New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,816
2,000
Wanabodi,
Bado niko hapa mjini Dodoma, nikijivinjari katika viwanja vya Bunge kwa haya na yale.

Japo mpaka sasa kitendawili cha Waziri Mkuu bado hakijatenguliwa, nimeonelea niwatajie baadhi ya majina mapya kwenye new cabinet.

1. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka.
Huyu ndie mbunge mwenye highest profile. Asipokuwa PM then atapewa foreign. Sababu pekee ya kumrudisha Pinda inaweza kuwa ni ile ile iliyomrudisha Sumaye, cost implication na sio performance.

2. Mwingine ni Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, sasa ameingia Bunge la JMT, atapewa important portfolio kumuandaa ama kuwa rais wa Zanzibar kisha kuja bara, au kuwa VP 2015.

List inaendelea, unaweza kuongeza listi kwa mtazamo wako ila lazima utoe sababu sio kutaja taja tuu majina.
Pasco
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,733
2,000
January Makamba kwa kazi nzuri ya kumlinda Kikwete inayofanywa na baba yake-fadhila!!

Nchimbi, Ni prote'ge mkubwa wa Kikwete tangu uchaguzi wa 2005, alikuwa naibu sasa atampa wizara kamili.

Ghasia na Mwantumu Mahiza, hawa ni maswahiba wa Salma Kikwete na Jakaya hawezi kupuuza ushauri wake kama alivyoonyesha kumshukuru kwa kumsaidia kampeni; mmoja atapata uwaziri na mwingine kuteuliwa ubunge na unaibu!!

Ngeleja ataendelea kwa kuwa kibaraka wa Rostam ; ataendelea kutumiwa kubaka uchumi wetu kama alivyofanya kipindi kilichopita.
 
Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,697
1,250
Pasco, u already know that there are lot of allegations that Mafisadi they are behind restoration of this government right from Election Process and now Speaker. Anna may not know, but that is a fact behind the scene.

That being the case people like Masha; Batilda; January will come back.

Of highest interest ni kuona Lowassa atapewa nini? Kama kweli anayo dream ya kugombea 2015, lazima atafute the stepping stone. JK cannot say no to what EL wants. That we know 100%.
 
smwansasu

Member
Aug 19, 2009
14
0
What matters to me is the size of the cabinet. An overbloated cabinet is very expensive. We do need some experienced people among them but not an enviromentally friendly cabinet with a lot of recycled ministers from Nyerere/Mwinyi era. Wape vijana wachache wachape kazi
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,816
2,000
Mwingine ni Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
 
Kidogo chetu

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,432
2,000
Engineer Christopher chiza anaweza kurudiswa kama uwiano wa mikoa utazingatiwa hasa kigoma ambako NCCR Wametawala
Prof mwandosya
John magufuli kwa uchapaji kazi uliotukuka
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,816
2,000
Kuna vichwa vingine viwili navyo ni Gregory Teu, Mbunge wa Kongwa, huyu alikuwa naibu wa CAG, Ludovick Utouh, kutokana na kazi nzuri ya CAG, huyu jamaa atapewa deputy wa MoF.
 
DoubleOSeven

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
661
0
Pasco, u already know that there are lot of allegations that Mafisadi they are behind restoration of this government right from Election Process and now Speaker. Anna may not know, but that is a fact behind the scene.

That being the case people like Masha; Batilda; January will come back.

Of highest interest ni kuona Lowassa atapewa nini? Kama kweli anayo dream ya kugombea 2015, lazima atafute the stepping stone. JK cannot say no to what EL wants. That we know 100%.

............. RA wants EL for Primiership. As of the day b4 yesterday, Mr Six refused to be deputy PM under EL!!!
By the way, members, did Anna Makinda just ... and I mean just... woke up n decided to give speakership a shot??? nay, nay nay!! Three fisadis, RA, EL and that TICTS guy are very well entrenched in the process. the lady happens to be developing a real estate somewhere, that thing we call apartments, and as already alleged, she is in debt. Guess who came in dangling that carrot to rid of her financial burden??? Need I name. No and didnt think so. Whereas the lady had no intention to vie for that office at the beginning, she did a turncoat, went on to challenge Mr Six! her apartments would be completed minus a nagging bank loan, huge one at that.

EL, RA, That TICTS fella, et al are having quite a laugh!
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Wanabodi,
Bado niko hapa mjini Dodoma, nikijivinjari katika viwanja vya Bunge kwa haya na yale.

Japo mpaka sasa kitendawili cha Waziri Mkuu bado hakijatenguliwa, nimeonelea niwatajie baadhi ya majina mapya kwenye new cabinet.

1. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka.
Huyu ndie mbunge mwenye highest profile. Asipokuwa
PM then atapewa foreign. Sababu pekee ya kumrudisha
Pinda inaweza kuwa ni ile ile iliyomrudisha Sumaye,
cost implication na sio performance.

list inaendelea, unaweza kuongeza listi kwa mtazamo wako ila lazima utoe sababu sio kutaja taja tuu majina.

Mark James Mwandosya, huyu bwana ni msomi mwelewa, na siyo fisadi.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,816
2,000
samweli sitta,lazima apoozwe kwa hila za kumtosa kwenye uspika,likely akapewa wizara ya ulinzi,baada ya masha kuangukia pua
Elinasi, kama Sitta amechinjiwa baharini kwenye uspika kwa tuhuma an sababu zozote na ile statement ya upendeleo kwa wanawake ni kisingizio tuu, basi Sitta hapewi chochote, atabakia Mbunge tuu.
 
Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,452
2,000
Mizengo Pinda:pM

J.P.Magufuli:
Atapewa Mambo ya ndani iliyokuwa ya Masha.

Aggrey Mwanri:
Atapewa uwaziri kamili wa TAMISEMI

Kigwangala:
Naibu Afya

S.Sita :
Viwanda na biashara

Mama Tibaijuka:
Nyumba na makazi.

.
 
Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,237
1,500
Katika serikali ya CCM chochote chaweza kutokea. Baraza la mawaziri siyo chochote kwa sababu wanaoongoza nchi siyo hao. Wanaochaguliwa na kuteuliwa ni vivuli tu vya wanaoongoza nchi. Niwataje viongozi wachache kwa majina na kwenye mabano nimewaweka wale ambao ni vivuli:
1. Rais wa nchi:Rostam Aziz ( Jk)
2. Waziri Mkuu:Edward Lowasa(Pinda)
3. Spika: Andrew Chenge (Anne Makinda)
kwa uchache hao wawili wanatosha.

Nani asiyejua katika nchi hii kuwa Jk hawezi kusema kitu mbele ya Rostam na Lowasa? Ni nani asiyeweza kujua kuwa Andrew Chenge hakuwa na nia ya kugombea nafasi ya uspika bali lengo lake ni kumharibia Sitta ili wampenyeze mwakilishi wa mafisadi? Andrew aliwezaje kusafishwa na TAKUKURU wakati angombea uspika lakini Uingereza wanaendelea kumbana kwamba bado suala lake halijaisha? TAKUKURU ni chombo kilicho chini ya ofisi ya Rais kwa hiyo wanayoyatamka yana baraka zake na kwa hiyo ni uamuzi wa mafisadi. JK atajitenga vipi na mafisadi wake?

Kwa hiyo tusiwaze mno baraza la mawaziri la serikali ya CCM bali tutegemee ni mafisadi wepi wataingia, wana unafuu gani katika ufisadi au ni wawakilishi wepi wa mafisadi wataingia.
 
Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,697
1,250
............. RA wants EL for Primiership. As of the day b4 yesterday, Mr Six refused to be deputy PM under EL!!!
By the way, members, did Anna Makinda just ... and I mean just... woke up n decided to give speakership a shot??? nay, nay nay!! Three fisadis, RA, EL and that TICTS guy are very well entrenched in the process. the lady happens to be developing a real estate somewhere, that thing we call apartments, and as already alleged, she is in debt. Guess who came in dangling that carrot to rid of her financial burden??? Need I name. No and didnt think so. Whereas the lady had no intention to vie for that office at the beginning, she did a turncoat, went on to challenge Mr Six! her apartments would be completed minus a nagging bank loan, huge one at that.

EL, RA, That TICTS fella, et al are having quite a laugh!

Mkuu hizi ndo facts tunazitakaa.

TICTS fella is Nazir Karamagi right?

Tell us more about Anna Makinda estate projects, financing scandal and Loan issue and how the Fisadis were involved.

Kule Arusha I was there last week nilionyeshwa kijana moja wa karibu na vigogo wa CCM nyumba ambazo EL anamiliki ambazo alizininua AICC kwa njia za michoro . . . . Na sasa kazipangisha. Ni nyingi.
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,698
1,225
Mark James Mwandosya, huyu bwana ni msomi mwelewa, na siyo fisadi.

Ni kweli bwana mtoto wake alivyo-someshwa that time... yeye sio fisadi kwa sababu hayuko kwenye kambi ya JK... double standard.

Kuna watu wameitwa mafisadi bila kuwa na issue yoyote... hii ya Mark it was clear... lakini du! it depend unapendwa au hupendwi... ukipendwa lolote lile sawa.
 
DoubleOSeven

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
661
0
Katika serikali ya CCM chochote chaweza kutokea. Baraza la mawaziri siyo chochote kwa sababu wanaoongoza nchi siyo hao. Wanaochaguliwa na kuteuliwa ni vivuli tu vya wanaoongoza nchi. Niwataje viongozi wachache kwa majina na kwenye mabano nimewaweka wale ambao ni vivuli:
1. Rais wa nchi:Rostam Aziz ( Jk)
2. Waziri Mkuu:Edward Lowasa(Pinda)
3. Spika: Andrew Chenge (Anne Makinda)
kwa uchache hao wawili wanatosha.

Nani asiyejua katika nchi hii kuwa Jk hawezi kusema kitu mbele ya Rostam na Lowasa? Ni nani asiyeweza kujua kuwa Andrew Chenge hakuwa na nia ya kugombea nafasi ya uspika bali lengo lake ni kumharibia Sitta ili wampenyeze mwakilishi wa mafisadi? Andrew aliwezaje kusafishwa na TAKUKURU wakati angombea uspika lakini Uingereza wanaendelea kumbana kwamba bado suala lake halijaisha? TAKUKURU ni chombo kilicho chini ya ofisi ya Rais kwa hiyo wanayoyatamka yana baraka zake na kwa hiyo ni uamuzi wa mafisadi. JK atajitenga vipi na mafisadi wake?

Kwa hiyo tusiwaze mno baraza la mawaziri la serikali ya CCM bali tutegemee ni mafisadi wepi wataingia, wana unafuu gani katika ufisadi au ni wawakilishi wepi wa mafisadi wataingia.

... interesting. What about the proxy for Tanzania, meaning, Tanzania (RA).
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,816
2,000
Mark James Mwandosya, huyu bwana ni msomi mwelewa, na siyo fisadi.
Mungi, ni kweli Prof. Mwandosya na Magufuli ni wachapa kazi hodari. Kwa vile uchaguzi wa Makinda ndio turufu ya kwanza kuelekea 2015. Katika kuzichanga karata, Prof. Mwandosya na Magufuli, wanaweza kuonekana threat na kiwingu cha njia nyeupe kwa mgombea wa timu ya mafisadi.
 
Shomoro

Senior Member
Aug 22, 2010
111
195
Nahisi Prof P. Msolla atapewa ile wizara inayodili na kilimo na maswala ya mifugo. Jamaa ni product ya SUA hivyo ataendeleza ile dhana ya Kilimo Kwanza ya mheshimiwa rais.
Prof Tibaijuka ningependa apewe wizara inayohusiana na elimu ili aturudishie viwango kwenye elimu yetu.
Sitashangaa kama mtangazaji Juma Nkamia ataukwaa hata unaibu wa maswala ya michezo. Who knows bana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom