Tumshauri Dr. Joyce Ndalichako

Tumshauri Dr. Joyce Ndalichako

1. Nyie mnajua lililokuwa linatokea NECTA kuliko Waziri Kawambwa ambaye NECTA ilikuwa chini yake?

2. MNA uthibitisho wowote wa kubagua Waislamu zaidi ya maneno yanayosikika mitaani?

Soma tamko hili la Waziri Kawambwa (ambaye ni muislamu pia) juu ya hayo uyasemayo.

Mkuu usituchukulie serious, we sometimes crack some jokes!
 
Afute pia GPA kwa sekondari na arudishe Division kwani GPA hazina mashiko
 
.............................Dr Joyce Ndalichako kuwa mbunge na hatimaye waziri wa elimu, sayansi,teknolojia na ufundi.

l) Ninamuomba waziri aboreshe mazingira ya kazi kwa walimu kwa kuwapatia makazi bora ya kuishi tofauti ilivyo hivi sasa.

ll) Pia masilahi kwa walimu iboreshwe ili waweze kufanya kazi zao kwa moyo na uadilifu mkubwa.

lll) waziri aipitie upya mitaala yetu ya elimu ili iweze kufanyiwa marekebisho kulingana na mahitaji ya elimu yetu kwa sasa.

ENDELEA...

Wale wanaofanya mzaha na thrd hii waendelee tu! Naongeza haya:
1. Sera mpya ya elimu haifai. Ipitiwe upya na muhimu ni kuachana na kiswahili ngazi za juu. Rudisha mpangilio wa zamani. yaani Kiswahili hadi darasa la nne. Darasa la tano kuendelea tutumie kiingereza. Kila mtu na hata wanasiasa watoto wao wanasoma kwa kiingereza.

2. Mkatae Katibu mkuu wako. Hafai na hana mwelekeo wowote wa kuboresha elimu. Hajwahi kusikia ugumu wa elimu kutokana na masomo aliyosoma. Ndiyo maana anatuletea mambo ya merits. Usanii tu!

3. Mkurugenzi wa NECTA hafai kabisa! Ondoa kiumbe huyo. Hata ktk masomo yake alikuwa ni mtu wa kuigiza tu na hakuna alipofanya la maana.

4. Ingilia kati watu wa VETA. Hawataki kujitanua badala yake wao ni kupiga dili tu na wizi mkubwa ktk vyuo vyao.

5. Kamisheni ya sayansi, COSTECH ipatiwe uongozi mpya. Hao waliopo ni tatizo la miaka yote hawana la kufanya zaidi ya safari. Futa bodi yao ambayo imekuwa ni ya wanasiasa badala ya watafiti wenye uwezo.

6. Rekebisha mitaala na hasa ya sayansi ambayo ilichezewa ili ufaulu uongezeke badala ya ufahamu.

7. Hao watu wa sayansi an technolojia, waangalie sana maana kumbe wapo kwa ajili ya kujifunza badala ya kuonyesha ufahamu wao. Kila wakati wao ni ziara za mafunzo! Hata wakurugenzi!
 
Wewe ulifurahi alichokuwa anakifanya wakati akiwa katibu mkuu balaza la mitihani? Mnasema tunamuonea kama kweli tunamuonea kwanini aliomba radhi baada ya kuona malalamiko ya waislam ni ya msingi? Pili nitajiridhisha vipi kuwa hatarudia tabia yake? Tatu kwanini nisiamini kutokana na chuki alizonazo dhidi ya waislam hata amrisha walimu wote wa kiislam wakatupwa vijijini na yeye kubaki na wagalatia wenzie maeneo ya mijini?
Una akili duni kama ya nguruwe! umejaa chuki, ujinga na upumbavu kiasi cha kutojua unaandia kitu gani! ni lini na wapi aliwaomba radhi watu wa hovyo kama wewe na kwa kosa lipi alilolifanya?
 
Ipite Comprehensive research itakayotueleza kwanini Kidato cha 5&6 ni kupoteza muda kwanini Sekondari isiwe miaka 5 then unakwenda polytechnic au university mojakwamoja.

Una akili
Kwa kuanza anza na proposal yako au project utupe hint s adhawishike
 
Toeni hoja ni kwa namna gani elimu iboreshwe,tupate elimu bora.
 
Aongezee maafisa elimu na ukaguzi wa shule ufanyike kila wakati.walimu ambao wanafundisha vijijini wapewe motisha.
 
1. Nyie mnajua lililokuwa linatokea NECTA kuliko Waziri Kawambwa ambaye NECTA ilikuwa chini yake?

2. MNA uthibitisho wowote wa kubagua Waislamu zaidi ya maneno yanayosikika mitaani?

Soma tamko hili la Waziri Kawambwa (ambaye ni muislamu pia) juu ya hayo uyasemayo.

Friday, June 8, 2012
at 10:37 AM
KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2012
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2012
1.0 UTANGULIZI
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita 2012 yaliyotangazwa rasmi tarehe 01/05/2012. Tarehe 28/5/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipokea barua kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu yenye Kumb. Na. BSK/W/012/01 ya tarehe 22/5/2012 iliyoeleza kutoridhika na ufaulu wa watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge kwa kuwa waliona matokeo yaliyotangazwa hayakuwa na uhalisia wa uwezo wa wanafunzi. Kutokana na barua hiyo, Serikali ilifanya uchunguzi kwa kuangalia mambo yafuatayo:
? Kulinganisha alama za watahiniwa zilizojazwa katika vituo vya usahihishaji mitihani na zile zilizohifadhiwa katika Kompyuta, yaani database ya Baraza la Mitihani ili kubaini kama kuna tofauti yoyote; na
? Kulinganisha alama za somo la Islamic Knowledge zilizochakatwa na Mfumo wa Kompyuta na sampuli ya alama zilizokokotolewa kwa kutumia kikokotozi (calculator).
2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
? Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi. Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo
kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya ?Paper? tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.
1
? Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una ?paper? mbili na siyo ?paper? tatu. Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia ?paper? tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia ?paper? mbili.
3.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI
? Baada ya kugundua dosari hiyo kwa somo la Islamic Knowledge, uhakiki ulifanyika kwa masomo yao yote ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2012 yaliyokuwa na ?paper? zaidi ya moja ili kujiridhisha endapo uzito sahihi ulitumika katika kupata wastani wa alama za watahiniwa. Matokeo ya uhakiki huo yalionesha kuwa alama sanifu zilizokokotolewa na mfumo wa kompyuta ni sawa na alama zilizokokotolewa na Kikokotozi. Hivyo hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo mengine.
? Matokeo ya somo la Islamic Knowledge yaliyotangazwa awali yamerekebishwa kwa kutumia Paper mbili kama inavyotakiwa ili kuendana na mabadiliko ya Fomati ya somo hilo. Marekebisho hayo yaliridhiwa na Baraza la Mitihani katika Kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 31/05/2012. Aidha, Kikao kati ya wajumbe wa Baraza la Mitihani na wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kilifanyika tarehe 31/05/2012 ambapo walielezwa kuwa Wakuu wote wa Shule wenye watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge wataandikiwa barua rasmi kufahamishwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika na barua hizo ziliandikwa tarehe 01/06/2012. Pia walifahamishwa kuwa matokeo yao yote ya masomo mengine hayana dosari yoyote na yanabaki kama yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Matokeo hayo yamewekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani na pia yatatangazwa kwenye magazeti.
? Pamoja na marekebisho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaunda Kamati ya wataalamu kuiwezesha serikali kujiridhisha zaidi na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Mitihani ili kuepuka dosari ya aina hiyo isijitokeza tena kwa siku zijazo.
? Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya
2
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.
4.0 HATMA YA WANAFUNZI WALIOREKEBISHIWA MATOKEO KATIKA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU
Wizara inapenda kuwahakikishia watahiniwa waliorekebishiwa matokeo yao kwamba, kwa kuwa zoezi la usajili bado linaendelea hadi tarehe 30/06/2012, waliorekebishiwa matokeo yao watapata fursa ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu endapo wana sifa stahiki. Aidha, kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, maombi ya mikopo hufanyiwa kazi rasmi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu kukamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo, hapatakuwa na athari yoyote kwa watahiniwa husika kupata mikopo endapo watakidhi vigezo vinavyotakiwa.
5.0 HITIMISHO
? Napenda kuhitimisha kwa kuwasihi wazazi, walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa na imani na Baraza la Mitihani la Tanzania kama chombo chetu chenye dhamana kisheria ya kuendesha mitihani nchini. Hapakuwa na hujuma yoyote iliyofanyika kwa watahiniwa ambao matokeo yao yamerekebishwa. Kosa lililojitokeza ni la kibinadamu, halikufanywa kwa makusudi wala kwa lengo lolote la kuhujumu kundi fulani la watahiniwa. Marekebisho yameshafanyika na matokeo stahiki yameshatolewa. Aidha, uhakiki uliofanyika kwa masomo yao mengine unaonesha kuwa hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo yote.
? Kutokana na dhana ya baadhi ya watu kuwa kunakuwa na upendeleo kwa baadhi ya watahiniwa wa makundi fulani katika usahihishaji
napenda kuwakumbusha kuwa wakati wa mitihani, watahiniwa
huandika namba zao za mitihani na siyo majina. Katika taratibu za
usajili wa Baraza la Mitihani hakuna kipengele chochote kinachomtaka mtahiniwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa. Vilevile, utaratibu unaotumika kuwapata wasahihishaji huzingatia uwezo wao kitaaluma na uzoefu kazini. Aidha, katika fomu ya mapendekezo ya uteuzi wa wasahihishaji hakuna mahali popote ambapo Mkuu wa Shule hutakiwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa ya mwalimu
anayependekezwa kusahihisha mitihani.
? Utaratibu unaotumika kusahihisha mitihani hautoi mwanya wa upendeleo. Katika kudhibiti uwezekano wa kupendelea mtu yeyote kila msahihishaji husahihisha swali moja tu na kisha humpatia msahihishaji mwingine asahihishe swali linalofuata. Aidha, kila msahihishaji hutakiwa kuweka vifupisho vya majina yake (initials) ili ufuatiliaji uweze kufanyika kadri itakavyohitajika. Pia uhakiki wa usahihishaji hufanyika kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa kazi na kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa amepata alama anazostahili. Dosari zinazobainika zimekuwa zikirekebishwa katika mchakato wa usahihishaji na wasahihishaji wanaobainika kuhusika na dosari hizo wamekuwa wakichukuliwa hatua stahiki mara zinapobainika.
? Pamoja na hayo niliyoyaeleza nina taarifa kuwa yanapangwa maandamano ambayo yanalenga suala hili hili la kutoridhika na matokeo ya awali ya somo la Islamic knowledge. Kwa kuwa suala hili limeshapatiwa ufumbuzi, nawasihi wananchi wajiepushe kushiriki maandamano hayo kwa sababu suala la msingi lililo wafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo, maandamano hayo hayatakuwa na tija.
IMETOLEWA NA DKT SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAREHE 07/06/2012

Wewe ni popoma, shukuru kawambwa si kila siku mlikuwa mnamlalamikia kuwa ni waziri mzigo? Imekuwaje leo unatuletea libarua lake? Au ndio baniani mbaya kiatu chake dawa? Hivi bila waislam kupiga kelele hiyo barua ingeandikwa?
 
Awaboreshe maslahi ya walimu. Pia awafute kazi walimu wanaotumia vyeti vya watu wengine.
 
Ndugu Ndalichako.

Boresha sana ELIMU YA AWALI...Tafiti nyingi zimeonesha faida lukuki za Elimu ya awali kwa mustakabali wa maisha ya mtoto kielimu, kijamii Na kiuchumi.
Anzia hapa...kwenye vyuo vya diploma ya ualimu wa msingi kuna department ya kuandaa waalimu wa shule za awali. TATIZO wakufunzi wanaowandaa hao walimu hawajui A wala B ya mtoto kwa undani maana hawakusoma EARLY CHILDHOOD EDUCATION.
tafadhali waziri, ajiri vijana wahitimu wa ECE kutoka UDSM/UDOM wafanye hiyo kazi badala ya kuwaacha jobless au kuwapeleka sekondari kufundisha masomo ambayo hawajayasomea chuo.
 
Hakika tulioomba Huyu mama kuteuliwa tunamshukuru Rais kwa kusikiliza kilio chetu.Ombi langu kwa waziri ni kuwa walimu wanadhalilika kwenye nyumba za upangaji pamoja na mgawanyiko kati ya walimu wanaoishi nyumba za selikari na wale waliopanga.Tunaomba bajeti ijayo walimu wasioishi nyumba za selikari wapewe house allowance japo kidogo kwa ajili ya kodi ya nyumba.
 
Naomba Mungu awasamehe tu akina Mungai, Mwantumu, Kawambwa, Mulugo ... Waliharibu sana!
 
Wale wanaofanya mzaha na thrd hii waendelee tu! Naongeza haya:
1. Sera mpya ya elimu haifai. Ipitiwe upya na muhimu ni kuachana na kiswahili ngazi za juu. Rudisha mpangilio wa zamani. yaani Kiswahili hadi darasa la nne. Darasa la tano kuendelea tutumie kiingereza. Kila mtu na hata wanasiasa watoto wao wanasoma kwa kiingereza.

2. Mkatae Katibu mkuu wako. Hafai na hana mwelekeo wowote wa kuboresha elimu. Hajwahi kusikia ugumu wa elimu kutokana na masomo aliyosoma. Ndiyo maana anatuletea mambo ya merits. Usanii tu!

3. Mkurugenzi wa NECTA hafai kabisa! Ondoa kiumbe huyo. Hata ktk masomo yake alikuwa ni mtu wa kuigiza tu na hakuna alipofanya la maana.

4. Ingilia kati watu wa VETA. Hawataki kujitanua badala yake wao ni kupiga dili tu na wizi mkubwa ktk vyuo vyao.

5. Kamisheni ya sayansi, COSTECH ipatiwe uongozi mpya. Hao waliopo ni tatizo la miaka yote hawana la kufanya zaidi ya safari. Futa bodi yao ambayo imekuwa ni ya wanasiasa badala ya watafiti wenye uwezo.

6. Rekebisha mitaala na hasa ya sayansi ambayo ilichezewa ili ufaulu uongezeke badala ya ufahamu.

7. Hao watu wa sayansi an technolojia, waangalie sana maana kumbe wapo kwa ajili ya kujifunza badala ya kuonyesha ufahamu wao. Kila wakati wao ni ziara za mafunzo! Hata wakurugenzi!

We unamjua vizuri huyo kiongozi wa necta wa sasa au ndo basi kuponda kila kitu ndo kawaida yenu. Tatzo mna mapungufu ya akili kila mtu mkubwa mnamchukia nchi hii. Muulize naibu waziri wa zamani wa tamisemi elimu atakuambia shughuli ya huyo dr msonde.na unajua sababu za ndalichako kuondoka necta
 
Una akili duni kama ya nguruwe! umejaa chuki, ujinga na upumbavu kiasi cha kutojua unaandia kitu gani! ni lini na wapi aliwaomba radhi watu wa hovyo kama wewe na kwa kosa lipi alilolifanya?
Ewe mgalatia usiokuwa na akili ni nani aliyekuroga?
 
pandisha madaraja walimu walioenda kujiendeleza kisomo sio kuwarudisha palepale
 
kwa mfano kuna mwalimu kakaa muda mrefu kazini alikua na grade A akafikia mshahara mkubwa tuuu almost zaidi ya mshahara wa kima cha chini cha mwalimu mwenye degree baadae akaenda kujiendeleza na akapata degree ya elimu lakini aliporudi kazini wanamwambia achague aendelee na mshahara wake wa grade A au aanze upya na mshahara wa degree kima cha chini ambao kimsingi ni kidogo kulinganisha na mshahara aliofikia wa grade A sasa kwann mtu akijiendeleza asije kulipwa mshahara kutoka na muda wake kazini na pia elimu yake aliojiendeleza

mwenye msaada wowote juu ya hili naomba amsaidie
 
Back
Top Bottom