Tumpongeze sana Rais. Hapa sasa kweli mambo ni mazuri

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
kwa sasa huwezi kujua kama bwana zitto kabwe yupo Tanzania au hayupo . huyu mpigania haki zetu watanzania. kwa sasa haki anapata sidhani kama ana sababu tena ya kupiga kelele. ametulia hii ni ishara kuwa rais anatimiza anayoyasema. anatimiza ahadi zake. zitto namjua angekuwa hapewi haki kungewaka moto. lakini kwa haki ipo naona mambo yanaenda burdani kabisa.

namshukuru sana rais kipindi hiki chake nimeshajenga nyumba mbili ya tatu nakaribia kumalizia. dodoma mbili na dar moja. ndani ya miaka hii michache yake. je akipewa 15? haya ndo matunda tunataka kuyaona. siyo ya matajiri kuishi maisha magumu. sisi tunataka matajiri waishikama wapo peponi pesa si zipo? kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake hakuna kuingiliana. magufuli alituchelewesha sana kipindi chake. mimi muda wake wote nilijenga nyumba moja tu tena kwa mkopo na vijcent kidogo binafsi. lakini kwa rais samia sasa safari nazopata ni nyingi sana na semina za kumwaga ndani na nje ya nchi. kifupi watumishi mshindwe wenyewe tu kwa ubwege wenu.

mama anaupiga mwingi sana...pass 1,000,000 halafu bao la kisigino. utasema nini? zitto jitulize ndugu uklemema ya nchi. siyo mnaleta rais anataka kutubana tusile.....tukale wapi sana? ni kujitahidi tu kupata kamba ndefu sana kisiwe kikamba kifupi.
 
Back
Top Bottom