Rais wetu Samia anasifiwa sana, tena anafanya mambo makubwa kimya kimya, ni yepi hayo?

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,956
4,143
Ninachojua na kukiamini katika maisha ya kila mmoja, ni kule kupambana saana ili mtu uweze kurahisisha maisha, na kwa sababu hiyo ili uwe na uhakika wa kufanya mambo mengine mhimu ya maendeleo, lazima uishinde njaa kwanza na ndipo utapata balansi ya fedha za kuanzisha vitu vingine kama kujenga na kuanzisha miradi.

Kama hujaishinda njaa, hata choice variable anafahamu fika kwamba, hawezi kuwaza zaidi ya wapi akapate chakula ashibishe tumbo lake kwanza.

Najua, suala la mtu apate wapi chakula ale na kwamba ili aishinde njaa, inambidi apambane yeye mwenyewe.

Kwenye hili, nasema hivi, watanzania ni wapambanaji, maana hawajawahi kwenda kuomba chakula kwa kiongozi yeyote.

Watanzania hawataki kiongozi asiyeumia pindi matarajio yao yanapoharibiwa na uongozi usiodhibiti mambo yanayosababisha maisha yao yawe ghali

Umeme ni kichocheo mhimu cha kufanya maisha kuwa maraisi, kudhibiti hali ya upotevu wa mapato serikalini, huchochea uchumi kwa serikali na kwa mtu mmoja mmoja,

Mwananchi anapokuwa na uhakika wa matibabu na yenye gharama ndogo, hiki pia ni kichocheo cha uchumi kwa mwananchi

Huduma mhimu zinapokuwa zinapatikana kwa njia halali bila rushwa, huchochea maendeleo kwa wananchi

Kodi zinapokuwa zinalipwa na watanzania wengi zaidi na kwa kidogokidogo tofauti na ilivyo sasa, watu wachache ndio wanaolipa kodi na kwa mapesa meeengi zaidi wengine wakiendelea kufanya biashara zao kwa magendo na rushwa, hiihuuwa uchumi wa waungwana.

Mh Rais wetu, anapewa sifa lukuki kwamba, anafanya mambo makubwa mno, tena ni kimya kimya, ndugu zanguni, mambo hayo ni yepi?

Umeme hakuna licha kwamba mvua ni nyiingi mpaka zinasababisha vifo kwa Watanzania.

Bidhaa bei ghali kiasi kwamba pato la mtu mmoja mmoja linaishia kwenye kutafuta chakula pekee.

Miradi mhimu ya kiserikali imeshindikana zaidi ya kuwa inasogozwa mbele tu kumalizika kwake.

Ufisadi ndio usiseme, report za CAG mbali na kwamba zinakuja na watuhumiwa ili kuchukuliwa hatua, lakini wapi, zinaishia kwenye makabati ya kumbukumbu.
 
Mtu anayefanya Makubwa hawezi kuogopa ushindani au wa ndani au wa nje.
 
Back
Top Bottom