GE2025 Tumshukuru Samia kwa kutuvusha mpaka hapa, lakini tumwambie ukweli: Viatu havimtoshi

GE2025 Tumshukuru Samia kwa kutuvusha mpaka hapa, lakini tumwambie ukweli: Viatu havimtoshi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Agent-47

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
783
Reaction score
2,780
Kwa ustaarabu kabisa, tunamshukuru mama kutufikisha hapa baada ya taifa kupata msiba na mripuko wa gonjwa la COVID19. Tunamshukuru, pamoja na kuwa uongozi wake umegubikwa na kashfa nyingi za rushwa na ukiukwaji mkubwa wa haki z binadamu. Tunamshukuru, amefanya alivoweza na miaka hii minne imekuwa kipimo kizuri sana kama anafaa.

Ukweli na usemwe, mama hana uwezo (achilia mbali mambo ya rushwa na utekaji). She is utterly inept. Na tunaposema hatoshi hatusemi hivo kwa chuki wala ushabiki. Ni kwa roho safi kabisa ya kuwa tunahitaji kiongozi mpya anayeweza kutupush kwenda mbele.

Dunia ya sasa inakimbilia kwenye technlogy, ukiona mataifa yanavogombania uzalishaji wa chips kwa ajili ya kutengeneza AI data centers, clean energy, personalized medicine na mambo kibao. Siye bado tuna angaika na visima na street lights.

Leo nipo hapa Taiwan, hawa jamaa wameanza kutengeneza one of the largest data centers ambazo zitakuwa zina serve Dunia katika Ulimwengu wa AI. Inafurahisha sana kuona mambo kama haya yanafanywa na mataifa madogo-kumaanisha ya kwamba wakiwepo viongozi makini mambo yanawezekana.

Mama pumzika, unazo pesa za kula hata kama utaishi miaka mingine 200. Liachie taifa lipate akili mpya.
 
Hata akiingia ajaye,nothing will change.
Tanzania na Afrika inahitaji viongozi aina ya Nyerere,Gadaf, Gamal,Sankara,Nkurumah,Goita, & Traore na bahati mbaya wakitokea western countries wana waua.
Inahitaji zaidi ya ujasiri Africa kuondokana na huu mkwamo.
 
Hata akiingia ajaye,nothing will change.
Tanzania na Afrika inahitaji viongozi aina ya Nyerere,Gadafuli, Gamal,Sankara,Nkurumah,Goita, & Traore na bahati mbaya wakitokea western countries wana waua.
Inahitaji zaidi ya ujasiri Africa kuondokana na huu mkwamo.
Sijaelewa mkuu. Pendekezo lako ni kuwa abaki tu hatuna jinsi nyingine?

Hata katika matunda, yapo yanayokuwa yameoza zaidi ya mengine. Ukitaka kutengeneza juisi si unayaondoa yaliyooza sana na kubaki na yenye unafuu?
 
Ukweli na usemwe, mama hana uwezo (achilia mbali mambo ya rushwa na utekaji). She is utterly inept. Na tunaposema hatoshi hatusemi hivo kwa chuki wala ushabiki. Ni kwa roho safi kabisa ya kuwa tunahitaji kiongozi mpya anayeweza kutupush kwenda mbele.

Mama pumzika, unazo pesa za kula hata kama utaishi miaka mingine 200. Liachie taifa lipate akili mpya.
Kila zama na zama zake, kila awamu na kitabu chake, na kila rais na kiatu chake, kumfitisha rais Samia kiatu cha Magufuli ni kumuonea bure! JK ni JK, JPM ni JPM na Samia ni Samia, tusiwalinganishe!.

Post in thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

The time ya kutekeleza haya, it's too little too late, October 29 ndio hiyo imefika, sasa kazi ni moja tuu, kutiki!.
P
 
Kila zama na zama zake, kila awamu na kitabu chake, na kila rais na kiatu chake, kumfitisha rais Samia kiatu cha Magufuli ni kumuonea bure! Post in thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

The time ya kutekeleza haya, it's too little too late, October 29 ndio hiyo imefika, sasa ni kazi moja tuu, kutiki
P

Sasa hapa ndugu Pascal Sijui umeandika nini. Kusema Samia ni mpango wa Mungu ni kukosa hoja za kwanini anafaha. Kuwa objective kidogo, inasaidia.

Kuwa raisi si kwamba unakuja na sifa (kiatu) zako. Sifa na matakwa ya kiongozi bora wa kushika nafasi hii nyeti ziko wazi (hiko ndo kiatu). Na kwa bahati mbaya sana, Samia hana sifa za kuwa kiongozi wa taasis hii nyeti. Ndiyo maana ya kiatu hakitoshi. Wala kusema hivo si kwamba tunamringanisha na watangulizi. Sifa zake zinapelea.
 
Mtaimba sana mitandaoni lakini ukweli wabongo ni mafisi, waoga zaidi ya kuku...
Na 29, hatutaona yoyote mtaani., huu ndio ukweli uaminifu.....
Maoni yangu ni Reverse Psychology.... lakini ndio ukweli wenyewe...
Sasa wewe akili yako ipo kwenye maandamano. Upo fixated huko japo hautatoka 😆

Mimi hapa nimeleta hoja ya Samia kama anafaa kuwa raisi au hafai. Sijaongelea maandamano hata kidogo. Kama unaona anafaa sema kwanini siyo kulalamika.
 
Tukikupa viatu vyake vitakutosha ?
1760750541470.png
 
Kila zama na zama zake, kila awamu na kitabu chake, na kila rais na kiatu chake, kumfitisha rais Samia kiatu cha Magufuli ni kumuonea bure! Post in thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

The time ya kutekeleza haya, it's too little too late, October 29 ndio hiyo imefika, sasa ni kazi moja tuu, kutiki
P
Mayalla unajidhalilisha aisee, ulijijengea heshima kubwa umu kwenye forum, lakini unaibomoa, ni wazi sasa umekuwa chawa wa serikali ya Samia, kila kitu umeegemea upande mmoja, hutoi mawazo huru, ni kutetea tu.
 
Kila zama na zama zake, kila awamu na kitabu chake, na kila rais na kiatu chake, kumfitisha rais Samia kiatu cha Magufuli ni kumuonea bure! Post in thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

The time ya kutekeleza haya, it's too little too late, October 29 ndio hiyo imefika, sasa ni kazi moja tuu, kutiki
P
Anko Magu alishamjambisha kidogo tu, sasa hivi amekuwa joga vibaya sana. Kaamua kuwa chawa mwandamizi ili abaki salama , watanzania ni wasaliti wapiga kelele kwenye keyboard ila ground utakuwa mwenyewe.
 
Sasa hapa ndugu Pascal Sijui umeandika nini. Kusema Samia ni mpango wa Mungu ni kukosa hoja za kwanini anafaha.
Mungu ndiye huweka tawala zote za mataifa, ni Mungu alimleta JPM akamtwa akamleta Samia, hivyo ni mpango wa Mungu, kwa nini anafaa au hafai sii kazi yetu ni kazi ya Mungu mwenyewe ila ameweza mengi tuu.
Kuwa objective kidogo, inasaidia.

Kuwa raisi si kwamba unakuja na sifa (kiatu) zako. Sifa na matakwa ya kiongozi bora wa kushika nafasi hii nyeti ziko wazi (hiko ndo kiatu). Na kwa bahati mbaya sana, Samia hana sifa za kuwa kiongozi wa taasis hii nyeti. Ndiyo maana ya kiatu hakitoshi. Wala kusema hivo si kwamba tunamringanisha na watangulizi. Sifa zake zinapelea.
Huo ni mtazamo wako na tuna uheshimu ila nasi tuna mtazamo yetu kuwa she is the best ,uheshimu

Kwanza anza kuangalia ni lini watu walianza kumspot Mama Samia, mimi nilimspot 2010 New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!.
Wanabodi,
Bado niko hapa mjini Dodoma, nikijivinjari katika viwanja vya Bunge kwa haya na yale.

Japo mpaka sasa kitendawili cha Waziri Mkuu bado hakijatenguliwa, nimeonelea niwatajie baadhi ya majina mapya kwenye new cabinet.

2. Mwingine ni Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, sasa ameingia Bunge la JMT, atapewa important portfolio kumuandaa ama kuwa rais wa Zanzibar kisha kuja bara, au kuwa VP 2015.
Pasco
Bandiko hili ni la 2010, angalia hiyo 2010 tulisema nini kumhusu Samia, na nini kilikuja kutokea... mkiambiwa baadhi ya kauli zinaumba, mjue ni kweli kauli huumba!.

Kisha 2015 Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Kauli Umba ya kuunda VP mwananke kwa Tanzania
Kufuatia kilio cha muda mrefu cha wanawake kunyimwa fursa, je ni kweli tunao wanawake wenye sifa na uwezo wa kutupeleka kwenye 50/50?. Hebu na tuanzie na wanawake wenye sifa za urais, je tunao?

Hebu tuwakumbuke the top ten female politicians in Tanzania, na nafasi wanazoshika! Je, wamefikaje hapo, kwa kupanda wenyewe, au wamebebwa ndipo wakafika hapo? Je, wana sifa za urais?
  1. Top No.1 ni Mhe. Samia Suluhu Hassan.
    Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
    Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, ameingia Bunge la JMT for 5 years sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais. Ndiye alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Huyu ni presidential material, sasa ni kumuandaa kwanza kuwa rais wa Zanzibar kwa kumpumzisha Dr. Shein kipindi chake cha pili, kisha 2020 aje urais wa Muungano, ili hili ifanyike, itabidi, CCM iachane na ule utaratibu wake wa two terms za urais, kwasababu kusubiria 2025, kwa huyu mama itakuwa too little too late, age itakuwa imemtupa mkono.
Natoa wito kwa wanawake, kama ni kweli mna uwezo, jitokezeni kwenye urais, ili hata msiposimamishwa, angalau 2015, tuwe na makamo rais mwanamke, au Waziri Mkuu Mwanamke!

Paskali.
Tanzania ilipata VP, mwanamke kwa mara ya kwanza, baada ya uchaguzi wa 2015, kuna wengi wanadhani ilijitokea tuu, Tanzania kuwa na VP mwanamke!, hawajui kuwa huo u VP wa mwanamke, kuna watu wenye kauli zenye powers za kuumba, walitoa kauli za kutaka tupate VP mwanamke, toka Machi 8, 2015!.

Then Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa.

She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.

Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.

Paskali
Hii ni kauli umba ya kumuumbia mtu urais wa JMT.

na hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Angalia kwa makini hii kauli umba hapa iliumba nini?
Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.
Hoja za uwezo wa Samia kama ana uwezo wa urais na viatu vinamfiti au laa, nitakupitisha huko huko ili kama ni kupangua hoja upangulie kule.

P
 
Sijaelewa mkuu. Pendekezo lako ni kuwa abaki tu hatuna jinsi nyingine?

Hata katika matunda, yapo yanayokuwa yameoza zaidi ya mengine. Ukitaka kutengeneza juisi si unayaondoa yaliyooza sana na kubaki na yenye unafuu?
Historia hatujawahi kufurahia tulichonacho, alipoondoka Mwinyi kuja Mkapa watu walisema maisha magumu na Mkapa bora mzee ruksa, akaja Kikwete wakaja tena hapana bora Mkapa wizi umezidi, akaja JPM akatukanwa bora Kikwete na kaja Mama Samia anatukanwa bora JPM. Hakuna Raisi aliye madarakani asitukanwe. JPM alitukanwa sana akawa akitokea Kikwete tu sehemu anashangaliwa kama malaika katokea mpaka bungeni. Hata mimi nieowa mke mpya lakini hivi sasa vituko vya mke huyu naona mke mkubwa malaika....LOL

Anyway point yangu issue sio mtu ni mfumo wetu ni mbaya hatuna kama Taifa vision tunataka nini.
 
Hata akiingia ajaye,nothing will change.
Tanzania na Afrika inahitaji viongozi aina ya Nyerere,Gadaf, Gamal,Sankara,Nkurumah,Goita, & Traore na bahati mbaya wakitokea western countries wana waua.
Inahitaji zaidi ya ujasiri Africa kuondokana na huu mkwamo.
Tanzania inahitaji mabadiliko ya kimfumo si mtu, mifumo iko so weak kiasi kwamba inaendana na vibe la kiongoz anaekuwepo wakati huo na si kufuata misingi na sheria za nchi
 
Kila zama na zama zake, kila awamu na kitabu chake, na kila rais na kiatu chake, kumfitisha rais Samia kiatu cha Magufuli ni kumuonea bure! JK ni JK, JPM ni JPM na Samia ni Samia, tusiwalinganishe!.

Post in thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

The time ya kutekeleza haya, it's too little too late, October 29 ndio hiyo imefika, sasa ni kazi moja tuu, kutiki
P
Kwa hiyo wagombea wengine wa viti vya uraisi ni mpango wa shetani? Mbona hujasema kuhusu Salim Mwalimu n.k.
 
Hivi mkuu ww unaamini Mama Samia akiondoka kwenye hicho kiti huyo atakayekuja ndiyo atakuwa na hizo vision kubwa za kuestablish hizo AI Data centers.

Kwanza Africa hayo mambo siyo priority, na ukitaka kuprove Hilo pitia ilani za vyama vya siasa ndiyo utaelewa kuwa hii Africa bado sana.

Na kwa bahati mbaya watu wenye Maoni kama hayo ya kuifanya Africa iweze kuadvance katika hizo level , wanapigwa Vita.

COSTECH inapromote creativity, TCRA inakuja kuua creatity kupitia kivuli Cha regulations.

THISI IS AFRICA.
 
Back
Top Bottom