Tumtengeneze Mwigulu kuwa Rais bora ajae

Ili mfanye utekaji na mauaji?

Fisadi na muuaji Mwigulu amezunguka karibu mikoa yote akitetea mauaji ya maelfu ya Watanganyika ya MO29.

Na ni huyo huyo aliwahi kuwaambia wananchi maskini kuwa wakishindwa kulipa utitiri wa Tozo wahamie Burundi
Waliuliwa Mungiki toka Kenya. Eti wakenya waliletwa kuja kuwafundisha watanzania namna ya kuchoma yao.
Watu wanalinganisha Kenya na Tanzania kimakosa. Kenya imeuzwa wakati tz ni mali ya watanzania. Wakenya wanahangaika huku na huko wakitafuta maisha waliyoporwa na wazungu na mabwanyenye weusi wakenya wenzao. Kila unachokiona Kenya sio cha wakenya.
 
Je wewe umejitengeneza kuwa kiongozi Bora WA familia yako?
 
Leta video au picha moja ya maiti ya mkenya iliyorudishwa Kenya baada ya kuuwawa Tanzania October 29.

Na hao "Mungiki" unaowaosema pengine uliwaunda wewe muda wanaingia maafisa wa uhamiaji wa Tanzania walikuwa wapi?
 
Kaka mm niko vizuri sana kwenye upande huo. Kiongozi bora ni yule ambae ni kiongozi wa yeye mwenyewe, familia, ukoo na jamii inayomzunguuka kabla ya kuwa kiongozi wa umma.
 
Leta video au picha moja ya maiti ya mkenya iliyorudishwa Kenya baada ya kuuwawa Tanzania October 29.

Na hao "Mungiki" unaowaosema pengine uliwaunda wewe muda wanaingia maafisa wa uhamiaji wa Tanzania walikuwa wapi?
Yaani kwa idadi ya watu waliouliwa inayotangwa na chadema kama ingekuwa ya kweli basi tungeona matulubai mengi nchi nzima ya misiba ya watu hao waliouliwa, maana nyumba yenye msiba haijifichi bana.

Hapa mtaani kwetu aliuliwa kijana mmoja na polisi ambae alikuwa haandamani, lakini kosa lake lilikuwa kuwazomea askari wa doria wakati wakipita mitaani kwetu. Kijana yule aligoma kutii amri ya kukaa ndani badala yake alikuwa akiwachungulia kwenye kona ya ukuta wa nyumba. Nadhani walikuwa wanadhani kuwa alikuwa anawalenga ndipo wakamuwahi yeye. Ukiambiwa usitoke nje wanamaanisha usitoke nje kweli.
 
Leta picha au video moja ya maiti ya mkenya acha stori nyingi.

Habari ya kusema CHADEMA wametangaza misiba mimi nimezungumzia wapi?

Mimi nimesema wewe ndio uweke hapa picha , video au link ya msiba wa mkenya aliyeuwawa kwenye maandamano .

Haukuona maturubai mengi sababu maiti zilichukuliwa na kufukiwa Kondo kwenye kaburi la halaiki.

Kwahiyo huyo kijana ni "Mungiki"?

Kwahiyo askari wa Tanzania walifundishwa mtu akiwazomea wanatakiwa kumpiga risasi?

Hivi wewe unaelewa hata chimbuko la Mungiki ???
 
Mbona Magufuli alishamfukuza uwaziri baadae akamchagua tena
Hujiulizi kwanini amlimchagua tena? Kwasasa CCM hakuna mtu kama Mwigulu.

Sisi tunaozulula sana kwenye mabara mengine tunaona namna wenzetu walioendelea walivyokuwa mstari wa mbele katika kulipa na kukusanya kodi; hawana mchezo na ulipaji kodi. Mwigulu ameifanya nchi ikusanye na kulipa kodi kikamilifu; hasa kupitia matumizi ya simu za mkononi, mafuta na umeme. Kupitia matumizi ya umeme, mafuta na simu kila mtu analipa kodi, yaani amepanunia wigo wa kulipa kodi. Kutengeneza mifumo ya ki-electronic ya kufanya malipo imesaidia ulipaji kodi kwa njia rahisi na kudhibiti mapato pia. Serikali chini ya mwigulu inatamba kujenga miradi mikubwamikubwa na kugharamia uchaguzi kwa fedha zetu wenyewe.

Mwigulu anaoenekana very simple lakini yuko complex na strong kwelikweli. Hata uwekezaji kwenye bandari tunaotamba nao kutuingizia fedha nyingi ni matokeo ya kazi yake ya kuchora ramani ya kiuchumi.

Ndugu zangu Mwigulu ni assets hata kama kuna wanaombeza kwa muonekano wake wa nje. Hakuna maisha bila kulipa kodi, hii ni dunia nzima. Viongozi wakatoliki wana tabia moja mbaya sana ya kuendekeza misamaha ya kodi; uchochoro ambao umekuwa ukilipotezea fedha nyingi taifa. Na misamaha mingi inanufaisha taasisi za dini zinazofanya biashara kwa mlango wa nyuma. Mfano, Utakuta shule ya dini inapewa msamaha wa kodi kwenye ujenzi, vifaa na uendeshaji lakini shule hiyohiyo iliyosamehewa kodi inatoza ada ya TSH 7m kwa mwaka kwa mwanafunzi. Hospitali inasamehewa kodi na inapewa ruzuku lakini inatoza Tsh. 500,000 kwa mama mjamzito kujifungua kawaida tu. Wanadhani watanzania ni wajinga au wamelala fofofo.
 
Leta picha au video moja ya maiti ya mkenya acha stori nyingi.

Habari ya kusema CHADEMA wametangaza misiba mimi nimezungumzia wapi?

Mimi nimesema wewe ndio uweke hapa picha , video au link ya msiba wa mkenya aliyeuwawa kwenye maandamano .

Haukuona maturubai mengi sababu maiti zilichukuliwa na kufukiwa Kondo kwenye kaburi la halaiki.

Kwahiyo huyo kijana ni "Mungiki"?

Kwahiyo askari wa Tanzania walifundishwa mtu akiwazomea wanatakiwa kumpiga risasi?

Hivi wewe unaelewa hata chimbuko la Mungiki ???
Unapoambia baki ndani maana yake tii sheria kwanza ya kukaa ndani. Kukaa ndani kunatenganisha kati ya raia wema na mungiki (wavimbamacho), na hii ni duniani kote iko hivyo. Kujificha kwenye viwambaza vya nyumba kunahesabiwa kwamba unajaribu kulenga shabaha askari ili kuwadhulu. Kule jeshini siku zote unafundishwa kumuwahi adui kabla adui hajakuwahi wewe. Kulizomea jeshi ni jitihada za kulidogosha, kulibagaza na kulifanya lisiheshimike. Lakini namkwambia baada ya yule kijana kula za kichwa hakukuwa na kijna hata mmoja aliyetoka nje tena mtaani pale kwa sababu yoyote ile. Yaani kuna watu ambao hadi waone ndio waamini.
 
Hatutaki CCM mbona hamtuelewi Yani hata mumuandae malaika
Yaani chama chenye viongozi ambao wanashindwa kutofautisha kati ya mali ya Samia na mali ya umma ya watanzania wote kinastahili kukabidhiwa nchi?. Hebu usilete utani wako. Viongozi wa kile chama walijua 100% kuwa mpango wao utakwenda kusababisha vifo vya watu wengi sana, lakini hawakujali hilo. Bahati mbaya zaidi wao walihakikisha kuwa wao wenyewe na familia zao wako sehemu salama kabisa wakati wengine unaumizwa na kuuliwa. Utahitaji watu kama hao waende Ikulu kutuongoza?

Acha porojo kaka. Kule Kenya hata leo hii watu wanafukuliwa kwenye makabuli ya halaiki pamoja na kujidai wana katiba mpya na nzuri na haki na demokrasia. Tuache upumbavu

View: https://youtu.be/bO9dLbFHRmw?si=3QnxvVVZi7TUPY_N
 
Unapoambia baki ndani maana yake tii sheria kwanza ya kukaa ndani. Kukaa ndani kunatenganisha kati ya raia wema na mungiki (wavimbamacho), na hii ni duniani kote iko hivyo
Hujajibu swali, huyo aliyezomea polisi na kupigwa risasi ni. "MUNGIKI"?

Saa hizi umebadili tena tafsiri ya :MUNGIKI" unawaita wavimba macho , je unajua chimbuko la Mungiki?
. Kujificha kwenye viwambaza vya nyumba kunahesabiwa kwamba unajaribu kulenga shabaha askari ili kuwadhulu. Kule jeshini siku zote unafundishwa kumuwahi adui kabla adui hajakuwahi wewe. Kulizomea jeshi ni jitihada za kulidogosha, kulibagaza na kulifanya lisiheshimike.
Kwahiyo polisi waliua MUNGIKI wangapi , na maiti zao zilizikwa Kenya county gani?
Lakini namkwambia baada ya yule kijana kula za kichwa hakukuwa na kijna hata mmoja aliyetoka nje tena mtaani pale kwa sababu yoyote ile. Yaani kuna watu ambao hadi waone ndio waamini.
Mbona hujibu swali unanitolea mfano wa "yule kijana" huyo kijana ni MUNGIKI kutoka koo ipi , ya Kamau , Njoroge ,Kariuki, Mwangi Kimani , Maina, Muriuki au ni ipi?
 
Hujajibu swali, huyo aliyezomea polisi na kupigwa risasi ni. "MUNGIKI"?

Saa hizi umebadili tena tafsiri ya :MUNGIKI" unawaita wavimba macho , je unajua chimbuko la Mungiki?

Kwahiyo polisi waliua MUNGIKI wangapi , na maiti zao zilizikwa Kenya county gani?

Mbona hujibu swali unanitolea mfano wa "yule kijana" huyo kijana ni MUNGIKI kutoka koo ipi , ya Kamau , Njoroge ,Kariuki, Mwangi Kimani , Maina, Muriuki au ni ipi?
Huyu alikuwa mmatumbi tu wa hapahapa, kaja mjini kutoka kijijini kwao baada ya kumalisha shule. Alidhani mjini kuna nafuu kumbe sio kabisa. Aliishia kufungua "studio" ya kuingiza nyimbo kwenye simu na kuuza CD. Ni miongoni mwa vijana wetu wanaodhani hali yake mbaya kiuchumi inaweza kwisha kama Lissu na Heche wataingia Ikulu kwa kuondosha CCM. Mungiki wengi walifia kwenye maeneo ya matukio walikoelekezwa kwenda kuchoma moto na kuvamia. Alikufa nilisikitika pia kwakuwa nilimuona kwa macho, lakini kwa upande mwingine ilisaidia sana wazazi kuwa wakali sana kwa vijana wao waliotaka kufanya kama alivyofanya yule kijana na wenzake. Actually, yule kijana hakuwa peke yake kule nje ila wenzake walikimbia sana baada polisi kupiga risasi hewani ya kuwatawanya. Kijana alijifanya shujaa haogopi polisi. Unajua tena kwa shujaa ni vilio tu siku zote.

Unajua bwana wazazi tuwe karibu sana na watoto wetu ili wawe salama kama vile wanavyofanya akina Lissu, Lema, Mnyika, Heche na wengine walivyowapeleka watoto wao sehemu salama nje ya nchi. Wewe utakuwa mzazi mpumbavu kuacha watoto wako wauliwe wakati Lissu, Heche, Lema watoto wao wanawalinda wasife kipumbavu.
 
Yaani chama chenye viongozi ambao wanashindwa kutofautisha kati ya mali ya Samia na mali ya umma ya watanzania wote kinastahili kukabidhiwa nchi?. Hebu usilete utani wako. Viongozi wa kile chama walijua 100% kuwa mpango wao utakwenda kusababisha vifo vya watu wengi sana, lakini hawakujali hilo. Bahati mbaya zaidi wao walihakikisha kuwa wao wenyewe na familia zao wako sehemu salama kabisa wakati wengine unaumizwa na kuuliwa. Utahitaji watu kama hao waende Ikulu kutuongoza?

Acha porojo kaka. Kule Kenya hata leo hii watu wanafukuliwa kwenye makabuli ya halaiki pamoja na kujidai wana katiba mpya na nzuri na haki na demokrasia. Tuache upumbavu

View: https://youtu.be/bO9dLbFHRmw?si=3QnxvVVZi7TUPY_N

Kheri ww uliyempumbavu
 
Hujajibu swali, huyo aliyezomea polisi na kupigwa risasi ni. "MUNGIKI"?

Saa hizi umebadili tena tafsiri ya :MUNGIKI" unawaita wavimba macho , je unajua chimbuko la Mungiki?

Kwahiyo polisi waliua MUNGIKI wangapi , na maiti zao zilizikwa Kenya county gani?

Mbona hujibu swali unanitolea mfano wa "yule kijana" huyo kijana ni MUNGIKI kutoka koo ipi , ya Kamau , Njoroge ,Kariuki, Mwangi Kimani , Maina, Muriuki au ni ipi?
Mungiki wengi kazi yao ilikuwa kuwachonganisha vijana wetu wazembe na serikali yao ili wauliwe. Kulikuwa na idadi fulani ya watu waliotakiwa kufa ili malengo ya maandamano yaweze kufikiwa kwa bahati mbaya idadi hiyo haikufikiwa (miscalculation). Kuna watu waliuliwa na waandamaji, kuna waliouliwa na vyombo tiifu vya usalama, na kuna watu walitakiwa kufa kwa mapigano ya kulipiziana visasi kati ya wanaCCM na wanaChadema. Lengo lao halisi lilikuwa kufikia idadi inayokidhi kuitwa kimbari; ili ICC na wadau wao wengine waweze kutumia idadi hiyo kuchukua hatua dhidi ya serikali na viongozi wake. Ndiyo maana baada ya tukio lile wavimbamacho walikuwa bize kutaka kujua idadi ya waliokufa na wakati mwingine walitaja idadi kubwa ya uongo ili kufikia idadi inayohitajika na ICC na wadau wao wengine.

Mpango huo umefeli kabiiiisaaaa, kwakuwa wananchi waliochomewa mali zao, kuumizwa na kuuliwa hawakulipiza kisasi kwa yoyote zaidi ya kuwalaani chadema. Akili zao zilitarajia kuwa kama wakichoma ofisi za CCM na wanaCCM wangechoma ofisi za chadema. Lakini haikwenda hivyo, zoezi likaishia hapo.
 
Hujiulizi kwanini amlimchagua tena? Kwasasa CCM hakuna mtu kama Mwigulu.

Sisi tunaozulula sana kwenye mabara mengine tunaona namna wenzetu walioendelea walivyokuwa mstari wa mbele katika kulipa na kukusanya kodi; hawana mchezo na ulipaji kodi. Mwigulu ameifanya nchi ikusanye na kulipa kodi kikamilifu; hasa kupitia matumizi ya simu za mkononi, mafuta na umeme. Kupitia matumizi ya umeme, mafuta na simu kila mtu analipa kodi, yaani amepanunia wigo wa kulipa kodi. Kutengeneza mifumo ya ki-electronic ya kufanya malipo imesaidia ulipaji kodi kwa njia rahisi na kudhibiti mapato pia. Serikali chini ya mwigulu inatamba kujenga miradi mikubwamikubwa na kugharamia uchaguzi kwa fedha zetu wenyewe.

Mwigulu anaoenekana very simple lakini yuko complex na strong kwelikweli. Hata uwekezaji kwenye bandari tunaotamba nao kutuingizia fedha nyingi ni matokeo ya kazi yake ya kuchora ramani ya kiuchumi.

Ndugu zangu Mwigulu ni assets hata kama kuna wanaombeza kwa muonekano wake wa nje. Hakuna maisha bila kulipa kodi, hii ni dunia nzima. Viongozi wakatoliki wana tabia moja mbaya sana ya kuendekeza misamaha ya kodi; uchochoro ambao umekuwa ukilipotezea fedha nyingi taifa. Na misamaha mingi inanufaisha taasisi za dini zinazofanya biashara kwa mlango wa nyuma. Mfano, Utakuta shule ya dini inapewa msamaha wa kodi kwenye ujenzi, vifaa na uendeshaji lakini shule hiyohiyo iliyosamehewa kodi inatoza ada ya TSH 7m kwa mwaka kwa mwanafunzi. Hospitali inasamehewa kodi na inapewa ruzuku lakini inatoza Tsh. 500,000 kwa mama mjamzito kujifungua kawaida tu. Wanadhani watanzania ni wajinga au wamelala fofofo.
Mwigulu hana lolote wadanganye ambao hawaishi Tanzania

Deni la Taifa linapaa kila uchwao alafu unasema tunakusanya sana hayo makusanyo yanafaida gani ilihali deni kila siku linapaa
 
Mungiki wengi kazi yao ilikuwa kuwachonganisha vijana wetu wazembe na serikali yao ili wauliwe.
Nitajie jina la kiongozi aliyeongoza hicho kikundi cha uchonganishi.
Kulikuwa na idadi fulani ya watu waliotakiwa kufa ili malengo ya maandamano yaweze kufikiwa kwa bahati mbaya idadi hiyo haikufikiwa (miscalculation).
Hizi data umetoa wapi?

Nipe hiyo idadi iliyokusudiwa na pia watu wangapi waliandamana hadi kutofikia hiyo idadi
Kuna watu waliuliwa na waandamaji, kuna waliouliwa na vyombo tiifu vya usalama, na kuna watu walitakiwa kufa kwa mapigano ya kulipiziana visasi kati ya wanaCCM na wanaChadema.
Naomba idadi ya wanachadema waliouwawa kwenye maandamano.

Naomba pia idadi ya MUNGIKI waliouwawa kwenye maandamano.

Zezeta unatangatanga tu , ulianza walioandamana ni Mungiki saa hizi umehama tena unasema walioandamana ni CHADEMA kulipa visasi kwa CCM.
Lengo lao halisi lilikuwa kufikia idadi inayokidhi kuitwa kimbari; ili ICC na wadau wao wengine waweze kutumia idadi hiyo kuchukua hatua dhidi ya serikali na viongozi wake. Ndiyo maana baada ya tukio lile wavimbamacho walikuwa bize kutaka kujua idadi ya waliokufa na wakati mwingine walitaja idadi kubwa ya uongo ili kufikia idadi inayohitajika na ICC na wadau wao wengine.
Hiyo idadi ya kufikiwa kwa mauaji ya kimbari ni ipi?

Huna habari hadi leo tunaenda mwezi wa 5 policcm hawajatoa idadi ya waliouwawa wala majeruhi?

Unafikiri kwanini hawataki kutoa?
Mpango huo umefeli kabiiiisaaaa, kwakuwa wananchi waliochomewa mali zao, kuumizwa na kuuliwa hawakulipiza kisasi kwa yoyote zaidi ya kuwalaani chadema.
Wewe zezeta mbona hujibu maswali yangu unaongea vitu ambavyo sijakuuliza ?

Maswali yangu ni hebu nitajie idadi ya Mungiki walioingia Tanzania.

Idadi ya Mungiki waliouwawa na kukadhibiwa miili yao wizara ya mambo ya nje ya Kenya.

Hayo maswali kwako ni magumu kuyajibu au?
Akili zao zilitarajia kuwa kama wakichoma ofisi za CCM na wanaCCM wangechoma ofisi za chadema. Lakini haikwenda hivyo, zoezi likaishia hapo.
Kwahiyo sio Mungiki tena ndio waliochoma ofisi za CCM bali ni CHADEMA?

Hebu nipe idadi ya wanachadema waliohusika kuchoma ofisi.

Na leta idadi ya Mungiki waliochoma ofisi.

Ukishindwa hapa sina muda wa kuendelea na mjadala na wewe.
 
Back
Top Bottom