Tumshauri Dr. Joyce Ndalichako

Tumshauri Dr. Joyce Ndalichako

Ahakikishe hakuna muislam kufika form one wote waishie darasa la saba tu, wafanyakazi wa kiislam awapige chini wote waliokuwa wizara ya elimu, akiyafanya hayo ndani ya miaka miwili tu anakuwa mwenye heri! Najua hawezi kushindwa kama aliweza kufanya alichokifanya alivyokuwa katibu mkuu
Be serious sometimes! am bored stiff with your none sense comments herein.
 
kwa mfano kuna mwalimu kakaa muda mrefu kazini alikua na grade A akafikia mshahara mkubwa tuuu almost zaidi ya mshahara wa kima cha chini cha mwalimu mwenye degree baadae akaenda kujiendeleza na akapata degree ya elimu lakini aliporudi kazini wanamwambia achague aendelee na mshahara wake wa grade A au aanze upya na mshahara wa degree kima cha chini ambao kimsingi ni kidogo kulinganisha na mshahara aliofikia wa grade A sasa kwann mtu akijiendeleza asije kulipwa mshahara kutoka na muda wake kazini na pia elimu yake aliojiendeleza

mwenye msaada wowote juu ya hili naomba amsaidie

Hilo tatizo mkuu ni changamoto, linafanana na waliojiendeleza fani tofauti na walioajiriwa nayo, ila ni suala la muda tu litapatiwa ufumbuzi, ila hujatoa alternative maana kwa grade A mtu alipandishiwa mshahara ipasavyo kulingana na muda aliokuwepo kazin, sasa Degree ndio umeipata sasa huwez ukasema uchukue wa Grade uliyofikia then ujumlishe na wa Degree ni ngumu pia inategemea na uhitaji kwenye halmashauri wakati unaenda kusoma labda wao walihitaj huyo wa Grade A.
 
Hilo tatizo mkuu ni changamoto, linafanana na waliojiendeleza fani tofauti na walioajiriwa nayo, ila ni suala la muda tu litapatiwa ufumbuzi, ila hujatoa alternative maana kwa grade A mtu alipandishiwa mshahara ipasavyo kulingana na muda aliokuwepo kazin, sasa Degree ndio umeipata sasa huwez ukasema uchukue wa Grade uliyofikia then ujumlishe na wa Degree ni ngumu pia inategemea na uhitaji kwenye halmashauri wakati unaenda kusoma labda wao walihitaj huyo wa Grade A.

nilimaaanisha wamlipe mshahara kama mtumishi mwenye degree lakini aliekaa muda mrefu kazini nafkiributakua umeelewa nilimaanisha nn mkuu
 
apiganie teaching allowance kwa walimu tena ilipwe tarehe 15 kila mwez

mishahara mwisho wa mwez auboreshe. akianza tofaut na hilo atatumia ubabe hautasaidia

walimu ni kama wanamgomo baridi kitambo.

urejeshe heshima ya Mwalimu. Mh ndalichako, walimnyang'anya MWL hata cheo chake na kumdhalilisha. mw wa degree kama kada zingine alikuwa akiitwa afisa elimu Daraja 2... sasa wamempa mjina mwingine wa kibaguzi. waliita utekelezaji wa waraka wa maendeleo ya utumishi namba moja wa mwaka2014 muundo wa utumishi chini ya elimu. huu ni waraka wa kihuni
askari kila katikati ya mwezi wanalipwa laki tatu na ushee. kwanini waalimu hawalipwi posho kama hiyo? hata kama mimi nipo sector mbaya/risky, hata wasiponilipa mimi basi wawalipe waalimu...
 
askari kila katikati ya mwezi wanalipwa laki tatu na ushee. kwanini waalimu hawalipwi posho kama hiyo? hata kama mimi nipo sector mbaya/risky, hata wasiponilipa mimi basi wawalipe waalimu...
Upo katika idara/sekta gani mkuu ambayo hauhitaji kulipwa posho hata kama mazingira yako ya kazi ni hatarishi?
 
Pamoja na yote hayo tunamuomba mh waziri ahakikishe anawaondoa katika ofisi za elimu na katika kata (waratibu elimu kata) wote wasiokuwa na sifa na kuwaweka wale wenye sifa stahiki. Kwa mfano hakuna sababu kwa hali ya sasa kuwa na afisa katika ofisi ya elimu au mratibu elimu kata mwenye ngazi ya cheti au stashahada wakati kuna walimu wengi wenye Shahada au Shahada ya uzamili waliopo darasani. Hivi kiuhalisia mratibu mwenye cheti anawezaje kusimamia elimu katika shule ya sekondari iliyopo ktk kata yake? Au mratibu mwenye cheti anawezaje kumsimamia mwalimu mkuu au mkuu wa shule mwenye shahada au Shahada ya uzamili? Tukumbuke kuwa ualimu ni professional na siyo cheo cha kisiasa.
 
Sina shaka na Joyce Ndalichako ni mchapa kazi kweli na hapa Mh. Rais Dr. J.J.Magufuli hajakosea kabisa. Walimu ondoeni wasiwasi.
 
Kwasasa imekuwa kawaida watu waliopata grade hafifu kwenye mitihani ndo wanakwenda ualimu. Na hata wanapokwenda vyuo wengi hupitishwa tu bila kuwa na weledi wa masomo wanayofundisha. Imefika wakati waalimu wapande madaraja kulingana na uwezo wao katika masomo wanayofundisha.

Kwa wale wa sekondari nashauri walimu wafanye mitihani ya kitaifa ya sekondari pamoja na wanafunzi wao kwa masomo wanayofundisha. Kigezo cha kupanda daraja iwe ni ufaulu katika masomo wanayofundisha kwa alama ya A maana mwalimu anatakiwa kuwa mbele ya mwanfunzi. Haina maana mwalimu kulalamika hajapanda daraja kwasabu eti kafundisha miaka fulani. Hii itasaidia maana hawa walimu walishatoka vyuo hawajiangaishi kujiendeleza binafsi kwa kujisomea vitabu. Watu wanajali kupata kazi na mshahara basi tu.

Naomba hili pia lifanyike kwa shule za msingi na walimu wafaulu masomo yote ya msingi kwa alama ya A. Mi nimeona hii njia inatumika kwenye shule binafsi kwa walimu wanaotafuta ajira. Mwalimu anapewa mtihani waliopewa wanafunzi wake na kisha anaambiwa akawasaidie wanafunzi kufanya masahihisho ya mtihani. Walimu wengi hupata maksi ndogo kuliko wanafunzi wanaotaka kuwafundisha. Walimu wengi waliishia kuchekwa na wanafunzi na wakati mwingine kujiondoa wenyewe. Sioni njia nyingine maana watu wakipata ajira hawana mufa wa kujiendeleza wenyewe.
 
Unashauri walimu wafanye mitihani ya wanafunzi ndiya wapandishwe madaraja?
 
We unamjua vizuri huyo kiongozi wa necta wa sasa au ndo basi kuponda kila kitu ndo kawaida yenu. Tatzo mna mapungufu ya akili kila mtu mkubwa mnamchukia nchi hii. Muulize naibu waziri wa zamani wa tamisemi elimu atakuambia shughuli ya huyo dr msonde.na unajua sababu za ndalichako kuondoka necta

Msonda nimesoma naye masters, najua alikuwa mtu wa aina gani. Naomba unyamaze kama unahusudu mtu anayeitwa dr.
 
Tatizo la walimu in walimu waenyewe hivyi kwel kabisa kama wana umoja haswa hii teaching allowance ilipaswa iwepo kitambo tuu,bt bado muda upo wadau wa elimu tuhamasishane sekta ya elimu iboreshwe tupate maendeleo ya kweli tz.
 
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr JPM jana alikamilisha uteuzi wa baraza la mawaziri kwa zile nafasi alizokuwa ameweka kiporo.

Katika uteuzi huo amemteua Dr Joyce Ndalichako kuwa mbunge na hatimaye waziri wa elimu,sayansi,teknolojia na ufundi. Hongera Dr Ndalichako.

Ikumbukwe kuwa wizara hii ya elimu ina changamoto nyingi sana hali inayosababisha wadau wa elimu kupiga sana kelele juu ya hatima ya elimu ya watoto wetu kitaifa na kimataifa.

Hivyo basi,ninaomba tutumie fursa hii kumshauri waziri mwenye dhamana mambo ya msingi ambayo tunadhani akiyasimamia kikamilifu na kwa uadilifu mkubwa atainusuru elimu yetu ambayo kwa hakika ipo rehani. Mimi naanza kwa hili:

l) Ninamuomba waziri aboreshe mazingira ya kazi kwa walimu kwa kuwapatia makazi bora ya kuishi tofauti ilivyo hivi sasa.

ll) Pia masilahi kwa walimu iboreshwe ili waweze kufanya kazi zao kwa moyo na uadilifu mkubwa.

lll) waziri aipitie upya mitaala yetu ya elimu ili iweze kufanyiwa marekebisho kulingana na mahitaji ya elimu yetu kwa sasa.

ENDELEA...

Awashuhulikie maafisaelimu wakatili wanowaadhibu walimu ovyoovyo na kuwavunja moyo wa kufanya kazi.Alama 100 za kuwapeleka wanafunzi kiadato cha kwanza ni za chini sana zifike 200.waende sekondari wenye uwezo.Walimu wapandishwe madaraja na kulipwa mapunjo kwa wakaati.Mishahara ya walimu iongezwe kwa 60% ya mishahara ya sasa.Walimu wote waishi karibu na shule.
 
Bro. NECTA hawahusiki na malipo YA wasimamizi mitihani, mhusika ni wakurugenzi wa halmashauri, manispaa na majiji.

Hiyo michango ya Tsh.50,000 ya watahiniwa kama gharama ya mtihani, huwa anaiweka nani mfukoni?
 
kwa ukitaka kuchukua uafisaelimu wa mtu watu wakachukue masters tu, wenye masters wakimaliza vyeo watapelekwa wapi. Watu wanasoma kuboresha utendaji wao sio kuangusha vyeo vya watu!
Mkuu ndioo maana wana mawazo finyuu saana hatakutoa maamuzii yaoo, kazi kuwatisha walimu na kuwa nyanyasa pasipoo sababu, yotee hayoo ni elimu ndogoo, . Wakasomee
 
Back
Top Bottom