinga pekee anaweza kulinganisha marehemu Salim Ahmed Salim na tapeli, fisadi Mwigulu.

Huyo fisadi amesaidiana na Sa100 kupandisha deni la Tanganyika kutoka T60 hadi T 127 ndani ya miaka 4 tu kwa maslahi ya Wazanzibar!!
 
Usiwe mpumbavu wewe unamuona wapi na kwa kigezo gani?
Kaka najua kwanini unasema hivyo. Nyerere, Mkapa na Magufuli walikuwa wakatoliki. Hii haikutokea kwa bahati mbaya tu, sisi tunalijua hilo.
 
Aliyemwita mwizi asitwambie sisi, aende mahakamani tuone kama sio chuki tu dhidi yake. Ni kama wale wehu waliokuwa wanajifanya ni wanasheria nguli lakini hawampeleki Abduli mahakamani kwa ufisadi wake anaotufanyia watanzania; hawampeleki mahakamani Rostam Azizi kwa ufisadi wake
Mahakama gani mkuu, hizo mahakama-ccm zinazoendeshwa kwa maelekezo kutoka juu?
mmoja anatuambia eti mtu wa gesi ya kupikia ulipaswa kuuzwa Tsh 2000 tu, hata chupa ya bia haiuzwi hivyo, pakiti ya singara ni zaidi ya tsh 2000.
Kwa mfano unajua bei ya petrol Iran?
 
Watu wana ushahidi broo

Ni mjinga pekee anaweza kulinganisha marehemu Salim Ahmed Salim na tapeli, fisadi Mwigulu
Kama una ushahidi na chama kina wanasheria wengi na mahiri mnasubiri nini kufungua jarada la kesi? Badala ya kung'unikia jf kuwa Mwigulu, Abudli, Rostam, sijui Ridhiwani, na nani ni mafisadi nenda mahakamani hata ile ya East Afrika, Afrika au Dunia kama hii hapa hamuiamini ili watanzania waujue ukweli. La sivyo nyamaza.
 
Badala ya kung'unikia jf kuwa Mwigulu, Abudli, Rostam, sijui Ridhiwani, na nani ni mafisadi nenda mahakamani hata ile ya East Afrika, Afrika au Dunia kama hii hapa hamuiamini
Ili mfanye utekaji na mauaji?

Fisadi na muuaji Mwigulu amezunguka karibu mikoa yote akitetea mauaji ya maelfu ya Watanganyika ya MO29.

Na ni huyo huyo aliwahi kuwaambia wananchi maskini kuwa wakishindwa kulipa utitiri wa Tozo wahamie Burundi
 
Ili mfanye utekaji na mauaji?

Fisadi na muuaji Mwigulu amezunguka karibu mikoa yote akitetea mauaji ya maelfu ya Watanganyika ya MO29.

Na ni huyo huyo aliwahi kuwaambia wananchi maskini kuwa wakishindwa kulipa utitiri wa Tozo wahamie Burundi
Kwenye ziara zile ukiwasikiliza wananchi hawana kero ya Katiba wala uchaguzi. Kero zao zinahusu wafugaji na wakulima, ardhi, kupokonywa urithi na dugu, barabara, maji, umeme, nk. Wavimbamacho wetu huku mjini wanasema "wananchi" wanataka hiki wanataka kile kana kwamba walifanya kura ya maoni (white paper) kuhoji wananchi wanataka nini. Ukweli hakuna chadema huko wilayani na hata ule uhaini ulikuwa umefanywa hukuhuku waliko wavimbamacho; sehemu zilipo airports.
 
Ww itakuwa ni mzee, au kijana zombie. Watu hao tu ndio wanaweza kuandika huu ujinga ualiondika hapa. Yale mauji yalifanyika ili kulinda kikundi kidogo kukaa madarakani kwa shuruti, na wala sio kulinda amani. Kulinda amani yangetumika maji ya washawasha na mabomu ya machozi.

Halafu mahali nimekuona ww ni mjinga, ni hapo unaposema wazungu bado wanataka vitu toka kwetu. Ni hivi, hakuna chochote wazungu watataka kwenye nchi wakakiosa tena bila kutumia nguvu. Kama huamini nenda kaangalie mikataba yote ya raslimali ni nani wameingia. Kuhusu bidhaa zao hawana muda hata wakuzileta huku maana wanajua sisi ni masikini, hivyo wameacha tuuziwe bidhaa fake toka China, kwani zakwao hatufiki bei. Hivyo unavyosema wanavitaka wanaweza kuvipata hata sasa tena kwa bei cheap. Na bidhaa zetu wananua kwa bei poa kwani hazina ubora. Kuhusu cheap labour sisi ndio tunazamia kwao kusaka maisha.
Hatuendi ikulu kwa kupindua, maana hiyo ni njia hatari sana inayohitaji hesabu nyingi. Walisusia uchaguzi ili waende Ikulu kwa mapinduzi. Kaka sio rahisi kiasi hicho.

Ni mazombie tu ambao wataamini porojo za kwamba yale hayakuwa mapinduzi. Miscalculated (failed) cue. Yaani ulisema mwenyewe hadharani mchana kweupe kuwa mtaaasi na kweli maasi yakatokea na kunuka palinuka kweli damu za watu. Hii mifuko ya vitabu vya sheria mahakamani haiwezi kutuzuga watanzania kutuambia sio wewe uliyepanga mapinduzi eti kwakuwa ulikuwa mahabusu wakati wa tukio. Ujinga kama huu hata Ikungi hawaukubali. Lazima mlipe gharama za mali zote mlizoharibu na watu waliokufa, mifuko mikubwa ya vitabu vya sheria na uhodari wa kusema havitumiki huku Afrika, mtalipa tu.
 
Back
Top Bottom