Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr JPM jana alikamilisha uteuzi wa baraza la mawaziri kwa zile nafasi alizokuwa ameweka kiporo.
Katika uteuzi huo amemteua Dr Joyce Ndalichako kuwa mbunge na hatimaye waziri wa elimu,sayansi,teknolojia na ufundi. Hongera Dr Ndalichako.
Ikumbukwe kuwa wizara hii ya elimu ina changamoto nyingi sana hali inayosababisha wadau wa elimu kupiga sana kelele juu ya hatima ya elimu ya watoto wetu kitaifa na kimataifa.
Hivyo basi,ninaomba tutumie fursa hii kumshauri waziri mwenye dhamana mambo ya msingi ambayo tunadhani akiyasimamia kikamilifu na kwa uadilifu mkubwa atainusuru elimu yetu ambayo kwa hakika ipo rehani. Mimi naanza kwa hili:
l) Ninamuomba waziri aboreshe mazingira ya kazi kwa walimu kwa kuwapatia makazi bora ya kuishi tofauti ilivyo hivi sasa.
ll) Pia masilahi kwa walimu iboreshwe ili waweze kufanya kazi zao kwa moyo na uadilifu mkubwa.
lll) waziri aipitie upya mitaala yetu ya elimu ili iweze kufanyiwa marekebisho kulingana na mahitaji ya elimu yetu kwa sasa.
ENDELEA...